Kifo cha Nelson Mandela na funzo kwa CCM sikio la Kufa

makoye2009

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,638
1,218
Mwana wa Afrika,Mwanamapinduzi,Mwanasiasa mahiri,Mpiganaji,Shujaa na kipenzi cha Dunia nzima Nelson Holhlala Madiba Mandela ametutoka duniani tarehe 5/12/2013.Ni msiba mkuu ulioisibu dunia nzima. Bila shaka kila mtu ni shahidi kuwa mazishi ya huyu mwana wa Afrika yatakuwa ni ya kihistoria na yatakumbukwa daima.


Baada ya kusema hayo basi ningependa kuwauliza ndugu zangu wa CCM na Serikali yao kama kuna kitu wamejifunza toka kwa Madiba. CCM ni chama mabacho hakitaki kujifunza lolote kutoka kwa yeyote hata kama ni malaika. Tunajua CCM walishindwa na wameshindwa kujifunza chochote kutoka kwa Mwasisi na Baba wa Taifa hili marehemu Julius Kambarage Nyerere!

Pamoja na makelele yanayopigwa kila siku na Vigogo wa CCM ya eti kumu enzi Mwalimu imekuwa ni porojo na longolongo za kisiasa tu kwenye majukwaa.Ni dhahiri kwamba CCM wameshindwa kufuata nyayo za Mwalimu na hawataweza. Baada ya Kifo cha Madiba juzi tumeanza kusikia kauli zile zile za kinafiki za Wana CCM wakijidai kumsifua Mandela na huku wakidai kuwa wataendelea kuenzi maisha aliyoishi Mandela hapa duniani!

Huu ni unafiki na uongo wa mchana kweupe. Kama CCM wameshindwa kumuenzi Baba wa Taifa wataweza kweli kumu enzi Nelson Mandela aliyekuwa Rais wa Kwanza mweusi wa Afrika Kusini? Jibu ni kwamba hawawezi asilan! Nitatoa mifano 2 tu ya matendo hai ya Nelson Mandela ambayo amewafanyia Wana Afrika Kusini ambayo ni funzo kubwa sana kwa Binadamu yeyote. Kwanza Mandela alipotoka Jela tu baada ya miaka 27 aliamua kuwasamehe Wabaya wake hao Makaburu(Boers) na kuahidi kutolipiza kisasi na ikawa hivo mpaka ameondoka duniani. Hapa Madiba alikuwa akitimiza maandiko ya Biblia inaposema,''Mpende ADUI yako na umwombee'' Hakika huyu alikuwa ni mwana wa Mungu kwelikweli.

Kuna kitendo alicho wahi kukifanya baada ya kuingia Ikulu kama Rais. Akiwa madarakani marehemu Nelson Mandela alikwenda ziara ya Kiserikali nchi za nje. Alichofanya Mandela ni kukabidhi Ikulu kwa Mpinzani wake Chifu Buthelezi na akaenda zake nje ya nchi mpaka aliporudi!!!Fikiri juu ya Rais aliyeko Madarakani halafu aende ziara nje ya nchi na amkabidhi Ikulu kiongozi wa Chama cha Upinzani!!!Hiki siyo kitu cha kawaida. Wazia tu mtu kama Rais Kiwete anavyo talii kwa ziara za masafa nje ya nchi halafu aondoke na amwachie Ikulu kiongozi wa Upinzani kama Dr. Slaa au Prof. Lipumba......! Nina hakika kwa siasa za Bongo tena za CCM hilo jambo ni ndoto!

Najua CCM hawawezi kufanya lolote kati ya hayo 2 aliyoyafanya Mandela akiwa hapa duniani. Hawawezi. CCM ni chama chenye chuki na wapinzani. Tumeona jinsi vyama vya upinzani vinavyoonewa na kunyanyaswa na Srerikali ya Chama Twawala. Wapinzani wanapigwa mabomu ya kuua,risasi za moto na mabomu ya machozi. Wapinzani wanazuliwa kesi za uhaini na ugaidi. Wapinzani wanatukanwa na kuzomewa Bungeni hata pale wanapotoa hoja na michango yenye kuboresha na kujenga nchi yetu Tanzania. Halafu mtu anasimama jukwaani na kutamba ati tuna mu enzi Mandela au Baba waTaifa bila aibu!!!CCM acheni upuuzi huo na badilikeni. Tunataka kuona mabadiliko ya kweli muwa enzi hawa wazee Mandela na Baba wa Taifa Nyerere kwa vitendo.

Kama mtaendelea na ukaidi wenu wa kutowa heshimu na kuwa enzi hawa wazee waliojaliwa kuwa na busara na hekima za hali ya juu hakika mnajitafutia BALAA NA LAANA. Ninachoweza kusema tu ni kwamba,CCM NI SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA. CCM haina muda mrefu itafutika na kusahauliwa kwenye vitabu vya historia ya dunia hii huku dunia ikiendelea kuwakumbuka na kuwa enzi Nelson Madiba Mandela na Julius Kambarage Nyerere.

R.I.P galant soldier and son of Africa Nelson Madiba Mandela.

Kwa heri Tata.
 
Back
Top Bottom