Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA THELATHININA SABA
MTUNZI: Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI NA SITA: na hapo ndipo mjomba wake alipompeleka kwa shekhe mmoja wa msikiti wa Mchanga Ujuma, na kumfanyia kisomo kikubwa sana kisomo ambacho kilifanywa kwa siku tatu, kisomo ambacho kilimfanya Jessenia aamini kuwa sasa amesha ondokana na lile Jini, lakini ukweli alikuwa anajidanganya, maana tatizo lilikuwa pale pale, na sasa ikafikia wakati Jessenia alianza kumtilia mashaka babu Mangeu, ambae ni jirani yao pale msingini…….. ENDELEA….
Ukweli licha ya kwamba Jessenia alipata ufahamu akiwa anamuona mzee Mangeu pale pale kwenye nyumba yao na wakazi wa msingini na mitaa ya Jirani, wakimshutumu kuwa mchawi kutokana na mtindo wa Maisha yake, ila kwa yeye mwanzo ilikuwa tofauti kidogo, siku zote alikuwa anamsalimia vizuri na kwa sauti iliyojaa upendo, wa babu kwa mjukuu, lakini Jessenia alianza kukaa mbali na babu huyu mwenye sura iliyo chongwa kitu chenye ncha kali, na kuwekea alama za kutisha, akiwa na umri wa miaka tisa na kuendelea, ni baada yakusikia shutuma nyingi za babu Mangeu, zikimuhusisha na ushirikina.
Miaka miwili baada ya tukio la pale Tibirinzi, na Jessenia kufanyiwa kisomo, ijumaa moja iliyoonyesha kuwa na shamra shamra za maandalizi ya vyakula maalumu, ambavyo mara nyingi huliwa siku za siku kuu, mfano pilau biryani na mapocho pocho mengine kama vile kaimati sambusa za nyama keki, na hata kashata na kachori, ni wazi kabisa kuwa kulikuwa na wageni walio tarajiwa, japo Jessenia hakuambiwa ni wageni gani ambao walikuwa wanaandaliwa chakula kile.
Ni kweli mida ya saa saba pale nyumbani kwao, walipata wageni sita, ambao kati yao palikuwa na wazee watu wazima wanne na vijana wawili, mmoja kati yao alikuwa ni mtanashati kwa muonekano, wake maana ukiachilia kanzu yake mpya pia hata Ngozi ya uso wake ilionekana kuwa na nuru, ambayo iliashiria kuwa kijana huyu ni mtu mwenye Maisha mazuri yenye uhakika wa kula leo kesho hata kesho kutwa, kwa kifupi alionekana kuwa ni kijana kama sio toka kwenye Maisha mazuri basi ni kijana mwenye uwezo mkubwa kifedha, japo kati ya hao sita ni huyo kijana pekee ndie alikuwa mgeni machoni pa Jessenia, ambae mara baada ya kumaliza kuwahudumia kwa chakula wageni wale, lakini mazungumzo yalipoanza tu yeye na shangazi yake waliondolewa pale sebuleni na kuwaacha wanaume peke yao, na baada ya kikao kufikia katikati ndio akaitwa yeye na shangazi yake, “binti yetu huyu hapa, kama nilivyo kueleza yeye ni mwanamke mwenye astaha, sio kiguu na njia, amelelewa katika maadili mema” alisema mjomba wake Jessenia, na hapo zikapita salam kwa mara ya pili, muda wote Jessenia na yule kijana mtanashati wakitazama kwa macho ya wizi, huku kijana yule akijitabasamulisha, Jesenia yeye alikuwa akiduwaa huku akijaribu kubashiri kitakachofuata baada ya hapo, muda wote Ussi alikuwa ametulia kimya anasikiliza toka kwa baba yake.
