Kigoma Yazizima kumlaki Dr Slaa

Kigoma Yazizima kumlaki Dr Slaa

What about this?

Breaking news;- slaa adhalilishwa kigoma kaskazini jioni hii. Akimbia mkutano:


Wakuu,


Taarifa za uhakika kutoka kwa katibu wa JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI CHADEMA ndugu RAMA RUAHA, ni kwamba Katibu mkuu wa CHADEMA Padri SLAA leo alikuwa afanye mikutano miwili katika vijiji viwili baada ya kukimbia NGOME KUU YA ZZK ''MWANDIGA'' na kukimbilia kuweka mikutano ifanyike kijiji cha NYARUBANDA na mwingine KIDAHWE.


Taarifa kamili ni kama ifuatavyo


(i). MKUTANO WA NYARUBANDA. - Itabidi PADRI SLAA aishukuru mvua iliyowatawanyisha wananchi wenye HASIRA walioanza kumshambulia SLAA kwa mabango, maneno makali na mawe, huku vijana wake wa REDBRIGED wakionyesha kuishiwa nguvu na kuomba msaada wa POLISI.


SLAA anayejidai kichwa ngumu leo ameishukuru mvua hiyo iliyositiri AIBU YAKE YA KARNE YA KUPOPOLEWA NA MAYAI VIZA NA MAWE.


(ii). MKUTANO WA KIDAHWE - Katika Hali ile ile ya WAHA WA KIGOMA kumchukia DOKTA SLAA kwa kuwafanya wendawazimu na kuwataka washerehekee MAZISHI YA KIJANA WAO, huku SLAA ILIMBIDI AINGIE MITINI.


NDIO, SLAA AMESHINDWA KUTOKEA MKUTANONI KIDAHWE BAADA YA KUAMBIWA KUWA WANANCHI WA ENEO HILO WANA HASIRA NA CHUKI KUBWA DHIDI YAKE, VIONGOZI WA CHADEMA KIDAHWE WALIKATAA HATA KUMUWEKEA MEZA YA KUSIMAMA KUHUTUBIA, GARI LA M4C LILILOONGOZANA NA VIBARAKA WAKE LILIAMBULIA MATUSI MAKUBWA NA MAWE MFULULIZO KISHA KUPEWA TAHADHARI KUWA MLETENI SLAA AONE CHA MTEMA KUNI.


KWA KIFUPI KABISA SLAA AMEUMBUKA KWA KUSHINDWA KUHUTUBIA JIMBONI KWA ZITTO KABWE,


WENYEWE WANASEMA ''slaa hawezi kutuulia mwanetu halafu anakuja kutuimbia NGOMA za kikweo tucheze, sisi sio wapuuzi''


namuomba MOLEMO, BEN SAA NANE, TUMAINI MAKENE, WAITARA NA WENGINEO WOTE WAJE HAPA KUBISHA AMA KUTHIBITISHA TOFAUTI''
 
Mkuu Raphryder mbona kama umechanganyikiwa? naona kama jasho linakutoka na akili haimini kama dr slaa anaweza kupata nyomi hii kigoma

Mkuu @ Nemasisi, nichanganyikiwe na nini mkuu, ni huruma tu imenijia kuona babu mtu mzima anapiga stori na watoto,halafu anadhani yupo mkutanoni! Ni hili tu!
 
fanya hivi! tutawafundisha hadi lini?

attachment.php
 
Asanteni makamanda.CHADEMA kanyaga twende... mpaka kieleweke!!!
 
Mkuu @ Nemasisi, nichanganyikiwe na nini mkuu, ni huruma tu imenijia kuona babu mtu mzima anapiga stori na watoto,halafu anadhani yupo mkutanoni! Ni hili tu!
sawa mkuu nadhani macho yetu wote yameon, ila wakati wengine tumeona nyomi wengine mmeona nyomi ya watoto, safi sana
 
Mimi hapana, ila kapora mke wa mwingine.
Tatizo la PROCDM na CCM si wabunifu hata kidogo, hawana jipya zaidi ya hayo ya uzinzi kuanzia mwaka 2009 mpaka leo na lingine la ulaghai , mara saccos. watu wakiona ID zenu wanajua ndo haya mtaandika . muniajiri mimi niwafanyie kazi hiyo ya ubunifu.
 
Watu wameshawasili uwanjani hapa Community Centre mjini Kigoma kwa ajili ya ujio wa Gwiji wa Siasa Tanzania na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa.

Wengine tayari wameshaanza kuchukua nafasi zao. Ngoma inachezwa hapa kama maandalizi ya kumpokea Katibu Mkuu Dkt. Slaa.

Manji wa ngoma hii anaitwa Mapigo Saba, ambaye anajinasibu kuwa ana miaka 61, anazidi kuwahanikiza watu waendelee kujongea hapa.

Anasema vijana makini, wazee makini na akina mama makini wako CHADEMA. Watu wanamsubiri kwa hamu mgeni wao!

