Mzee, manunuzi ya Serikali ni kupitia utaratibu wa Zabuni za Umma (Public Procurements). Wazabuni wanapowasilisha zabuni zao hujumuisha na bei ya faida. Ingekuwa ni ufisadi zaidi iwapo Srikali ingeweza kununua moja kwa moja toka kwa "dealers" nadhani unajua jinsi tusivyokuwa waadilifu kwenye fedha ya Umma!!.
Na hata katika Kuuza magari ya Serikali utartibu ungekuwa wa kutangaza kama zabuni nadhani matatizo kama haya yangepungua, lakini katika kuuza vifaa kama garai, siku zote Serikali imekuwa ikiuza kama "kifaa chakavu" na mara nyingi kuna kuwa na "collusion" kati ya afisa anayetaka kununua, mtendaji mkuu wa Idara/ Wizara husika, Watebdaji wanaohidhinisha wa Wizara ya Miundo Mbinu, Utumishi na Hazina.
Ukichunguza utaona kuwa magari mengi, mazuri na yenye thamani yamekopwa kwa bei ndogo sana na Mawaziri, Watendaji Wakuu (R.C, DC, RAS, DED, CEOs, Makatibu Wakuu na Wakurugenzi wa Idara na sio maafisa wa kawaida. Na wengi wanakopeshana hata zaidi ya mara tano mtu huyo huyo mmoja!.
mkuu,tsh 155m ni £77,500 na LAND CRUISER V8 bei inaanzia £58,110 sasa ikiwa na few extra kwa ajili ya ''waheshimiwa'' wetu si ajabu ikafika hio £77,500.
nasikitika sana serikali kutumia hela nyingi hivi kwenye gari moja wakati zahanati hazina vitanda,shule hazina madawati,wengine wanasomea chini ya mbuyu etc