Kijana huna haja ya kuharakisha kuoa eti uwahi kupata watoto usije kuitwa babu

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,908
19,112
Kuna hii tabia ya watu waliokata tamaa ya maisha wanadhani kuwahi kuoa na kuwahi kupata watoto ndio suluhisho la matatizo yao, basi wanataka kulazimisha kila mtu awe kama wao.

Watu kama hao hawana uhakika na maisha yao wanategemea watoto waje kuwasaidia, sina shida kuhusu kuwahi kuoa kama umeamua mwenyewe ila sio ili uwahi kupata watoto eti usije kuitwa babu wa wanao.

Tuangalie mifano hai, Obama kazaliwa mwaka 1961,akaoa 1991 akiwa na miaka 30, akazaa 1998 akiwa na miaka 37, Clinton amezaliwa 1946,kazaa 1980 miaka 34.

Putin amezaa mwanae wa kwanza akiwa na miaka 33, rais wa china kazaa mwanae akiwa na miaka 38, hiyo ni mifano michache tu ipo mingi.

Kama unategemea watoto waje wakusaidie mbeleni kwenye maisha wahi kuoa, kama hujajipanga na maisha yako ya mbeleni na ukadhani mbadala ni watoto waje wakusaidie wahi kuoa.

Mliokata tamaa ya maisha oeni ili muwahi kupata watoto msishinikize kila mtu awe na mawazo kama yenu.
 
A goog point to note!!!
 
Akili za kuambiwa changanya na zako ila kuzaa mapema ni vizuri zaid
Lolote lile ukilikamilisha mapema ni jema zaidi ya kuchelewa ...

Kwanza mtoto ukimlea ukiwa bado una nguvu / kijana inakuwa vyema zaidi kuliko mwanao kuwa na hisia kuwa wewe ni babu yake! Binafsi najisikia raha nikikaa na mwanangu tukaanza kujadili mambo ya maana nyumbani, kumshirikisha kwenye shughuli zangu n.k.

Wa kuchelewa endeleeni kuchelewa, wakati tukiwa tunakula raha za uzeeni nyie ndo mtakuwa mnasomesha watoto.
 
Kweli kabisa mkuu kupata watoto mapema ni raha sana
 
Mkuu lazima tuishi kukingana na mazingira yetu na hali yetu ya kiuchumi kwa mtu husika. Kwetu huku bongoland miaka 28 tayari mtu alishakuwa bibi au babu kutokana na ugumu wa maisha, akiwa na stress za kutosha kutokana na changamoto za maisha pamoja na ndoto zisizofanikiwa za kuwa na maisha mazuri, kipato kizuri na makazi mazuri na hata demu/mke mzuri. Bado lifespan ya 'mbongondese" ikiwa chini ya 60 kwa nini mtu asiwe na shauku ya kupata mtoto mapema kabla hajaaga dunia?
 
Back
Top Bottom