Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,403
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametuma ujumbe wa salamu za pole kwa Rais wa Tanzania, John Magufuli; Watanzania wote pamoja na familia kufuatia kifo cha Rais Mstaafu Benjamin Mkapa
Katika ujumbe wake, Rais Kenyatta amemuomboleza kiongozi huyo kama mtu bora wa Afrika Mashariki aliyefanya kazi kwa bidii kwa ajili ya amani na maendeleo ya Kanda ya Afrika Mashariki
Rais Kenyatta ameitakiwa familia ya Rais huyo Mstaafu na Watanzania wote kwa ujumla faraja kutoka kwa Mungu wakati huu wa kuomboleza kuondokewa na Kiongozi wao
Benjamin William #Mkapa aliyefariki usiku wa kuamkia leo hospitalini alikokuwa amelazwa alikuwa Rais wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2005 kupitia chama cha CCM
=====
Kiongozi wa Chama cha Upinzani cha ‘Orange Democratic Movement (ODM)’ cha Kenya, Raia Odinga ameomboleza kifo cha Rais Mstaafu wa Tanzania wa awamu ya 3, Benjamin Mkapa kilichotokea usiku wa kumkia leo
Amesema, “Mkapa alikuwa rafiki mkubwa wa watu wa Kenya, muumini mkubwa wa Pan Africanism na muamini mkubwa wa ushirikiano wa Kusini-Kusini”
Ameongeza, “Kenya tunabakiwa na kumbukumbu kubwa kwa namna alivyohusika pamoja na Dkt. Kofi Annan (Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa) na Graca Machel kusaidia nchi hii kurudi katika amani baada ya vurugu kufuatia Uchaguzi Mkuu wa 2007-2008
PIA SOMA:
= > Breaking News: - TANZIA: Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa afariki dunia