Naam mzee Juma Mohamed akamtazama Seni, “Seni hawa wageni unao waona ni kwaajili yako, ni kwamba huyu kijana (alisema mjomba huku anamuonyesha yule kijana mtanashati) anaitwa Mahadhi Idd Salum, baba yake ni balozi wetu huko #Mbogo_land, na yeye huko huko Mbogo Land, kama Engeneer msaidizi wa majengo makubwa na barabara, kwenye kampuni moja ambayo inamilikiwa na mtazania anae fanya shughuri zake nchini humo” hapo mjomba wake Jessenia, alitulia kidogo akimtazama Jessenia ambae alikuwa ameinamisha kichwa chini, hawakujuwa kama alikuwa anatabasamu, maana ni wazi alishaanza kuhisi nia na dhumuni la ugeni ule pale nyumbani kwao, “nia ya ujio wao nikwamba Mahadhi anahitaji kukuchumbia na kufunga ndoa na wewe kisha muondoke na kwenda kuishi Mbogo_Land” alisema mzee Juma Mohamed, pasipo kuweka bayana, moyoni Jessenia alikuwa anashangilia ushindi, japo hakupanga kuolewa ilimradi ameolewa, yani na mtu ambae hakuzoeana naewala kufahamiana nae vyema, lakini kwa sasa hakuwa na chaguo jingine zaidi ya kuolewa na kuhama hapa pemba, pengine angekaa mbali na hilo jini linalomwandama.
Kikapita kimya kifupi kila mmoja kama anasiliza kinachoendelea, mpaka mzee mmoja kati ya wale wageni, alipoamua kuweka sawa, “Jessenia binti yetu, maamuzi yako ni yapi, je umekubali kuchumbiwa na kijana wetu, huyu ni mpemba mwenzetu, japo amekaa sana huko nje” alisema yule mzee na wote wakakubaliana nae kwa kichwa, kabla hawajatulia kumsikiliza Jessenia atasemaje, “madhari wazazi wangu wamekupokea hapa nyumbani, basi nyie ni watu wema na mimi sina kipingamizi” alisema Jessenia ambae, kiukweli hakuwahi kutoka nje ya pemba toka kuzaliwa kwake.
Hapo watu walishikana mikono kama pongezi kwa kila kitu kwenda sawa, wale wageni waliagana huku wakipanga kufanya haraka sana kupangwa kwa mahali na kufanya harusi, ili wanandoa waondoke zao kueleka nchini kwao, huku nyuma walimuacha Jessenia akiwa amejifungia chumbani akiwaza na kuwazua jinsi atakavyoanza Maisha mapya na mume wake, “nitamzoea tu” aliwaza Jessenia, ambae aliwaacha mjomba na shangazi yake pamoja na Ussi wakijadiliana kitu, bila shaka ilikuwa ni kuhusu ugeni wa leo.
Lakini likatokea jambo la kushangaza kwa Jessenia siku ya pili, mida ya saa nne, wakati Jessenia alikiwa anatoka nyumbani kwao kuelekea mjini yaani chake kufanya manunuzi, ni pale aliposikia akiitwa na toka nyuma yake, “Jessenia, asalam alaykum” ilikuwa ni sauti ya mzee Mangeu, moyo wa Jessenia ulilipuka kwa mshtuko, maana sifa za mzee huyu hazikuwa nzuri sana, ni kuhusishwa na ushirikina na akizingatia yake ambayo yanawatokea wanaume ambao anatarajia kuingia nao katika mahusiano.
Mwanzo Jessenia alitaka kuondoka pasipo kumjibu mzee Mangeu, lakini Jessenia alipokumbuka kuwa alifanyiwa kisomo, akasimama na kugeuka, “walaykum salam babu” aliitikia Jessenia katika hali ya utulivu wa kujilazimisha, huku anamtazama mzee huyu, mwenye sura ya kushangaza, ambae alikuwa ameachia tabasamu pana, ambalo pasipo hofu ya kufanyiwa ulozi Jessenia angecheka kwa nguvu, baada yake akacheka kimoyo moyo, “hongera Seni, nasikia umepata mchumba na unaenda kuolewa, japo sina uhakika kama hilo litatimia” alisema babu Mangeu, huku tabasamu likiendelea kushamili usoni mwake.
Ukweli Jessenia alishtuka sana, maana ilikuwa na uhakika hakuna mtu ambae amemueleza mzee huyu juu ya kuchumbiwa kwake, na hata ile kauli yake ya kwamba “sina uhakika kama hilo litatimia” akamtazama mzee huyu kwa macho ya tahadhari, kisha akaondoka zake kuelekea mjini, huku njia nzima akiwaza kauli ya babu Mangeu.
Zilipita siku nne, ndipo ilipokuja taarifa ya kuletwa kwa barua ya uchumba kwaajili yake pale nyumbani kwao, toka kwa kijana Mahadhi Idd Salum, tukio ambalo lingefanyika siku inayofuata, yani jumamosi, tukio ambalo halikufanikiwa, maana siku ya pili ambayo ingekuwa siku ya tukio, ililetwa taarifa ya kifo cha Mahadhi ya kwamba alikutwa amekufa chumbani kwake asubuhi, muonekano wa mwili wake alikuwa amekauka na kubadilika rangi kuwa mweusi sana, ungesema alikufa siku kadhaa zilizopita, polisi pamoja na madaktari wamejaribu kufanya uchunguzi na kukosa kufahamu chanzo cha kifo hicho, ambacho kinafanana na vifo kadhaa ambavyo viliwahi kutokea siku za nyuma, ambavyo vilihusishwa na Imani ya kwamba waliuliwa na jini, ambalo liliwanyonya damu.
Lilikuwa ni pigo kubwa sana kwa Jessenia, alilia kwa uchungu mkubwa sana, sio kwamba alimpenda sana Mahadhi ila ukweli ni kwamba, alilia kwa kuona kuwa bado lile jini lina muandama, na kwamba Maisha yake yatakuwa ni ya bila kuolewa, aliyakumbuka maneno ya babu Mangeu, kwamba sina hakika kama hilo lita timia, ina maana yeye alikuwa anajuwa juu ya jini linalomsumbua, na kwanini ajuwe, maana ilikuwa ni siri ya familia, “lazima yeye ndie atakuwa anahusika juu ya hili” alisema Jessenia, akiwa anamueleza Mjomba wake, ambae alitumia busara kumzuwia Jessenia asiende kuongea na mzee Mangeu, “Seni, hebu achana nae, cha kufanya wewe jitahidi uwe mbali nae, si unaona jinsi wanajamii wanavyo mtenga kutokana na tabia yake ushirikina” alisema mzee Juma Mohammed, yani baba yake Ussi, na kufanikiwa kumshawishi mpwa wake.
Maisha yaliendelea sasa Jessenia alibadili muenendo wa Maisha yake, akianza kunywa wine kwa siri, ambazo alizipata kwa msaada wa binamu yake Ussi, ambae licha ya kuonekana kuwa anaswali lakini nyakati za usiku alikuwa anaenda Mess kwenye starehe, huku akibadili wanawake kila kukicha, pia Jessenia alikuwa anajaribu kwenda matembezi yeye mwenyewe ili kujiliwaza, na matembezi yake makubwa yalikuwa ni kule uwanjani, kwenye mpira wa kikapu, mchezo ambao alitokea kuupenda sana, vijana walimtongoza kila kukicha, iwe wenyeji na wageni pia, wote walijaribu bahati zao, japo yeye aliwakatalia, sio kwamba wote hakuwapenda, ila ukweli ni kwamba hakutaka kuwasababishia matatizo.
Miezi sita baadae kuna kijitabia kilianza kwa Ussi, akionyesha wazi kumtamani binamu yake, ambae alianza kumfanyia michezo yenye dalili za kimahaba, vitu ambavyo kutokana na ukame aliokuwa nao Jessenia alijikuta anataka kuangukia kwenye penzi la kaka binamu yake, kosa mzee Mangeu kuingilia kati, basi Ussi angekuwa ndie mwanaume wa kwanza kula kitumbua cha Jessenia, maana michezo yao ilifika pabaya, Ussi alifikia hatua ya kushika chuchu za dada yake na sehemu nyingine nyeti, kama vile kumtekenya na kumkumbatia kumbatia, vitendo ambavyo viliaza kumfanya Jessenia aanze kutamani tena ngono, lakini safari hii ikiwa ni ngono na kaka yake binamu, kilicho saidia mschana huyu asitanue miguu yake kirahisi na kupewa dudu ni mambo mawili, moja ni tabia ya binamu yake huyo kuwa mwingi na wa habari, yani alikuwa na wanawake wengi sana, ambao kila siku alikuwa anawabadilisha, pili alihofia kuwa endapo atajaribu kufanya hivyo, basi inaweza kupelekea kifo cha binamu yake huyo, siku moja ya jumamoss, mida ya saa kumi na mbili Jesseni akiwa anatoka zake Tenesi, kutazama mazoezi ya baskert ball, wakati anakaribia nyumbani kwao, mara akasimamishwa na mzee Mangeu, “Seni asalam alaykum” alisalimia Mangeu ambae ni kama alionekana amekasirishwa na jambo fulani, maana uso wake ulikuwa umekunjika kwa hasira na kuzidi kutisha, kutokana na muonekano wake wa zile kovu usoni mwake, ambazo vijana walikuwa wanaziita ngeu, Jessenia alimtazama yule mzee kwa jicho la hasira na kutaka kufungua geti ili aingie ndani, “sikiliza Seni, kiburi hakito kusaidia, na kwamba sishindwi kuingia humo ndani kukufuata, hasa pale ninapohitaji kuongea na wewe jambo muhimu, ingekuwa vyema kama utaniheshimu, nadhani unakumbuka, mara ya mwisho kuongea na wewe nilikumbai nini juu ya mchumba wako, alie toka #mbogo_land, na leo nakuambia jambo jingine, ole wako utembee na Ussi, kitakutokea kitu ambacho utakijutia Maisha yako yote” alisema Mangeu na kuondoka zake, akimuacha Jessenia anajiuliza kwa mshangao, “huyo mchawi amejuwaje kama kaka Ussi ananivizia” aliwaza Jessenia kwa shangao akiwa amesimama pale mlangoni.
Hata baadae alipoingia ndani alimkuta Ussi akiwa amekaa sebuleni anakunywa pombe nyingi sana, “karibu mrembo wangu, njoo tunywe pamoja wine yako hii hapa” kitu kile kilimshangaza sana Jessenia, sababu licha ya ulevi wake wa kila siku, lakini Ussi hakuwahi kuleta pombe pale nyumbani, “wewe unafanya nini hivyo, mjomba na shangazi wapo wapi?” aliuliza kwa sauti ya chini yenye mshangao, “wameenda Wete kulala huko, watarudi kesho jioni” alisema Ussi ambae alikuwa ameshaanza kulewa, “unasema kweli! hebu kwanza nikamuulize dada wa kazi” alisema Jessenia huku anaeleka upande wa jikoni, ambako alikuta vyakula vimeshaandaliwa vyote, lakini hakukuwa na mtu yeyote, “weweeee dada ameenda kwao kangagani, atarudi kesho asubuhi” alisema Ussi kwa sauti iliyochangamka, kama vile anashangilia ushindi fulani, moja kwa moja Jessenia akajuwa kuwa Ussi alikuwa ana lake jambo, maana sio kawaida yake kuwepo nyumbani mida ile, lazima angekuwa ameenda wawi.
Hapo Jessenia akapakuwa chakula, akala kabisa na kisha akajiunga na kaka yake binamu, kwa kuanza kunywa wine yake sambamba na binamu yake ambae, kila dakika alikuwa anazidi kulewa, wakati huo Jessenia, hakujuwa kuwa nia ya Ussi ni kula kitumbua chake, yeye alijiachia zake wakinywa pombe pamoja, huku wakiongea na kutaniana kama ilivyo mazoea ya tabia mpya waliyo kuwa wameianzisha, na leo walikuwa wawili tu ndani jumba lile kubwa la kifahari…… Itaendelea
 
Nimejisukuma na wheelchair yangu kuwai nafasi. Arosto ni hatari kwa afya wadau. Leo afadhali kashtua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom