Wamuua Kaka yao kwa shoka baada ya kuchoshwa na vipigo vya mara kwa mara

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Inadaiwa kuwa watoto hao (majina yamehifadhiwa) ambao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo, walifanya tukio hilo kutokana na vipigo vya mara kwa mara kutoka kwa kaka yao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi (ACP) Alex Mkama, akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu, alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia juzi.

“Hili tukio limetokea Kitongoji cha Ugogoni, Kijiji cha Mbamba. Kijana huyu (inadaiwa) ameuawa kwa kupigwa na shoka kichwani na wadogo zake wawili akiwa kalala,”alisema.

Kamanda Mkama alisema chanzo cha tukio hilo ni kutokana na kuwapo kwa ugomvi wa mara kwa mara. Kaka huyo anadaiwa alikuwa akiwapiga na kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji.

“Huwa wanaishi kwa pamoja (wote watatu) kwa kujilea wenyewe. Watoto wameeleza kuwa kaka yao amekuwa akiwapiga na kuwanyanyasa na muda mfupi kabla ya tukio, alitoka kuwachapa na baada ya kufanya hivyo, alikwenda kujilaza kwenye kiduku (nyumba za Wasukuma) iliyoko hapo hapo nyumbani kwao.

“Akiwa amejipumzisha hapo, wadogo zake walikula njama na kwenda kumpiga na shoka kichwani na ndipo alipofariki dunia. Tunawashikilia watoto hawa tukiendelea na uchunguzi,” alisema Kamanda Mkama.

Alisema wakati tukio hilo likitokea, mama yao alikuwa amekwenda kwenye matibabu kwa mganga na baba yao alishatengana nao.

Kamanda alisema baada ya watoto hao kufanya tukio hilo, walimjulisha mama yao kuwa wamempiga kaka yao na amefariki dunia.

“Ndipo mama yao akatoka kwa mganga na alipofika (nyumbani) akakuta mtoto wake amefariki dunia na hawa wadogo wakiwa wamekamatwa na viongozi wa serikali za mitaa na kufikishwa kituo cha polisi,” alisema.

Kamanda Mkama ametoa wito kwa wazazi kujikita kwenye malezi mazuri ya watoto wao kwa kuwa roho za kikatili zinatokana na malezi ya hovyo.

“Kama wazazi watajikita katika maadili mazuri ya kuwalea watoto wao hatutegemei kuona matukio kama haya. Wazazi wasikwepe wajibu wao wa kulea watoto wao,” alisema.


Chanzo: Nipashe
 
WATOTO wenye umri wa miaka 13 na 15, wakazi wa kijiji cha Mbamba, Kilosa mkoani Morogoro wanadaiwa kumuua kaka yao, Wenja Maduka (20), kwa kumpiga shoka kichwani wakati amelala.

Inadaiwa kuwa watoto hao (majina yamehifadhiwa) ambao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo, walifanya tukio hilo kutokana na vipigo vya mara kwa mara kutoka kwa kaka yao. /
Inadaiwa kuwa watoto hao (majina yamehifadhiwa) ambao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo, walifanya tukio hilo kutokana na vipigo vya mara kwa mara kutoka kwa kaka yao. /

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mzazi kapoteza watoto wa 3 ,mmoja kafa wengine wanafungwa hao ila bado wadogo.

Dunia ni majanga tu.!!
 
Back
Top Bottom