Kijana usije Dar es aalaam kabla hujahakikisha unakuja kufanya nini, huku watu wanaishi maisha ya umaskini uliokithiri.

Kuna kiwanda cha kutengeneza jinsi cha Wahindi hapa Dar, malipo kwa siku 35 chakula juu yako.
Kwa mwezi ndo wanalipwa 105,000 Tshs kwa waliowaajiri. Sasa huu ni ukombozi au unyonyaji uliozidi utumwa?
Kazi zinaanza 08:00 mpaka 19:00.
Ndg Mpendwa... Hivyo umethibitisha kuwa WAHINDI ndo wakombozi na watoa ajira...?? Lakini kazi kwa makubaliano bila kushuurutishwa au kuLazimishwa !!! ( wee ni mbaguzi sana ) siyo vizuri kujumuisha watu!!!
 
Daah Mnazidi kutubagua Tu sisi wa mikoani sio vizuri wakuu sisi wanyewe tunapenda hayo mambo ya fesibuku
Tafuta pesa mkoa nenda dar kale upepo2 urudi mkoa au dominate ishu zako mkoa dar uende ukafungue branch dar pagumu sana japo chance za kupata pesa zipo kikubwa uweze kukubali kufanya kazi ngumu ndani ya miaka mi4 uku unajiwekea akiba au uwe na ufundi utafute jina miaka3 au 4 ndiyo utaweza kutusua ila iviivi aiseee utakaa ata miaka20 lakini hutapata chochote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm nashauri waliomaliza chuo kwanza wasipende kurudi mikoa waliyokulia kama anasoma chuo dar au Moro au mbeya mwaka mmoja kabla ya kumaliza chuo aanze kufanya chochote apo alipo kama biashara aanze au kilimo aanze itamsaidi sana ata akimaliza atakuwa kwenye nafasi kubwa ya kuendeleza alichoanza na atajua muelekeo wake wa maisha mbeleni ukirudi home unakuwa katika nafasi kubwa ya kuanza kutafuta kazi jambo ambalo kwa sasa ni gumu sana kupata lakini ukifanya kitu chochote unajivalue mwenyewe ata ukienda kuomba kazi hutakuwa na stress za nikikosa itakuaje
Kwa hiyo kijana aliyemaliza chuo unamshauri nini abaki Dar kutafuta kazi au arudi nyumbani?

Mtu akija dar kutafuta Maisha bila issue ya maana ,Je vigumu kutoboa huko dar.

Unawashauri nn Vijana ,wanaomaliza masomo yao wanao ishi mkoani , wabaki dar au warudi nyumbani

Kwahiyo wimbi kubwa sana la kijana wanaokimbilia dar ,Likifika huko linateketea tu au ?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ata unipe nn kuishi dar siwezi kwakweli yani mfanyakazi anayelipwa 450,000 kwa mwezi karagwe na mfanyakazi anayelipwa 1,000,000 akiwa dar wa karagwe anafanya maendeleo makubwa ndani ya muda mfupi kuliko wa dar. Sema watu wamekalilishwa kwamba maisha mazuri yapo dar ila ukweli ni kwamba fursa zipo vijijini uku tulipo ukizichanga vzr haina kufeli.
 
Maisha yako ghali. .. mjini huwez kupata kiwanja kwa m5 Lakn mikoa mingne pembeni ya mjini ukiwa na m3 au 4 unapata kiwanja

Mkuu Arusha viwanja vipo hadi milion 1.6 tena kiwanja halali na kimepimwa na hakipo kijijini vipo eneo linalokuwa kwa kasi sana Maji ya Chai.

