Kigogo auziwa shangingi la Sh155 Milioni kwa milioni 6 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigogo auziwa shangingi la Sh155 Milioni kwa milioni 6

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdondoaji, May 15, 2010.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  KATIBU Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Hilda Gondwe anadaiwa kuomba auziwe kwa Sh6 milioni gari la serikali aina ya Toyota Landcruiser VX maarufu kama shangingi lililonunuliwa miaka mitatu iliyopita kwa Sh96 milioni.

  Taarifa za biashara hiyo zimeibua hisia kwa wakazi wa mkoa huo huku wengi wakihoji imekuaje gari hilo la serikali liuzwe kwa bei hiyo ndogo wakati bado liko kwenye hali nzuri.  Mwishoni mwa mwaka jana, gari hilo lenye namba za usajili STK 1867 lililokuwa likitumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro (RC), Monica Mbega lilikarabatiwa na kampuni ya Toyota ya jijini Dar es Salaam kwa Sh11 milioni.


  Vyanzo vya habari vimedokeza kuwa gari hilo lililonunuliwa miaka mitatu iliyopita kwa Sh96 milioni, halikustahili kuuzwa kwa bei hiyo kutokana na matengenezo makubwa lililofanyiwa Agosti mwaka jana.


  Kwa kawaida magari ya serikali huwa hayalipiwi kodi, lakini kama gari hilo lingenunuliwa kwa bei ya soko, kuingizwa nchini na kulipiwa kodi mbalimbali ikiwamo ile ya 0ngezeko la Thamani(VAT), lingekuwa na thamani ya Sh155.7 milioni.


  Shangingi lenye bei kama hiyo likiingizwa nchini linatakiwa kulipiwa Sh24 milioni kama kodi ya uagizaji (Import duty), Sh23.7 milioni kama VAT na Sh12 milioni ambazo ni kodi ya ushuru wa forodha.


  "Kila mtu ameshangaa sana kwa sababu hilo gari ni kama jipya kwa sababu mwishoni mwa mwaka jana lilifanyiwa matengenezo makubwa kwa Sh11 milioni, leo linauzwaje kwa bei ya kutupa kiasi hicho?" Kimehoji chanzo hicho.


  Gari hilo lilifanyiwa ukarabati mkubwa baada ya RC Mbega kukataa kutumia gari lililokuwa likitumiwa na mtangulizi wake, Mohamed Babu ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera.


  Alitaka lifanyiwe matengenezo na kurejea katika hali yake ya upya kabla ya kuanza kulitumia.


  Kwa sasa serikali imenunua gari jipya aina ya Toyota Landcruicer V8 VX kwa thamani ya Sh190 milioni ambalo ndilo linalotumiwa na RC Mbega ambaye pia ni Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).


  Habari zimedai kuwa tayari Katibu Tawala huyo ambaye ndiye mtendaji mkuu wa shughuli za ofisi ya RC, na ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya kabla ya kushushwa cheo na kuwa RAS, ameshalipia gari hilo.


  Vyanzo hivyo vya habari vimedai kuwa japo yapo magari mengine ya serikali likiwamo Toyota Landcruiser VX lenye namba STK 2634 ambayo yamechakaa, lakini aliliandikia STK 1867 kuwa limechakaa na halifai tena.


  Taarifa hizo zimedai kuwa zipo dalili kuwa kigogo huyo wa serikali ana mpango wa kulitumia gari hilo katika kampeni za kuusaka ubunge katika Jimbo jipya la Tunduru katika Uchaguzi Mkuu ujao utakaofanyika Oktoba mwaka huu.


  Gondwe ambaye anatarajia kustaafu serikalini Novemba mwaka huu, alitumia kikao cha Ushauri cha Mkoa (RCC) kilichofanyika juzi chini ya Uenyekiti wa RC Mbega kutangaza rasmi nia yake hiyo ya kugombea ubunge mwaka huu.


  Lakini akizungumza na gazeti hili, Gondwe alisema kwa wadhifa wake, hana mamlaka ya kujiuzia gari la serikali.


  Alisema alifuata taratibu zote katika kuomba kununua na hatimaye kupata bali cha kununua gari ambalo amesema hadi sasa hajaanza kulitumia.  "Nisema tu kwamba mimi sina mamlaka ya kujiuzia gari, nimefuata taratibu zote. Niliandika barua kwenda utumishi kuomba kununua gari, Utumishi nao wakawaandikia Miundombinu na baada ya kumaliza mchakato wao Miundombinu wakanijibu," alisema Gondwe na kuongeza:


  "Kwa kesi ya hiyo gari nimekubaliwa na nikapewa hati. Sasa ukishafikia hatua hiyo, unapaswa kwenda Hazina na kulipia kodi TRA ili upate documents origional (nyaraka halisi)


  Aliendelea kusema kuwa hadi sasa hajalichukua gari hilo kwa kuwa hajamaliza kulipa kodi TRA ambayo tayari ameanza kufuatilia hatua zake.


