sema ukiua huwezi kuwa na uhakika je uliyemuua ndiye ama siye !! na ukiruhusu hivyo Askari anaweza kutumia mwanya huo kuua kwa sababu zake zingine afu akasema jambaz sugu.Halafu wakianza kuuawa utasikia haki za binadamu wanakuja, Huwa sijui wanatetea haki za binadamu wa wapi?? Polisi msako uendelee
Naona wewe una akili kama hao polisi za kutesa mtu hata kama hahusiki.Awekwe korokoroni kwa kushindwa hata kutoa msaada wa kupiga yowe
Unaamua kuuliwa kisa kupambania simu yako ya ef 70Unamuua binadamu mwenzako kisa simu mali yake.
Unaamua kuuliwa kisa kupambania simu yako ya ef 70
cc: BavichaHalafu wakiuliwa kuna watu wanakuja kuwatetea humu ndani... Aliyeua naye auwawe
Kihistoria Mwananyamala kwa Manjunju hadi kwa mama Zakaria ni kambi za wahalifuMwananyamara hapo town na ndio iliko ile ofisi yao ila yanatokea haya.
Mheshimiwa, maisha yetu yapo hatarini daily.
😒😒Unaamua kuuliwa kisa kupambania simu yako ya ef 70
cc: Bavicha
Ni kisasi hiki.Mkazi wa Mwananyamala, Manjunju mkoani Dar es Salaam, Billal Hoza (21), amefariki dunia baada ya kuvamiwa na kundi la vijana waliomchoma kisu sehemu mbalimbali za mwilini na kumpora simu.
Vijana hao wapatao watano walimvamia kijana huyo aliyekuwa amekaa nje ya nyumba yao na kumchoma kisu mgongoni, upande wa moyo. Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea juzi saa 3:30 usiku, wakati Hiza na rafiki yake wakiwa wamekaa barazani nyumbani kwao, wakichezea simu.
“Wakati wanachezea simu walipita vijana kama wanne, kati yao mmoja akamfuata huyu kijana (Hoza) akampokonya simu, akaendelea kutembea na wenzake, ndipo Hoza akamfuata, akambana na kumtupa chini na mmoja wao akatoa kisu na kumchoma."
Bongo ni hatari mzee na uhatari wake hatuna vifaa vya kuwabaini hao wezi ni bahatisha bahatisha tuu na wezi wengi wanajua kuwa wanaowafanyia umafia hawana siraha yeyote ndio maana tunasikia haya matukio na wenye siraha pana vipengele vya kuwabana hata wakitumia siraha zao..itokee mtu awafyatue panya road watano utasikia kaua kisa simu kumbe mtu alikua anaokoa maisha yake sio simu..Unamuua binadamu mwenzako kisa simu mali yake.
Iringa ikiwemo! Juzi nilikuwa huko, nikalala maeneo ya barabara 2, asubhi natoka kuwahi stendi nikakatiza nyuma maeneo hilo ghorofa la hapo stendi ya zamani walivyokuwa wamejazana almanusra nitimue mbio. Wako busy wanavuta mimoshi yao tuKwa sasa watakuwa wametorokea mikoani kujificha
Laana za kujitakia tuUnamuua binadamu mwenzako kisa simu mali yake.