Kihoja: bibi mchawi akamatwa machame(mfumoni)

MR. DRY

JF-Expert Member
Oct 5, 2011
637
122
Kihoja hiki kimejiri muda wa saa 7 mchana pale bibi akiwa angania alipodondoka chini maeneo ya mfumoni(wenyeji mnapajua).
Bibi huyo aliambatana na mtoto mmoja wa kike kwa wenyeji wanasema alishafariki miaka 3 iliyopita.
Raia na mwenyekiti wa kijiji walipokuwa wakimuhoji alikuwa akitoa majibu yaliyoacha watu midomo wazi:
Anasema anawatu zaidi ya arobaini alionao kimazingira!
Yeye ndo alisababisha ajali ya fuso la nyanya na coaster pale maeneo ya kibosho road.
Amesema kipindi anaishi maeneo ya narumu kuna shule alikuwa akiwaingia wanafunzi na kuanguka.

Baada ya hapo ndo watu wakasema lazima wammalize na yeye, polisi kuingilia kati na kutawanya watu kwa mabomu ya machozi na kumpeleka bibi kituo cha polisi boma ngombe na baadhi ya raia kushikiliwa.
Nawasilisha.
 
polisi wanaishi kwa ajili ya hivyo vibibi usione wengi wanawalinda wako kazini wanaona maisha yao hatarini wakiwaondoa
 
Mtu kama huyo hapaswi kuuwawa. Ana hazina ambayo tukiitumia tutafika mbali. Hebu polisi mpeni chakula kwanza ashibe then mjaribu kumuhoji taratibu.
 
Aaaah, sasa wewe unapoamka kuelekea katika shughuli zako lazima ujue pia na wengine wana shughuli zao, kuna vibaka, machangu, wanahabari na pia wachawi kama hao, log off
 
watake radhi tutaanza kutoa picha zenu za shynyanga na mwanza mpoaka mnaanza kuua babu na bibi zenu sasa ama nianze sema ndio
 
yaani hata yeye kapata ajali!!??..hizi ajali zimezidi.au alikiuka masharti?basi kama vipi wamuambie awarudishe.mia
 
Yaani kama watu hatutamrudia Bwana Yesu tutateswa sana. Kuna Nesi mmoja nae katika jiji la Lusaka kakiri mwenyewe baada ya kubabwa kuwa ni miongoni mwa kundi la wachawi. Na idara yake anayofanyia kazi za kichawi ni katika kupoteza watoto wachanga pindi wanapozaliwa. Sasa fikiria kina mama wazito wanamwamini nesi kuwazalisha huku akiwa ni mkuu wa wachawi matokeo yake ni nini?
.
 
i cant believe this comes from machame, uchawi mkali namna iyo!
Dah... Mungu tuhurumie.

Mkuu. Machame siku hizi ni zaidi ya Sumbawanga,
mwanzoni mwa mwaka huu kuna mama mmoja tena ambaye ni mkwe wa rafiki yangu alikamatwa na fuvu la binadamu ndani ya nyumba yake huko maeneo ya Kisereni.. Pia mwaka jana kuna matukio kama haya mengi tu ya liripotiwa..
 
Huyo bibi asiuawe, kwani tuna muhitaji sana aje kwenye jukwaa letu la Sayansi na Teknolojia..tuna maswali mengi ya msingi ya kumuuliza ili tuweze kushirikiana nae katika kuboresha teknolojia ya usafiri huo wa anga.
Hii itaisaidia Serikali yetu ambayo haina uwezo wa kununua ndege mpya, pia itaipunguzia gharama za uendeshaji wa usafiri wa anga.
 
... TATIZO... Hatutasikia tena nini kiliendelea na final conclusion is always elusive..!
 
Huyo bibi asiuawe, kwani tuna muhitaji sana aje kwenye jukwaa letu la Sayansi na Teknolojia..tuna maswali mengi ya msingi ya kumuuliza ili tuweze kushirikiana nae katika kuboresha teknolojia ya usafiri huo wa anga.
Hii itaisaidia Serikali yetu ambayo haina uwezo wa kununua ndege mpya, pia itaipunguzia gharama za uendeshaji wa usafiri wa anga.

Mkuu huweze kuimprove chochote kwenye ile technologia yao ... Kwani ..Ukichukua teknolojia ya sanyansi ukajumlisha ..UBINAFSI, ROHO MBAYA, CHUKI KALI, KINYONGO, KIJICHO NA HISIA HASI ZOOOTE ...UNAPTA UCHAWI!

Nikiwa na maana kuwa ukichukua maarifa ywanayotumia hawa wachawi ... na... kuondoa..UBINAFSI, ROHO MABAYA, UCHUNGU MOYONI, VINYONGO NA HISIA HASI ZOTE ...UNAPATA SAYANSI NA TECHNOLOGIA!

Kinachotakiwa kujifunza hapa ni kuwa ... Hisia hasi ... zinauwezo wa kujenga uchawi na giza kwenye jamii.

NA

Pasipo na hisia hasi za chuki, hasira, kinyongo, kijicho, nk ... pana ..UPENDO.. ulio mwanga wa kweli wa kustawisha jamii!

Hata hivo ndio maana msemaji mmoja kasema habari ya turejee kwa YESU ...AMABYE SOMO LAKE KUU NI UPENDO Kama nuru ya Ulimwengu!!

MWITO: Tujielimishe ukweli kuhusu hisia hasi!!
 
ni imani tu za kishirikina.. huyo bibi she might be a psychic patient apelekwe hospitali ya vichaa
 
Jamani nashangazwa sana na hili suala. Mbona ni mara chache sana kusikia vibabu vikikamatwa kwa kupaa, haswa ukizingatia kwamba vigagu wengi ni sisi wakinababa? Kila nikiangalia list ya wachawi waliochomwa moto kule kanda ya Magharibi, 90% ni wakina mama na vibibi, inakuwaje?
 
Back
Top Bottom