Habari wana JFs,
Nina rafiki angu wa miaka mingi ambae tumekua karibu kama ndugu ameniomba ushauri kama mtu wake wa karibu, lakini nimepata mtihani kidogo katika kumpa majibu kutokana na uzito wa jambo lake.
Nilimshauri kulileta humu kwa kutotaja majina yake ilimradi tu aone ushauri na busara za wana JFs.
Ni kijana ambaye yuko kwenye mid 30s ambae anajitafuta kimaisha mpaka hivi sasa. Baba mzazi alishatangulia mbele haki na akabaki na mama mzazi ambae hakuishi nae kwa kipindi kirefu toka akiwa mdogo kwa kuwa alikua akiishi na baba mzazi pindi wazazi wake walipotengana.
Changamoto kubwa ni kwamba kijana huyu alikua na upendo mkubwa sana kwa mama ake huyo lakini kadri miaka inavyokwenda upendo unazidi kufifia kutokana na tabia ya mama kutompendeza kijana huyo. Mama siku zote amekua ni mtu wa kumtafuta kijana wakati akiwa na shida binafsi (kifedha) na shida ambazo mara nyingi inakua ndani ya uwezo wa kijana huyo. Na hata ikitokea siku kijana akawa anaumwa au kuna changamoto anapitia mzazi anakua hana muda wa kumtafuta mtoto wake na kumjulia hali au kuulizia tu mambo yake yanaendaje. Ikija simu ya mzazi huwa ni kusema nna shida na kiasi kadhaa namba unisaidie basi.
Kwa hivi sasa imefika hatua kijana ameona hili jambo haliko sawa na anataka aongee na mzazi wake amwambie ukweli kuwa halimpendezi ili ikiwezekana abadilike awe kama wazazi wengine kwa kuonyesha upendo kwa watoto wao na kuwajali.
Swali, je amwambie mama yake kuwa hapendezwi na tabia au akae kimya tu maisha yaendelee huku akiwa na masononeko moyoni?
Karibuni kwa maoni yenu na ushauri wana JFs