Sent using akili yangu
 
Kuna kiwanda cha kutengeneza jinsi cha Wahindi hapa Dar, malipo kwa siku 35 chakula juu yako.
Kwa mwezi ndo wanalipwa 105,000 Tshs kwa waliowaajiri. Sasa huu ni ukombozi au unyonyaji uliozidi utumwa?
Kazi zinaanza 08:00 mpaka 19:00.
Pole sana kama hizi habar ni za kweliiii???? Mkuu nchi hii ahimu inaendeshwa kisheria, usipotoshe wala usizidishe uchochezi!! Hapa kuna wizara maalum kusimamia KAZI na BIASHARA !! iweje wasilifahamu madhila ya viwandani?? WAHINDI washajenga KIWANDA hilo ni jambo jema kwa NCHI,, UENDESHAJI NI WETU SASA..!!
 
Ukweli mtupu...ukibahatika kuona maisha ya watu wengi utashangaa, ni maisha ya kilofa ila kijanja..ujanja janja mwingi, utapeli, utu kwa mbali sana, watu wanabangaiza zaidi, they most do for survival, hata akijenga ni kijanja janja tu..(sio wote, )..wachache walioikamata Dar ndo wanawafanya wengi waishi maisha ya pasu kwa pasu..ilimradi siku ziende, ..na misemo ile mingi ya kimaisha ipo Dar...utasikia Dar hulali njaa, kwani ukiwa bush au nje ya dar ndo utalala njaa...Njoon kutafuta Dar, jiji linalomeza maisha ya wengi, na wengine wanajifia bila taarifa wanazikwa ovyo. Mhimu kujua aliyosema mtoa post, kabla hujaja Dar. Watu wanaishi na hawatoki dar hata kama wanapata shida sana kama wanavyominywa na kukanyagana ktk mwendokasi !!
Karibu Dar, jiji lenye changamoto na kupungua kwa utu...usije na jembe huku..utalima lami!! Njoo na kichwa tu..mengine utayakuta,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashukuru, umenielewa vyema sana.

Wewe itakuwa ndiye uliyeelewa vizuri sana.
It was just a Joke!! Lakini kwa kwelil ni sehemu ndogo sana ya mji wa Dar es salaam inayostahili kuitwa jiji. Dar ni muunganiko wa vijiji vingi sana vilivyoendelezwa kiujenzi bila mpangilio. Matokeo yake wanaotoka mikoani huwa si sehemu ya mji bali huishia kuishi kwenye maeneo yaliyokuwa vijiji zamani si sana.

Miji yenye fursa ni ile iliyopangaliwa kwani huchanganya makazi na shughuli za binadamu zinazoweza kuwaletea watu kipato. Dar watu karibia asilimia 80 wakiamka asubuhi ni LAZIMA waelekee Posta ama Kariakoo na ndiyo maana usafiri wa kuelekea huko ni balaa wakati wa Asubuhi na ni utumwa jioni wakati wa kutoka Posta ama Kariakoo.

Na kwa Dar es salaam hakuna Kiwanda chenye uwezo wa kuajiri watu zaidi ya 10,000 kwa maana nyingine kwenda Kariakoo ni lazima uwe ni mchuuzi na kwenda Posta basi wewe ni mwajiriwa ama mfanyabiashara. Jee anayekuja toka mikoani ataanzia wapi ili apande ngazi na kufikia uwezo wa kuwa maeneo hayo.

Dar kuna Umaskini wa kutupwa sema watu wake wanauvumilia kwa kuwa wengine Dar ndiyo "mkoani" kwao!!
 
Mkuu Arusha viwanja vipo hadi milion 1.6 tena kiwanja halali na kimepimwa na hakipo kijijini vipo eneo linalokuwa kwa kasi sana Maji ya Chai.

Sent using akili yangu
Mkuuu maji ya chai na mjini in mbali sana bora ungesemea USA..
 
Mimi binafsi nimeshachoka na hizi discussion za dar na mikoani wapi bora. Nasema hiviii.. KILA MTU AISHI PALE ANAPOONA YEYE KWAMBA PANAMFAA! Watu wote wa mikoani wakihamia dar hapatakalika, na pia watu wote wa dar wakirudi mikoani hakutakalika. Wee komaa hapo hapo ulipo na wala usitake kujua sehemu zingine mambo yakoje.
 
Back
Top Bottom