KIFO CHA HAWARA (mkono wa jinni)
SEHEMU YA THERASINI NA NNE
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA THERASINI NA TATU: ” alipiga kelele Jessenia huku anikikumbatia kwa nguvu na niliona mwili wake ukikakamaa na kutetemeka, ndio wakati na mimi nilimwaga Watoto, huku na yeye akitulia huku wote tukihema juu juu kama tumemaliza mbio ndefu, nikamuona Jessenia analalia tumbo na kutanua miguu na mikono, nikaamua kutumia mbinu za jandoni, yaani kumfanyia kijimasaje kidogo, lakini kabla sijafanya hivyo nikasikia vishindo vya mtu toka koridoni, vikija usawa wa mlango wa chumba kile tulicho kuwepo mimi na Jessenia na kukoma pale mlangoni, nikatazama mlango nikaona kitasa kinanyongwa taratibu……. Endelea
Bahati nzuri mlango nilikuwa nimeufunga kwa ndani, hivyo mlango haukufunguka, nikamtazama Jessenia, yeye alikuwa bado amejilaza, damu zilizoganda zilionekana mpaka eneo la makalio yake, nikaanza kumfanyia massaje huku macho yangu yapo mlangoni, ambapo pia kulikuwa na suruali yenye mkanda wenye AGP yangu, ambayo tayari ilikuwa na mkebe wenye risasi kumi “asante….” Ilikuwa sauti nyororo ya kivivu, sambamba na kijicheko cha kivivu, wakati namkanda eneo la kiuno, “asante ya nini Jesse” nilimuuliza Jessenia, huku naendelea kumkanda na mcho yangu nime yaelekeza mlangoni, ambapo bado kitasa kilikuwa kinanyongwa taratibu kwa kurudia rudia, niwazi mtu huyo hakutaka tuliokuwa ndani tujuwe ujio wake.
Jessenia alitulia kidogo kama anafikiria ajibu nini, “hujuwi ulicho nifanyia Eric, ukweli mpaka sasa simian kilichotokea, hata hivyo umenipa furaha sana, nimesikia raha” alisema Jessenia kwa sauti ile ile ya kivivu iliyonyororeka na kuvutia, niwazi hakuwa anaelewa kinachoendelea, “mimi ndie napaswa kusema asante kwa kunipa nafasi ya pekee kuwa mwanaume wako wa kwanza, na pia kutimiza ndoto yangu ya kuwa na mwanamke mzuri kama nilivyo tamani siku zote katika Maisha yangu, hakika nitakupenda daima” nilimueleza Jessenia kwa sauti tulivu, ambavyo nilihakikisha haina dalili ya kwamba kuna kitu kinaendelea mangoni.
Hapo nikamuona Jessenia anageuka na kunitazama, “Eric nikweli utanioa na kuondoka na mimi kwenda bara?” aliuliza Jessenia, huku akishindwa kuendelea kunitazama usoni, na kurudi kulala kama alivyolala mwanzo, wakati huo nikasikia vishindo vikielekea nje na kukomea eneo la katikati, “yah! unadhani kuna mwanaume anaeweza kukuacha mwanamke mzuri na mrembo kama wewe” nilisema hivyo huku nasogeza mdomo kati kati ya mgongo wa Jessenia na kumkiss kidogo, halafu nikachukuwa simu yangu na kufanya kama naibofya hivi, “Eric hujajuwa kitu ambacho umekifanya ni kitu ambacho …….” Alisema Jessenia akishindwa kumaliza kuongea kwasababu mimi nilianza kuigiza naongea na simu, “hallow kaka” nilianza kuongea kwa sauti, huku mkono mmoja nikiendelea kumkanda Jessenia, mgongoni, “kaka niambie…..yah, bado nipo hapa, hapana sijaona mtu, labda kama yupo chumba kingine……poa poa nakusubiri, ok! kumbe upo nao, aina noma njooni mimi nipo hapa mtanikuta hapa” nilisema kwa sauti ya juu, huku nasikilizia nje, hapo nikasikia vishindo vya mtu akitoka nje, nikasogea dirishani na kusogeza panzia pembeni na kuchungulia, “vipi wakinani hao watakuja humu ndani” aliuliza