Kigoma: Askari Polisi watatu wauawa kwa mishale

Kigoma: Askari Polisi watatu wauawa kwa mishale

Kosa kubwa kwa utawala huu ni zile kamati za Ulinzi na usalama za wilaya kuwa chini ya DC hazipo huru kufanya majukumu yao, wakiona mapungufu hawana uhuru wa kutuma taarifa direct makao makuu ili kuwe na utatuzi mzuri matokeo yake kila taarifa huwasilisha kwa DC na baadhi ya DC hupuuzia au kuchelewa kutoa maamuzi sahihi na baadhi hutumia kero kama fursa za kutengeneza pesa ikiwemo kuwabambikia kesi wananchi nk, ni wakati idara ya usalama wa Taifa ifanye kazi kwa Uhuru kama zamani kipindi cha Nyerere ili Uonevu, Uovu na mapungufu ya viongozi wa wilaya yawe yanaanikwa mapema.
 
Serikali huwa naishangaa sana,nchi INA mapori lukuki wanayaangalia tu,lakini wakisikia wananchi wapo sehemu flani wanaishi eti nao ndio utasikia wanapataka hapo,kwa nini wasiende sehemu zisizo na watu? Li nchi likubwa mapori makubwa na mengi why sehemu wanapoishi wakulima?

Kibaya kuliko vyote huko kijijini wataenda kukamata kijiji kizima wazee watoto, waliokuwemo, wasiokuwemo, kunbakumba itapita humo humo na lazima Uonevu utakuwa mkubwa ikiwa ni fursa kwa Polisi kutengeneza mazingira ya Rushwa, kufa kufaana, Polisi wamevunja sheria na wananchi wamejihami lakini sasa wananchi watapigwa sana na wengi watabambikiwa kesi na kufungwa. Taasisi za haki za binadamu zimulike huko kuanzia sasa.
 
Busara itumike, polisi kutumia nguvu na wananchi kutumia nguvu sio jambo zuri. Hapo ninachoona polisi wataongezeka kutoka maeneo mengine kuwakabili hao wananchi. Mkifanya hivyo mtaumiza watoto, wagonjwa, wanawake na wazee.

Mkienda mezani mutapata suluhu nzuri ya hilo jambo kuliko kumwagana damu.
 
Busara itumike, polisi kutumia nguvu na wananchi kutumia nguvu sio jambo zuri. Hapo ninachoona polisi wataongezeka kutoka maeneo mengine kuwakabili hao wananchi. Mkifanya hivyo mtaumiza watoto, wagonjwa, wanawake na wazee.

Mkienda mezani mutapata suluhu nzuri ya hilo jambo kuliko kumwagana damu.

Tayari Polisi wapo huko na taarifa zilizopo sasa ni kuwa wananchi wengi wamepigwa sana kuna kamata kamata ya hovyo hovyo inatembea pasipo kuangalia wagonjwa wala vikongwe.
 
R.I.P askari na wananchi wote waliopoteza maisha.Tatizo la askari wetu hata hivyo ni kwamba wako too mechanical, hawana weledi kabisa, hasa kwa upande wa negotiations na dispute management.Pia wengi wanatumia nafasi kama hizo kama njia ya kujipatia kipato.Katika mazingira hayo utu unawaisha kabisa!Kuna haja ya kufanya juhudi za makusudi ili kuliongezea jeshi letu weledi unaotakiwa na kubadili mtazamo wa askari wetu(mindset).
Hii ni kweli .Pia jeshi letu la polisi guqa hawasemi ukweli wanapohusishwa na mauaji ya raia.
 
Tatizo ni rushwa
Hawa wakiwakuta wafugaji maeneo yasiyo rasmi wanadai fedha Mwishowe mfugaji anahisi eneo kama vile la kwake maana amelipia
 
mkuu ukipita Tabora na baadhi ya maeneo ya kigoma utawashukuru polisi kwa hizi operation

Jamaa wanatuletea jangwa hawa.
Wana ugomvi wa kudumu na miti hawa jamaa.
hata hawajiulizi kama miti yote ingeisha majani ya malisho wangepata wapi.
 
