Kila mtu atawashangaa watu wa Kigoma akisikia kuwa watu wa Kigoma wamejiunga kwa wingi na chama kipya cha siasa cha ACT. Ingawa kila mtu anayo haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa katika mfumo wa vyama vingi lakini haki hiyo lazime iwe na uhalisia ndani yake. Zitto alipata umaarufu kupitia chadema chama ambacho sasa kimekuwa hadi kufikia kuwa chama kikuu cha upinzani nchini ambacho kinaogopwa sana na chama cha CCM pamoja na watu wengine ambao wanadhani kuwa kama CCM kitashindwa na maslahi yao nayo yatakuwa yako hatarini.
Chadema pamoja na Zitto ndani ya chadema na mikakati yao walikuwa wanakaribia sana kulishika makalio dume la nyati. Juhudi hizi za kulipapasa dume makalio zinadhoofishwa na akina Zitto na washirika wake kwa kuanzisha tuhuma nzito kwamba chama ambacho alijiunga nacho akiwa na umri wa miaka 16 tu eti hakina demokrasia. Hii sio kweli hizo ni juhudi mahususi za kulikwepesha dume na aibu ya kushikwa makalio yake kirahisi japo kwa kuondoa angalau hata kura 100 tu kutoka kwa wapinzani.
Wananchi wa Kigoma kujiunga na chama kinda cha ACT kwa kumfuata Zitto watakuwa wanaingia kwenye historia ya watanzania waliopinga na kuchelewesha kuondoa dhuluma nchini sawa na akina Zuberi Mtemviu enzi za TANU na Nyerere. Zitto anatumia ukabila (U-Kigoma) na uelewa mdogo wa wananchi katika kufanya biashara ya kuchelewesha kuing'oa CCM madarakani.
Hakuna mtu mwenye akili lazini ambaye ataamini kuwa Zitto amefanya yale aliyoyafanya ya kudai uongozi ndani ya chadema kwa njia za pembeni na kukipeleka chama mahakamani kwasababu ndani ya chadema hakukuwa na demokrasia ya kutosha, hii sio bahati mbaya tu, bali kuna jambo.
Kigoma kuweni macho na wanasiasa hawa wanaowarudisha nyuma juhudi zenu za kutafuta nafuu za kisiasa kwa kuanzisha vyama vipya vitakavyowachelewesha kuwafikisha nchi ya ahadi. Kataeni kuwa ma-ndondocha. Binafsi ninawasikitikia wananchi watakaonaswa na mtego wa kitoto kama huu kwa kujiunga na ACT.