Jessenia, huku na yeye anainuka kutazama dirishani, lakini kwa tahadhari kubwa, ambapo hakukaa sana na kujilaza kitandani, baada ya kuona kwamba hakuona chochote alicho kitarajia, akiniacha mimi nina tazama upande wa kulia, ambako niliweza kumuona mtu mmoja alievalia tofauti na yule wa mwanzo, ambae alivaa suruali ya jinsi, huyu alikuwa amevaa kapturah ya kaki na tishet jeusi chini alivalia sendo, akipita pembezoni mwa maua yaliyopandwa upande huo, nilijaribu kumtambua lakini nilishindwa, Zaidi niliweza kugundua kuwa jamaa huyu ni mmoja wa wale waliokuja mwanzo, maana na yeye alikuwa amebeba kijifuko cha plastic kama kile walichobeba wale wa mwanzo,
Naam hapo nilishaanza kuhisi jambo, fulani kwamba kuna jambo lilikusudiwa kufanyika ni jambo ambalo pengine hata Jessenia alifahamu, hivyo nilitakiwa kukabiliana na jambo hilo, nikiwa bila mwanamke huyu, “twende tukaoge” alisema Jessenia huku ananigusa dudu yangu ambayo bado ilikuwa imetulia kwa uchovu, “utaiamsha hiyo we shauri zako” nilimtania Jessenia, huku nashuka toka kitandani na kumshika mkono, ili nimuinue kitandani, nae akanipa mkono wake na kumtoa kitandani halafu nikamkumbatia, “nilitamani leo tulale wote” nilimuambia Jessenia kwa sauti tulivu, japo moyoni mwangu nilikuwa najuwa kuwa haiwezekani, “mh! Jamani si utaniuwa sasa yaani usiku kucha” alisema Jessenia, huku akitazama kitandani, ambapo palikuwa na doa kubwa la damu, “haaa! Sio hivyo, kulala pamoja sio kufanya mapenzi usiku kucha, kuna muda wa kunywa wine na muda wakuongea” nilifafanua, huku yeye anachomoka kwenda kutoa shuka kitandani, “hapa kambini kuna duka kubwa, tunapitia kununua shuka” alisema Jessenia, ambae alilitoa lile shuka na kulitupia pembeni, halafu akatandika lile moja lililobakia, halafu akatoa kanga moja kwenye mkoba wake na mimi nikajifunga tauro kiunoni, halafu tukaingia bafuni, ambako tulitumia nusu saa nzima, kwasababu kule bafuni hatukuweza kuacha ipite, nikutokana na vimichezo vidogo vidogo tulivyo vianzisha, tukajikuta tunapena dudu kwa mara nyingine.
Ilisha timia saa tisa, ndio muda tuliotoka bafuni, nikampigia simu Wasenga na kumuita aje pale Green House, nikijifanya nahitaji chupa mbili za maji, bahati nzuri alikuwa njiani anatoka Wawi mess kuwapeleka wale maafisa, ambao kule ndio kwenye makazi yao, “poa nakuja kaka dakika tano tu!” nilifanya hivyo makusudi, ili kama kuna mtu yoyote basi asiweze kufanya lolote, tulivaa taratibu huku tukifanyiana mizaha midogo midogo na kusaidiana kuvaa, ni kama Jessenia alisha juwa kinachokuja kutokea, maana alibeba nguo mbili mbili kwenye lile begi lake, safari hii alivaa gauni jepesi la pink, na juu akivaa baibui la kijivu na mtandio mweupe, na niqab ya pink, viatu vyake vikiwa ni vyeupe, na kingine kilicho nishangaza na kunivutia, nilimuona akipulizia manukato ya aina tatu, kila nguo ya mwilini mwake alipulizia maunukato yake, kuanzia chupi gauni la ndani na lile baibui, hakika alipendeza sana, ungesema kuwa alikuwa anaenda sehemu muhimu sana au kwenye mualiko mkubwa sana, usingesema kuwa ni mpemba wa hapa chake chake, ungesema ni mwarabu wa dubai au oman, hata mimi nilievaa suruali ya kaki na tishirt nyeusi, iliyonishika vyema na raba nyeusi miguuni mwangu.
