Kijana Mvietnam aliyeamua kuacha kazi iliyokuwa inamlipa milion 120 kwa siku baada ya kuchoshwa na umaarufu

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,045
Kama kuna jambo linalolipa ukipatia ni game development. Basi mwaka 2012 kijana mmoja wa Vietnam aliyekuwa na umri wa miaka 25, akiwa kaanzisha kampuni yake ya kutengeneza magame ya simu ambayo mengi hayakuwa yamefanya vizuri maana yeye alikuwa anatengeneza games za 2D wakati dunia ilikuwa inahamia kwenye games za 3D, alitengeneza game kwa ajili ya iOS lijulikanalo kama Flappy bird. Lilikuwa game simple lakini ukianza kulicheza basi unakuwa addited.

Ndani ya game hilo lilijumuisha kugonga gonga screen ya simu ili kufanya ndege aliyekuwa anaruka akwepe vikwazo. Game hilo aliliwweka kwenye Apple Store lakini nalo halikupata watumiaji kwa miezi kadhaa, mara ghafla mwaka 2013 mwezi wa pili, watu walianza download gamehilo kwa kasi. Baada ya muda mchache game hilo ndiyo ikawa app inayoongoza kusownlodiwa.

Game likawa maarufu, na jamaa akawa maarufu watu wakaanza kumfuatilia twitter, vyombo vya habari vya nchi mbalimbali hasa Marekan vikawa vinaomba mahojiano lakini anagoma. Ikafika kipindi ikawa inakadiliwa kuwa anatengeneza dollar 50,000 kwa siku kutokana na matangazo yaliyomo kwenye game. Hii habari ilipotoka ndipo ikawa balaa. Huko kwao vietnam akawa star, hawezi tena kutoka nje, nyumba ya wazazi wake ambao mpaka muda huo hawakujua kuwa mtoto wao ni tajiri na mashuhuri ikavamiwa na mapaprazi. Ndipo wazazi kupata hizo habari.

Basi kijana akaanza kuwa na stress maana hakupenda huo umaarufu, akawa hawezi tena kuishi maisha yake ya kawaida. Wazazi wakaanza kuwa na wasiwasi na kijana wao. Vyombo vingine na watu walio na mtima nyongo wakawa wanasema Nitendo imfungulie mashitaka kwa kuiga mazingira ya game la super mario.

Kijana akaona isiwe tabu, akaandika twitter kuwa amechoshwa na umaarufu na maisha yake yalivyobadilika. Hivyo samahani sana, hilo game analiondoa maana halimpi furaha bali amenza kujuta kulitengeneza. Na kweli kesho yake flappy bird ikawa haipo tena Apple store.

Kijana akawa kimya wengine wakadai kajiua, kila mtu akawa anasema anachodhani. kumbe kijana alikuwa kachill tu.

Kwa sasa amerudi, anaendelea kutengeneza magame lakini hayapati ule umaarufu kama wa flapy bird. Anasema japo maisha yake hayako kama zamani lakini walau ana amani.

flappy.jpg


Bwan Don Guyen

don guyen.jpg
 
Hii ni dhairi wewe ni miongoni mwa wale waafrika ambao kama unataka kuwaficha kitu, basi kiweke kwenye MAANDISHI.

Kama huamini alichoandika...Google jina la mhusika upate na ya ziada.

Milango ya fahamu iko mitano, sio lazima ung'ang'anie KUSIKIA kuna kuona na kuonja pia.
Comments ziwe fupi fupi plz
 
Aisee namkumbuka huyo jamaa, aliona pesa na umaarufu anaopata uegeuka kuwa mzigo. alichofanya ni kufuta game ili aishi maisha ya kawaida aliyoyazoea.

ummarufu alioupata huyu bwana game yake ilikuwa inatrend nchi nyingi, pia alipata followers zaidi ya laki.

Kwa siku alikuwa anaingiza zaidi ya milioni 100,

Pesa zikizidi na matatizo yanakuwa makubwa, kijana hakuzoea kuishi maisha ya kuwa maarufu na kufatwa fatwa na makamera, akapiga chini hilo game lililokuwa linamwingizia pesa ila linamfanya aishi maisha ambayo hajazoea.

heri kula kande kwa uhuru kuliko biriani gerezani
 
Back
Top Bottom