Tayari Polisi wapo huko na taarifa zilizopo sasa ni kuwa wananchi wengi wamepigwa sana kuna kamata kamata ya hovyo hovyo inatembea pasipo kuangalia wagonjwa wala vikongwe.
Inasemekana na mabaka pia
 
Watu hawelewi hiyo sheria yenu wakiona mapori na ni Watanzania wanafanya makazi au ufugaji huko porini kinachotakiwa ni kutoa Elimu na kuwapa maeneo ambayo yatatatua kero yao mnapoenda na siraha na huku wao hawana njia ya kutatua tatizo lililopo mnatengeneza mauaji kwenu au kwao..

RIP Makamanda.
Hili tatizo la kuongeza maeneo yaliyokua ya wazi kuyafanya hifadhi wakati yapo mpakani na vijiji ndo matokea yake haya ardhi haiongezeki binaadam tunaongezeka kila kukicha vip uoungunze eneo la wazi kulifanya hifadhi hata kama ni kufuata taratibu lakini ieleweke watu wanaongezeka na Mifugo inaongezeka maana ya maeneo hayo ya wazi ni kwa ajili ya mifugo kilimo na uwindaji wawanya kwa kufuta sheria bila kuingia hifadhi..lakini biashara imewekwa mbele kuliko utu.
Poleni wafiwa
 
Hapo Kuna wasukuma na watutsi ni shida mpeta yote hadi Kijiji cha katoto Kuna tatizo sana wanaharibu mazingira kwa kukata miti ovyo na over grazing MTU ana ng'ombe elfu 50 ardhi Hana alafu uhamiaji haramu upo sana hapo kisa kulindana na rushwa iliyokidhiri
 
Polisi yawabidi kufanya kazi yao kwa weledi. Haya yamesemwa sana, yakishazoeleka kila mtu atadharauliwa sasa
 
Ukisoma huu uzi ndo unagundua namna gani policcm wanachukiwa na wananchi..

Hii ni dalili mbaya sana kwa taifa letu maana wakitokea waasi waka-exploit hii chuki ya raia dhidi ya policcm serikali itapata taabu sana!

Hekima ikitumika haya yote yatakwisha.
 
Hivi inakuaje police anatumia risasi ya moto kwa mwanachi mlipa kodi ambao ndo mshahara wake police au wanazani wanalipwa na chama
 
Watu wameanza kuacha sasa kuwa waoga mungu ibarikivtanzania maana tunakoelekea[emoji17][emoji17][emoji17]
 
Mimi ni msukuma na huwa napita sana njia hiyo Tabora_kigoma, kwa kweli uharibifu wa mazingira unaofanywa na hawa ndugu zangu ni mkubwa sana, tena sana.
Nadhani hapa Elimu inatakiwa sana, lakini pia unaweza kuta tamaa ya pesa na mali kwa baadhi ya wasimamizi wa sera na sheria serikalini nayo inaweza ikawa inasababisha matukio kama haya.
Nadhani wizara zinazohusiana na maliasili, mazingira, ardhi, kilimo, ufugaji, sheria na usalama wa mambo ya ndani wanatakiwa kuunda joint venture katika kulishughulikia hili.
Kwa maeneo ya wazi na makubwa katika nchi hii na idadi yetu Tanzania ilivyo ndogo, sisi siyo wa kupigania vieneo na kuuana kama hivi!
Hoja si wasukuma bali ni udhaifu wa usimazi wa sera na sheria za matumizi ya aridhi na rasimali zake. Udhaifu huu hausabishwi na kabila la watu bali uko “systemic” na ndani ya taasisi za serikali na watumishi wake. Makazi holela miijini kama Dar es Salaam au Mwanza milimani bi zao la mapungufu ya wizara ya ardhi na halisabishwi na wachaga, wasukuma au wandamba. Wamesukumwa na udhaifu wa Serikali na rushwa katika maamuzi ya upatikanaji, matumizi na umiliki wa aridhi. Naamini wasukuma wa Nguruka ni Watanzania ambao wanaishi katika vijiji halali na inawezekana vijiji wanamoishi vina mipango ya matumizi bora ya Ardhi lakini haisimamiwi inavyotakiwa. Tusiyape sura ya ukabila matatizo ya matumizi ya ardhi iwe vijijini au mijini tuanze kusema mbona ni wa wanyakyusa tu
 