Hapo nilijikuta na toa pongezi kwa kilie nilicho kiona, “jesse nilidhania kuwa wewe ni mzuri kwa jinsi nilivyokuona mwanzo, sasa nimegundua kuwa wewe ni mzuri Zaidi ya vile nilivyofikiria” nilimueleza Jessenia kwa sauti tulivu nikimaliza kwa kumikiss kwenye paji lake la uso, “asante” alijibu huku ananikumbatia, na wakati huo huo tukasikia gari likisimama nje ya nyumba, na yeye akashusha niqab yake usoni na tukatoka nje, ambako tulipokea maji kwa Mwasenga na tukaingia ndani ya gari tukiwa na chupa yetu ya wine na chakula chetu, ambacho Jessenia alikuja nacho, tayari alikuwa amechukuwa ile shuka iliyochafuka na sisi tukaenda upande wa geti kuu la kuingilia kambini, tukaingia kwaajili ya kuingia super market, ambamo tulinunua shuka na baadhi ya vitu ambavyo tuliviona vinafaa mimi ndie nilielipia.
Tulitoka pale dukani yaani kambini na kuelekea mjini, huku njiani tukinywa wine yetu na chakula chetu, huku tukiongea na kufanyiana michezo ya kimahaba, tuliranda randa mitaani huku tukiendelea kufurahi, muda mwingi Jessenia ambae alionekana mwenye tabasamu na kutokuamini kilichotokea, nilimuona ananitazama kwa macho fulani ya kunitafakari, kiasi cha kujiziuka kabisa, “mbona una nitazama hivyo Jesse?” kuna wakati niliamua kumuuliza, “hapana , kwani lazima kuwe na sababu mtu kumtazama mpenzi wake” alijibu Jessenia ambae akiwa ndani ya gari alikuwa ametoa ile niqab usoni mwake na mimi nilikuwa nimepandisha vioo mpaka juu.
Mida ya saa tatu usiku ndio mida ambayo nilimuacha Jessenia nyumbani kwao, na kumbuka alisisitiza kuwa nimpigie mara nitakapofika tonyumbani, “na usichelewe basi, sio ukakae huko Wawi mpaka wanawake wasio na haya wakutamani” alisema Jessenia, akionyesha wivu wa wazi kabisa, “usijali mamaaa, nikitoka hapa naelekea kambini” nilimjibu kwa sauti tulivu iliyojaa upendo, huku naingiza gia na kuondoka zangu, leo sikutaka kufanya kosa kama la jana, ambalo lilisababisha nivamiwe na Mangeu, hivyo niligeuza gari na kuondoka kwa haraka, lakini wakati namaliza makazi ya watu na kuingia kwenye kile kichaka cha kutokea barabarani.
Nikakumbuka kutazama kwenye Side Mirror, ambapo niliweza kumuona babu Mangeu akija mbio mbio kufuata upande ule niliokuwa naelekea mimi, niwazi alikuwa ananifuata, maana alikuwa anapunga mkono kunisimamisha, sikumjali na baada yake nilikanyaga mafuta kutokomea upande wa barabarani.
Njiani nikiwa naelekea Macho manne, nilikuwa na jaribu kuwaza ujio wa watu wale ambao, walikuwa wanachungulia pale Green House pasipo kujari kwamba lile ni kambi la jeshi, na swali kubwa ni kwamba kama lengo ni wivu kwanini walikuwa wanakuja kwa kuvizia, baada ya kuja wazi wazi na kumtoa Jessenia, sasa je wange nifanya nini endapo wangefanikiwa kuingia ndani, niliwaza sana pasipo kupata jibu.
Niliingia Wawi Messi na kuegesha gari pale maegesho, ambapo leo palikuwa na magari kama sita ya kiraia, likiwepo pamoja na lile gari la Ussi, na gari la saba lilikuwa ni lile la jeshi ambalo Mwasenga alisema kuwa yupo nalo zamu, ukwei nilitamani kuona jinsi Ussi atakavyo nitazama kwa hasira, ni kutokana na ule wivu wake uliofikia hatua ya kutuma watu wanifuatilie, nilishuka toka kwenye gari kisha nikalock milango ya gari na kwenda ndani ya ukumbi wa pale Messi, ambapo niliweza kuona watu wengi wakiwa wamezunguka meza zao, huku wakinywa na kufurahi kwa pamoja, leo watu walikuwa wengi kidogo tofauti na siku nyingine za kati kati ya week, lakini wengi walionekana kuwa ni askari na wafanyakazi wa serikalini, sikushangaa sana, maana zilikuwa ni tarehe za mwisho wa mwezi.
