Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE
MTUNZI: Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA: sikuacha kutazama nje mara kwa mara kuona kama Jessenia alikuwa anaona kile ninacho kifanya mchezoni, nae nikamuona akiwa ananitazama, na mara kwa mara macho yetu yalikutana na yeye kutabasamu na kutazama chini kwa haraka ungesema pengine kuna kitu tulitoka kukifanya, hali ile ilinifanya nijihisi vizuri sana, niliona kama mazoezi yanachelewa kuisha, maana nilitamani kuondoka na Jessenia kwenye gari hili nililokuja nalo, pengine ningepata furasa ya kuwa karibu na mwanamke huyu, na pengine kuweza kufikisha ujumbe wangu kwake, lakini nilishtuka mida ambayo adhana ilisikika na sisi kusitisha mazoezi, ndipo nilipotazama pale alikuwepo Jessenia lakini sikumuona tena……ENDELEA……
Moyo wangu ulinyongea, hata hivyo nilijiandaa haraka na kuingia ndani ya gari, kisha nikaondoka kuelekea upande wa Markiti kama ujuavyo katika barabara hii kulikuwa na chochoro chache sana, hivyo ilikuwa kama nilivyotegemea, maana mita kama mia mbili toka msikitini yaani mwishoni mwa soko, nilimkuta Jessenia akiwa anatembea taratibu kuelekea upande wa barabara kuu ya wete kwenda mkoani, nadhani alisha gundua kuwa lile gari nilikuwa nalo mimi, maana alipoliona tu akasimama na kulisubiri huku analipungia mkono kuwa nisimame, na mimi nikafanya hivyo mara tu baada ya kumfikia, na yeye akafungua mlango na kuingia ndani ya gari, ikitangulia harufu nzuri ya perfume, “asalam alaykum Eric” alisalimia Jessenia, huku harufu nzuri ikitangulia na kujaa ndani ya gari, “walaykum salam, sikukuona wakati unaondoka” nilimueleza Jessenia, ambae alikuwa anajiweka vizuri kwenye seat kwa kukusanya gauni lake refu, lisibanwe na mlango atakapo ufunga, “nilionadoka mapema ili unikute njiani, sikutaka tuondoke wote maana wapemba wanamaneno sana, ni vyema hukuchelewa kuja, maana nataka unipeleke macho manne nipate urojo halafu utanirudisha, nyumba sivyo?” alisema Jessenia, huku anafunga mlango, huku mimi nikitazama jinsi makalio yake yalivyo enea kwenye seat ya gari ya mbele ya abiria, kwakifupi urojo ni aina fulani ya chakura ambacho kinafanana kiasi fulani na mtori, ila wenyewe unawekwa viungo vingi sana, hapo kabla nilikuwa na sikia tu lakini sikuwahi kuona wala kuonja, “ok! twenzentu vipi lakini kuhusu kuchelewa nyumbani, nilimuuliza Jessenia, nae akacheka kidogo, “wala usiwe na shaka, mwenye maneno ni Ussi lakini mjomba na shangazi wao wanasema kidogo yanaisha, lakini Ussi hata siku tatu anaongea hayo hayo” alisema Jessenia huku nikiondoa gari kueleka upande wa Macho manne.
Naam tukiwa tuna elekea Macho manne umbali wa kilomita nne toka Chake, nilitamani kuuliza juu ya yule babau Mangeu, lakini nilisita kwasababu nilikumbuka kuwa yule mzee alikuwa amejificha, hivyo Jessenia hakuwa amemuona, kwa maana hiyo ningekosa namna ya kuanza kuhoji nilicho kusudia kuhoji, hivyo nikapiga kimya na yeye akawa kimya anabonyeza bonyeza simu yake, kabla haja vunja ukimya, “Eric, vipi jana ulifika salama nyumbani?” aliuliza Jessenia huku anageuka kunitazama, kwa jicho fulani hivi lililojaa urafiki, jicho ambalo kama mtu mwingine asie fahamu angesema kuwa ni mpenzi wangu, jicho ambalo lilinisisimua, “nilifika salama kabisa” nilijibu kwa sauti tulivu na hapo wote tuka tabasamu, huku yeye akionekana kuona aibu, “nilitamani nikuulize kama umefika salama, lakini sikuwa na namba yako ya simu” alisema Jessenia huku anacheka cheka, “ok! kwahiyo itakuwa ni vyema nikikupatia sio?” nilimuuliza Jessenia, ambae alikubali mara moja, “sasa je kwani huoni itakuwa vizuri” alisema Jessenia, huku kicheko chake kikiwa kinaendelea, wakati huo nilikuwa na kata kona kuingia barabara ya Wawi, “haya andika hiyo namba” nilimueleza Jessenia na kuanza kumtajia namba za simu, ambayo aliisave alivyojuwa yeye.