Updates 1.....

Kila kitu kiko sawasawa hapa, mathalani kuna jenereta la dharura kama umeme utakatika.

Red brigade wako imara karibu kila kona ya uwanja huu kuhakikisha ulinzi uko sawasawa. Kuna stori inatafutwa na kuandaliwa nje ya uwanja hapa.

Wanahabari tumeshanyaka mpango mzima unaoandaliwa maana inavyoonekana huku ndani mipango yao hawataweza kufanikisha kwa sababu ya uimara wa ulinzi wa Red Brigade na usalama wa Chadema.

Kuna waandishi wa magazeti ya...wameshaandaliwa na tayari wamepelekwa hapo nje ambapo kuna kitu kinaandaliwa.

Update 2....

Watu wametulia kbs hapa Uwanjani, wakiendelea kumsubiri kwa hamu mgeni wao. Watu wanazidi kumiminika uwanjani.

MC anaendelea kuwasisitiza wananchi wengi walioko pembeni mwa uwanja waungane na wenzao wengi pia walioko mbele ya jukwaa.

MC anaomba wimbo wa ''SLAA ANAWEZA''. Anasema huo wimbo unakubalika sana Kigoma anasema kuna siku kwenye harusi moja, Bwana Harusi aliwashangaza waalikwa alipoomba wimbo huo kwa ajili ya kutokea ukumbini.

Anasema maudhui yake ni murua na leo mtu mwenyewe yuko hapa. Waliyempigia kura za kutosha mwaka 2010 kwa sababu wanamuamini na wanaamini katika chama chao, CHADEMA.

Updates 3....

Dkt. Slaa ameingia uwanjani tayari wananchi waliokuwa pembeni na nje ya uwanja, wanakimbilia karibu na jukwaa kumuona na kumsikiliza Katibu Mkuu huku uwanja ukilipuka kwa shangwe kuu.

Kikundi cha Mapigo Saba kinaitwa kwa ajili ya kuimba wimbo maalum kwa ajili ya mgeni rasmi.

Mkiti Mwalimu Adam anachukua mic kufungua mkutano. Katibu Mkuu ameshaketi jukwaani tayari. Anazungumza mawili matatu na Mkiti wa Kanda ya Magharibi, Mohamed Mambo. Tayari mkutano umefunguliwa watu wanashangilia hapa.

Mapigo saba anasema wana nyimbo 2 kwa ajili ya Dkt. Slaa. Anasema Chadema Kigoma kuna amani.

Mratibu wa ziara, Mwita Waitara Mwikabe anachukua nafasi yake kuendesha itifaki ya mkutano. Sasa wanatambulishwa madiwani wa CHADEMA hapa.

Diwani wa Uvinza anawafurahisha watu kwa kusema CHADEMA ni mpango Mungu, tunasonga mbele, hakuna kurudi nyuma. Watu wanashangilia hapa.

Sasa anapanda Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji anatoa taarifa namna CHADEMA kupitia Halmashauri yake inasimamia shughuli ya maendeleo.

Viongozi wa chama wanaendelea kujitambulisha. Leo kuna kikao cha Baraza la Mashauriano la mkoa, hivyo kuna viongozi wengi, baada ya Katibu wa Mkoa, Msafiri Wamalwa sasa kapanda Katibu wa Kanda ya Magharibi, Christopher Nyawanji.

Anatambulisha wasaidizi wake kwenye ofc ya kanda. Sasa Waitara anatoa taarifa fupi ya ziara tangu ianze Dec 4.

Updates 4.....

Sasa baada ya Mkiti wa Kanda, amepanda Katibu Mkuu Dr Slaa ambaye anashangiliwa mpaka inakuwa shida kusikilizana. Ameanza kwa kutoa dakika moja ya kukaa kimya, kwa sababu ya misiba iliyotokea kwa viongozi wawili wa CHADEMA Mkoa.

Updates 5....

Katibu Mkuu, Dkt. Slaa, ambaye amemaliza mkutano punde, amewaacha wananchi na hamu ya kuendelea kumsikiliza wakati akishusha nondo za mahesabu ya ruzuku na mapato mengine ya chama.

Sasa anaelekea kwenye kikao cha ndani, Baraza la Mashauriano la Mkoa.

Umati umetanda kila kona pembeni ya barabara wakimshangilia Dr Slaa na kusema CHADEMA ndiyo mkombozi wa Kigoma na Tanzania.Dr Slaa naye anashusha vioo vya gari na kupunga mikono kwa furaha kama heshima kwa wana Kigoma kwa mapokezi makubwa sana waliyompatia!!

Source:Afisa Habari Mkuu CHADEMA Tumaini Makene

VIVA OPERESHENI TUJIDANGANYE..... kinachouma ni kuwa kina Mzee Slaa wanajikamatia posho ya 250,000 kwa siku za walipa kodi wa Tanzania kuendsha propaganda ya kujimaliza!
 
Back
Top Bottom