Nilitazama meza kadhaa, lakini sikumuona Mwasenga, zaidi niliwaona wakina Malambo na wenzake, yani wakina JC Luge, Komba na wengine, ambao walinipungia mkono kwa mbali, na mimi nikawapungia na kuendelea kutazama, mpaka nilipomuona Ussi ambae leo tofauti na siku nyingine alikuwa peke yake, ametandaza chupa kadhaa za pombe kali, alikuwa ananitazama kwa macho makali sana, macho yetu yalikutana nikaona vyema nijifanye sija yaona macho yake, hivyo nikampungia mkono, lakini yeye akakwepesha macho na kutazama meza yake na kuchukuwa simu iliyokuwa mezani, akaibofya na kuiweka sikioni ni wazi alikuwa anawasiliana na mtu, nikaachana nae na kuendelea kumtafuta Mwasenga, ambae nilimuona akiwa amekaa gizani kabisa,
na yule mwanamke askari aliesema kuwa ni mke wake, nikaanza kutembea kuifuata meza yao.
Lakini baada ya kupiga hatua kadhaa nikakumbuka kama kuna kitu nimekiona kwa Ussi, nikatazama tena kule alikokaa Ussi nikiwa na lengo la kumtazama yeye, nilimuona anaongea na simu kwa msisitizo huku anaonyesha mikono kwa vitendo na kugonga meza kwa hasira ya chini chini, lakini lengo langu halikuwa kumtazama anavyoongea, lengo langu lilikuwa ni kumtazama alivyovaa, ukweli alikuwa amevaa tishet jeusi na kaptura ya kaki, ni kama yule ambae alikuja pale Green house mara ya mwisho, mwili ulinisisimka, kwa kugundua kuwa ni Ussi ndie aliefika nyumbani kwangu mara tu baada ya kuondoka kwa wale vijana wake wawili. ……… Endelea
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA THELATHINI NA TANO
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI NA NNE: Lakini baada ya kupiga hatua kadhaa nikakumbuka kama kuna kitu nimekiona kwa Ussi, nikatazama tena kule alikokaa Ussi nikiwa na lengo la kumtazama yeye, nilimuona anaongea na simu kwa msisitizo huku anaonyesha mikono kwa vitendo na kugonga meza kwa hasira ya chini chini, lakini lengo langu halikuwa kumtazama anavyoongea, lengo langu lilikuwa ni kumtazama alivyovaa, ukweli alikuwa amevaa tishet jeusi na kaptura ya kaki, ni kama yule ambae alikuja pale Green house mara ya mwisho, mwili ulinisisimka, kwa kugundua kuwa ni Ussi ndie aliefika nyumbani kwangu mara tu baada ya kuondoka kwa wale vijana wake wawili. ………
Nilitembea mpaka nilipoifikia meza ya Mwasenga ambae aliponiona yeye na mke wake walinipokea kwa shangwe, “hongera shem” alisema yule mke wa mwesenga, huku wote wawili wakicheka, na mimi nikajikuta nacheka, hasa baada ya kuhisi wananipa hongera ya nini, “shem achana na hayo mambo, ila mimi sio mkaaji sana, naelekea camp” niliwaeleza wawili wale, lakini Mwasenga mwenyewe akanidaka juu juu, “haaa kaka toka umempata yule mtoto umeacha pombe kabisa” alitania Mwasenga na mke wake akaongeza, “tena tuna subiri kadi za harusi” hapo tukaachia kicheko, “nyie mnauhakika gani bwana, pengine ni Rafiki tu, si muna mjuwa yule mtoto alivyo mgumu” nilijaribu kupinga swala lile, “mh! Kwajinsi nilivyoona tule tumacho tunaona aibu, kaka ushafungua mlango, halafu ujuwe nini, kaka yake aliponiona tu Naingia hapa Messi akanifuata kuuliza upo wapi, nikamuambia kuwa umeenda mkoani kuna mzigo umeenda kuupokea” alisema Mwasenga na hapo tuka cheka kwa pamoja, na kwa bahati mbaya nikatazama kule alikokuwa Ussi, nikamuona ananikata jicho la hatari, muda huo alikuwa amesha maliza kuongea na simu, “jamani kaka anawivu yule utadhani anataka kumtomb..mwenyewe” alisema mke wa Mwasenga ambae tayari alikuwa amelewa kama mume wake, “kaa basi upate hata bia moja” alisema Mwasenga, maana bado nilikuwa nimesimama, “dah! ukweli sitoweza kukaa maana kesho mapema ninakipindi, nimekuja kuomba usafiri nikuachie gari lako, maana naona linazidi kunizowea” nilisema huku nacheka kidogo, huku moyoni nikipanga kuondoka haraka, maana sikuiamini ile simu ya Ussi, “shem huyu hatoki hapa, we nenda tu na gari, tena lipo jingine, la kwangu atatumia kama anahitaji kutumia gari, labda kama mafuta yamekushinda” alisema mke wa Mwasenga, ambae ni mdogo kidogo kwa umri ukilinganisha na sisi, “poa jamani basi wacha niondoke kesho tutakuwa pamoja” nilisema huku namgusa begani Mwasenga kisha nikaanza kutembea kuelekea nje, na wao wakiniaga juu kwa juu, “poa poa shem, kesho”.
