Kifo cha kweli cha Adolph Hitler: Hebu tuachane kwanza na ile ya kujiua kwa tindikali au kukimbilia kwake Argentina

Dunia haitakiwi kuruhusu watu wa aina hii tena Duniani.Kiufupi Dunia na wanadamu wamepitia maswaibu mengi ya mateso na mauaji ya kikatili katika kutafuta ustaarabu uliopo.sasa hivi.

Kila mtu anaethubutu kuturudisha huko ni bora atangulie yeye maana kulibakia kidogo Tzn turudi zama za giza ambazo bado North korea wako.
North mzee baba Kashapoa ,Ntakuja na Nyuzi yake Hapa Insha'aallah
 
Wakuu naomba kuuliza kwanini Hitler alikuwa anaua wayahudi?
Lengo lake lilikuwa lipi hasa huyu jasusi?
Sababu halisi ni ya kiroho zaidi, lengo lilikuwa ni kuzuia kuanzishwa kwa taifa la Israeli, kwa kuwaua wayahudi, kwa wale wasiojua Israel ni saa ya dunia. kuna uwezekano yeye Hilter alikuwa anatumika bila kujua kama anatumika.
 
Kivipi mkuu?
 
Huyu jamaa ana haki ya kujiuwa maana kama angeangukia kwenye mikono ya Stalin ingekuwa balaa,naimani kwa hasira za Stalin angeamua kumuingilia kinyume na maumbile na mwisho wa siku angempika supu

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Kivipi mkuu?
Shetani kupitia binadamu anaweza kupredict future ya dunia, kwa kuangalia nini kumeweka ndani yake, sasa dunia huwa inapita nyakati mbali mbali katika kuelekea mwisho wake,

baada taifa la Israeli kuwa limefutika katika uso wa dunia ilitabiliwa kuwa wayahudi watarudishwa nyumbani na kuanzisha taifa lao, maana yake dunia inaingia katika msimu mpya, sasa lengo la kuwaua wayahudi wote ni kujaribu kuzuia mpango wa Mungu wa kuanzisha taifa la Israeli.

Sasa Israeli inatumika kama saa ya kujua sasa tuko katika nyakati gani kuelekea mwisho wa dunia, na hii kwa sababu matukio mengi kuelekea siku ya mwisho yako ndani ya maisha ya taifa la Israeli.

Somson wa ndani ya biblia aliwaua wafilist kwa sababu alikuwa analipiza kisasi kwa kuwa walimpola mke wake, lakini ukweli ni alikuwa anatimiza kusudi la Mungu la kuwaua wafilist waliokuwa wwnawatesa wana wa Israel, yaani hiyo ndio ilikuwa kusudi lake,

kwa hiyo ni sawa Hilter alikuwa na sababu zake ila bila kujua kuwa lengo ambalo yeye alikuwa may be halijui ni kuzuia kuanzishwa kwa taifa la Israeli, ili dunia isiingie katika msimu mpya. Tatizo ni ngumu kuzuia kusudi la Mungu.
 
Sawa mkuu, shukraani kwa mchango wako
 
Sababu halisi ni ya kiroho zaidi, lengo lilikuwa ni kuzuia kuanzishwa kwa taifa la Israeli, kwa kuwaua wayahudi, kwa wale wasiojua Israel ni saa ya dunia. kuna uwezekano yeye Hilter alikuwa anatumika bila kujua kama anatumika.
Anhaa umenifumbua macho kidogo
 
Jeshi la Ujerumani la wakati wa Hitler( wehrmacht) lilikuwa ni jeshi imara na lenye nguvu.Kuna neno Hitler alikuwa analitumia kumaanisha speed ambayo hili jeshi lake linaitumia kupigana vita.Neno lenyewe ni Blitzkrieg ni neno la kijerumani likimaanisha Lightening War yaani vita yenye spidi ya radi(ule mwanga wa radi unaopiga kwa spidi).

Hitler alikuwa anamaanisha jeshi lake linavamia nchi za ulaya na kuzikamata kwa spidi ya radi.Jeshi hili la Ujerumani lilipokuwa linazivamia nchi mbalimbali kama Poland na hata Soviet Union,lilikuwa linaambatana na vikosi fulani ambavyo vilikuwa na kazi maalumu na wala si kupigana vita.Vikosi hivi vilikuwa vinaitwa Einsatzgruppen kwa kijerumani.Kwa jinsi vikosi hivi vilivyokuwa vinafanya kazi tunaweza kuviita Mobile Killing Squad.Kwa sababu vilikuwa vinatoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kutekeleza mauaji.Jeshi la Ujerumani lilikuwa kazi yake kupigana vita ila hawa einsatzgruppen walikuwa na kazi maalumu ya kudeal na Jews na walikuwa hata wanalalamikiwa na jeshi la ujerumani kwa mauaji waliyokuwa wanafanya lakini jeshi halikuwa na namna kwasababu order ya mauaji ilikuwa inatoka kwa Hitler.

Kazi kubwa ya hivi vikosi ilikuwa; pale jeshi la ujerumani likishavamia nchi fulani na kuikamata einsatzgruppen kazi yao ilikuwa kuwazunguka wayahudi katika miji na vijiji mbalimbali na si wayahudi tu na hata watu fulani fulani ambao walikuwa wanatakiwa kuuwawa kama wasomi na watu wengine muhimu pia hata wale ambao walikuwa wanapinga uvamizi.Ukiachana na einsatzgruppen pia nchi zilizokuwa zinavamiwa na ujerumani kulikuwa kunamwagwa Police fulani wanaofanya kazi zao kwa siri,hawa walikuwa wanaitwa Gestapo(Geheime Staatspolizei) au tuwaite Germany Secret Police,hii ilikuwa ni kama Intelligence Agency ya Nazi Germany.Madikteta huwatumia sana hawa secret police kutengeneza fear.Hawa Gestapo wa Hitler hata ujerumani kwenyewe walitengeneza hofu kubwa kwa wajerumani na walikuwa wanaogopeka sana.

Wayahudi (watoto,wanawake,wazee) baada ya kuzungukwa na hivi vikosi vya einstatzgruppen na Gestapo walikuwa wanaongozwa kwenye sehemu maalumu mfano nje ya miji na kwenye maeneo yaliyojitenga huko waliamrimshwa kuchimba Mashimo baada ya hapo wanajipanga pembezoni mwa hayo Mashimo na kupigwa risasi nyuma ya kichwa na kudondokea kwenye hayo Mashimo kisha yanafukiwa.Saa nyingine walikuwa wanalazimishwa kuvua nguo na kuuliwa wakiwa uchi nguo hizo zilikuwa zinachukuliwa na kupelekwa ujerumani,na si nguo tu walikuwa wanachukua na vitu vingine vya wayahudi wanaowaua kama hela,mikufu,miwani,meno ya dhahabu mdomoni na vinginevyo.

Hali ilikuwa mbaya sana Imagine watu wanavuliwa nguo baba,mama na watoto wote wako pamoja hakuna cha mzee wala mtoto wote wanavuliwa nguo.

kwa siku moja einsatzgruppen walikuwa wanaweza kuuwa maelfu watu japo namna hii ya uuaji ilikuwa inawaletea madhara kisaikolojia hata wauaji wenyewe imagine,unawauawa watoto wadogo wa miaka mitatu minne na kuendelea na wewe ni baba wa familia. Na kila siku hawa wauaji walikuwa wanapeleka idadi ya watu waliowaua kwa siku bila shaka ni kwa heinrich Himmler mkuu wa SS(Schutzstaffel) au kwa kijerumani walikuwa wanamuita Reichsfuhrer-SS yaani kiongozi wa SS kitaifa

Baada ya wakuu wa vikosi hivi kuona askari wao wanaathirika sana na kuua kwa risasi ndipo mwaka 1941 walikaa kikao na kupata suluhu ya namna ya kuwauwa wayahudi kwa ufanisi.Suluhu hii iliitwa "the final solution to the Jewish question" sobibor ni miongoni mwa zao la kikao hiki.

Kabla hawajaja na solution hii kuna engineer wa kijerumani alitengeneza gari ambalo kwenye Kebin lilikuwa na gas chamber,gari hilo lilikuwa linatumika Kuwaua wayahudi kwa njia ya gesi ya sumu japo lilikuwa haliko efficient,lilikuwa linaweza kuua watu wachache wachache.Ni hivi engine ya lile gari ilikuwa inabomba ambalo lilikuwa linapeleka hewa ya carbonmonoxide kwenye cabin hivyo mtu akiingizwa kwenye cabin na ikawa sealed ile engine ikiwashwa ule moshi au tuseme gas inayotoka kwenye engine inaingia kwenye cabin na yule mtu aliefungiwa kwenye cabin anaivuta huku akiwa hapati oxygen hivyo baada ya kama dk 25 anapoteza maisha.Wakishakufa mlango wa cabin unafunguliwa wanasubiri dakika kadhaa kisha wanazitoa Maiti na kuwaingiza watu wengine.

Hizi ni baadhi ya picha za siri walizokuwa wanapiga wenyewe wauaji ambazo zilipatikana baada vita mobile killing squad(einstatzgruppen) wakionekana wakifanya mauaji kwa wayahudi.

View attachment 1741771

View attachment 1741772

View attachment 1741773

View attachment 1741774

Na hili ni gari(Gas van) ambalo lilikuwa equipped na gas chamber kwenye cabin kwa ajili ya mauaji
View attachment 1741776

IMG_20210805_170925_208.jpg
 
Back
Top Bottom