dovillenproperty
JF-Expert Member
- Nov 24, 2014
- 3,203
- 2,227
Naamini akili zako zimeliwa na kaswende ya ubongo nakushauri tafta daktari mapema.
Duh! Hatareeee
Naamini akili zako zimeliwa na kaswende ya ubongo nakushauri tafta daktari mapema.
hatuko tayari kuongozwa na mnafiki
Haya bana, endeleeni kuongozwa na Viongozi wenye kuithamini Kaskazini tu!
Katika miaka yote ya siasa mkoani Kigoma, jimbo la Zitto K limekuwa na maendeleo kupita majimbo mengine ya KG, ninatamani Ubunge ungekuwa wa mikoa Zitto akawa mbunge wa mkoa na yakafanyika yaliyofanyika jimboni kwake.
Siasa ni siasa tu, umewahi kujiuliza hela za Sabodo za visima zilienda wapi? Maana hakuna kisima hata kimoja kilichochimbwa na wala chama hakikutoa mrejesho wa matumizi ya ile fedha.
Hakuna mwanasiasa atakayekuneemesha mkuu, wanatetea matumbo yao tu.
Waombe radhi waha tafadhari lekebisha kauli yako.
Zitto ni zaidi ya waha wote
wewe una matatizo na huijui Kigoma. Hakuna lami unayoweza kujenga kuunga mkoa bila kupita Mwandiga.
Ni sawa na kusema huwezi kuunga Dar kwa lami bila kupitia mkoa wa Pwani
ujumbe wako wana kigoma wameusikia lakini kuingia chama kingine kwa kutumia utashi wako huo sio undondocha kukaa kwenye chama bila kutumia utashi wako huo ndo undondocha by the way una define vipi undondocha????
Kila mtu atawashangaa watu wa Kigoma akisikia kuwa watu wa Kigoma wamejiunga kwa wingi na chama kipya cha siasa cha ACT. Ingawa kila mtu anayo haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa katika mfumo wa vyama vingi lakini haki hiyo lazime iwe na uhalisia ndani yake. Zitto alipata umaarufu kupitia chadema chama ambacho sasa kimekuwa hadi kufikia kuwa chama kikuu cha upinzani nchini ambacho kinaogopwa sana na chama cha CCM pamoja na watu wengine ambao wanadhani kuwa kama CCM kitashindwa na maslahi yao nayo yatakuwa yako hatarini.
Chadema pamoja na Zitto ndani ya chadema na mikakati yao walikuwa wanakaribia sana kulishika makalio dume la nyati. Juhudi hizi za kulipapasa dume makalio zinadhoofishwa na akina Zitto na washirika wake kwa kuanzisha tuhuma nzito kwamba chama ambacho alijiunga nacho akiwa na umri wa miaka 16 tu eti hakina demokrasia. Hii sio kweli hizo ni juhudi mahususi za kulikwepesha dume na aibu ya kushikwa makalio yake kirahisi japo kwa kuondoa angalau hata kura 100 tu kutoka kwa wapinzani.
Wananchi wa Kigoma kujiunga na chama kinda cha ACT kwa kumfuata Zitto watakuwa wanaingia kwenye historia ya watanzania waliopinga na kuchelewesha kuondoa dhuluma nchini sawa na akina Zuberi Mtemviu enzi za TANU na Nyerere. Zitto anatumia ukabila (U-Kigoma) na uelewa mdogo wa wananchi katika kufanya biashara ya kuchelewesha kuing'oa CCM madarakani.
Hakuna mtu mwenye akili lazini ambaye ataamini kuwa Zitto amefanya yale aliyoyafanya ya kudai uongozi ndani ya chadema kwa njia za pembeni na kukipeleka chama mahakamani kwasababu ndani ya chadema hakukuwa na demokrasia ya kutosha, hii sio bahati mbaya tu, bali kuna jambo.
Kigoma kuweni macho na wanasiasa hawa wanaowarudisha nyuma juhudi zenu za kutafuta nafuu za kisiasa kwa kuanzisha vyama vipya vitakavyowachelewesha kuwafikisha nchi ya ahadi. Kataeni kuwa ma-ndondocha. Binafsi ninawasikitikia wananchi watakaonaswa na mtego wa kitoto kama huu kwa kujiunga na ACT.
Data zipo, lakini data ambayo wewe ni rahisi kuielewa na kuikumbuka ni hii hapa: Zitto amedai kuwa chadema hakuna demokrasia ya kweli, inahubiri mambo ambayo itayatekeleza itakapokamata dola ambayo yoyo yenyewe haiyatekelezi ndani ya chama, hivyo chadema itawezaje kuchukua nchi?. Kwani chadema ni nini? chadema ni mkusanyiko wa viongozi, wanachama na wapenzi wake, Zitto alikuwa mwanachama na kiongozi muhimu wa chadema ambaye alipaswa kusikika kwa viongozi, wanachama na wapenzi wote wa chadema akishauri chama kuhusu mambo yasiofaa kwa demokrasia ndani ya chama kwa kutumia vikao halali vya chadema. Badala yake Zitto amesikika pale tu alipokuwa anajiandaa kufanya mapinduzi ya uongozi kwa njia zisizo rasmi. Ndiyo maana tunasema Zitto alikosea kwa makusudi sio kwa bahati mbaya, maana "kunguru hana kibiongo ukiona kibiongo ameinama anaokota kitu na kitu hicho kinaweza kuwa kijiti, kijiwe, nyama yako, nguo yako ya ndani, au kitu kingine cha thamani, hivyo wahi kumkurupusha kabla hajaruka nacho ukapata hasara". Ndiyo maana nawapongeza chadema kumkurupusha kunguru kabla hajasababisha uharibifu mkubwa.
mkuu nilikua sijajua hivi kumbe zito kabwe ni muanzilishi wa chama cha ACT??
naomba vizibitisho,napenda kulifahamu hili