Nilitoka nje na kuingia kwenye gari ambako nilikuta simu yangu inaita, nilipoitazama nikaona kuwa ni Jessenia alikuwa anapiga, kabla sijawasha gari nikaipokea simu kwanza, na kuiweka sikioni, “hallow mamaaa hujalala bado” niliongea kwa sauti nzito na tulivu, lakini ilidakwa juu kwa juu kwa kushusha pumzi ndefu, “jamani Eric, nitalalaje wakati bado hujaniambia kama umeshafika salama” alisema Jessenia huku akijitahidi kuficha hali aliyokuwa nayo wakati anapiga simu, “nani kasema nimefika ndio kwanza natoka wawi” niliamua kumueleza ukweli, “lakini weye, sa unafanya nini hapo si nimekuambia uwahi nyumbani Eric” ilikuwa ni sauti ya ukali kidogo, “ndio naenda mpenzi, wala usiwe na wasi wasi” nilisema kwa sauti ya kumbembeleza, “nenda ufike bwana, sio vyema kutembea usiku, unajuwa nina hofu kiasi gani juu yako, nikikupoteza wewe sitoweza kuishi Eric, mpaka sasa siamini kama….” alisema Jessenia na kusita ghafla, nikama kuna jambo alitaka kuliongea bila kutarajia, “huamini nini Jesse, unaweza kuniambia hutaki kunipoteza kivipi?” nilimuuliza Jessenia ambae kiukweli nilijuwa kuna jambo fulani analifahamu na anasita kuniambia, hapo nikamsikia akishusha pumzi ndefu, “Eric wewe ni muhimu sana kwangu tofauti na unavyo fikiria, naomba vuta subra tutaongea kesho” alisema Jessenia kwa sauti ambayo siwezi kusema ya kubembeleza ila kiukweli ilikuwa na kitu kama hisia kali sana, ni sauti ambayo ilionyesha wazi maneno iliyobeba yametoka moyoni, nilihisi kuwa sikustahili hadhi aliyonipa, “jambo gani hilo Jesse, unanipa hamu ya kusikia” nilimueleza Jeseenia ambae alicheka kidogo, ni kicheko cha kivivu, “Eric, usiwe na shaka ni muhimu kwako kusikia, ila naomba na wewe uniahidi jambo moja” alisema Jessenia, kwa sauti tulivu yenye msisitizo wa uhitaji wa kile alichosema, “nimesha kuahidi kabla hujaniambia, kwasababu sitoenda tofauti wala kukunyima kile ninachopaswa kukupa” nilimueleza Jessenia huku nawasha gari na kuingiza gia, kisha nikaondoa gari kuelekea barabarani pasipo kuwasha taa za gari, nilitegemea taa za nje ya ukumbi, “Eric, kwa chochote nitakacho kuambia naomba usiniache, hakika sitokuwa na mwanaume mwingine ambae anaweza kuchukuwa nafasi yako” aliongea Jessenia na hapo akanisisimua kidogo, ni kitu gani ambacho anaweza kuniambia na mimi nikakubali kumuacha mtoto mzuri kama huyu, au ndio maana alikuwa anawakatalia wanaume kila kukicha, kwamba kuna jambo ambalo linamfanya asiweze kuwa na mwanaume, “Jesse ondoa wazo hilo katika kichwa chako, kabla sijakupata nilishaondoa wazo la kukuacha sidhani kama unaweza kunifanyia kitu ambacho nitasema sasa basi” nilimueleza kwa sauti nzito tulivu, wakati nilikuwa naisogelea barabara kuu ya kuelekea vitongoji, nikawasha taa za gari maana sasa nilisha toka eneo la ukumbi, sasa basi ile washa taa nikashtuka kumuona babu Mangeu akiwa anakuja upande Messi, mwili ukasisimka, “Eric, sio tu nimebahatika kupata mwanaume aliezaliwa kwaajili yangu, ila pia nimepata mwanaume ambae anae niondolea furaha ya bandia na kupiatia furaha ya kweli” alisema Jessenia kwa sauti iliyojawa na furaha na kumalizia kwa kicheko cha aibu, ni kama maneno ya Jessenia siku yazingatia sana, maana nilikuwa na mtazama mzee huyu, ambae alikuwa anatembea kuelekea messi huku analitazama gari kwa umakini mkubwa, kama vile anajaribu kulitambua, hapo nikabofya kile kitufe cha kulock milango, simu ikiwa sikioni, Jessenia akianza kuita, “hallow! Hallow Eric unanisikia” alisema Jessenia kwa sauti fulani ambayo ungesema alidhania ninamfanyia msihara, japo mimi sikuwa katika utani nilikuwa na mtazama yule mzee kwa mshangao mkubwa, hakika nilijiuliza mzee amefikaje hapa Wawi kwa haraka namna hii, maana ukweli ni kwamba usiku kama huu, hakukuwa na usafiri wa aina yoyote wa jamii, zaidi ya magari na pikipiki binafsi, wakati huo nilikuwa natembea taratibu nikiisogelea barabara.
Naam ni kama machale yalinicheza kwa kulock milango ya gari, maana wakati nataka kuingia barabarani nikasikia mvumo wa piki piki, iliyokatika mwendo mkali sana, toka upande wa Macho manne ukijaupande huu wa wawi, nikalazimka kusimama ili pikipiki hiyo ambayo sasa nilianza kuona mwanga wake ikija kwa speed ipite kwanza ndipo niingie barabarani, sasa basi ile nasimama tu, nikasikia mlango wa kushoto wa abiria wa mbele ukikamatwa kitasa chake na kujaribiwa kufunguliwa, nikatazama kwa haraka kwenye mlango ule, nikamuona Mangeu anajaribu kufungu mlango, lakini mlango haukufunguka, bahati nzuri kwangu nilikuwa nimesha ulock, nikaona sasa vita imesha kuwa kubwa, na huyu babu anajambo lake kwa Jessenia, na inawezekana ikawa Jessenia ndie yule mwanamke anaeonekanaga kabla ya matukio ya mauwaji kutokea, hivyo nikasema nilazima nikutane na Jessenia haraka sana pengine ndio ikawa mwanzo nzuri wa upelelezi wangu, sikutaka kuhangaika na yule babu, ambae niliomba asije akatumia uchawi wake, kufungua mlango wa gari, nilitamani kukanyaga mafuta kuingia barabarani, lakini mbaya zaidi ile pikipiki tayari ilishakaribia na kupita kwa speed kari kuelekea upande wa vitongoji, sikuizingatia sana, na mimi nikakanyaga mafuta kuingia barabarani lakini baada ya kukata kona kulia kuelekea Vitongoji, nikakatakulia kuelekea macho manne, pasipo kumjali Mangeu, ambae alisimama akinitazama kwa mshangao, huku amejishika kiuno.
