Kigoma: Askari Polisi watatu wauawa kwa mishale

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
24,996
Reaction score
61,231
ASKARI polisi watatu akiwamo Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Nguruka, Uvinza mkoani Kigoma, Ramadhan Mdimi, wameuawa kwa kupigwa na silaha mbalimbali za jadi ikiwamo mishale wakati wakitekeleza majukumu yao pembezoni mwa mpaka wa kijiji cha Mpeta .

Mauaji hayo yanatokana na mgogoro wa ardhi katika eneo la Ilunde na askari hao walifika kuwaondoa wananchi eneo hilo walioanzisha makazi na kufanya shughuli za kilimo na ufugaji bila kufuata sheria na taratibu za ardhi tangu mwaka 2004.

Gazeti hili lilifanya mahojiano na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mpeta, Petro Kejo, kuhusu mgogoro huo na kukiri kwamba kazi ya kuwaondoa wananchi hao imetumia nguvu kubwa.

"Sababu kubwa ni eneo kubadilishwa matumizi kutoka ardhi ya kawaida ili iwe ranchi ya uwekezaji. Sasa raia wanahisi hawatendewi haki kwa nini igeuzwe ranchi wakati wanatozwa fedha za michango ya maendeleo ya jamii na wanapiga kura kuwachagua viongozi.

“Kama shida ni mwekezaji, wako tayari walipe gharama hizo lakini waachwe waendelee na shughuli zao za kilimo na ufugaji. Hakuna eneo lililotengwa kwa ajili ya wakulima na wafugaji," alisema.

Alisema wananchi wamechukizwa na kitendo cha askari polisi kuwapora mazao kama mahindi, mchele na kuku katika kaya zao huku wakichoma moto baadhi ya nyumba wakati wa operesheni ya kuwaondoa katika eneo hilo, iliyofanyika Alhamisi wiki hii.

Alisema hali hiyo ilisababisha hasira kwa wananchi ambao walijikusanya na kuwavamia askari hao na kusababisha mauaji ya watu watano.

"Wananchi waliopigwa risasi na kufa ninaowajua ni wawili na majeruhi watano. Maiti moja iko katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa ya Maweni na aliyeuawa Salu Deusi (21). Polisi hawasemi ukweli kwa ndugu wa marehemu kama maiti iko hospitalini, wanadai hawajui. Hii inawaumiza raia kwa uongo wakati wanaishi hapo kwa zaidi ya miaka 15," alisema.

Alisema juzi ndipo waliokota maiti ya Mkuu wa Kituo cha Polisi, Ramadhan Mdimi, huku miili ya askari wenzake wawili ikiwa bado inatafutwa na vyombo vya dola.

"Operesheni hii imeathiri utulivu wa wananchi na mali zao na tunaishauri serikali ya wilaya ifanye mazungumzo na wananchi kwa kushirikiana na serikali ya kijiji na iwe imetenga maeneo rafiki ya wafugaji na wakulima kutoka mikoa ya karibu hasa wafugaji na wakulima kutoka Shinyanga," alisema Kejo.

Nipashe ilizungumza na Diwani wa Mganza, Evodius Kapukutu, kuhusu mgogoro huo na kukiri kuwa, aliyekuwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Nguruka na mwenzake wawili, walipoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yao .

"Hawa wafugaji wametoka Shinyanga na wameingia kinyemela na kila wanapoelezwa kufuata sheria za ardhi na taratibu, hawaelewi. Wao wanajua ardhi ni ya wote, mbaya zaidi hufanya mikutano yao ya siri baada ya kikao cha wazi na serikali," alisema.

Chanzo: Nipashe
 
Watu hawelewi hiyo sheria yenu wakiona mapori na ni Watanzania wanafanya makazi au ufugaji huko porini kinachotakiwa ni kutoa Elimu na kuwapa maeneo ambayo yatatatua kero yao mnapoenda na siraha na huku wao hawana njia ya kutatua tatizo lililopo mnatengeneza mauaji kwenu au kwao..

RIP Makamanda.
 
R.I.P askari na wananchi wote waliopoteza maisha.

Tatizo la askari wetu hata hivyo ni kwamba wako too mechanical na hawana weledi kabisa, hasa upande wa negotiations na dispute management.Pia wengi wanatumia nafasi hizo kama njia ya kujipatia kipato.Katika mazingira hayo utu unawaisha kabisa!

Kuna haja ya kufanya juhudi za makusudi ili kuliongezea jeshi letu weledi unaotakiwa na kubadili mtazamo wa askari wetu(mindset).
 
Tunawaombea makamanda wetu pamoja na wote waliopoteza maisha wapumzike kwa amani.

Haya matatizo, ni vyema Serikali kuyachukulia kwa uzito wake. Isije fika sehemu utaratibu huu watu kutoana roho ukawa wa kawaida na tukaliingiza taifa letu kwenye machafuko makubwa.
 
Ila twende mbele turudi nyuma.

Wanasiasa na viongozi wengine wanasumbua sana, inakuwaje umuache mtu aweke makazi hapo kwa zaidi ya miaka kumi, kisha leo unakuja kumuondoa tu, kirahisi hivi.

Hatua zingine zichukuliwe mapena kabla ya kugusa hisia za watu.
 
Watu wapo hapo zaidi ya miaka kumi leo mnatunga Sera zenu uko mnakaa mmejifungia ndani peke yenu, bila washirikisha kwakua tz mshaigeuza Republic of gangster mkajua mtawaondoa bila kuwambia wanaenda wapi, mnafika unatumika ubabe unategemea nini
kitokee kama si mauaji

maana wanaichi washachoka ona sasa mauji yametokea vyombo husika mnapopewa hizi dhamana tumieni busara watu washachoka, mnapotumia nguvu mnahatarisha maisha yenu, kazi ya serikali haina urithi ukifa wewe ndio umeuwa familia yako una watoto wapo shule nk, ukifa nani atawalea ebu tumieni busara hata kama agizo kutoka juu.
 
Ila twende mbele turudi nyuma.

Wanasiasa na viongozi wengine wanasumbua sana, inakuwaje umuache mtu aweke makazi hapo kwa zaidi ya miaka kumi, kisha leo unakuja kumuondoa tu, kirahisi hivi.

Hatua zingine zichukuliwe mapena kabla ya kugusa hisia za watu.
Alafu ukizingatia mapori lukuki yamejaa wanaishi ndezi tuu
 
kwa ninavyowajua wasukuma hizi Operations ni sawa tu

viburi sana hawa jamaa na ni waharibifu wakubwa wa mazingira.
Mimi huwa napita sana njia hiyo Tabora_kigoma, kwa kweli uharibifu wa mazingira unaofanywa na hawa ndugu zangu ni mkubwa sana, tena sana.
Nadhani hapa Elimu inatakiwa sana, lakini pia unaweza kuta tamaa ya pesa na mali kwa baadhi ya wasimamizi wa sera na sheria serikalini nayo inaweza ikawa inasababisha matukio kama haya.
Nadhani wizara zinazohusiana na maliasili, mazingira, ardhi, kilimo, ufugaji, sheria na usalama wa mambo ya ndani wanatakiwa kuunda joint venture katika kulishughulikia hili.
Kwa maeneo ya wazi na makubwa katika nchi hii na idadi yetu Tanzania ilivyo ndogo, sisi siyo wa kupigania vieneo na kuuana kama hivi!
 
Halafu ikitokea umefanyiwa uhalifu na majambazi uende wapi?Au utaenda kambi za JWTZ kufungua mashtaka?Usiwachukulie askari polisi wote siyo watenda haki ndugu yangu,kuna wengine ni wema na wanafanya kazi kwa weledi.Kwa hali ilivyo kwetu raia,hata JWTZ wangepewa jukumu la polisi,tungewalaumu tu,na yawezekana tungesema wanakula rushwa zaidi ya polisi na wanaonea raia.
Mbona polisi wachache mnooo ingekuwa zaid
 
ASKARI polisi watatu akiwamo Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Nguruka, Uvinza mkoani Kigoma, Ramadhan Mdimi, wameuawa kwa kupigwa na silaha mbalimbali za jadi ikiwamo mishale wakati wakitekeleza majukumu yao pembezoni mwa mpaka wa kijiji cha Mpeta .
Mauaji hayo yanatokana na mgogoro wa ardhi katika eneo la Ilunde na askari hao walifika kuwaondoa wananchi eneo hilo walioanzisha makazi na kufanya shughuli za kilimo na ufugaji bila kufuata sheria na taratibu za ardhi tangu mwaka 2004.

Gazeti hili lilifanya mahojiano na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mpeta, Petro Kejo, kuhusu mgogoro huo na kukiri kwamba kazi ya kuwaondoa wananchi hao imetumia nguvu kubwa.

"Sababu kubwa ni eneo kubadilishwa matumizi kutoka ardhi ya kawaida ili iwe ranchi ya uwekezaji. Sasa raia wanahisi hawatendewi haki kwa nini igeuzwe ranchi wakati wanatozwa fedha za michango ya maendeleo ya jamii na wanapiga kura kuwachagua viongozi.

“Kama shida ni mwekezaji, wako tayari walipe gharama hizo lakini waachwe waendelee na shughuli zao za kilimo na ufugaji. Hakuna eneo lililotengwa kwa ajili ya wakulima na wafugaji," alisema.

Alisema wananchi wamechukizwa na kitendo cha askari polisi kuwapora mazao kama mahindi, mchele na kuku katika kaya zao huku wakichoma moto baadhi ya nyumba wakati wa operesheni ya kuwaondoa katika eneo hilo, iliyofanyika Alhamisi wiki hii.

Alisema hali hiyo ilisababisha hasira kwa wananchi ambao walijikusanya na kuwavamia askari hao na kusababisha mauaji ya watu watano.

"Wananchi waliopigwa risasi na kufa ninaowajua ni wawili na majeruhi watano. Maiti moja iko katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa ya Maweni na aliyeuawa Salu Deusi (21). Polisi hawasemi ukweli kwa ndugu wa marehemu kama maiti iko hospitalini, wanadai hawajui. Hii inawaumiza raia kwa uongo wakati wanaishi hapo kwa zaidi ya miaka 15," alisema.

Alisema juzi ndipo waliokota maiti ya Mkuu wa Kituo cha Polisi, Ramadhan Mdimi, huku miili ya askari wenzake wawili ikiwa bado inatafutwa na vyombo vya dola.

"Operesheni hii imeathiri utulivu wa wananchi na mali zao na tunaishauri serikali ya wilaya ifanye mazungumzo na wananchi kwa kushirikiana na serikali ya kijiji na iwe imetenga maeneo rafiki ya wafugaji na wakulima kutoka mikoa ya karibu hasa wafugaji na wakulima kutoka Shinyanga," alisema Kejo.

Nipashe ilizungumza na Diwani wa Mganza, Evodius Kapukutu, kuhusu mgogoro huo na kukiri kuwa, aliyekuwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Nguruka na mwenzake wawili, walipoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yao .

"Hawa wafugaji wametoka Shinyanga na wameingia kinyemela na kila wanapoelezwa kufuata sheria za ardhi na taratibu, hawaelewi. Wao wanajua ardhi ni ya wote, mbaya zaidi hufanya mikutano yao ya siri baada ya kikao cha wazi na serikali," alisema.

Chanzo gazeti la nipashe
Hii ni adhabu kwao kwa nini wanafanya kazi kienyeji hivvyo? Hata huko Tarime DC amekuwa akiwatuma OCD na Polisi kwenda kuwapiga wananchi wachimbaji wadogo wadogo masikini wanyonge kuwapora madilni na mali zao kisha kuwabambikia kesi na bado akaona haitoshi kaufunga Mgodi wote, Wananchi wapo wanajipanga kufanya fujo kubwa endapo OCD ataenda tena na Polisi wake kuwapiga, nguvu ya umma huwa hatari kwa Polisi pindi wakichoka na Uonevu.
 
Serikali huwa naishangaa sana,nchi INA mapori lukuki wanayaangalia tu,lakini wakisikia wananchi wapo sehemu flani wanaishi eti nao ndio utasikia wanapataka hapo,kwa nini wasiende sehemu zisizo na watu? Li nchi likubwa mapori makubwa na mengi why sehemu wanapoishi wakulima?
 
Back
Top Bottom