Kijue kisa cha mlevi aliyeiba ndege na kwenda kuipaki Baa

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,722
10,226
"MWAMBA ALIYEIBA NDEGE KWA UBISHANI"

Mwaka 1956 mwanaume mmoja aitwae Thomas Fitzpatrick au "Tommy Vitz" waliwekeana dau wakiwa Bar na mlevi mwenzake kuwa anaweza kuiba ndege na kwenda kutua katikati ya mji kwa kutumia muda mchache.

Baada ya mabishano ya kuwekeana kibunda Tommy Vits alikwenda kuiba ndege usiku katika chuo cha urubani Teterboro na kwenda kutua mtaa wa #Manhattan na kuegesha karibu na #Bar waliyokuwa wanabishania.

Tommy alikamatwa na kufikishwa mahakamani lakini mmiliki wa ndege hiyo alishangazwa na tukio la Tommy na kuamua kufuta kesi kwa kuona hakuna uaribifu wowote uliofanyika katika ndege hiyo.

Mahakama ilimtoza Tommy faini ya dola 100 kwa kuvunja sheria za jiji na kuachiwa huru.

Miaka miwili mbele Tommy alikutana na mtu mwengine Bar akiwa anashusha 'kilevi' kwa bahati mbaya mtu huyo alikuwa anabisha kwamba hakuna aliyewahi kufanya kitendo kile (kuiba ndege na kutua mtaani) bali ni hadithi za tu za kutunga.

'Mwamba' Tommy hakukubali akaweka tena dau na huyo mtu kisha kwenda kuiba tena ndege na kutua katikati ya mjini, ila safari hii kwenye upenyo mwembamba zaidi huku akiwa amekwepa nguzo za umeme na maegesho ya magari kiasi kwamba baadhi ya watu walijua ndege hiyo imeletwa hapo kwa kuvutwa na gari.

Tommy alikamatwa na kufikishwani tena mahakamani.

Jaji alipomuona Tommy alimwambia 'sikutegemea ungerudishwa hapa tena kwa kosa lilelile"
Tommy akamjibu "ilikuwa ulevi mhe.."
Akahukumiwa kwenda jela miezi sita.

Baada ya matukio hayo mawili maarufu, Bar husika ya "NewYork CityBar" ilibuni kinywaji cha kuchanganya maarufu Cocktail iitwayo "TomyVitz" au "the late night flight"

Tommy alijiunga na jeshi kwenye vuguvugu ya vita ya #Korea

Vitz amefariki dunia mwaka 2009 akiwa na watoto watatu.

Chanzo:
Mtandaoni

1699366263071.jpg
 
View attachment 2806988
Story nzuri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom