Kigamboni wamepata Mbunge!

Nzenzu

JF-Expert Member
Aug 10, 2011
858
164
Ni mara chache sana husimama na kuzungumza, michango yake mara nyingi huwa ktk njia ya maandishi. Jamaa ni Mbunge wa NYINYIEM a.k.a MAGAMBA akiwakilisha wakazi wa Kigamboni (jina simjui), Leo akichangia bajeti ya Waziri Mkuu JAMAA KAGOMA KUIUNGA HOJA MKONO. Dah! Hongera zake pia kwa Jirani yake ktk Sitting Plan Esther Bulaya (kwa darasa ampalo)! Jamani Wabunge wa Magamba badilikeni!
 
.....huyo mbunge ukimya wake bungeni umenifanya mpaka ni sahau jina lake.kwa kweli silikumbuki.hivi inaitwa nani vile wadau?
 
huyo huyo Dr. Faustine, yuko safi sana. Nimemsikia leo Channel 10 ktk kipindi cha BARAGUMU akizungumzia kiini macho cha Mji Mpya wa kigambon!
 
Ni Dr Faustine Ndungulile, alipokuwa South Africa alikuwa akiumia sana na mambo yanayoendelea nchini, ukimya wake Bungeni labda unatokana na kuona kuwa yanayojadiliwa hayana maslahi.
 
Anaitwa Dr Faustine Ndungulile

Amoengea kwa umakini na hisia kali, lakini nitamwamini pale atakapo shikilia msimamo wake wa kukataa badget ya pinda mpaka mwisho. Maana asije akawa anafuta mkumbo wa Kina Paul Zambi na Anna Kilango wanabwatuka maneno mengi kisha huishia kuunga mkono 100%. NAmpongeza Ndugulile kwa kufikisha ujumbe kwa PINDA lakini aendeleze msimamo wake kama kina Mpina na Filikunjombe.
 
Ndio walewale, kunguru kujimwagia majivu ili aonekane YANGEYANGE, kumbe upepo ukipita rangi yake nyeusi inabaki.

Atakuja kubadilika tu kwa kupiga kura ya NDIOOOOOOOOOOO!!!!!! siku ikifika au asipopiga kura ya NDIOOOOOO basi hatohudhuria siku hiyo bungeni eti anaonyesha msimamo kumbe ni mnafiki tu.

Kama akiwa shujaa yambidi kuhudhuria na kupiga kura ya SIYOOOOOOOOOOOO!!!!!!!

TUSUBIRI siku YA MWISHO KWANYE KURA!!!!! tutajua kama ni kifaa au ni kigae.

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Back
Top Bottom