  "Gari lenyewe bado liko hapa, sijalichukua bado nafuatilia kukamilisha malipo TRA ," alisema.


  Mtazamo: Ndio maana wahisani hawatupi pesa zao washastuka kuwa zinaliwa na watu serikali wewe gari la milioni 155 after 3 years linauzwa sijui depreciation gani imetumika kujistify kuliwrite-off. halafu jamaa anauziwa milioni 6 jamani hii si aibu.
   
 2. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  I can guarantee you shangingi aka VX doesn't cost that much yaani hiyo ni bei mtu atakae nunua a brand new one from show room, akaituma bongo about two and half more of that price
   
 3. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  .

  Maneno makali sana haya mzee hata kama hasira, taratibu mzee..

  otherwise, huyo Mama alienunua hilo Shangingi inaonekana alikuwa akishindania na mtu ambaye hajaridhika na hivyo kuamua kuyaanika haya. Lakini kama ni kuuziana magari chee huko Serikalini ni yakawaida tu na watu wana magari zaidi ya Matano wamenunua kwa bei za nafuu zaidi ya hiyo kwa staili ya kukopeshana!!.
   
 4. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ngoja nikwabie this is just too much, kwanini hawa watu hawaji na njia nyingine zaku zuia infalation ni kwa sababu ya ushenzi kama huu. Wanachangia in a big f@cken sense, hawaelewei the cost of the taxation inazuia certain goods ku drive the market down tena quality ones.

  Hawaelewi the quality of life kutokana na nchi maskini uwezi ku-compare na ulaya. Nimekua nasoma posti nyingi sana ambazo watu wamekuwa wakitupa lawama on dollar. Apart from people who earned there wages in shillings and have to convert it into dollars ndio wanaweza lalamika.

  More than that just suck this mkullo and the rest and hire the people who understand what economics is all about. We need people who are creative and come up with innovative ways of dealing with infalation and maintaining a ceiling prices from import goods in a country that doesnt produce anything at twice the price is just creating a recipe for disaster more of that when i wake up.

  Im just tired of reading nonsense honestly, huwa najiuliza what the **** do we know si ajabu watu wana pinga vitu wasivyovijua much. Mods please bun me i cant help being here but im tired of nonsense as well.
   
 5. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,805
  Likes Received: 20,763
  Trophy Points: 280
  mkuu,tsh 155m ni £77,500 na LAND CRUISER V8 bei inaanzia £58,110 sasa ikiwa na few extra kwa ajili ya ''waheshimiwa'' wetu si ajabu ikafika hio £77,500.

  nasikitika sana serikali kutumia hela nyingi hivi kwenye gari moja wakati zahanati hazina vitanda,shule hazina madawati,wengine wanasomea chini ya mbuyu etc
   
 6. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Niambie nichungulie wapi kwa sababu hata hiyo vogue with the highest specification aifiki over £60,000 tafadhali.
   
 7. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #7
  May 15, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Huyu mama nilifanyiaga field pale wizara ya afya Dar wakati huo akiwa Katibu mkuu, alikuwa mkali kinoma.

  Lakini hebu nasi tuwe fair. Atakapolipa hizo kodi zinazotakiwa kwa ajili ya hili gari, yaani: Sh24 milioni kama kodi ya uagizaji (Import duty), Sh23.7 milioni kama VAT na Sh12 milioni ambazo ni kodi ya ushuru wa forodha, pamoja na hiyo bei aliyonunulia ya milioni 6 atakuwa amelipa jumla ya sh milioni 65.7. Kwa hiyo mwandishi naye kakurupuka. Si kweli ati gari ya milioni 155 imeuzwa milioni 6, huyu mama atailipia jumla ya milioni 65.7. Ndio maana Mzee Mkapa alikuwa anawaita waandishi wa aina hii 'mbumbumbu'.
   
 8. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #8
  May 15, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  dont you think the tax is over ambitous and limits the quality of good imported and raises the prices out of proportion as a rersult tunaishia ku-import midabwada ambayo aishi kuleta ajali.
   
 9. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #9
  May 15, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,805
  Likes Received: 20,763
  Trophy Points: 280
  toyota.co.uk bonyeza LC8
   
 10. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #10
  May 15, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,805
  Likes Received: 20,763
  Trophy Points: 280

  Price

  Back to Range Rover homepage
  Explore
  Accessories
  Photos & Videos
  On the road price - Includes Government Road Fund Licence for 12 months and Government Vehicle First Registration Fee, and cost of offsetting CO2 for the first 45,000 miles driven.


  Models List price (£) CO2 Offset (£) VAT (£) On the road price (£) TDV8 Vogue 55,719.58 140 9,775.43 66,640.00 TDV8 Vogue SE 61,200.43 140 10,734.57 73,080.00 TDV8 Autobiography 65,285.53 140 11,449.47 77,880.00 5.0 V8 Supercharged Autobiography 68,996.70 165 12,103.30 82,270.00 Prices applicable from 1st April 2010.


  hio ni landrover.com
   
 11. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #11
  May 15, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni kweli kabisa mkuu wangu, kagari mtumba unakanunua FOB dola 1,200, ukikafikisha nyumbani kwako inakuwa jumla umelipa si chini ya milioni 6, zaidi ya dola 4,000. Yaani gharama zaidi ya mara 3. Huu ni wizi wa mchana.
   
 12. mujusi

  mujusi JF-Expert Member

  #12
  May 15, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 237
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kweli sehemu zingine hali mbaya sana hebu on watu wengine wanvyotumia hizo cwrolla badala ya VX. Jamani hebu tubadilike na kuwafikiria wengine kama vile Mungu yupo kwa wachache LOO!
   

  Attached Files:

 13. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #13
  May 15, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  We kweli unakaa kijijini embu tembelea thatchers (east london) kuanzia alhamisi ulafu uone madogo wakibongo wanaendesha madudu gani kabla sijabishana na wewe upuuzi. kwa sababu najua how much they bought it and how much they cost in dealerships hiyo internet sijui inaleta bei gani za ajabu.  Mi nalala sasa hivi usiku wangu ulikuwa mrefu.
   
 14. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #14
  May 15, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,805
  Likes Received: 20,763
  Trophy Points: 280
  kweli usiku wako ulikuwa mrefu,hizo ni facts,nenda wewe mwenyewe kwa dealer kama huamini
   
 15. Ncha

  Ncha JF-Expert Member

  #15
  May 15, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hizo kodi halipi kama zilivyokuwa zilipwe, hata TRA wanaconsider depriciation, hiyo gari itachukuliwa thamani yake ya sasa ndio kodi ikadiriwe. anaweza lipa jumla kama 20m au less
   
 16. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #16
  May 15, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mtazamo: Ndio maana wahisani hawatupi pesa zao washastuka kuwa zinaliwa na watu serikali wewe gari la milioni 155 after 3 years linauzwa sijui depreciation gani imetumika kujistify kuliwrite-off. halafu jamaa anauziwa milioni 6 jamani hii si aibu.[/QUOTE]

  D = (C-S) /N

  D = depreciation
  C = original cost (pesa ya kununlia)
  S = salvage value (pesa ya kuuzia)
  N = number of years (muda gari limetumika)

  hivyo basi kwa hesabu zilizopo;
  Depreciation = (155.7m - 6m)/3yrs
  =49.9million

  hivyo kila mwaka hilo gari lilikuwa likipungua thamani yake halisi kwa kiasi cha Tshs. 49.9 million
   
 17. O

  Omumura JF-Expert Member

  #17
  May 15, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Jamani hayo madudu kama ya huyo RAS wa kilimanjaro ni mengi mno serikalini, hao jamaa hawajui shida
  walizonazo wananchi, kazi yao ni kushindana kununua magari ya kifahari, ufisadi kama huo wanaufanya
  Ma RAS wa mikoa yote kujiuzia magari ya serikali kwa bei ya kutupa.
   
 18. Shakazulu

  Shakazulu JF-Expert Member

  #18
  May 15, 2010
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 940
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kaka kwa vile upo ulaya (Reading - UK) ndio unaona wliopo Africa hawanazo? Kuwa na busara kidogo unapotoa maoni yako hapa jamvini.
   
 19. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #19
  May 15, 2010
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ...my take ni kwamba yapo magari kibao yaliyouzwa ki-aina hiyo. Ni mengi mno!!! Sasa huyu mama Gondwe hayuko peke yake. Hawa jamaa wahusika (Wizara ya Miundombinu) wangepaswa kufungua show room...teh teh teh...kuongeza uhalali ili migari hiyo iuzwe at par na bei ya sokoni. Na ile migari ya kifahari inayokuwa replaced kila kukicha pale Ikulu nayo iingie humo humo kwenye show room! teh teh teh!
   
 20. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #20
  May 15, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Naomba tukubaliane kimsingi kuwa hata milioni 20 bado ni pesa nyingi sana kwa mfanyakazi wa serikali kama huyo mama. Na Wamurubhere katutolea mahesabu ya depreciation hapo tumeyaona, kwa hiyo nasisitiza tumtendee haki huyu mama, shutuma tu bila taarifa au uchambuzi wa kitaalamu hazina tija.
   
Loading...