Kijana usije Dar es aalaam kabla hujahakikisha unakuja kufanya nini, huku watu wanaishi maisha ya umaskini uliokithiri.

Habari za asibuhi!
Napenda kuwaasa vijana wenzangu kuwa Dar es salaam si mahali pa kusaka maisha kichwa kichwa, kwamba utafute nauli tu na kusema unakuja dar kwa mjomba, Dada, kaka, rafiki n.k kutafuta maisha.
Huku wengi ni wapangaji, tena wamepanga kwenye mazingira hatarishi(machafu), wengi hugombania daladala, jioni mkitoka kazini hubanana kwenye magari kama ng'ombe wanapelekwa mnadani.
Wengi ni vibarua, watumwa wa Wahindi na Wachina. Wengi hulipwa 100,000- 150,000 tshs. Wengine laki na nusu -laki tatu, hao ndo huonekana wana unafuu.
Wengi hula Milo 2 tu kwa siku.
Msivutiwe na picha wanazopost fb, Dar nguo ni kama bure, wengi hununua sabufa, sofa siti 2 au 3 tu na TV hapo ndo anasema kayapatia.
Ni heri ukomae huko home, ujenge hata kibanda chako. Huku utageuzwa mtumwa, ndugu wengi wana roho mbaya, hii sijui inasababishwa na nini?
Kazi ambayo ni rahisi kuipata Dar ni ulinzi, kazi ambayo ni ya kinyonyaji na hatarishi.
Hivi hizi story za Usije dar bado zipo siku hizi,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu inaonyesha ufahamu wako mdogo sana .
Sasa mambo ya James delicious yamekujaje hapa?
Kabla hujakonti komenti zako za kipumbavu ni vyema usome threads za mtu husika angalau tatu ili ujue kama anastahili komenti yako.
Mdoa mada wewe upo kijiji gani? Tuanzie hapo!usije ikawa na wewe upo Dar wanakujames delicious

Sent by Diaspora
 
Tumezika wengi sana kwa UKIMWI.
Hii hasa kwa wadada,wanaota ndoto kuwa ukiwa Dar mambo yatakuwa poa,lakini wakishaingia mujini mambo yanabadilika,wanaishia kubadilisha wanaume na hatima ya yote ni UKIMWI..
 
Mimi mwenyewe nashindwa kuondoka kwasasa kwakuwa nimeshajijengea ngome ila kama ningebaki Home region mpaka sasa nahisi ningekuwa mbali zaidi.
Ila ukisoma title vizuri utaelewa nimesemaje, nimesema cha kwanza ni kujihakikishia juu ya nini unakuja kufanya na si kutupa jarife ziwani bila kujua litakutana na nini majini.
Hivi hizi story za Usije dar bado zipo siku hizi,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwanini kilimanjaro na arusha. Kuna shida gani kwani
Upunguani tu wa vijana. .....
Maisha ya mikoani sasa hivi ni kama ulaya. .mikoani ukiacha mkoa wa arusha na moshi kipato cha tsh 200000 kwa mwezi ndani ya miaka yako mitano unakuwa tayar na nyumba navyo sema nyumba namaanisha nyumba kweli. ...
Vijana huku bodaboda wananyumba zao utafikir za wakurugenzi. ..

Acha waendelee kupiga picha kwenye saloon za wenzao na kwenye mageti ya wahindi huku wenzao mikoani wanachanja mbuga. ...
Siku wanarudi mikoani tutawaajili kulisha nguruwe

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miye mjomba wangu yangu aje mjini mpaka leo anakaa gheto, maisha yake ya ujanja ujanja tu miwani mikubwa kanyoa panki kuchomekea na kuvaa macheni shingoni na Pete tangu tupo darasa la kwanza mjomba maisha yake ya ujanja ujanja tu mpaka tunamaliza shule mjomba bado anamtegemea Dada yake mama yetu kiufupi simuelewagi uncle

Uncle kuoa ataki, kurudi shamba tanga ataki yani yeye usela tu kakomaa nao mjini
 
Kwa hiyo kijana aliyemaliza chuo unamshauri nini abaki Dar kutafuta kazi au arudi nyumbani?

Mtu akija dar kutafuta Maisha bila issue ya maana ,Je vigumu kutoboa huko dar.

Unawashauri nn Vijana ,wanaomaliza masomo yao wanao ishi mkoani , wabaki dar au warudi nyumbani

Kwahiyo wimbi kubwa sana la kijana wanaokimbilia dar ,Likifika huko linateketea tu au ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole, basi tena jiji lishamharibu

Siku hizi kuna kitu kinaitwa RECRUITMENT PORTAL. Kazi unaomba online, ukipakia tu taarifa zako sahihi unaweza kuomba kazi popote bila gharama.
Ni heri kubaki kijijini ulime mazao ya biashara. Unaweza kujikuta mpaka unaajiriwa tayari una nyumba yako, gari n.k hasa ukiwa kwenye mikoa ya kitropiki.
Kwa hiyo kijana aliyemaliza chuo unamshauri nini abaki Dar kutafuta kazi au arudi nyumbani?

Mtu akija dar kutafuta Maisha bila issue ya maana ,Je vigumu kutoboa huko dar.

Unawashauri nn Vijana ,wanaomaliza masomo yao wanao ishi mkoani , wabaki dar au warudi nyumbani

Kwahiyo wimbi kubwa sana la kijana wanaokimbilia dar ,Likifika huko linateketea tu au ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za asibuhi!
Napenda kuwaasa vijana wenzangu kuwa Dar es salaam si mahali pa kusaka maisha kichwa kichwa, kwamba utafute nauli tu na kusema unakuja dar kwa mjomba, Dada, kaka, rafiki n.k kutafuta maisha.
Huku wengi ni wapangaji, tena wamepanga kwenye mazingira hatarishi(machafu), wengi hugombania daladala, jioni mkitoka kazini hubanana kwenye magari kama ng'ombe wanapelekwa mnadani.
Wengi ni vibarua, watumwa wa Wahindi na Wachina. Wengi hulipwa 100,000- 150,000 tshs. Wengine laki na nusu -laki tatu, hao ndo huonekana wana unafuu.
Wengi hula Milo 2 tu kwa siku.
Msivutiwe na picha wanazopost fb, Dar nguo ni kama bure, wengi hununua sabufa, sofa siti 2 au 3 tu na TV hapo ndo anasema kayapatia.
Ni heri ukomae huko home, ujenge hata kibanda chako. Huku utageuzwa mtumwa, ndugu wengi wana roho mbaya, hii sijui inasababishwa na nini?
Kazi ambayo ni rahisi kuipata Dar ni ulinzi, kazi ambayo ni ya kinyonyaji na hatarishi.
Ndg Mpendwa... Hivyo umethibitisha kuwa WAHINDI ndo wakombozi na watoa ajira...?? Lakini kazi kwa makubaliano bila kushuurutishwa au kuLazimishwa !!! ( wee ni mbaguzi sana ) siyo vizuri kujumuisha watu!!!
 
Back
Top Bottom