Kigugumizi cha Membe katika vita dhidi ya ufisadi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigugumizi cha Membe katika vita dhidi ya ufisadi...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Dec 3, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  Ilipokuwa kupigania matunda ya ufisadi wa rada kurudishwa nyumbani......................bw. membe alikuwa mstari wa mbele na alifikia hadi kudai ya kuwa kukataa kwa serikali ya uingereza ilikuwa inafanya ukoloni mambo leo.......................lakini inapokuwa dhuluma ya uongozi uliopo dhidi ya raia wanyonge wa hili taifa kupitia kashfa za meremeta, rada, epa, kujivua gamba ndani ya chama chake cha ccm...................................n.k..................................membe huwa kimya au hupatwa na kigugumizi kizito kukemea maovu ndani ya jamii yetu.................kweli kimya kingi kina mshindo mkuu.................

  hela ya epa iliyorudishwa wajanja tayari wameitafuna........................lakini hutamsikia membe akiongea lolote hapo..........hapo hana macho ya kuona lolote......hela ya rada iliyorudishwa tayari ipo kwenye mahesabu ya kutafunwa kwa mara ya pili...................................membe huko hayupo hutamsikia........................yeye kazi yake ni kupandisha sauti na huku udenda ukimdondoka kwa kutetea na kupigania kuwanyamazisha mabalozi waliopo nchini wasikemee maovu ndani ya jamii yetu akidai kwa kufanya hivyo ni kuinglia uhuru wetu.............................

  lakni inapokuja kutembeza bakuli yupo mstari wa mbele kurudi kwa hao hao wakoloni mamboleo kudai kibaba cha unga..................hawa ndiyo bora viongozi badala ya viongozi bora.............................na hivi sasa wanajipanga kutwaa dola............

  huko tuelekeako kutakuwa kubaya maradufu kulikoni tulipo hadi hapo tutakapoanza kutafakari aina ya ubora wa viongozi tulionao................................................
   
 2. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  ni mswahili mwingine anayetaka nafasi ya urais'unafikiri kwa nini amebadilisha dini uzeeni?
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,600
  Likes Received: 82,160
  Trophy Points: 280

  Ahsante sana Mkuu Ruta...wote wanaotajwatajwa kwamba ndio watakuwa wagombea wa magamba 2015 wako kimya kabisa kwenye issue ya ufisadi halafu ndio wanataka kuiongoza nchi!!! Utawezaje kuiongoza nchi wakati ulishindwa kusimama hadharani kutetea maslahi ya nchi pale nchi ilipokuwa inaporwa usiku na mchana? Halafu ukishaingia Ikulu ndio utaweza kutetea maslahi ya nchi? Wote hawa ni wasanii tu wanataka kujinufaisha tu.
   
 4. M

  Mabewa Senior Member

  #4
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 30, 2011
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu mm nipo upande wake ila amenitisha kwa ukimya wake japo najua anapigana chini ya daraja mana namjua yule komandoo ila tupe full details amebadilisha dini gani?kutoka dini gani?na lini...weka vitu mkuu.
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa Mhe Membe na ufisadi si rahisi sana kutenganisha maana hata siku moja hajawahi kukemea janga hili la taifa hadharani wala kuonyesha juhudi zozote za dhati kuutokomesha kabisa nchini.
   
 6. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  inasikitisha sana,mbona hajajibu watuhumiwa wa rada serikali itawafanyaje?ila kudai pesa anakua na kihere here.
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Dec 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Membe hana usafi wowote, watu wanasubiri atangaze waziwazi nia yake ya kugombea urais ndio wafungue kabati!
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  HE ALIBADILISHA DINI???
  naipata kwako!
   
 9. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Alibadilisha dini ili akidhi vigezo vya JK ili aachiwe kiti!!
   
 10. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kama waziri wa Mambo ya nje lazima anafuatilia siasa za marekani na jinsi Herman Cain wa Republican party anavyoumbuliwa madudu yake yanayomfanya asistahili kuwa mgombea wa urais; kwetu hapa ufuska sio dili lakini kwa madudu ya Membe yatakayofumuka akitangaza nia ya kutaka kugombea hiyo itakuwa Tsunami!! Salama yake akae kimya atulie ama sivyo madudu yake aliyokuwa anafanya na rafiki yake muethiopia mfanyabiashara aliyekuwa anaishi Mbezi beach yatafumuka, na hii ni tip of the ice-berg!
   
 11. Alwatan

  Alwatan JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kwani Lowassa nayeye amewahi kukemea ufisadi gani mkubwa zaidi ya kutisha watumishi wa halmashauri???...

  Wote hawafai.

  Masfisadi kweli noma, mmeamua kumtungia amebadili dini uzeeni? Hebu tuambieni kivipi mseminary yule mpaka abadili dini,
  mafisadi wakishika nchi hii ndiyo tutajua walivyotayari kufanya lolote kulazimisha wanalolitaka wao liwe.
   
