Kifo cha kweli cha Adolph Hitler: Hebu tuachane kwanza na ile ya kujiua kwa tindikali au kukimbilia kwake Argentina

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Dec 7, 2019
3,837
6,372
Wasalaam,

Kumekuwa na Hadithi nyingi sana Kumuhusu diktekta maarufu , mwamba wa Ujerumani Adolph Hitler, katika hatma yake Wengine wakidai alichomoka kwenda kwa wafadhili wake wa Argentina kustirika Aibu ya kushindwa Vita, wengine Wakadai alijitumbukiza kwenye Tindikali Eti baadala ya Mabaki ya nguo zake kukutwa pembeni ya Tindikali nadharia hiyo hata mimi miaka ile nakua ilikaa kwenye Ubongo wangu, wengine wakasema Diktekta huyo alikufa kwa kushambuliwa na Mbu yule mdudu wa Malaria ,habari zipo nyingi nyingi.

Screenshot_20210326-151054.png

Katika utafiti wa wanasayansi wa Ufaransa walichambua vipande vya meno ya Adolf Hitler ili kudhibitisha kuwa alikufa mwaka 1945, baada ya kujipatia sumu (cyanide) na kujipiga risasi kichwani. Utafiti huo, uliochapishwa katika Jarida la ulaya la Internal Medicine, Mei 2018, hii ilimaliza kabisa nadharia nyingi juu ya kifo cha Adolf Hitler kupitia uchambuzi wa kisayansi wa meno na fuvu la dikteta Huyo.

"Utafiti wetu unathibitisha kwamba Hitler alikufa mwaka 1945,"

mwandishi mkuu wa utafiti huo Philippe Charlier aliiambia AFP.

"Ni Meno halisi ya Hitler na hakuna shaka"

Screenshot_20210326-151743.png

PHILLIPE CHARLIER

Ingawa imejulikana hivyo kwamba Hitler alikufa katika jumba lake la Utawala pale Berlin, lakini uvumi wa kutoroka na kukimbia ni mwingi sana.
Utafiti wao unathibitisha kwamba hakufanikiwa kukimbia

"hakukimbilia Argentina kwa manowari, wala hakwenda katika kituo kilichofichwa "

Alisema Charlier

Inaelezwa Mwishoni mwa Aprili 1945, wakati vikosi vya Soviet vilipovamia Berlin, .
Hitler alifanya mipango ya kujiua hii ni baada ya kuagiza vidonge vya Sumu kabla hajaacha wosia wa mwisho.
Siku mbili kabla , Mussolini alikuwa amepigwa risasi na kikosi cha warusha risasi na kisha kunyongwa hadharani ,katika uwanja huko Milan Italia.
Hatima kama hiyo ilionesha hiltler hakutaka imtokee akachukua maamuzi kama hayo. Akajiua.

Aprili 30, miili ya Hitler na mkewe Eva Braun, ilipatikana ndani ya jumba hilo, huku ikiwa na shimo la risasi

Screenshot_20210326-150654.png

Aprili 2018, Chapisho la Kiingereza la kumbukumbu za mkalimani wa Urusi ilidokeza jinsi alivyokabidhiwa meno kadhaa mnamo 1945, na akapewa jukumu la kulinda rekodi zote kuanzia meno, na habari za dikteta za na vyote vinavyomuhusu vilibaki mikononi mwa Urusi

Baada ya mazungumzo ya miezi kadhaa, Secret service ,Ya Urusi ,FSB na serikali ya Urusi ziliwapa watafiti ruhusa ya kuchunguza kipande cha fuvu na vipande vya meno yake. Kipande cha fuvu kilikuwa na shimo upande wake wa kushoto, sawa na jeraha la risasi,
Ingawa wanasayansi hawakuruhusiwa kuchukua sampuli kutoka kwenye fuvu hilo, walibaini katika utafiti huo, muonekano wa sura ya fuvu hilo ilionekana kufanana kabisa na picha za fuvu la kichwa la Hitler lililochukuliwa mwaka mmoja kabla ya kifo chake.

Screenshot_20210326-150746.png

Picha za meno zilizochapishwa katika utafiti huo zinaonyesha taya iliyotengenezwa na meno chuma. na inaelezwa Wakati wa kifo chake waliandika katika ripoti kuwa Hitler alikuwa na meno manne tu yaliyosalia.katika kinywa chake.

Screenshot_20210326-151126.png

Uchambuzi huo ulithibitisha madai yaliyotajwa hapo, lakini hawakuweza kuthibitisha kabisa kama hitler alichukua sumu (cyanide) kabla ya kujipiga risasi. Lakini mabaki ya rangi ya Ubluu kwenye meno yake fake(metal), watafiti waliandika, inawezekana chemical Reaction ilifanyika katika meno yake bandia na sumu hiyo wakati wa kifo

Swali mabaki mengine yalizikwa AU???

"Bila kuchukua sampuli kwa uchambuzi, ni ngumu kusema kwa uhakika"

"Hatukujua ikiwa alikuwa ametumia Sumu ya (cyanide) kujiua au ikiwa ni risasi kichwa, ila kuna uwezekano wa vyote kufanyika "

Charlier alisema.

Screenshot_20210326-150559.png

Kwa vyovyote vile, utafiti unaweza kusaidia hatimaye kuweka kando stori za kukimbia kwa hitler Argentina kupumzika Vurumai la Vita, na habari zingine zingine juu ya kifo chake.

DA'VINCI XV

Hitler naamini alijiua kwenye fuhrer bunker.Hii ni sehemu ambayo ilikuwa chini ya ardhi.Wakati anakaribia kupoteza kwenye vita ya pili ya dunia alikuwa anajificha kwenye hii sehemu yeye na wasaidizi wake kama kina herman goring na yule aliyekuwa waziri wake wa propaganda za kiNazi joseph gobbles.

Katika kitabu chake kinachoitwa Mein Kempf hitler anatueleza alivyokuwa anafikiria kujiua baada ya mapinduzi yake ya kuchukua nchi kufeli mwaka 1923 na alifungwa jela,alipokuwa jela alikuwa na mawazo ya kujiua,mapinduzi haya yalikuwa yanaitwa beer hall pusch.

Kwa kutaka kule kujiua alipokuwa jela kunaonesha kabisa ni mtu ambaye kujiua kwake ni jambo la suluhu pale mambo yanapo muendea mrama.Hivyo kuna uwezekano alipoona ujerumani inapoteza vita ya pili ya dunia akaona ajitoe roho.

Miongoni mwa wasaidizi wake ambao pia walijiua ni Heinrich Himmler(Mkuu wa jeshi la schutzstaffel),Herman Goring(Reich marshal) na joseph goebbels(waziri wa propaganda)

Kuna siku nitakuja na mada inayowaelezea hawa waliokuwa wanaitwa schutzstaffel kwa kifupi SS ambao kofia zao zilikuwa zina alama ya fuvu la kichwa kuashiria ni watu wa kifo.Hakujawahi kutokea wauaji hapa duniani kama hawa jamaa.Ile idadi ya wayahudi milioni 6 waliouwawa wakati wa Hitler hawa jamaa wanaoitwa ss ndio walikuwa wanahusika.
19444700_401.jpg

Huyu pichani anaitwa Himmler ndio alikuwa mkuu wa vikosi vya schutzstaffel nchi nzima.Huyu ndio alikuwa mtekelezaji mkuu wa mauaji ya wayahudi

Nadhani wayahudi walipokuwa wanaona mtu mwenye nguo kama za huyu hapa chini wakati ule wa utawala wa Hitler basi wayahudi walikuwa wanakiona kifo kipo karibu yao
20210327_122046.jpg
 
View attachment 1735324
Huyu pichani anaitwa Himmler ndio alikuwa mkuu wa vikosi vya schutzstaffel nchi nzima.Huyu ndio alikuwa mtekelezaji mkuu wa mauaji ya wayahudi
Hatare
 
Wasalaam,

Kumekuwa na Hadithi nyingi sana Kumuhusu diktekta maarufu , mwamba wa Ujerumani Adolph Hitler, katika hatma yake Wengine wakidai alichomoka kwenda kwa wafadhili wake wa Argentina kustirika Aibu ya kushindwa Vita, wengine Wakadai alijitumbukiza kwenye Tindikali Eti baadala ya Mabaki ya nguo zake kukutwa pembeni ya Tindikali nadharia hiyo hata mimi miaka ile nakua ilikaa kwenye Ubongo wangu, wengine wakasema Diktekta huyo alikufa kwa kushambuliwa na Mbu yule mdudu wa Malaria ,habari zipo nyingi nyingi.

View attachment 1735002

Katika utafiti wa wanasayansi wa Ufaransa walichambua vipande vya meno ya Adolf Hitler ili kudhibitisha kuwa alikufa mwaka 1945, baada ya kujipatia sumu (cyanide) na kujipiga risasi kichwani. Utafiti huo, uliochapishwa katika Jarida la ulaya la Internal Medicine, Mei 2018, hii ilimaliza kabisa nadharia nyingi juu ya kifo cha Adolf Hitler kupitia uchambuzi wa kisayansi wa meno na fuvu la dikteta Huyo.

"Utafiti wetu unathibitisha kwamba Hitler alikufa mwaka 1945,"

mwandishi mkuu wa utafiti huo Philippe Charlier aliiambia AFP.

"Ni Meno halisi ya Hitler na hakuna shaka"

View attachment 1735003
PHILLIPE CHARLIER

Ingawa imejulikana hivyo kwamba Hitler alikufa katika jumba lake la Utawala pale Berlin, lakini uvumi wa kutoroka na kukimbia ni mwingi sana.
Utafiti wao unathibitisha kwamba hakufanikiwa kukimbia

"hakukimbilia Argentina kwa manowari, wala hakwenda katika kituo kilichofichwa "

Alisema Charlier

Inaelezwa Mwishoni mwa Aprili 1945, wakati vikosi vya Soviet vilipovamia Berlin, .
Hitler alifanya mipango ya kujiua hii ni baada ya kuagiza vidonge vya Sumu kabla hajaacha wosia wa mwisho.
Siku mbili kabla , Mussolini alikuwa amepigwa risasi na kikosi cha warusha risasi na kisha kunyongwa hadharani ,katika uwanja huko Milan Italia.
Hatima kama hiyo ilionesha hiltler hakutaka imtokee akachukua maamuzi kama hayo. Akajiua.

Aprili 30, miili ya Hitler na mkewe Eva Braun, ilipatikana ndani ya jumba hilo, huku ikiwa na shimo la risasi

View attachment 1735004

Aprili 2018, Chapisho la Kiingereza la kumbukumbu za mkalimani wa Urusi ilidokeza jinsi alivyokabidhiwa meno kadhaa mnamo 1945, na akapewa jukumu la kulinda rekodi zote kuanzia meno, na habari za dikteta za na vyote vinavyomuhusu vilibaki mikononi mwa Urusi

Baada ya mazungumzo ya miezi kadhaa, Secret service ,Ya Urusi ,FSB na serikali ya Urusi ziliwapa watafiti ruhusa ya kuchunguza kipande cha fuvu na vipande vya meno yake. Kipande cha fuvu kilikuwa na shimo upande wake wa kushoto, sawa na jeraha la risasi,
Ingawa wanasayansi hawakuruhusiwa kuchukua sampuli kutoka kwenye fuvu hilo, walibaini katika utafiti huo, muonekano wa sura ya fuvu hilo ilionekana kufanana kabisa na picha za fuvu la kichwa la Hitler lililochukuliwa mwaka mmoja kabla ya kifo chake.

View attachment 1735009

Picha za meno zilizochapishwa katika utafiti huo zinaonyesha taya iliyotengenezwa na meno chuma. na inaelezwa Wakati wa kifo chake waliandika katika ripoti kuwa Hitler alikuwa na meno manne tu yaliyosalia.katika kinywa chake.

View attachment 1735005

Uchambuzi huo ulithibitisha madai yaliyotajwa hapo, lakini hawakuweza kuthibitisha kabisa kama hitler alichukua sumu (cyanide) kabla ya kujipiga risasi. Lakini mabaki ya rangi ya Ubluu kwenye meno yake fake(metal), watafiti waliandika, inawezekana chemical Reaction ilifanyika katika meno yake bandia na sumu hiyo wakati wa kifo

Swali mabaki mengine yalizikwa AU???

"Bila kuchukua sampuli kwa uchambuzi, ni ngumu kusema kwa uhakika"

"Hatukujua ikiwa alikuwa ametumia Sumu ya (cyanide) kujiua au ikiwa ni risasi kichwa, ila kuna uwezekano wa vyote kufanyika "

Charlier alisema.

View attachment 1735007

Kwa vyovyote vile, utafiti unaweza kusaidia hatimaye kuweka kando stori za kukimbia kwa hitler Argentina kupumzika Vurumai la Vita, na habari zingine zingine juu ya kifo chake.

DA'VINCI XV

Hitler naamini alijiua kwenye fuhrer bunker.Hii ni sehemu ambayo ilikuwa chini ya ardhi.Wakati anakaribia kupoteza kwenye vita ya pili ya dunia alikuwa anajificha kwenye hii sehemu yeye na wasaidizi wake kama kina herman goring na yule aliyekuwa waziri wake wa propaganda za kiNazi joseph gobbles.

Katika kitabu chake kinachoitwa Mein Kempf hitler anatueleza alivyokuwa anafikiria kujiua baada ya mapinduzi yake ya kuchukua nchi kufeli mwaka 1923 na alifungwa jela,alipokuwa jela alikuwa na mawazo ya kujiua,mapinduzi haya yalikuwa yanaitwa beer hall pusch.

Kwa kutaka kule kujiua alipokuwa jela kunaonesha kabisa ni mtu ambaye kujiua kwake ni jambo la suluhu pale mambo yanapo muendea mrama.Hivyo kuna uwezekano alipoona ujerumani inapoteza vita ya pili ya dunia akaona ajitoe roho.

Miongoni mwa wasaidizi wake ambao pia walijiua ni Heinrich Himmler(Mkuu wa jeshi la schutzstaffel),Herman Goring(Reich marshal) na joseph goebbels(waziri wa propaganda)

Kuna siku nitakuja na mada inayowaelezea hawa waliokuwa wanaitwa schutzstaffel kwa kifupi SS ambao kofia zao zilikuwa zina alama ya fuvu la kichwa kuashiria ni watu wa kifo.Hakujawahi kutokea wauaji hapa duniani kama hawa jamaa.Ile idadi ya wayahudi milioni 6 waliouwawa wakati wa Hitler hawa jamaa wanaoitwa ss ndio walikuwa wanahusika.
View attachment 1735324
Huyu pichani anaitwa Himmler ndio alikuwa mkuu wa vikosi vya schutzstaffel nchi nzima.Huyu ndio alikuwa mtekelezaji mkuu wa mauaji ya wayahudi
Hivyo vikosi vya Schutzastaffel bado vipo had I Leo ?
 
Hapana baada ya vita baadhi ya wahalifu wa dola la ujerumani walikamatwa wakafunguliwa mashtaka kwenye mahakama ya Nuremberg(Nuremberg trial).Organization ya schutzstaffel ilitangazwa kuwa ni criminal organization na ikawa banned pamoja na hata wale polisi wa siri wa utawala wa kiimla wa Hitler (Gestapo) walitangazwa kuwa ni criminal organization na baadhi ya viongozi wake walihukumiwa vifungo na wengine kunyongwa wakikiwemo wale waliokuwa kwenye administration ya death camps na concentration camps kama buchenwald, sobibor, treblinka, belzec na nyinginezo.

Hizi death camp zimeuwa wayahudi wengi sana hasa kwenye vile vyumba vya hewa ya sumu(Gas chamber).
 
Hitler naamini alijiua kwenye fuhrer bunker.Hii ni sehemu ambayo ilikuwa chini ya ardhi.Wakati anakaribia kupoteza kwenye vita ya pili ya dunia alikuwa anajificha kwenye hii sehemu yeye na wasaidizi wake kama kina herman goring na yule aliyekuwa waziri wake wa propaganda za kiNazi joseph gobbles.

Katika kitabu chake kinachoitwa Mein Kempf hitler anatueleza alivyokuwa anafikiria kujiua baada ya mapinduzi yake ya kuchukua nchi kufeli mwaka 1923 na alifungwa jela,alipokuwa jela alikuwa na mawazo ya kujiua,mapinduzi haya yalikuwa yanaitwa beer hall pusch.

Kwa kutaka kule kujiua alipokuwa jela kunaonesha kabisa ni mtu ambaye kujiua kwake ni jambo la suluhu pale mambo yanapo muendea mrama.Hivyo kuna uwezekano alipoona ujerumani inapoteza vita ya pili ya dunia akaona ajitoe roho.

Miongoni mwa wasaidizi wake ambao pia walijiua ni Heinrich Himmler(Mkuu wa jeshi la schutzstaffel),Herman Goring(Reich marshal) na joseph goebbels(waziri wa propaganda)

Kuna siku nitakuja na mada inayowaelezea hawa waliokuwa wanaitwa schutzstaffel kwa kifupi SS ambao kofia zao zilikuwa zina alama ya fuvu la kichwa kuashiria ni watu wa kifo.Hakujawahi kutokea wauaji hapa duniani kama hawa jamaa.Ile idadi ya wayahudi milioni 6 waliouwawa wakati wa Hitler hawa jamaa wanaoitwa ss ndio walikuwa wanahusika.
View attachment 1735324
Huyu pichani anaitwa Himmler ndio alikuwa mkuu wa vikosi vya schutzstaffel nchi nzima.Huyu ndio alikuwa mtekelezaji mkuu wa mauaji ya wayahudi

Nadhani wayahudi walipokuwa wanaona mtu mwenye nguo kama za huyu hapa chini wakati ule wa utawala wa Hitler basi wayahudi walikuwa wanakiona kifo kipo karibu yao
View attachment 1735633
shukraani mkuu🙏🙏
 
Back
Top Bottom