Bonde la Baraka
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 4,580
- 7,938
Habari za asibuhi!
Napenda kuwaasa vijana wenzangu kuwa Dar es salaam si mahali pa kusaka maisha kichwa kichwa, kwamba utafute nauli tu na kusema unakuja dar kwa mjomba, Dada, kaka, rafiki n.k kutafuta maisha.
Huku wengi ni wapangaji, tena wamepanga kwenye mazingira hatarishi(machafu), wengi hugombania daladala, jioni mkitoka kazini hubanana kwenye magari kama ng'ombe wanapelekwa mnadani.
Wengi ni vibarua, watumwa wa Wahindi na Wachina. Wengi hulipwa 100,000- 150,000 tshs. Wengine laki na nusu -laki tatu, hao ndo huonekana wana unafuu.
Wengi hula Milo 2 tu kwa siku.
Msivutiwe na picha wanazopost fb, Dar nguo ni kama bure, wengi hununua sabufa, sofa siti 2 au 3 tu na TV hapo ndo anasema kayapatia.
Ni heri ukomae huko home, ujenge hata kibanda chako. Huku utageuzwa mtumwa, ndugu wengi wana roho mbaya, hii sijui inasababishwa na nini?
Kazi ambayo ni rahisi kuipata Dar ni ulinzi, kazi ambayo ni ya kinyonyaji na hatarishi.