Nilikanyaga mafuta mengi kuelekea upande huo wa macho manne, lengo la kuelekea huko niliona kuwa nikienda moja kwa moja upande wa vitongoji lilipo kambi la Ali khamis nitampa nafasi babu Mangeu ya kunifuatilia mpaka ninakokaa, na kupata nafasi ya kunitumia jini lake linifanyie kazi ya kukausha damu yangu, na hapo ndipo nilipoona heri wivu wa Ussi kuliko hasira za Mangeu, “huyu mzee kwanini ana hasira juu ya Jesse?” nilijiuliza huku nazidi kukanyaga mafuta kuipita pikipiki moja ndogo aina ya Vesper mpya kabisa, ambayo ilikuwa imeegeshwa pembeni ya barabara pasipo mtu yoyote kusimama pembeni yake, ni mita chache toka kwenye barabara ya kuingilia pale Mess, wakati huo nilikuwa naiweka simu kwenye seat ya pembeni yaani ya abiria wa mbele.
Ukweli swala la kumkimbia mzee Mangeu sikutaka kumhusisha Mwasenga wala mtu yoyote mwingine, nilipanga nipambane nalo mimi mwenyewe, “lazima nikutane na Jessenia usiku huu, nijuwe kinachoendelea vinginevyo kabla ya jua kuchomoza nitakuwa nimesha ungana na wakina Vuai” niliwaza hivyo huku nikihisi kuwa pengine mimi kuna hatari kubwa mbele yangu, maana hata maneno ya Jessenia yalikuwa yana nishangaza, “hallow Eric upo salama kweli, hebu ongea basi nikusikie” ilinishtuliwa sauti ya Jessenia toka kwenye simu, sauti iliyokuwa katika wasi wasi mwingi, ndipo nilipokumbuka kuwa sikuwa nimekata simu, nikainyakuwa na kuiweka sikioni, “Jesse nipo njiani nakuja kwenu, naomba nikukute nje” nilisema na kukata simu na kuitupia tena kwenye seat, huku napunguza mwendo kuingia njia panda ya macho manne kuelekea chake, nikakata kona kuelekea upande wa chake, na kuunganisha na mafuta mengi.
Niliendesha gari mpaka kwenye kituo cha mafuta cha chake chake, ambapo nilisimamisha gari kwenye maegesho ya kituo hicho, ambacho palitawaliwa na giza kwa asilimia kubwa, pale kituoni nilimkuta mtu mmoja tu, ambae siwezi kusema kuwa alikuwa mlinzi, maana hakuwa na kitu chochote ambacho kingeweza kumtambulisha kuwa ni mlinzi, kuanzia mavazi mpaka silaha hakuwa nayo, “asalam alaykum kaka” nilisalimia nikiwa nimesha shuka, “walaykum salam kaka, lakini huduma tumefunga ni mpaka Kesho asubuhi” alisema yule jamaa, haikunishangaza sana, maana mji huu unaenda na muda, “samahani kaka lengo langu ni kuegesha gari kwa muda mfupi, kuna mtu anenda kumtazama mara moja hapo msingini nakuja sasa hivi” nilimueleza yule jamaa ambae hakuwa na kipingamizi, “hata ukitaka kulala mpaka asubuhi hapa ni salama kabisa” alisema yule jamaa, kisha na mimi nikajipapasa kama nilikuwa na vitu vyangu ambavyo naviamini, kama vile AGP na simu yangu, ambayo bado nilikuwa nimeiacha kwenye gari, nikafungua mlango na kuichukuwa, kisha nikafunga milango na kutoka kuelekea msingini, nikitumia njia ya mkato ambayo alinionyesha yule jamaa, wakati huo simu yangu ilikuwa inaita mfululizo, nilipotazama nikaona kuwa mpigaji alikuwa ni Jessenia, nikaipokea, “Eric, una nini lakini mbona wanitisha hivyo mwenzio” aliuliza Jessenia kwa sauti iliyojaa wasi wasi, “vipi umesha toka nje, mimi natembea kwa miguu nakuja kwenu” nilimueleza Jessenia kwa sauti kavu, isiyo ya kimapenzi wala kubembeleza” “nimetoka kwaajili yako, lakini natafuta matatizo kwa mjomba, maana nimetoka bila taarifa, nipo njia ya kueleka njia panda ila ungeniambia kwanza kuna nini” alisema Jessenia kwa sauti ya kubembeleza, “mimi natokea huku sheri, chake chake, nivyema kama ungekuja upande huu” nilimueleza Jessenia kwa sauti ile ile na yeye akakubaliana na mimi…… Haya sasa Eric anawindwa na mzee mangeu anawindwa na ussi pamoja na vijana wake, je watampata? ... Itaendelea