KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
NUMBER +255 743 632 247
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE: nilisema hivyo kwa sauti tulivu kama mwanzo, lakini nilimuona Jessenia kama ananyongea na na kuegemea seat ya gari, “nani huyo Aisha, lakini yeye tayari ana mchumba” alisema Jessenia kwa sauti iliyo tulia kidogo, “hapana sio Aisha ni wewe Jesse, sijui kama utanifikiriaje lakini ukweli ni kwamba ninakupenda…” kabla sijamaliza kuongea nikashangaa kuona mschana huyu akinishika kichwa changu na kunikivutia kwake, sikujuwa kama alikuwa anasogeza mdomo wake shavuni kwangu, maana nilipogeuka kumtazama, alichokuwa anataka kujifanya ghafla nikashtuka kuona midomo yetu ikikutana ilikuwa ni ajari……ENDELEA….
Nikamuona Jessenia anatoa midomo yake kwa haraka huku anacheka chini chini na kutazama chini kwa aibu, “lione kwanza nani amekuambia ugeuke mwenzio nilitaka nikuchum shavuni” alisema Jessenia kwa sauti iliyojaa aibu na kuambatana na kicheko cha chini, huku akiziba uso wake kwa vidole vyake laini, “hooo! samahani hata sikujuwa kama unataka kufanya hivyo, ila asante sana” nilimuambia Jessenia kwa sauti nzito na tulivu, huku nikijaribu kupeleka mkono wangu kwenye mgongo wake na kulaza kiganja changu mgongoni hapo, kisha nikaanza kafanya kama nampapasa kwa kumpooza fulani, nikamuona kama anatetemeka kwa kusisimkwa, huku akiachia kijicheko cha aibu, “kwanini usema samahani si umesema unanipenda” alisema Jessenia huku akiwa bado ameziba uso wake kwa viganja vya mikoni yake.
Ukweli kwa kauli hiyo mwili ulinisisimka sana, maana ilionyesha wazi kuwa amekubali niwe mpenzi wake, unajuwa kwa uzuri na sifa za Jessenia, na kwa habari nilizo zipata kwamba ame wanyima penzi lake watu wakubwa wenye uwezo mkubwa wa kifedha na muonekano wa kitanashati, kama vile wakina Malambo na vijana wengi sana hapa kisiwani, inakuwaje mimi nimpate kirahisi namna hii, “Jesse inamaana umekubali kuwa na..?” niliuliza kwa sauti ile ile tulivu na nzito, huku naendelea kumpapasa mgongo wake na kabla sijamaliza kuuliza nikamuona anaitikia kwa kichwa.
Ukweli sikuamini macho na msikio yangu, nika panga kujiridhisha kwa kufanya jambo fulani ambalo lita nihakikishia ushindi wangu juu ya mrembo huyu, hivyo nikamshika kidevu chake taratibu kwa vidole viwili na taratibu nika ugeuzia uso wake upande wangu, nikamuona na yeye anajilegeza na kugeuka kwangu, huku anaonda viganja vyake usoni mwake, na kujaribu kunitazama kwa macho yake ambayo ghafla niliyaona yamekuwa ya kilevi yaani yamelegea kama vile ana usingizi, huku midomo yake ikionyesha tabasamu laini.
Hapo nikaona kuwa Jessenia alikuwa anasubiri kuona nitafanya nini, hapo kwa kutegea ili nione atanizuia au ataniachia, nikasogeza uso wangu taratibubu kuusogelea uso wake, huku nikimtazama usoni kwa macho yaliyojaa ushawishi, nikamuona na yeye akiwa anashindwa kunitazama na kufumba macho yake, huku analegeza midomo yake mizuri na mimi nikagusanisha midomo yetu na kukiss, halafu nikamtazama kuona kama amechukuliaje swala lile, nikamuona anafumbua macho yake legevu na kunitazama usoni, hakuweza kufanya hivyo hata kwa sekunde mbili, nikamuona ana tazama pembeni, na hapo nikamuwahi tena na kumgeuzia kwangu, kisha nikasogeza mdomo wangu kwenye mdomo wake ambao ulikuwa umefumba, nadhania alidhania nitamkiss kama mwanzo, lakini safari hii nililamba midomo yake nikamuona ametulia, nikamlamba tena safari hii midomo ya chini hapo nikamuona anailegeza midomo yake na kufutia kitu ambacho kilinifanya nijihisi nipo ndotoni, maana tulianza kunyonyana ndimi zetu taratibu, huku Jessenia akiamishia mikono yake kwenye mabega yangu na kunibana kwake ni kama hakuhitaji kitendo kile kiishe mapema, kitu ambacho hata mimi nilikipenda sana, japo kilinipa wakati mgumu kwa maungo yangu ya siri, yaani ya kiume, maana yalianza kuinuka na kujitutumia vibaya sana.
