Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

KIFO CHA HAWARA (mkono wa jinni)
SEHEMU YA KUMI NA TATU
MTUNZI: Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA MBILI : na hapo kuibukia kwenye mtaa fulani tulivu wenye nyumba kadhaa nzuri za kisasa zilizo jengwa kwa kuachiana nafasi huku baadhi zikiwa na uzio mkubwa sana, zikionyesha ni majumba ya watu wenye fedha ndefu, yaani matajiri, kilicho nivutia ni sehemu moja ambayo tuliweza kupita kijumba kimoja kidogo cha udongo kilichoezekwa kwa bati chakavu kikiwa kimezungukwa na vichaka vya mihogo na miti ya misheri sheri, ambacho kwa usiku huu tuliweza kuona kikiwa kinawaka taa kama sio koroboi ya chemri basi ni kandiri, huku kijumba hicho kikipakana na uzio mkubwa uliopambwa na taa za rangi mbali mbali……..ENDELEA….
zilizo tuwezesha kuona waya maalumu za umeme wa ulinzi, huku wigo huo mrefu ukitufanya tushindwe kuliona vizuri jumba lililopo ndani yake lililo onekana ghorofa moja tu ya juu, “hivi ina maana matajiri wa kipemba wameshindwa kukiamisha hiki kizee?” aliuliza Komba, “unajuwa hata mimi huwa nikipita hapa huwa natazama halafu nakosa jibu” alisema yule afisa wa mahusiano na uchunguzi, huku tukizidi kushuka chini kueleka mtaa ambao ulikuwa unaanza kuchangamka kama vile uswahilini tofauti na kule tulikoanzia
Naam Ukweli nilishangaa sana kuona tunakoelekea kuwa ni mtaa uliochangamka sana, mfano wake ni mitaa kama kibamba au mbezi, “kwahiyo hilo tukio limetokea huku na walishindwa kumpata huyo mtu aliefanya mauwaji?” niliuliza kwa mshangao, “kaka hii ndiyo pemba, wewe unamsikiliza mzee Mwanauta, nani anaweza kumkamata jini kirahisi hivyo” alisema Komba na JC akadakia, “we fikiria, unaambiwa vifo kama hivi vimetokea mfululizo kwa miaka mingi sana, toka mwaka tisini na nane tisini na tisa” alifafanua JC, ni kweli historia inasema hivyo, nakumbuka nilisoma kwenye maelezo ya mwanzo kabisa kuwa vifo vinavyo husishwa na jini vilisha tokea kwa watu kadhaa na wote wakiwa ni wanaume, wanne kati ya wanaume hao walikuwa ni wanafunzi wa sekondari ya Msingini, “kwani huyu wa leo nae amekutwa amebadilika rangi” niliuza kama mshamba ili wasigundue kuwa nilikuwa katika uchunguzi, “hoo! Unaambiwa hivi, jamaa amekauka vibaya sana, na ilikuwa kwa muda mfupi sana wamemkuta mweusiiiii” alisema JC, na wakati huo mwasenge alikuwa anakata kona kuingiza gari kwenye chochoro moja ambapo tulianza kuona magari yakiwa yameegeshwa na pia tulianza kuona watu wengi, “kwahiyo watu walijuwaje kama kuna tukio kama hilo, au marehemu kuna watu alikuwa anaishi nao” niliuliza nikiwa na matumaini ya kupata taarifa muhimu, kuna dogo mmoja alikuwa anahojiwa inasemekana alikuwepo pale anacheza game kwenye computer, sasa sjajuwa kilitokea nini, ila maelezo zaidi nitayapata kesho kwa insp Haroub” alisema JC, huku gari linasimama kwenye sehemu ambayo magari mengine yalikuwepo, na sisi tuka shuka na kusogea walipokwepo watu wengine.
Hakika watu walikuwa wengi sana, mmoja wapo alikuwa ni kijana Ussi ambae alikuwa amekaa na baadhi ya wazee wa makamo, na sisi tukasalimia na baadhi ya watu huku tukisogelea pale alipokuwepo Ussi na wale wazee, ambao walikuwa wamevalia kinadhifu, wapo waliovaa kanzu na wapo waliovaa kawaida, yaani shati na suruali au tisheti, wapo walio onekana kuwa na uwezo mkubwa wakimaisha na wapo walio onekana kuwa na hali ya chini ya kimaisha, wapo wazee wa makamo na pia walikuwepo vijana kama vile Ussi na wenzake wachache wakiongea hili na lile, maongezi yao yaliegemea kwenye utani, “asalam alaykum” tulisalimia kwa kushikana mikono na kila mmoja, tulipo maliza tukatafuta sehemu za kukaa pale juu ya mkeka, tukiwa tumevua viatu vyetu, tuliweza kujiunga na wenyeji wetu, akiwepo bwana Ussi ambae muda mwingi alikuwa anachezea simu yake kama vile anatuma na kupokea ujumbe, pale msibani nilikutana na vijana wengi ambao nimefahamiana nao kule kwenye mazoezi ya baskert ball mjini chake chake, “jamani hebu tuache utani, hivi hili jini lenye njaa ya damu namna hii limetokea wapi?” aliuliza mmoja wa wale wazee ambae pia muonekano wake alionekana kuwa ni mtu mwenye fedha, “ukweli bwana Mohamed, inabidi tukae na hawa vijana kesho baada ya kutoka mazikoni ili watueleze walicho kifanya mpaka wanaadamwa namna hii, maana hii ni hatari sasa” alisema mzee mwingine akilitaja jina la yule mzee wa kwanza kuwa ni mzee Mohamed, ambae alionekana kutulia kidogo akiwaza jambo, alitumia kama dakika nzima mpaka kujibu, “mmmmh! sawa ni sawa… lakini… unadhani kuwa kuna jambo walilifanya mpaka yanatokea haya?” aliuliza mzee Mohamed ambae ni kama alikuwa anatilia shaka wazo lile, “sasa kama sio hivyo unadhani huyu jini kwanini anafanya hivyo?” aliuliza mzee mwingine sio yule wa pili, “hata mimi nadhani itakuwa vyema tukae na hawa vijana ili watueleze kilicho tokea, maana hii sio kawaida, mambo haya tulisha ya sahau, sasa naona yamerudi tena kwa kasi” alichangia mzee mwingine wakati huo mimi na wale makamanda wakina Malambo tulikuwa kama wasikilizaji, “ila nakumbuka hata wakati ule haya mambo yalipotea yenyewe baada ya watu kadhaa kuuwawa na walikuwa vijana wadogo tu ambao hawakukosea chochote” alisema mzee Mohamed.
Naam licha ya kutulia pale kama wasikilizaji, mimi nilikuwa natazama huku na huko, kuangalia kama ninaweza kumuona mtu ambae nina weza kupata habari kwake, pia nilizingatia mbinu fulani ya kijasusi ya kuwa ukifanya tukio fulani, lazima uende eneo husika ukatazame madhara au faida iliyotokea kwa kile ulichokifanya, hivyo niliamini lazima hata huyo jini atakuwepo eneo lile kwa kificho au wazi wazi, pia nilikuwa natazama mazingira haya na kutafakari kuwa huyu alipotoka ndani ya nyumba hii akaelekea upande gani na alitoweka vipi, “ni sawa ilikuwa hivyo hapo zamani, na hatukufanya lolote mpaka ilipo toweka yenyewe, lakini sasa lazima tupate ufumbuzi wa kudumu, ikiwezekana watu watumwe kojani (kisiwa kidogo)” alisema mzee mwingine na wote wakaonekana kuungana mkono, huku wakipanga kuliongelea lile mara baada ya kumaliza mazishi, wakati huo nikamuona Malambo anamsogelea Ussi, ambae katika watu ambao niliwaona wameguswa na msiba ule ni yeye, maana sio tu unyonge na simanzi, pia alikuwa mwenye wasi wasi mwingi sana, pengine alihofia kukumbwa na Jini hilo linalo wafyeka vijana na kumuuliza sehemu kilipo kitabu cha lambilambi, nae akaonyesha upande wa mbele karibu na nyumba kubwa, “Eric tunaweza kwenda kuandika kwenye kitabu kama unachochote” alisema Malambo kisha akawaeleza wakina Komba hivyo hivyo, kisha tukainuka pamoja na kuelekea kwenye kitabu.
Wakati wa kuandika nilikuwa na tazama eneo hili kwa umakini sana, huku nikipata picha ya kwamba kwa binadamu wa kawaida ingekuwa ngumu sana kumuona kama angefanikiwa kutoka na kuvuka nyumba mbili tatu, “kwanini kama jini alionekana akitoka na asinge potelea ndani moja kwa moja” nilijiuliza pasipo kupata jibu, huku macho yangu yakitua pembeni kidogo ya eneo lile walilokaa waombolezaji, hapo nikamuona mzee mmoja mkongwe sana, ambae alionekana ni wa hali ya chini sana kiuchumi, ni mzee ambae sio tu nguo zake chakavu zilizo mtambulisha ufukara wake, lakini pia hata muonekano wake wa nywele zilizo jiviliga zikipambwa na mvi na ngozi ya mwili wake mikononi na usoni iliyopauka, akiwa amekaa chini kwenye mkeka, huku macho yake ameyaelekeza kwenye kundi la wale watu tuliokuwa tumekaa nao, na wakati mwingine akitutazama sisi.
Kikubwa ambacho kilinivutia kwa huyu mzee ni muonekano wa uso wake, ukweli alikuwa na makovu mawili makubwa sana usoni kwake, moja likianzia juu ya jicho la kushoto na kupitia kati kati ya macho yake mawili, likishuka juu ya mgongo wa pua na kukatiza kwenye shavu la kulia likiishia kwenye kidevu eneo la taya ya mdomo wa babu huyu upande huo huo wa kulia, huku kovu la pili likilala upande wa kushoto wa uso wa babu yule, kuanzia juu karibu na usawa wa paji la uso, mpaka kwenye usawa wa kidevu na kumfanya aonekane kama kituko fulani cha kuogofya, ni wazi alishambuliwa kwa kuti chenye makali, mfano wa panga au kisu kikubwa, “oya wakubwa hee, hapa tunakaa nusu saa tu, saa tatu kamili mimi naaga” alisema Malambo wakati tunarudi pale tulipokuwa tumekaa, “itakuwa poa sana, maana si unajuwa mida ya kuwahi viti hii, watu wakijaa pale mess tutakunywa bia tukiwa tumesimama” alisema afande komba huku tukiendelea kutembea mimi nilikuwa busy namtazama yule mzee ambae macho yake alikuwa ameyaelekeza kule kule tulipokuwa tunaelekea, na utazamaji wake ulikuwa ni wakipekee, ungesema alikuwa anamtazama mtu aliegombana nae.
Tulienda na kukaa pale tulipokuwa tumekaa mwanzo, tulikuta maongezi yanaendelea na hapo ndipo nilipo pata mambo mapya manne, ambayo niliamini yatakuwa msaada kwangu, “hivi jamani hawa polisi walikumbuka kutazama camera za nyumba ya Masoud” aliuliza kijana mmoja ambae tulikuwa tumekaa nae pale, Mwenye umri kama wetu, na hapo nikajikuta naitazama ile nyumba iliyopo mbele yetu, ukweli haikuonyesha dalili ya kuwa na camera za ulinzi, “mh! kwani hii nyumba ina camera?” nilijikuta namuulizia mtu niliekaa nae jirani, ambae sio kati ya wale makamanda, “sidhani kama walifanya hivyo, lazima wangeeleza walicho kiona” safari hii alijibu, JC Luge, yule afisa mahusiano na uchunguzi, na ndio wakati ambao yule jirani yangu alipo jibu swali langu, “marehemu alikuwa anakaa macho manne mtaa wa maskini hajengi” alijibu yule kijana ambae, muonekano wake ni kama kijana wa pale pale mtaani, ni kutokana na uvaaji wake mwepesi, ambae alitaja jina la mtaa ambao mchana wa leo niliusikia kwa mara ya kwanza, nakumbuka Saphia alisema kuwa kaka yake anakaa mtaa huo.
Jibu la kijana yule lilinipa picha ya kwamba, yale magari ya polisi yalikuywa yana tokea huko ambako lilitokea ilo la mauwaji, “mzee Mohamed hebu mpigie insp Haroub mjulishe juu ya hilo” alisema mmoja kati ya wale wazee, “mh! uanadhani hawaja ona kama kuna camera, au wameziona na kuamua kitunza siri za kiuchunguzi, au wameshindwa kuona chochote, maana jini lina maajabu yake bwana” alisema mzee Mohamed, ambae ni kama hakuwa anaafiki lile swala la kupiga simu polisi, “we wasiliana nae kama wamesha uona atakuambia” alisisitiza mzee mwingine, na hapo nikamuona mzee Mohamed anatulia kidogo kama anawaza jambo, kwa sekunde kadhaa, kisha akamtazama kijana Ussi, ambae kama kawaida yake alikuwa anachezea simu yake kila baada ya sekunde kadhaa, “Ussi hebu nenda kanichukulie simu kwenye gari” alisema mzee Mohamed, “ndiyo baba” alijibu Ussi, huku anasimama na kuelekea kule kwenye maegesho ya magari, na hapo nilipo gundua jambo la tatu, kuwa mzee Mohamed ndie baba yake Ussi, la kwanza likiwa ni kujuwa mtaa aliokuwa anaishi marehemu, la pili kuwa nyumba ya marehemu ilikuwa na camera, “lakini kwani Ussi hakuwa na rafiki yake wakati wa tukio” aliuliza mmoja kati ya wazee wale, “lakini yeye anasema kuwa alimuona mchana akiwa amebeba mwanamke kwenye vesper hakumjuwa ni nani alikuwa amevaa niqab” alisema moja kati ya vijana tuliokuwanao pale, na hapo ndipo nilipo gundua kitu cha nne, kuwa alieuwawa ni Masoud Vuai, kwasababu ndie mtu ambae mimi na Ussi tulimuona akiwa amebeba mwanamke alievaa niqab kwenye vesper, hakika nilishtuka kiasi cha mapigo ya moyo kuanza kunienda mbio, hapo hapo nika vuta picha ya yule mwanamke mrefu mwenye kunukia marashi ya kupendeza niliekutana nae mida ile ile, na baada ya muda mfupi tuka muona Masoud anatokea upande ule ule, akiwa na mwanamke ambae sikumtambua kama ni yeye au sio yeye, na alielekea upande wa macho mane (yani macho mnne), na hilo lilikuwa ni jambo la nne kulitambua, “lakini huyu kijana nae alianza lini mambo ya kubeba wanawake bila kufunga ndoa?” aliuliza mmoja kati ya wale wazee, “ukweli inashangaza, Masoud sio muasharati kabisa, sasa imekuwaje akashawishika kutongoza mwanamke asiemjuwa” alisema mwingine na hapo yule mzee Mohamed, ambae ni baba yake Ussi Mohamed Juma akadakia, “huwezi kujuwa ilikuwaje mpaka kijana kama Masoud kuamua kumtongoza mwanamke huyo, pengine ni mrembo kweli kweli, si unajuwa majini kwa kuvutia wanaume” alisema mzee yule ambae muonekano wake hata uongeaji wake ni wakifedha fedha, “ni kweli bwana Mohamed, siku hizi vijana wanasema wanapenda nyama nyama, matokeo yake wanafia kwa hawara, na yeye anakuwa hawara” alisema mzee alieshauri apigiwe simu insp Haroub, hapo watu walikaribia kucheka, “unaona sasa inabakia kuwa KIFO CHA HAWARA, hakuna ndoa hapo” alisema mzee mwingine na yule ambae alisisitiza kuhusu kupigwa simu polisi akaongeza, “halafu kinacho waponza ni usiri, kama wangekuwa wanatongoza kwa kuambiza pengine ingesaidia, labda wenzake wange mshtua kuwa huyo sio binadamu, si unaona sasa Masoud kime mkuta kilicho mkuta Abdulqadir ” ukweli maongezi hayo japo yalikuwa ni mazuri ya kufurahisha, lakini hayakuwa na faida yoyote kwangu, hapo nilipata hamu ya kuwahi nyumbani kwa Masoud kuchukuwa HD nikaichunguze.
Kabla Ussi hajarudi, nilimuona Malambo akimnong’oneza JC jambo fulani, lakini JC akajibu kwa sauti kidogo, “subiri kidogo Ussi arudi tusikie watakacho ongea na insp Haroub” nadhani walikubaliana hivyo, na zilipita dakika kumi nyingine tukisubiri Uss kurudi, huku mimi napanga ya kwangu kichawani, kwamba nifike kwenye hiyo nyumba ambayo imetokea tkio hilo kabla ya polisi hawajafika ili nipate HD (Hard Disc) ya security camera na kwenda kuitazama kupitia computer yangu kule green house, swali likabakia je nitafikaje na kuitambua hiyo nyumba, nikamtazama yule kijana mwenzagu niliekaa nae karibu, “hivi unajuwa Massoud nimefahamiana nae jana tu! sikujuwa kama anakaa Maskini hajengi” nilimchokoza yule kijana, nae akajaa “mbona sehemu ya wazi kabisa ni nyumba inayotazamana na kile kiwanja kidogo cha volley ball” naam hapo nikatabasamu kimoyo moyo, sasa kilichobakia ni kusubiri simu kwenda kwa insp.
Naam Ussi alitumia dakika kama kumi na tano mpaka kurudi akiwa hajabeba simu, “baba simu yako utakuwa umeiacha nyumbani, maana kwenye gari lako haipo” alisema Ussi huku anakaa pale pale alipokuwa amekaa mwanzo, “hoooo! itakuwa niliiacha nyumbani wakati natoka jioni, dah! sasa tunafanyaje” alisema mzee Mohamed kwa sauti ya kujilaumu, “haina shida ukirudi utaenda kumpigia, mjulishe hilo jambo pengine inaweza kusaidia kuitambua sura ya jini na kuwatangazia vijana wamuepuke” alisema yule mzee mwingine, na hapo nikamuona Malambo anasimama na kuaga kwa niaba yetu, “wazee tunaomba tuwaache, kuna majukumu tunaenda kumalizia, ila kesho tutakuwa wote mazishini” alisema Malambo, huku na sisi tukisimama, “tunashukuru sana kwa ushirikiano wenu” alisema mmoja wa wale wazee, na hapo tutembea kuelekea kwenye gari.
Dakika kumi na saba baadae tuliingia Wawi messi, ambapo tulipakuta pana watu wachache tofauti na vile walivyo niambia, ungesema ni siku ya kawaida tu!, nilienda kukaa kwenye meza moja nikiwa peke yangu, wateja wengi walikuwa ni wanajeshi wenyewe na raia wachache, huku wanawake wakiwa wa kuhesabu, yaani ni wale wale wa siku zote, nasema hivyo kwa sababu nilikuwa nawaona kila siku, nilichagua meza tulivu na kukaa nikiwa na mwasenga ambae nilimuagizia bia yake wakati naagiza ya kwangu, wale maafisa wengine walikuwa wamekaa kwenye meza tofauti tofauti, niliagiza bia moja huku napanga namna ya kumtoa Mwasenga anipeleke mtaa wa Maskini hajengi ilinikafanye kazi yangu, na wakati nakunywa bia yangu nilikuwa nawaza na kutafakari juu ya bwana Masoud ambae ndie mtu alie uwawa, nikavuta picha ya yule mwanamke, ambae nilihisi kuwa anaweza kuwa ndie jini aliemuuwa Masoud, nikamfananisha na yule mwanamke alie bebwa na Masoud kwenye Vesper, ukweli wakati ule nilishindwa kupata jibu sahihi, kwa sababu sikuwa na uhakika wa upana wa umbo lake na kimo chake.
“Kaka leo inshu ya majini imeharibu mambo kabisa” alisema Mwasenga, huku tukiendelea unywa bia, na hapo nikapata njia ya kumshawishi Mwasenga anipeleke Maskini ajengi, “yaani kuna demu mmoja hivi ninahitaji kukutana nae, tena kabla ya saa nne halafu ni mitaa hiyo hiyo” nilimueleza mwasenga ambae alicheka kidogo, dah! bro we mkali yaani umesha nasa mtoto wakipemba? au ni wakutoka Tanga?” aliuliza Mwasenga, huku tukiendelea kunywa bia zetu “ni mwalimu pale Fidel Castor, si unajuwa kaka mji mgumu huu” nilisema kwa utani kumuaminisha Mwasenga ambae alicheka kidogo, tunaweza kuchomoka mara moja, sema inabidi tuwahi kabla ya saa tano” alisema mwasenga, na hapo sikutaka kupoteza muda, nikamshauri mwasenga, tuchukuwe bia mbili mbili za kunywa njiani, na tulifanya hivyo kisha tukaondoka zetu na bia kwenye gari, nilifanya hivyo kwakujuwa kuwa Mwasenga alikuwa anapenda sana pombe.
Dakika kumi tu zilitumika kufika kwenye uwanja wa Volley ball, ambao ulikuwa ni wa kienyeji, yaani wa vumbi wenye milingoti ya chuma, ambayo ilichakaa kwa kutu, uliopo kwenye eneo kubwa la wazi ambalo lilifaa kufanywa uwanja wa mpira wa miguu, “samahani mwasenga, hebu lisogeze gari kwenye uchochoro wa nyumba zile paleee” nilimueleza mwasenga wakati nashuka toka kwenye gari, na yeye akasogeza gari nilipo muelekeza yani kwenye nyumba za upande wa kulia wa uwanja ule, na mimi nika elekea kwenye nyumba ambayo nilielekezwa kuwa ya marehemu Masoud Vuai.
Nilifika kwenye ile nyumba ambayo ilikuwa imezimwa taa zote yaani za nje na za ndani, ishara tosha kabisa kuwa ndani hakukuwa na mtu, nilizunguka nyuma ya ile nyumba,
na kuusogelea mlango, hapo nikatoa kijitochi changu kidogo chenye mwanga mwembamba sana, ambayo ni maalumu kwa matumizi ya somea ramani vitani nyakati za usiku, au kwa kazi kama hizi za sehemu ambazo usiri unatakiwa, niliipata nikiwa Israel kwenye mafunzo ya SFA, (Specil Force Agent) nikatoa waya ambazo ni maalumu kwaajili ya kufugulia kufuri au vitasa vya milango ambavyo vimefungwa na funguo, nikauweka waya vyema kisha nikauchomeka kwenye kitasa na kuanza kuuzungusha, ni kitendo ambacho huwa natumia kwa sekunde chache sana, lakini nilishangaa kuona ninatumia dakika nzima bila mafanikio, nilishangaa sana, maana niliwahi kufungua vitasa vizuri na vya kisasa ambavyo ni vigumu zaidi kwa muda mfupi sana, lakini iweje hiki cha kawaida kabisa nimeshindwa kukifungua, “kumbuka huwezi kuufungua mlango ambao tayari upo wazi” nilikumbuka maneno ya professor Wang Sun, mkufunzi wa chuo cha ujasusi cha korea ya kusini, nikashika kitasa na kukinyonga na mlango ukafunguka kirahisi kabisa, na nilipotazama vizuri niligundua kuwa kitasa kile kilikuwa kimevunjwa, hapo kengele ya tahadhari ikagonga kichwani mwangu…….. jini anavunja vitasa au imekuwaje? Tutaendelea usiku
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom