Kigamboni New City Master Plan

We are not consistent with our view - Upande mmoja tunalalamika umaskini upande mwingine hatutaki watu kuja kuwekeza.<?xml:namespace prefix = o ns = "urn:schemas-microsoft-com:eek:ffice:eek:ffice" /><o:p></o:p>
Je tungekuwa kama hawa wenzetu Waingereza wameuza mpaka kambi ya jeshi(Chelsea Barracks) kwa kampuni ya nje(Qatari Diar)kuwekeza kwe project hii hapa chini?<o:p></o:p>

page_016_415x275.jpg
Na pia tusidanganyane kama kuna Mzawa anaweza kuwekeza kwenye project kubwa kama hiyo return yake ni ya muda mrefu.<o:p></o:p>
 
Uzuri wa mji utakusaidia nini? lazima ujenge uchumi kwa kuwashirikisha wananchi wako na si vinginevyo. matokeo yake watanzania wataishia kufagia katika hiyo mitaa unayoiona kwenye hizo picha. tunarudi kule kule tulikotoka.
Nina kubaliana na wewe lazima serikali lazima ishirikishe wananchi wake.Kwenye projects kama hizi serikali wanatoa kiwanja wanapewa percent fulani, hizo percent ndio wanaweza kuziuza kwa wananchi.Lakini kusema watanzania kushirikishwa kwenye hiyo project kwa 100pc ni ngumu kutoka na ukubwa hiyo project na kuna vipaumbele vingine.
 
Kiranga,

Nasema hivi: Je uliona wapi mji mpya unajengwa bila Masterplan? Tuanzie hapo, umeletewa Concept City unasema unataaka kuona kitu concrete, hata zege kabla ya kumwagwa kunakuwa na design stage.

Mambo mengine tuache ushabiki usio na msingi.

UDOM ilijengwa na inaendelea kujengwa na hata kama CDA walishindwa kazi Ujenzi wa UDOM na mji mpya wa Kigamboni ni ktu kizuri na ndiyo maana narudia kusema hii wanaochukizwa na hatua hii kamba ya kujinyongea ipo. hata kama itachukuwa karne moja kujenga kwa uwezo wetu wenyewe ni bora ifanyike hivyo. Nimechoshwa na kila kukicha hakuna kizuri tunachoweza kukifanya wenyewe mpaka kiwe kimefanywa na wengine.

Wengine wamediriki hata kusema ujenzi wa UDOM umeletwa kutoka nje. Kazi kweli kweli.

Experience ya miaka 30 iliyopita inanionyesha kwamba tu mahiri wa kujenga miji na maghorofa akilini, wakati ujenzi halisi hamna. Nilichosema hapo ni kwamba "seeing is believing".I am not saying this will not take off, but I am saying until I see it taking off I have no reason to believe.

Wa Nigeria na matatizo yao yote, walivyotaka kuhamisha mji mkuu kutoka Lagos kwenda Abuja wamekuja Tanzania kusoma plans zinafanywaje, tukawapa mikabrasha, wenzetu wakaenda kufanya kweli.Sisi walimu bado mpaka kesho tunaongea kuhamisha mji mkuu. Wao siku nyingi washamaliza. Hivi unataka niwe na imani na system kama hii ?

Wewe ushasema ni OK kuota huu mji mpya hata kwa miaka 100, unaonekana hukerwi na alinacha kwa miaka 100.

Clearly we can't see eye to eye, therefore we can't relate. Wala sishangai.
 
If wishes were horses even matonya could ride, plan yenyewe iko poa ila kwa uongozi huu itatekelezeka? Kazi bado tunayo!
 
Hizo ndoto tuu za Ali nacha, hii haitatokea in our generation.Pia haiwezekani sehemu iliyojistablish hivi ( kigamboni ya leo) ibadilishwe iwe kama ( hizo fotoshopu). Itaishia kwenye hiyo project ya mtu. Wakitaka kufanya hivyo waende sehemu mpya isiyokuwa na makazi
 
Mi hata sioni tatizo lolote la mabadiliko kama hayo kuja kama SHERIA NA TARATIBU zinzfuatwa. Kuna tatizo gani kama wanaomilika maeneo hayo kwa sasa watauza viwanja au maeneo yao kwa bei muafaka na kupisha uendelezaji kufanyika na wao wakahamia maeneo mengine? Uendelezaji kama huo hauanzii Tanzania, hufanyika duniani pote. Tatizo ni pale unapofanyika uporaji na unyang'anyi wa maeneo. Nadhani hilo ndilo watu wengi hapa wanahofia, hata mimi nitaungana nao kuhofu kama uporaji utafanyika. Lakini kama taratibu na sheria zitafuatwa, mi sioni tatizo.
 
Nadhani lile somo la siasa halikueleweka enzi zile tunazungumzia ubepari. Inanishangaza kuona watu wanahoji nani watafaidika na mradi huu? Wakuu Tanzania inaendeshwa kibepari and we are in it. Kwa hiyo ni hela yako tu!
 
Nadhani lile somo la siasa halikueleweka enzi zile tunazungumzia ubepari. Inanishangaza kuona watu wanahoji nani watafaidika na mradi huu? Wakuu Tanzania inaendeshwa kibepari and we are in it. Kwa hiyo ni hela yako tu!

My friend this is very possible na lazima ifanyika unadhani hawa watu wote wanaohamia Dar, biashara nk utawaaccommodate vipi kama siyo mipango kama hii. Niliuona huu mpango pia na i support it 100% ila tu serikali isije kuwa harsh kwa wananchi wake walioko huko kwa sasa. Haujui kwamba tayari project imeanza kwa sababu kama ni plot za residential si tayari zimetolewa? Kwa kutumia Public Private Partnership (PPP) inawezekana kabisa. Siyo kwamba mtu mmoja atamiliki eneo zima. Mwekezaji yeyote anaonyeshwa master plan na atajenga kwa kufuata master plan na archtectural features ambazo tayari zipo. Hapo kitakachokwamisha ni daraja tu japo nayo siyo big deal maana 148Billion au 168Billion inawezekana.
 
Jamani eeh, naomba taarifa zaidi kuhusu hili. Mpango wa mji huo unasemaje??
Mama anataka tukanunue kiwanja kule Kigamboni (Kibada, Mwasonga).. Je hii investment inafa? Isije ikatutokea puani?

nawakilisha..
 
Ni lini hii nchi itasema jambo au itakuwa na swala fulani halafu wanchi wake wakalielewa??
Nime-kuwa so confused most of the time ninaposikia issue za Kigamboni, where is the correct information? Nani wa kutoa information zinazoeleweka... na ni kwa nini hafanyi hivyo?
 
pole kaka naona unaongea kwa uchungu sana

lakini hakuna jinsi, BATCH yao ya kwanza ya CIA wa KITANZANIA ndio mwaka huu inatoka UDOM, na vijana wanapikwa kuikana nchi yao yenyewe na ndio watakuwa wakaaazi wa huo mji mpya, nia na malengo makuu ni kukama URANIUM ya Tanzania iwe mikononi mwao, wanataka kuitengeneza hii nchi kiasi kwamba hata raisi awe nani wao wanakuwa na link nzuri mno ya information

hii nchi imeshauzwa

kila nikiingia JF nikikutana na hizi news,moyo wangu unaumia sana-sana,,,
lazima nipate kiwanja pale ili nishuhudie kwa jicho langu jinsi itavokuwa,au ardhi ishauzwa CIA?
 
kigamboni tayari mna makazi,kulikoni kusimamisha watu wasijenge na izi pesa za malalamiko za fidia????
huu mradi ni mzuri ila maeneo si yako mengi sana tanzania?kwanini tuzidi kushonana dar?
kuna maeneo tena yenye rutba zuri tu ambapo huu mradi mkubwa ivi ungepelekwa kwa nia njema tu ya kuendeleza miji sehemu nyingine na pia nauliza je huu mradi kwa bajeti gani?
1.tanzania % ngapi
2.wafadhili (kina nani) % ngapi
3.na wadau wengineo % ngapi
4.kwa muda gani?
simple questions
 
kweli wewe unafukua. uko kitengo gani nji hii? ila kama ni kweli basi ni shwari maana masterplan ya kibamba nimeiona miaka 5 iliyopita
 
Dubai ilishauzwa kwa wazungu muda mwingi, nenda pale ukaone ilivyo, bombaaa...sisi tusiopenda kuuza tubakie na ardhi, tutakula mchanga. sasaivi makampuni ya magaribi yamejaa Dubai, yananunua hadi ardhi na kujenga magorofa ya ajabu, wauzile watu wa dubai kama hawafaidiki na hilo!
 
Dubai ilishauzwa kwa wazungu muda mwingi, nenda pale ukaone ilivyo, bombaaa...sisi tusiopenda kuuza tubakie na ardhi, tutakula mchanga. sasaivi makampuni ya magaribi yamejaa Dubai, yananunua hadi ardhi na kujenga magorofa ya ajabu, wauzile watu wa dubai kama hawafaidiki na hilo!

Dubai wananufaika wananchi wote..Tatizo Tanzania watanufaika wachache tu.
 
Mitanzania ndvy ilivyo! Dunia ya sasa ndy inaelekea kwny miji ya namna hiyo, angalia miji ya China inavojengwa, UAE ndy usiseme! Tanzania hatujiamini, tukiona mradi mkubwa mara zote utaskia maneno (ooh! ya mkapa, ya mama kikwete, ya richi wa monduli!) hayo maneno ya CIA na wamarekani "kujengewa" kigamboni ni ya kijiweni tu, wekeni diteli hapa nyie, mmeangalia huo mji utakuwa na uwezo wa kukaa wakazi wangapi? nplan haijaanza jana....fuatilia ardhi UPEWE data! Na ieleweke kabisa kigamboni si ya walala hoi, wewe kama ni mlala hoi usitegemee kupangishwa jengo la maana ambalo mtu amewekeza mabilioni ya dola!..wewe mlalahoi unataka upate kiwanja kule ujenge mgongo wa tembo umkatie kiwanja na mjomba wako!? acheni mawazo hasi! Kigamboni ni kwa kila mtu mwenye hela zake, kama wewe ni mlalahoi nenda shamba, au subiri utakuwa unaenda japo kutembelea shopping mall na kununua dawa ya meno. Hata marekani kwenyewe kuna sehem ambazo akipita mlala hoi anaskia baridi na anaona yuko mahali si pake! NJOONI SHAMBA TULIME!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom