Kiini macho cha Kamati ya January Makamba na Dowans

Nashauri tuandamane nchi nzima kushinikiza bunge kuvunjwa. Hii ni kutokana na wabunge kwa tiketi ya ccm, wakati wa semina elekezi iliyofanyika chini ya uenyekiti wa JK, kula njama ya kuikingia kifua serikali, kutokana na kashfa mbali mbali zinazoikabili. Kitendo hicho ni usaliti mkubwa kwa wananchi na hivyo haustahili kuvumiliwa.
 
WanaJF mie ninawapa home work kidogo tu, Huyu Dogo makamba si bure, ile barua yake kwa Ngeleja kaeni mkijua is a set up kwa Mdanganyika, kwanza aliomba mitambo iwashwe ilhari kesi iko mahakamani, pili hilooooooooooo limiliki la Dowans eti limejitokeza, Akili mkichwa Great Thinkers......mie yangu hayo tu, Fikiria mbali ona karibu....
 
Siku za karibuni baada ya Bunge kuteua wenyeviti na wajumbe mbambali wa kamati za kudumu za Bunge kusimamia sekta tofauti, imekuwa mwiba kwa baadhi ya mawaziri na watendaji husika katika sekta zao. Mojawapo ya sekta inayooneka kuwekwa katika tishio ni sekta ya madini na nishati. Mojawapo ya mambo anayozungumzia ni pamoja na haya;

January Makamba anadai siasa ndiyo imepeleka nchi gizani. Anamsuta Waziri wa Nishati na Madini kuwa aache kuorodhesha miradi ya uzalishaji umeme kwa sababu kinachohitajika ni umeme si orodha ya miradi. Tumewahi kusikia kauli kama hizi siku za nyuma pale kundi fulani la wanasiasa walipokuwa wanashinikiza taifa lifunike kombe ili mwana haramu aweze kupita.

Kadhalika aliahidi kuishinikiza serikali kutafuta suluhisho la mgao wa umeme nchini.

January Makamba anaweka hoja mezani kuwa mitambo ya Dowans iwashwe kwa mkataba wa muda wakati kesi yake inaendelea mahakamani. Ikibidi fedha zinazopatikana ziwekwe katika mfuko maalumu kusubiri kesi iliyo mahakamani. Rais Kikwete amekuwa akisema wazi kuwa hapendi serikali yake kuingilia uhuru wa Mahakama

Tumeshuhudia kuja kwa anayedaiwa kuwa ni mmiliki wa DOWANS nchini ili kufanya mazungumzo na serikali ili kuona uwezekano wa mitambo hiyo kuwashwa. Haya yote yanamweka Ngeleja katika kona mbaya kwa mtazamo wangu. Hata ikatokea kukawa na mabadiliko katika baraza la mawaziri, basiNgeleja anaweza kuwa kakalia kuti kavu na nafasi yake kuchukuliwa na Makamba.

Katikati ya harakati hizi, yapo madai kuwa January Makamba anakuja na pendekezo alilopewa na mafisadi kuwa, Dowans wapunguze au kusamehe deni wanaloidai TANESCO lakini nao wapate mkataba wa kuzalisha umeme kwa muda usio na ukomo.

Nimesema kuwa hayo ni madai, lakini kama itabainika kuwa kweli, basi, lugha yake ya kizalendo itageuka kuwa ya kidalali na isiyo ya kizalendo. Wakati hakuna bei itoshayo kununua uzalendo, lakini tuna hakika kuna bei ya udalali, na ni wenyewe Dowans wanaojua wametenga kiasi gani cha fedha kunadi mitambo yao ndani ya Bunge na Serikali.
 
...huyu January alitaka sana uwaziri na akaukosa, naona watu waliokuwa wanataka kumtumia wamemuweka kwenye ile kamati nyeti na amekuwa akiongelea hoja moja tu kama umegundua...yeye na dowans tuuu, tunajua ni dalali na anatumiwa tu na anaostahili kuwalipa fadhila kwa kumfikisha pale...ni muda tu tatabaini ukweli wake....na tutajua janja yake....
 
Mimi nafikiri hawa jamaa wanajuana vizuri!hakuna jipya wala tija!huyu mtoto wa makamba ni pandikizi la Lowasa!!
 
Wandugu huu ni mchezo wa kuigiza, huyu January ni wakala kamili wa mafisadi hana uzalendo wala uchungu wa tatizo la umeme!!! tukumbuke kuwa yeye amewekwa katika ubunge kwa kuwezeshwa na Rostam ikiwa ni malipo kwa Mh Shelukindo ambaye alikuwepo kwenye kamati ya Mwakyembe, hivyo basi amewekwa tena ili kuhakikisha Dowans inalipwa au kupewa mkataba mwingine na ikibidi atapewa uwaziri kuhakikisha adhma yao inatimia. KWAKO JANUARY TAFADHALI WATANZANIA WANALIA JUU YA NCHI YAO KUTOKANA NA UFISADI WENU!!!!!
 
Hata kama alitakiwa kuwa wazili wa aina yeyote...wewe muanzisha thread unatakiwa kujua fika kuwa January na February wote ni ndugu moja. hawawezi kutofautiana ni kutubeza.

Alafu katika thread yako naona kama unampigia chapuo jamaa (kama sijakusoma vizuri) jiulize Mvua zikianza kunyesha na mabwawa yakajaa huyu jamaa ataongea nini tena???? maana yeye tokea ameingia ni masuala ya mgao na kuwasha dowans tuuuuu... maji yakijaa hatakuwa na kazi kwa mtazamo wangu au hata vyombo vya habari havitamfuata tena maana hatakuwa na ishu tena.

Soma alama za ukutani kaka WOTE NI KIZAZI HARAMU CHA RA na EL.
 
Changa la macho na huyo mtoto wa makamba atawachanganya watanzania, ni huyo huyo anataka mitambo ya dowans iwashwe. Mpumbavu tu na rafiki zake kila siku mnampigia debe humu jamii forums lakini naona response ya watu wala hawaamki na kumsifu kwa lolote. Ukiona watu wa jamii forums wamemnyanyua mtu ujue anafanya kazi, nadhani January watu hawajamjua maana anaonekana kama msanii ndo maana watu wengi wanabaki kimya.
 
...huyu January alitaka sana uwaziri na akaukosa, naona watu waliokuwa wanataka kumtumia wamemuweka kwenye ile kamati nyeti na amekuwa akiongelea hoja moja tu kama umegundua...yeye na dowans tuuu, tunajua ni dalali na anatumiwa tu na anaostahili kuwalipa fadhila kwa kumfikisha pale...ni muda tu tatabaini ukweli wake....na tutajua janja yake....

Kwani haswa wewe shida yako ni nini? watanzania wamechoka na siasa wanataka umeme na hata kama ungekuwa unatika kwa shetani hatujali, we just need the power only usiwe mjinga
 
January ana baraka zote za JK na ikumbukwe kwamba alikuwa msaidizi wake wa karibu/mwandishi na ni mtoto wa rafiki yake wa karibu Makamba!

Ngeleja naye ni mtu wa karibu wa RA kwani alikuwa mwanasheria Vodacom ambayo yeye ni mmoja wa wamiliki wake! Na kwamba akiwa waziri anasimamia au kulinda pia miradi ya nishati na madini inayomilikiwa na RA!
 
Kwa ujumla hakuna kipya ninachokiona kwa Januari Makamba zaidi ya yeye kutaka kujinufaisha kwa kutanguliza maslahi yake kwa gharama za watanzania walalahoi. Chimbuko la Dowans ni nini kama si RichMond iliyoingizwa kwa kisingizio cha dharura ya tatizo la umeme ambapo kauli za kutotoa katika tatizo hilo ziliwafunika macho wananchi na kuwasadikisha kuwa kila kitu kilikuwa safi lakini kumbe nyuma yake ni uozo mtupu ambao tangu mwaka 2006 mpaka leo hatujaupatia ufumbuzi. nakubalina uvumi kwamba inawezekana J. Makamba katumwa kuiwakilisha Dowans kwa stahili hiyo ya kutanguliza maslahi ya umma mdomoni lakini ktk utendaji na moyoni wanatanguliza maslahi yao.
Kama Ngeleja akitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na J.Makamba yatakuwa yale yale ya wengi wanaojitanguliza lakini wakipewa nafasi wanatusahau. Namkumbuka Njelu Kasaka na kundi lake la G 55, hoja za kundi hili zote zilifunikwa baada ya kina njelu kuuvaa uwaziri, Je Januari atakuwa tofauti na wao?
Dr. Martin Luther King (Jr) katika hotuna yake ya mwaka 1960 alisema ''The most important human endeavour is the striving for morality in our actions. Our balance and even our existence depend on it. Only morality in our actions can give beauty and dignity to life''
In short I don't see what King said to our leaders.
 
Jamaan anapiga kazi....na akiweza kuchangia kusaidia kumaliza hili tatizo la umeme, nitamweka kwenye level moja na kina Mnyika.
 
Wote wanariporti kwa RA sasa iweje mmoja awe tishio kwa mwingine? ili kuwapiga changa la macho lazima mmoja aonekane apo upande wa raia (mpiganaji) ambaye ni January, sasa nyie watanzania wavivu wa kuchambua mambo kazi kwenu.

Nawaachia nyie, mimi nimeshaamua narudi kwetu kijijini, kule hatuna haja ya umeme wa longo longo kila kukicha. yaani ina maana Umeme kuwaka Tanzania lazima uwashirikishe Dowans?
 
Jamaan anapiga kazi....na akiweza kuchangia kusaidia kumaliza hili tatizo la umeme, nitamweka kwenye level moja na kina Mnyika.

in your dreams - like father like son, kaharibu CCM na mshauri wake mkuu ni mwanae huyu huyu unategemea nini?
 
January ana baraka zote za JK na ikumbukwe kwamba alikuwa msaidizi wake wa karibu/mwandishi na ni mtoto wa rafiki yake wa karibu Makamba!

Ngeleja naye ni mtu wa karibu wa RA kwani alikuwa mwanasheria Vodacom ambayo yeye ni mmoja wa wamiliki wake! Na kwamba akiwa waziri anasimamia au kulinda pia miradi ya nishati na madini inayomilikiwa na RA!
Kwa hiyo kwa hoja yako JK na RA lao moja maana vijana wao (Ngeleja na Makamba) wanafanya yale wakubwa wamewaagiza?
 
January Makamba na Ngeleja wote ni wapambe wa Rostam.
Wameagizwa kuhakikisha mitambo ya Dowans inawashwa ili kampuni hiyo ya kitapeli ya Rostam + EL + JK ichote tu pesa za watanzania.

HATUTAKI!
 
Hivi msemaji wa TANESCO ni January Makamba?

Naona na yeye analeta siasa tu
 
Back
Top Bottom