Ukweli katika jambo kubwa na muhimu kama hili huwa sifanyagi makosa, bila kutarajia nilikuta na shusha mikono yangu mpaka kiunoni kwa Jessenia na kuanza kutembeza viganja vyagu taratibu kwenye kiuno cha mschana huyu, ambae japo midomo yetu ilikuwa imekutana inafanya jambo, lakini nilimuona anajinyonga nyonga kutokana na mtekenyo wa viganja vyangu kiunoni mwake, huku akiendelea kuhema juu juu.
Ni kama wote wawili tulizama kwenye ule mchezo na kuufurahia, hasa nilipoanza kumsikia Jessenia akihema kwa pumzi nzito nzito na kuzidi kulegea, sijui nilikuwa nawaza nini, maana nilipoona muitikio nikazungusha mkono wangu wa kushoto kwenye paja lake la kulia, huku mkono wangu wa kulia nikileleta nyuma ya shingo yake karibu na kisogo, nikiupenyeza ndani ya hijab yake na kuanza kuchezea eneo hilo katikati ya shingo na kisogo, nikamuona anaacha kunyonya ulimi na kulegeza midomo yake huku pumzi zake zikitokea mdomoni, macho ameyafumba kuyalegeza.
Mpaka hapo sikuwa naamini macho yangu maana niliona kuwa mambo yameenda haraka sana tofauti na nilivyo tegemea au kuwahi kusikia sifa, tabia na uwezo wa mschana huyu mrembo ambae sio kwa pemba hata mikoa ya Tanzania bara ukiachilia nchi ambazo niliwahi kutembelea ambazo siwezi kusema kuwa sikuwahi kuona mwanamke mrembo ila kiukweli kwa macho yangu Jessenia aliwazidi kwa vitu vingi sana.
Sikuacha kuchezea sehemu ya kisogo chake ila niliamishia mdomo wangu kwenye shingo lake, na mkono wangu wa kushoto nikauaminishia kwenye ziwa lake la kulia na kuanza kulipapasa nikiitafuta chuchu, ni kama Jseenia aligundua jambo hilo, nikamuona ana kiweka sawa kifua chake na kujigeuzia upande wangu vizuri zaidi, na hapo nikaipata chuchu ya mwanamke ambayo licha ya kwamba ilikuwa ndani ya baibui lakini bado niliweza kuipata na kuihisi usimamaji wake.
Nilifanya mambo kwa kasi ungesema nilipania kugusa kila kitu chake kwa muda ule mfupi nilioupata mule ndani ya gari dogo, nilipekecha chuchu taratibu huku naendelea kupapa kisogo chake chenye nywele laini na ndefu kama mkia wa farasi, sikuacha kumnyonya shingo yake taratibu na kwa ufundi mkubwa sana, na sasa nilimuona Jessenia anaanza kutoa miguno ya kama ananung’unika kwa utamu, kuna kipindi nikama alikolezwa na jambo lile, nikamuona anajileta mzima mzima juu ya kifua changu na kunikumbatia kwa nguvu huku anajaribu kupapasa kifua changu, lakini ile anahangaika kupapasa kifua changu ndipo akajirudiasha nyuma kidogo na mgongo wake ukagusa stearing (msikanio wa gari).
Naam kilichofuatia hapo ni mlio mkubwa na mkali wa honi, uliosikika kwa sekunde mbili nzima na wote tukashtuka, na hapo ni kama Jessenia alizinduka toka kwenye wenge la mahaba, unajuwa kwanini nasema hivyo, kwa sababu ni kwamba mara baada ya kushtuka nakujitoa kifuani kwangu, nikamwluona Jessenia akiwa amejawa na hofu kubwa sana akageuka pande zote akitazama kushoto na kulia, mbele na nyuma, kama vile anahisi kuna mtu anatutazama, hofu ya wazi ikiwa imemtawala, na mimi nikamsaidia kutazama, ukweli hakukuwa na mtu, yoyote eneo lilile, hapo nikadhania kuwa Jessenia angetulia na sisi kuendelea na kamchezo ketu ambako sikujuwa mwisho wake ungekuwa nini,
Lakini ilikuwa tofauti kabisa na nilivyo waza, nilimuona Jessenia akinitazama kwa macho yaliyojaa hofu na umakini mkubwa, alinitazama kuanzia usoni mpaka kifuani, nikama alikuwa anakagua jambo fulani kwenye mwili wangu, ni kama hakuamini kilichotokea wakati ule, ukweli sikumuelewa, ili nishangaza sana wakati najiuliza kama tutaendelea au laa, nikamuona Jessenia akishika kitasa na kufungua mlango wa gari akatoka nje na kulifuata gate la nyumba yao kwa mwendo wa haraka sana, na alipolifikia akasukuma gate dogo, ambalo lilifungukaa na yeye kungia ndani na kufunga lile gate, muda wote huo ile hali ya wasi wasi haikumtoka.
Nilihisi kuwa Jessenia alikuwa anamuogopa mjomba wake, na bila kumsahau binamu yake ambae alikuwa na wivu mkubwa sana juu yake, nilihisi mambo mawili yana weza kutokea, kama sio mwisho wa urafiki wetu kwa urafi wa kula kitumbua nilio uonyesha, basi Jessenia mwenyewe amegundua kuwa alionyesha udhaifu mkubwa mbele yangu, “dah! nimelikoroga” nilijisema moyoni, na hapo ndipo nilikumbuka kuwa nipo mtaani kwa watu, nikatazama muda kwenye saa ya gari ilishatimia saa tatu za usiku, nikaingiza gia ya kurudi nyuma ili kutafuta sehemu ya kugeuzia, ambayo kwa haraka nilifikiria ile njia ya kuingilia kwenye ile nyumba ya udongo, nilirudi taratibu huku nikiwaza kilicho tokea, na wakati nakaribia ile njia ya kuingila kwenye eneo lile mara nikamuona mzee Mangeu akiwa amesimama kwenye ile njia huku analitazama gari, lakini nilipata wazo la kwamba hata kama alikuwa amekaa pale kwa muda mrefu akilitazama gari, asingeweza kuona kilicho kuwa kinaendelea ndani ya gari kutokana na giza lililokuwepo.
Hapo ndipo nilipohisi kuwa ule wasi wasi wa Jessenia ulikuwa ni wa kumuogopa huyu mzee, ndio akaamua kuondoka bila kunisemesha kitu, swali likaja ni kwanini mtoto wa tajiri kama huyu amuogope babu kama huyu, ambae ana maisha duni sana, au alikuwa ana tabia ya kusema kwa mjomba wake Jessenia, sikutaka sana kujiuliza hivyo nilituliza akili kidogo, japo nilikuwa na wasi wasi na mzee huyu, ambae ni kama alishajuwa kuwa nataka nigeuzie gari pale aliposimama, maana nilimuona akisogea pembeni kama vile ananipisha, ukweli japo usoni mwake alipondeka pondeka kwa yale makovu yake makubwa, lakini niliweza kuona dalili ya kuwa hakuwa na mpango wowote na mimi.
Lakini wazo langu lilikuwa tofauti kabisa, maana ile namaliza kuingia kwenye kile kijinjia na kukata kona, niskashtuka mlango wa abiria wa kushoto kwangu, yaani ule alioshuka Jessenia unafunguliwa kwa haraka na yule mzee akaingia ndani, nilikuwa nimefanya kosa kubwa sana sikuwa nimelock ule mlango, nikanyoosha mkono wangu kwa haraka kwenye begi langu ambalo lilikuwa na bastola lilikuwa seat ya nyuma, lakini sikulifikia maana lilikuwa mbali kidogo, nikamtazama yule mzee Mangeu ili nione uwezekano wa kumkabili kwa mikono mitupu, huku hofu yangu ikiwa ni kama atatumia uchawi na majini yake…….. INAENDELEA
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA THELATHINI
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
NUMBER +255 743 632 247
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA: Lakini wazo langu lilikuwa tofauti kabisa, maana ile namaliza kuingia kwenye kile kijinjia na kukata kona, niskashtuka mlango wa abiria wa kushoto kwangu, yaani ule alioshuka Jessenia unafunguliwa kwa haraka na yule mzee akaingia ndani, nilikuwa nimefanya kosa kubwa sana sikuwa nimelock ule mlango, nikanyoosha mkono wangu kwa haraka kwenye begi langu ambalo lilikuwa na bastola lilikuwa seat ya nyuma, lakini sikulifikia maana lilikuwa mbali kidogo, nikamtazama yule mzee Mangeu ili nione uwezekano wa kumkabili kwa mikono mitupu, huku hofu yangu ikiwa ni kama atatumia uchawi na majini yake …….. ENDELEA NAYO….
lakini nikamuona mzee huyu hakuwa na dalili yoyote ya kunishambulia, zaidi alinitazama kwa macho makali ya kuogofya, “endesha gari ukaniache hapo barabarani, kuna jambo nahitaji kuongea na wewe” alisema mzee Mangeu, kwa sauti yenye lafudhi ya kipemba, ambae hakuonyesha wasi wasi wowote na wala hakuwa na tahadhari yoyote juu yangu, kwamba ningeweza kumshambulia muda ule, hivyo niliamini kuwa anajivunia uchawi na majini yake.
Nikatii amri ya mzee yule pasipo kushurutishwa, hivyo nikaingiza gia ya kuondokea na kuondoa gari kuelekea kule alikosema, huku nikiwa na wazo fulani kichwani mwangu, moja ni kitu gani mzee huyu anataka kufanya kwangu au kuniambia, na kama kuna jambo la hatari anataka kunifanyia nitamkabili vipi, maana mpaka sasa sikuwa najuwa atanikabiri kwa njia ipi na ana uwezo gani katika njia yake ya kunikabili. hata hivyo nikaona itakuwa vyema nikianza kupima uzito wa kile anacho kusudia kunifanya, japo hisia zangu zilikuwa kwamba nakabiliana na kile kilicho wakuta wanaume wengi sana, wakiwepo Vuai na Abdulqadir, “utaratibu wako wa kuomba lift sijaupenda mzee siku nyingine utahatarisha maisha yako” nilisema huku naficha hali ya uoga niliyokuwa nayo, “nimependa ujasiri wako, hivi ni kweli wewe mwalimu au umekuja kwaajili ya upelelezi wa uchaguzi?” aliuliza babu Mangeu, kwa sauti tulivu kabisa yenye lafudhi ile ile ya kipemba, nilishtuka kidogo kusikia vile, lakini nilijikaza kidogo na kujifanya nacheka kidogo, “mzee kwani nafanana na hao watu unao sema?” niliuliza huku namtazama mzee Mangeu, ambae hakuwa na dalili ya kucheka wala kutabasamu, huku gari linaenda taratibu, kichwani nikipanga namna ya kujipapatua kwenye ambushi litakao tokea muda wowote, “kijana sihitaji kulijuwa hilo, cha msingi ni kwamba, wewe hapa pemba ni mgeni, hivyo tafadhari achana na watoto wa watu, unaweza usitimize malengo yako na ukajikuta una rudishwa kwenu kama mzigo” alisema yule mzee pasipo dalili ya utani wala urafiki, “mzee unamzungumzia Jesse?” nilimuuliza yule mzee nikijifanya sijajuwa anamzungumzia nani, “kijana sidhani kama huu ni muda wa ngonjera, cha msingi kaa mbali na Seni, simama unishushe” alisema yule mzee na hapo nikaona afadhari, nikakanyaga brack na kusimamisha gari, tayari tulikuwa njia panda.
Naam yule mzee akashuka na kufunga mlango wa gari nikaondoka zangu, huku nikimtazama kwenye side mirror na kumuona anatembea kurudi alikotoka, niliingia barabara kuu na kukanyaga mafuta kuelekea macho Manne, niliendesha gari kwa speed huku nikitafakari maneno ya mzee Mangeu, huku kichwani mwangu nikivuta kumbuku mbuku ya kile ambacho kilitokea kati yangu na Jessenia ndani ya gari pale nyumbani kwao, nilipofika macho Manne ambapo sasa watu walishaanza kupungua, nikaingia barabara ya Wawi, na kukanyaga mafuta kulekea Wawi Messi, ambapo niliegesha gari kwenye maegesho ya magari ambapo kama kawaida palikuwa na magari machache sana, na Leo palikuwa na amercan Jeep ambalo ni jipya kabisa, na lile gari la jeshi analo endeshaga Mwasenga, pia kulikuwa na gari nyingine mbili za kiraia, ambazo nazo zilionekana kuwa katika hali fulani ya upya, unajuwa magari mengi ya huku yanaonekana mapya kwasababu ya kwamba haya tembei umbali mrefu sana kama ilivyo Tanzania bara, gari la Ussi lile Toyota land cruise V8 sikuliona, nilishuka toka kwenye gari na kuelekea ndani nikiwa nimevalia truck na tishert, begi nililiacha kwenye gari, nilipoingia ndani ya ukumbi ambako kulikuwa na watu wengi wakicheza music, nikatazama upande ambao mala zote Mwasenga huwa anakaa, cha kwanza kuona ni kijana Ussi akiwa amekaa kwenye meza yake sehemu ile ile ambayo anapenda kukaa, akiwa na mwanamke mmoja mwenye muonekano wa kisasa, kutokana na suruali ya kubana na tishet pana aliyoivaa, huku wamesambaza bia mezani walizokuwa wanazifakamia kama vile hakuna kesho.
Sikuwajari sana, nikatazama meza ya tatu toka pale alipokuwepo kijana Ussi, ambapo mara zote Mwasenga hukaa, nikamwona yeye na wengine watatu, yaani walikuwa wanaume wawili na wanawake wawili, nao walikuwa wanakunywa bia zao, nikaisogelea ile meza huku napanga jibu la kumpa Mwasenga ambae nilimcheleweshea gari lake, “hooooo! Ticha, karibu kaka mbona umechelewa sana, inamaana hujaenda hata Camp?” aliniuliza Mwasenga ambae kiukweli ni jamaa mchangamfu sana, “kaka nilipata dharula Ticha Aisha aliniomba nimpeleke mchanga hujuma, aliitwa mara moja, hivi sasa ndio tunarudi” nilijitetea huku nawatazama wale wengine kwenye meza, ambao walikuwa ni wageni usoni mwangu, “dah pole kwa uchovu, sasa si utakaa kidogo upate wine unayoipenda toka #mbogo_land” alisema Mwasenga, huku anatazama kushoto na kulia kama angeona kiti ambacho hakikuwa na mtu, na kabla hajakiona nikamuwahi, “usihangaike Bro, mimi sio mkaaji, labla ningepata msaada wa kufika camp nikapumzike” nilimueleza Mwasenga nae akanielewa, “gari si unalo, we nenda nalo mimi nitalikuta kesho, ila kabla hujaondoka ngoja kwanza nikutamburishe kwa shemeji yako, ameingia leo toka dar” alisema Mwasenga huku ananionyesha mmoja kati ya wale wanawake wawili, ambae pia ni mwanajeshi mwenzie, na pia akanitambulisha kwa wale wengine, baada ya hapo wakaninunulia wine chupa moja ambayo nilitaka kuikataa, kwa sababu moja nilikuwa na chupa moja kule camp ambayo sikuwa nimeifungua.
