DAR iko overrated, Majority ya watu wanaishi maisha ya ovyo sana

CHIBA One

JF-Expert Member
Nov 16, 2018
560
2,087
Vijana wengi na watu wa mikoani, na pengine kwa kukosa Exposure hudhani Watu wanaoishi Dar wanafaidi sana pengine kwa Maisha mazuri, hali ya hewa nzuri na pesa za kukidhi kila mahitaji Yao.

Lakini asilimia kubwa ya watu Dar es salaam wanaishi mazingira magumu sana, Chumba kimoja kilichojaa ndoo na madumu ya maji, joto zaidi ya Nyuzi joto 30, Kulala na watoto chumba kimoja, Mvua zikinyesha maji yanavujia ndani pengine na Kusomba Nyumba kabisa.

Wakazi wengi wa Dar es salaam wanafanya shughuli zao zaidi ya km 10 kutoka kwenye makazi yao, na utakuta anauza utumbo wa kuku au anaenda kuuza bidhaa za Muhindi k.koo.

Kero haiishii tu kwenye Makazi. Mtu ataamka saa 10 alfajiri na atapanda daladala iliyojaa kama wako Jehanamu, kama ulinyoosha shati lako basi tegemea ukishuka litakuwa limesagwa kama ulikuwa unapigana. Mateso yako pale pale wakati wa kwenda na kurudi kazini.

Mara nyingi watu hawa huhangaikia kipato cha kati ya elfu 10 hadi elfu 30 kwa siku (ukiachilia Mbali ambao wameajiriwa na kufanya biashara ambao hawa ni tabaka la kati).

Kwa kuwa Dar ina shughuli nyingi za kujipatia hivi vipato vidogo vidogo, bado vipato hivi havitoshi kumfanya mtu akaishi maisha ya ahueni kwa maana ya kujenga Nyumba yake mwenyewe ambayo ina viwango na ubora mkubwa kama mikoani.

Kwahiyo pesa nyingi wanayopata vijana huishia kununua I phone na TV kubwa kuweka kwenye magheto yao ya chumba kimoja.

Kikubwa ukiwa na Maarifa na ubunifu katika utafutaji unaweza kupata mafanikio zaidi ukiwa mikoani zaidi hata ya Dar wanakokimbilia vijana.

Wanawake wa Dar ni waswahili na wanavaa mawigi ya rangi rangi, kope ndefu bandia, Matapeli wa Mapenzi, Wanashindana na Mashosti zao kuhakikisha wanahongwa zaidi kuliko rafiki zao na IQ zao ni ndogo.

Hiyo ndiyo Dar es salaam ambayo wakazi wake hujaa dharau wanapoenda Mikoani wakati hawana kitu.

Samwaleku.
 
Back
Top Bottom