ASKARI polisi watatu akiwamo Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Nguruka, Uvinza mkoani Kigoma, Ramadhan Mdimi, wameuawa kwa kupigwa na silaha mbalimbali za jadi ikiwamo mishale wakati wakitekeleza majukumu yao pembezoni mwa mpaka wa kijiji cha Mpeta .
Mauaji hayo yanatokana na mgogoro wa ardhi katika eneo la Ilunde na askari hao walifika kuwaondoa wananchi eneo hilo walioanzisha makazi na kufanya shughuli za kilimo na ufugaji bila kufuata sheria na taratibu za ardhi tangu mwaka 2004.

Gazeti hili lilifanya mahojiano na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mpeta, Petro Kejo, kuhusu mgogoro huo na kukiri kwamba kazi ya kuwaondoa wananchi hao imetumia nguvu kubwa.

"Sababu kubwa ni eneo kubadilishwa matumizi kutoka ardhi ya kawaida ili iwe ranchi ya uwekezaji. Sasa raia wanahisi hawatendewi haki kwa nini igeuzwe ranchi wakati wanatozwa fedha za michango ya maendeleo ya jamii na wanapiga kura kuwachagua viongozi.

“Kama shida ni mwekezaji, wako tayari walipe gharama hizo lakini waachwe waendelee na shughuli zao za kilimo na ufugaji. Hakuna eneo lililotengwa kwa ajili ya wakulima na wafugaji," alisema.

Alisema wananchi wamechukizwa na kitendo cha askari polisi kuwapora mazao kama mahindi, mchele na kuku katika kaya zao huku wakichoma moto baadhi ya nyumba wakati wa operesheni ya kuwaondoa katika eneo hilo, iliyofanyika Alhamisi wiki hii.

Alisema hali hiyo ilisababisha hasira kwa wananchi ambao walijikusanya na kuwavamia askari hao na kusababisha mauaji ya watu watano.

"Wananchi waliopigwa risasi na kufa ninaowajua ni wawili na majeruhi watano. Maiti moja iko katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa ya Maweni na aliyeuawa Salu Deusi (21). Polisi hawasemi ukweli kwa ndugu wa marehemu kama maiti iko hospitalini, wanadai hawajui. Hii inawaumiza raia kwa uongo wakati wanaishi hapo kwa zaidi ya miaka 15," alisema.

Alisema juzi ndipo waliokota maiti ya Mkuu wa Kituo cha Polisi, Ramadhan Mdimi, huku miili ya askari wenzake wawili ikiwa bado inatafutwa na vyombo vya dola.

"Operesheni hii imeathiri utulivu wa wananchi na mali zao na tunaishauri serikali ya wilaya ifanye mazungumzo na wananchi kwa kushirikiana na serikali ya kijiji na iwe imetenga maeneo rafiki ya wafugaji na wakulima kutoka mikoa ya karibu hasa wafugaji na wakulima kutoka Shinyanga," alisema Kejo.

Nipashe ilizungumza na Diwani wa Mganza, Evodius Kapukutu, kuhusu mgogoro huo na kukiri kuwa, aliyekuwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Nguruka na mwenzake wawili, walipoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yao .

"Hawa wafugaji wametoka Shinyanga na wameingia kinyemela na kila wanapoelezwa kufuata sheria za ardhi na taratibu, hawaelewi. Wao wanajua ardhi ni ya wote, mbaya zaidi hufanya mikutano yao ya siri baada ya kikao cha wazi na serikali," alisema.

Chanzo gazeti la nipashe

Kama kweli wananchi hao wamefanya kitendo hiki cha kinyama nadhani sasa hivi hawamo majumbani mwao kwa hofu...nadhani watakuwa wamekimbilia msituni kuishi kama wanyama wakihofia mkono wa dola...nasikilizia kwa makini kinachoendelea huko, huwezi kuwaua polisi na halafu ukae kwa amani.duniani kote ndivyo ilivyo, ukiua polisi inakula kwako....hata mafia huko Italia, Columbia na Marekani ni nadra kufanya kitendo cha kuua polisi.
 
Back
Top Bottom