Niliondoka pale Wawi huku nikianza kuwaza upya kuhusu mambo mawili yaliyonikuta jioni ya leo, siku yazingatia sana maneno ya mzee Mangeu, zaidi nilijaribu kutafakari kuhusu Jessenia, ambae kuachana kwetu sikuweza kukuelewa kama tutaendelea kuwa pamoja au la, niliwaza hayo hata wakati nilipofika camp na kumaliza kuoga na kuingia kitandani, ndipo niliposhika simu yangu, kuangalia kama kuna chochote, maana yalisha pita masaa kadhaa bila kuitazama simu hii.
Naam nilishtuka kwa nilichokikuta kwenye simu, ilikuwa ni sms ambayo ilitumwa kwa namba ngeni, sms ambayo ilinifanya nitabasamu, “Eric upo salama?” nilijisikia raha sana hasa nilipohisi kuwa mtumaji alikuwa ni nani, na alikuwa ametuma ujumbe ule nusu saa iliyopita, maana ilikuwa imetumwa kwa namba fulani ya mtandao wa simu wa hapa hapa kisiwani, “samahani hii namba ni ngeni je wewe ni nani?” niliandika hivyo na kuituma kwa mtumaji yule ambae nilijifanya sijamtambua, nikatulia na kusubiri jibu, ambalo halikutumia ahta sekunde tano, sio kuwa uliingia ujumbe, hapana simu yangu ilianza kuita, nilipotazama ilikuwa ni namba ile ile mpya, nikaipokea na kuiweka sikioni, “hallow Eric, upo salama…. Nina maana umefika salama nyumbani?” ilikuwa ni sauti fulani ambayo sio tu naweza kusema tulivu, ila ni utulivu wa kulazimiasha, utulivu ambao ulimezwa na pumzi ya hofu na wasi wasi, nilianza kuhisi kuwa pengine Jessenia aliona nikivamiwa na babu Mangeu, “Jesse kwanini una wasi wasi juu yangu” nilimuuliza Jessenia, kwa sauti tulivu yenye mshangao ndani yake, “hapana Eric, kwani ni vibaya mimi kujuwa kama umefika salama au la?” aliuliza Jessenia, huku sauti yake ikiwa bado kwenye mashaka fulani, “sio vibaya, lakini…” kabla sijamaliza kueleza nilichotaka na yeye akadakia, “kama ni hivyo ni sawa, basi nitakupigia baadae” alisema na kukata simu, na kuniacha nikiwa katika hali ya mshangao, nilitamani kumpigia tena, lakini nilisita kidogo, nikichelea kuonekana nina haraka sana.
Hapo nilisave ile namba kwa jina la Sweet Jesse, na kuiweka simu pembeni na kuanza kusaka usingizi, na wakati nasaka usingizi nikajikuta naanza kuwaza tena juu ya kilichotokea, hasa inawezekana vipi mzee Mangeu aje anipe onyo juu ya Jessenia, ina maana yeye amepewa kazi ya kumlinda huyu mschana ambae hajawahi kuiona sura ya mama yake na wala hamjuwi baba yake, au Jessenia ndie yule mwanamke ambae nilimuona akiwa na Vuai masaa machache kabla ya kifo chake, na kwamba ulinzi wa huyu babu ambae anaishi jirani na tajiri mjomba wake Jessenia ndie anaehusika na mauwaji hayo, na kama hivyo ina maana Jessenia anafahamu juu ya hilo, mbona alionyesha wasi wasi mkubwa hata alipopiga simu bado alionyesha wasi wasi akiulizia usalama wangu.
