Sasa hivi ni dhahiri kwamba Zitto ni mkabila na Chama chake kinaendekeza ukanda; kulikoni Leo Zitto Na ACT yake kuwatangazia vita wabunge walioko kigoma Na kwamba ili waendelee kuwa wabunge kigoma lazima wawe ACT!
Kama ACT ni Chama cha kitaifa kwa nini kisitangaze vita majimbo yote Au hata Na mikoa mingine ambayo ACT ina nguvu!
Jihadhalini sana Na Hiki Chama kwani pamoja Na kuwa ni Chama cha kisaliti pia ni Chama cha wana Kigoma!
Hivi ndivyo mwananchi(09.04.2015) inaripoti wakati ikihojiana Na Zitto kuhusiana Na mikakati yake Na Chama chake cha ACT.
Pia, amewatangazia vita wabunge wa majimbo manane ya Mkoa wa Kigoma, akijigamba kuwa ili waweze kuibuka na ushindi katika uchaguzi huo ni lazima wakubali kujiunga na ACT kwa kuwa chama hicho kimejipanga kuyabeba majimbo yote.
Akizungumza na waandishi wa Mwananchi katika ofisi za gazeti hili, Dar es Salaam jana, Zitto alisema ACT ni chama kilichojipanga na ndiyo maana haikuwa ajabu katika mkutano wake mkuu wa hivi karibuni kuhudhuriwa na wanachama zaidi ya 400 na kufanya uzinduzi wa aina yake, huku akisisitiza kuwa chama hicho kinaungwa mkono na watu wengi.
Tuna wagombea ubunge wengi wakiwamo wabunge wa sasa ambao katika Uchaguzi Mkuu Oktoba hawatagombea kupitia vyama vyao vya sasa. Wapo ambao hawatakwenda hata katika kura za maoni za vyama vyao na wameshafanya uamuzi, alisema.
Huku akizungumza kwa kujiamini, Zitto alisema wabunge hao ndiyo sababu ya chama hicho kuwa na uwezo wa kujiendesha na kufafanua kuwa ACT kinawakaribisha wabunge na makada wote kutoka vyama vya Chadema na CCM...
Kuhusu Kigoma
Nahitaji majimbo yote ya Kigoma kuchukuliwa na ACT bila kukosa hata moja na hili hata Serukamba (Mbunge wa Kigoma Mjini-CCM) analijua. Mwanasiasa anayetaka kuwa mbunge Kigoma lazima aje ACT, alisema Zitto ambaye pia alirejea kauli yake kuwa atagombea ubunge katika jimbo jingine lakini siyo Kigoma Kaskazini.
Kauli hiyo ya Zitto inawagusa wabunge wa sasa wa majimbo ya Kigoma ambao ni; Felix Mkosamali (Muhambwe), Moses Machali (Kasulu Mjini), Agripina Buyogela (Kasulu Vijijini) na David Kafulila (Kigoma Kusini), wote wa NCCR-Mageuzi na Peter Serukamba (Kigoma Mjini, Christopher Chiza (Buyungu) na Albert Obama (Manyovu) wa CCM.