 12. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #12
  Dec 3, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Du! Ndo maana sijamwona kanisani tokea pasaka, alikuwa akisali St. Joseph! akina Aloycius Mujulizi ni wengi kumbe..
   
 13. S

  Sheba JF-Expert Member

  #13
  Dec 3, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 210
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Napenda kutofautiana na mtoa hoja. Umeshindwa kutofautisha mambo mawili, WAJIBU na MAMLAKA. Siamini kuwa Waziri Membe ana nguvu na sifa ya kimungu ambayo mtoa mada anataka kumpa. Kwamba Membe anaweza kushitaki, kufunga na hata kuumba na kuhitimisha kila jambo. Membe ni Waziri wa Mambo ya Nje, Mjumbe wa NEC na Mbunge wa Mtama tu. Hana mamlaka ya kushitaki, kuteua wala kufukuza.

  Membe ni mmoja kati ya Mawaziri 13 waliowahi kuwa Mawaziri wa Mambo ya Nje toka tupate uhuru. Hakuna Waziri hata mmoja huko nyuma ambaye amewahi kuwa na mamlaka ya kushitaki, kufukuza wala kuteua. Hivyo, Waziri Membe si Waziri Mraba ni Waziri kama Waziri mwingine.

  Waziri Membe kama kiongozi anao WAJIBU wa kukemea maovu katika jamii ikiwemo ubadhirifu na ufisadi. Membe kwa bahati mbaya MAMLAKA aliyonayo inamdhibiti kushughulikia maovu na ubadhirifu ndani ya Wzara aliyokabidhiwa pekee, na MAMLAKA hiyo imeainishwa katika 'Instruments' alizokabidhiwa alipoapa.

  Kwa upande wa WAJIBU, Membe ndiye Waziri pekee katika Serikali ya Awamu ya Nne ambaye amethubutu kusema wazi kuwa wapo Watuhumiwa wa Rada nchini na wanapaswa kufikishwa mbele ya Sheria. Alilisema hili wakati akiwasilisha hotuba yake ya Bajeti mwaka huu( Rejea Hansard). Mawaziri wengine wote wamekuwa wakikwepa kulitamka hilo na wamekuwa wakidai kupatiwa ushahidi. Membe ametekeleza WAJIBU wake mkubwa zaidi wa kutetea maslahi ya taifa kwa kuvalia njuga fedha za Radar hadi Serkali ya Uingereza na BAE wakasalimu amri. Aidha, katika hili ameshirikisha hadi Bunge.

  Sasa Membe amekamilisha WAJIBU wake na ametumia vyema MAMLAKA yake kama Waziri wa Mambo ya Nje kusimama kidete na kuongoza mapambano hadi fedha zmepatikana. Hata kama angependa kwenda mbele zaidi kuwashitaki watuhumiwa, MAMLAKA yake haimruhusu. Hata pale palipokuwa na Kesi ya Mahalu ambayo ilianzia katika Ubalozi wa Tanzania Rome, MAMLAKA iliyoshitaki ilikuwa ni PCCP,DPP na Mwanasheria Mkuu.

  Nahitimisha hoja yangu kuwa Membe hana mamlaka ya Kimungu. Amekamilisha vyema WAJIBU wake na ndani ya MAMLAKA yake. Hata angekuwa na mabaya kiasi gani, anapaswa kupongezwa kwa hili. Swala la RADAR linapaswa kuulizwa kwa wenye MAMLAKA ya kuchukua hatua kuanzia pale alipomalizia Membe.
   
 14. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #14
  Dec 3, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,993
  Likes Received: 1,000
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni sisi wapiga kura hatupendi watu wanaokemea ufisadi...Dkt Slaa si alikemea sana ufisadi kabla ya uchaguzi 2010!!
   
 15. S

  Sheba JF-Expert Member

  #15
  Dec 3, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 210
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ha kumbe kabadili dini anasali mskiti gani?.
   
 16. sam2000

  sam2000 JF-Expert Member

  #16
  Dec 3, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  When you see a man changing his religion due to some influence from another person, that person is not fit to be leader at all!
   
 17. m

  mlagha Member

  #17
  Dec 3, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa mbona mtoa mada hataki kusema lolote kuhusu richmond au kwa mtoa mada suala hilo siyo muhimu ama linamhusu. Lamsingi nililotaka kujua hivi sasa hivi membe anasali mskiti gani? . Kuna ushahidi gani kuhusu madai kwamba membe kabadili dini.
   
 18. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #18
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  hapo ndipo kasheshe ilipo........................wagombea auraisi ndani ya ccm karibu wote wapo pale kupigania julinda wao na mlai zao walizozipata kwa njia ya uporaji hawana lolote la kulisaidia hili taifa............
   
 19. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #19
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  yeye anapigania mkate wake tu hana la ziada hapo........................mambo ya dini yawe kweli au la hayana maana kwa sababu kama yeye ni mtetezi wa dhuluma dhidi yetu dini yake haina msaada kwetu..........
   
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  nimezitaja baadhi tu na ndiyo maana nilisema n.k.................
   
Loading...