Naam tulisimamisha gari pembeni ya barabara pale macho mane mtaani, ambapo palikuwa pamechangamka sana, watu walikuwa wanafanya biashara mbali mbali za vyakula vya kisiwani hapa, huku watu wengi zaidi wakiwa wana nunua vyakula vile, “ngoja nivae uninja” alisema Jessenia huku anajivesha niqab, mimi nika shuka na kuzunguka upande wake na kumfungulia mlango kama wazungu wanavyofanya, lakini ile Jessenia anatoka tu akanidaka mkono na kunishika kwa maana ya kutaka tutembee wote tukiwa tumeshikana mikono, haikuwa shida kwangu, hivyo tulitembea taratibu kusogelea meza za vyakula mbali mbali, kama vile urojo chips vireja, pweza kababu na kachori. Pia walikuwepo samaki wa kila aina.
Ukweli ilikuwa ni jioni ya aina yake tulipata vyakula ambavyo nilivipenda na kuvifurahia, tuliongea na kucheka kwa pamoja wakati mwingine tukila na kutaniana tukifanyiana michezo kama watoto, nilijikuta natumia masaa mawili mahali pale ambapo tuliondoka saa tatu kasoro kuelekea mjini, ambapo tuliingia msingini moja kwa moja mpaka nyumbabi kwa kina Jessenia, leo sikuwa na wasi wasi, kwasababu nilikuwa na gari, hivyo Mangeu asinge nitisha, “Eric hivi kwanini hujaja na mkeo nae aione Pemba?” aliuliza Jessenia ambae nadhani nilishawahi kumueleza kuwa sikuwa na mke, hata hivyo nikajifanya sikumbuki kama nilishawahi kumueleza juu ya hilo, “bado sija bahatika kuoa Jesse” nilimjibu kwa sauti tulivu uliyojaa upole, nikamuona Jessenia akitabasamu kidogo, “ni kweli Eric, sasa kwanini hujaoa mpaka leo?” aliuliza Jessenia huku akicheka cheka, nikaona hii ndiyo nafasi ya kujaribu kutupia neno kwa mwanamke huyu, “mh! swali lako ni zuri lakini jibu lake linaweza kukufanya uone nakutongoza” nilimueleza Jessenia, kwa sauti fulani tulivu yenye ukosefu wa uchangamfu, “madhari umeniambia sito kufikiria hivyo, we niambie tu” alisema Jessenia wakati huo tukiwa tumebakia ndani ya gari, huku nje ya geti la kuingilia ndani mwao, “kiukweli japo ni mapema sana, labda ungehitajika muda kuliweka wazi swala hili, ila ni kwamba hapo mwanzo sikuwa tayari kuoa ila sasa nimesha muona mwanamke ambae anaweza kuwa mke wangu, japo nahitaji msaada wako ili kufanikisha hili” nilisema hivyo kwa sauti tulivu kama mwanzo, lakini nilimuona Jessenia kama ananyongea na kuegemea seat ya gari, “nani huyo Aisha, lakini yeye tayari anamchumba” alisema Jessenia, kwa sauti iliyo tulia kidogo, “hapa sio Aisha ni wewe Jesse, sijui kama utanifikiriaje lakini ukweli ni kwamba ninakupenda…” kabla sijamaliza kuongea nikashangaa kuona mschana huyu akinishika kichwa changu na kunikivutia kwake, sikujuwa kama alikuwa anasogeza mdomo wake shavuni kwangu, maana nilipogeuka kumtazama, alichokuwa anataka kujifanya ghafla nikashtuka kuona midomo yetu ikikutana, ilikuwa ni ajari…… ITAENDELEA
 
Inaendelea lini ?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom