Kiini macho cha Kamati ya January Makamba na Dowans

Kiini macho cha Kamati ya January Makamba na Dowans

Kusema kweli hii ya Dowans ni kama sinema, kwasababu mambo yanabadilika na hayatabiriki.

Ebu tujikumbushe kidogo matukio juu ya Dowans:
  • Dowans anaingia kwa mkwara na kuchukua nafasi ya Richmond
  • Kamati ya Mwakwembe inashauri mkataba wao uvunjwe kwasababu ni batili
  • Tanesco anavunja makataba
  • Dowans anakimbilia mahakama ya usuluhishi na kushinda kesi
  • Wananchi wanahoji nani mmiliki wa Dowans, Ngeleja anawataja wamiliki
  • Baadaye Rais anasema yeye hawajui wamiliki
  • Wabunge wa ccm wanasema wataongea nao deni lipungue
  • January Makamba anaandika barua kwa Waziri
  • January anapendekeza mitambo iwashwe kwa mkataba wa dhalura
  • Brugedia Gen. anajitokeza na kusema mmiliki lakini asipigwe picha
  • Kesho yake mitambo inawashwa kidogo
  • January Makamba anakuwa msemaji wa Dowans, Tanesco, Wizara na Kamati ya Bunge
  • Dowans anaanza kumnyemelea Tanesco na kumwambia atamfutia deni lake!
  • ........
  • .........
  • Ongeza mengine...!
Jamani Tanzania hii, kila kitu kinawezekana!

Maoni yangu:

Kikwete asipokuwa makini awamu zake za utawala zitakuwa defined na hii kitu inayoitwa Richmond/Dowans

Hii filamu ya Dowans ni kali sana. Imefunika zote, hadi ile filamu ya Gongolamboto imefunikwa na kumuacha Hussein Mwinyi anakula kuku tu no presha tena.
 
movie mpya inaanza, hii tuiite Dowans Pt. 2 (Relodaded) get ur popcorns ready!
 
Wapendwa imenilazimu sana kuuliza hili swali kwa mh huyu aliekuwa mwandishi wa rais kwa miaka kadhaa..jana ulisikia mh mmoja wa DOWANS akisema wamesamehe serikali na tanesco deni lao walilokuwa wakidai,..pasipo kuwa na adabu wala heshima mshenzi huyualidiriki kusema wameona hivyo kusikia VILIO vya watanzania ,,,hana adabu kabisa mshenzi mkubwa enzi za mwalimu angekuwa seregerea we unaitisha waandishi wa habari na kutukana serikali kama kampuni ya babako....

Nimewiwa kuuliza hivi maana huyu bwana akiwa bungen alitueleza anaitaj mkataba wa dowans usaniwe fasta fasta usizidi miezi 6...nimejiuliza kama serikali imekaa na miaka kadhaa hili wimbi la dowans...wakaambiwa mitambo mipya ni doller 200million mkakimbilia kuchukua chakavu kwa us million 540 amwoni ni upuuzi..huyu makamba anatuambia baada ya miezi sita wana njiagani mbadala ya kusitisha tatizo la umeme..ama ana kadili chake na Dowans

Kingine nimejiuliza mara mbili mbili huyu aliekuwa akingangania DOWANS DOWANS jana waandishi wamemuuliza mh MAKAMBA JANUARY uansemaje kuhusu huu msamaha..akadai hilo swala la TANESCO..NAJIULIZA ni kichwa kile kile kilichokuwa kikingania tusaini mkataba wa miezi mitatu mitatu wa DOWANS??iweje leohii aseme msamaha wa DOWANS aiwahusu..na ule mkataba aliokuwa akingangania nao hamuhusu??

PENYE NIA PANA NJIA MENGI TUTAYAONA MWAKA HUU
 
Nadhani Bwana January anatafuta umaarufu mapema ..... anzie bumbuli then tutamwona sio hapo alipo
 
Kijana nahisi amekalishwa kiti si chake kabisa kabisa Mungu amsaidie sana maana yuko kwenye dimwbwi la wauwaji na walanguzi wa NCHI
 
Pasco, hivi balozi wa tanzania nchini Marekani ni nani?

Tafadhali nikumbushe, Ni Mwanaidi Sinare Majaar au Dr. Eve Hawa Sinare?

Nimeona hay majina kwenye hiy headed paper nidhani labda nachanganya.
 
Wait a minute!

Hivi wakati wa EPA si tuliambiwa kwamba hayo mapesa ya EPA yalipangwa awali yapitie Stanbic Bank na walipochomoa yakaenda kupitishwa Barclays Bank? Na hii barua ya Rexattorneys inatuambia kwamba Richimondi waliposhindwa kuthibitisha uhalali wao, mchakato wa mkopo Stanbic Bank ulisitishwa na kuhamishiwa Barclays ambayo ilitoa mkopo?

Je, kuna sababu ya kuchunguza na kuichukulia hatua za kisheria Barkleys Bank kwa kurutubisha ufisadi hapa nchini?
 
Huyu January mtoto wa Makamba hana lolote, anamtumikia Rostam Aziz na Dowans yake. Anapiga debe ili watuibie pesa nyingi zaidi kuliko hata hizo za faini ya bilioni 94.

Dowans ililipwa sh 152 milioni kwa siku kama 'Capacity charge', (kwa mwezi sh bilioni 4.5) bado bei ya kununua umeme. Wakiuza umeme inaenda hadi kati ya sh bilioni 8 na 10. Kwa mwaka mmoja tu wanaweza kutuibia hadi sh bilioni 100.
Tayari inaizidi hata hiyo faini.

Wakisaini mkataba wa miaka labda mitano?
 
Mkuu Pdidy, hivi unaweza kuuliza majini kwa sheikh Yahya? Like father like son
 
Pasco, hivi balozi wa tanzania nchini Marekani ni nani?

Tafadhali nikumbushe, Ni Mwanaidi Sinare Majaar au Dr. Eve Hawa Sinare?

Nimeona hay majina kwenye hiy headed paper nidhani labda nachanganya.
MsandoAlberto, Balozi ni Mwanaidi Sinare Majaar, hawa sisters wote ni lawyers na ni vichwa vya ukweli.
Huko nyuma walikuwa na Law firm yao ikiitwa Epitome. Wakati Mwanaidi ni Balozi, dada mtu, yaani Dr. Hawa Senare ni part time mhadhiri wa UDSM, akifundisha Investment Law, na kwenye somo lake hilo, anafundisha vizuri sana huku akigharimia zile hand outs kwa fedha zake za mfukoni na kuzigawa bure darasa zima!. Somo lake ukipata C wewe ni kilaza kweli kweli, ni A, B+ na B tuu ndio zilitawala.
 
MsandoAlberto, Balozi ni Mwanaidi Sinare Majaar, hawa sisters wote ni lawyers na ni vichwa vya ukweli.
Huko nyuma walikuwa na Law firm yao ikiitwa Epitome. Wakati Mwanaidi ni Balozi, dada mtu, yaani Dr. Hawa Senare ni part time mhadhiri wa UDSM, akifundisha Investment Law, na kwenye somo lake hilo, anafundisha vizuri sana huku akigharimia zile hand outs kwa fedha zake za mfukoni na kuzigawa bure darasa zima!. Somo lake ukipata C wewe ni kilaza kweli kweli, ni A, B+ na B tuu ndio zilitawala.[/QUOTE]

Hapo penye red inaelekea ana huruma sana huyu!
 
issue ya dowans nikimpatia desel washington awe kama el na amir khan awe kama ra alafu tukaipeleka holly wood ... Hakyanani tutatengeneza hela balaaaaaa

wabongo wetu pamoja na kutojua kucheza muvi,wakicheza hii wataonekana mahodari wa sinema....wajanja waanze kuitengeneza....si itakuwa na parts km 20 na zaidi hivi!
 
atunzi wa hii tamthilia ya Dowans sijui wakoje..... yaani kama wamturudisha nyuma vile

hii itakuwa kama ile ya days of our lives isidingo..... haiishi hii kitu....
 
duuuuuuuuuuuuhhhhhhhhhh. sallu umepatia ndugu yangu. ana akili kama za babaake.
 
Huyu kijana wamemuonea kumpa hiyo kamati, watamburuza mpaka aone rangi zote, mafisadi wanataka mchezo!!!!
 
Wapendwa imenilazimu sana kuuliza hili swali kwa mh huyu aliekuwa mwandishi wa rais kwa miaka kadhaa..jana ulisikia mh mmoja wa DOWANS akisema wamesamehe serikali na tanesco deni lao walilokuwa wakidai, kuwa na adabu wala heshima mshenzi huyualidiriki kusema wameona hivyo kusikia VILIO vya watanzania..,,, hana adabu kabisa mshenzi mkubwa enzi za mwalimu angekuwa seregerea we unaitisha waandishi wa habari na kutukana serikali kama kampuni ya babako....

Nimewiwa kuuliza hivi maana huyu bwana akiwa bungen alitueleza anaitaj mkataba wa dowans usaniwe fasta fasta usizidi miezi 6...nimejiuliza kama serikali imekaa na miaka kadhaa hili wimbi la dowans...wakaambiwa mitambo mipya ni doller 200million mkakimbilia kuchukua chakavu kwa us million 540 amwoni ni upuuzi..huyu makamba anatuambia baada ya miezi sita wana njiagani mbadala ya kusitisha tatizo la umeme..ama ana kadili chake na Dowans

Kingine nimejiuliza mara mbili mbili huyu aliekuwa akingangania DOWANS DOWANS jana waandishi wamemuuliza mh MAKAMBA JANUARY uansemaje kuhusu huu msamaha..akadai hilo swala la TANESCO..NAJIULIZA ni kichwa kile kile kilichokuwa kikingania tusaini mkataba wa miezi mitatu mitatu wa DOWANS??iweje leohii aseme msamaha wa DOWANS aiwahusu..na ule mkataba aliokuwa akingangania nao hamuhusu??

PENYE NIA PANA NJIA MENGI TUTAYAONA MWAKA HUU

Punguza jazba Pdidy. Sina sababu ya kutokuamini kuwa Mh. Makamba ana akili nzuri tu. Ungeweza kuuliza maswali yako ya msingi kwa kuangalia issues kwenye suala husika bila kumshambulia mtu. Kwani kwa kufanya hivyo unaifanya hoja yako ionekane kuwa na character assassination plot.

Mfano hapo nilipo bold nimeshindwa kuelewa huyo mtu unaye mvurumishia matusi ya rejareja ni Mh. Makamba au Ni mwakilishi wa Dowans Tanzania?
 
Hapa wanaongelea Dowans Tz limited, mara tunaambiwaga Dowans Costa rica, mara Dowans Al-Adawi, mara sijui nini... waaaai, mi nimeshachoka.
 
Huyu aliwekwa na mafisadi kwa kazi maalum, hata kuupata ubunge waliomfadhili ni akina RA, YM(QG), na mafisadi papa wengine, walimpa fedha ya kuwanunua wagombea toka vyama vya upinzani na hivyo kupita bila kupingwa. Huyu ni product ya mafisadi na yuko hapo kuwatumikia.
 
Back
Top Bottom