Niliwaza hayo mpaka saa sita kasoro, nilipopokea simu toka kwa Jessenia ambae kama kawaida aliuliza kama nipo salama, “kwanini unauliza hivyo Jesse, si tumetoka kuongea usiku huu?” nilimuuliza lakini hakutoa jibu nililohitaji, “ok! Kesho asubuhi usiende kazini kabla hujanipigia” alisema Jessenia kwa sauti yenye mtindo wa amri japo ililegea kidogo na kukata simu, nilibakia nimetoa macho kwa mshangao, kwa sababu sikuelewa maana ya mschana huyu, ambae nilitamani nipate japo muda kidogo nionje kitumbua chake, japo nilishapewa onyo na mzee Mangeu, “kwanini anapiga simu mara kwa mara kuniulizia kama nipo salama au ndio aina ya mapenzi yake, maana kama angekuwa hanipendi asinge nipigia pigia” nilijiwazia mwenyewe, mwisho nililala na maswali mengi sana, nikitarajia kupata majibu kesho jioni endapo nitakutana na Jessenia kule mazoezini.
Sikumbuki muda ambao nilipitiwa na usingizi, ila nakumbuka mida ambayo nilishtuliwa na mtu alie kuwa anagonga mlango, nilikurupuka kitandani na kutazama dirishani, ambako mwanga wa jua ulikuwa umeshatanda kuonyesha kuwa kulisha pambazuka masaa kadhaa yaliyopita, “dah! Nimechelewa kazini” nilijisema kwa sauti ya chini, huku nachukuwa simu yangu kutazama muda, huku mlango ukiendelea kugongwa, licha ya kuona muda kwenye simu kwamba ni saa moja na robo, pia kulikua na missed call nyingi sana, kutoka kwa Jessenia na mwalimu Aisha, sikuhangaika nazo, nikainuka haraka na kuufuata mlango, nikaufungua na kukutana uso kwa uso na Mwasenga, “kaka vipi naona umelala sana, ni ile wine nini?” aliuliza Mwasenga huku anaingia ndani, “wine wapi kaka, sema nilichelewa sana kulala, yaani dah! hata sielewi imekuwaje” nilisema hivyo huku nachukuwa mswaki na taulo na kuelekea bafuni, nikimuacha Mwasenga akiwa ananisubiri.
Nilioga haraka na kupiga mswaki kisha nikiwa navaa tukawa tunaongea na mwasenga, “sasa kaka leo nipo zamu ya kuendesha gari, nadhani unaweza kulitumia gari langu katika safari zako za jioni” alisema Mwasenga, na kweli niliona itakuwa afadhari, hasa kwa usalama wangu wa kumuepuka mzee Mangeu endapo nitalazimika tena kwenda nyumbani kwa kina Jessenia, “haina noma kaka, wacha kwanza niwahi shule maana dah! Nimechelewa kweli kweli” nilimueleza Mwasenga ambae pia bahati nzuri hakuwa mkaaji sana.
Saa mbili kasoro ilinikuta nikiingia pale shuleni, ambapo nilikuta wanafunzi wakiingia madarasani, “we mwanaume kwanini hupokei simu lakini weye?” aliuliza mwalimu Aisha mara tu baada ya kukutana nae karibu na mlango wa ofisi ya staff, “nilikuwa nimelala, vipi ulikuwa na inshu yoyote?” nilimuuliza Aisha ambae pia alinitisha kidogo, maana bado nilikuwa nakumbuka kuhusu jana usiku nilipovamiwa kwenye gari na babu Mangeu, nilihisi labda na yeye anataka kunionya nikae mbali na Jessenia, “we huoni kama umechelewa, halafu unakaa hapo pua na mdomo na shule halafu unachelewa kufika kazini” alisema Aisha huku tunaingia ofisini.
Naam nakumbuka mida fulani nikiwa ofisini na mwalimu Aisha ameenda kufundisha darasani, ndipo nilipoamua kutuma sms kwa Jessenia, ambae nilikuta messed call yake moja tu, nyingi zikiwa za Aisha, nikaandika ujumbe kwa Jessenia, “sorry niichelewa kuamka, ila nipo fresh naenda kazini” nikaituma sms hiyo kwa Jessenia, nakutulia kusubiri jibu, ambalo sikuliona likiingia kwenye simu yangu, nilisiburi hata wakati mwingine nikahisi usingizi, lakini nilijitahidi kusubiri ujumbe toka kwa Jessenia, hata saa nne ilipoingia bado sikuona ujumbe, na mimi sikutaka kuandika sms nyingine kwa Jessenia.
Nakumbuka mida ile ya saa nne ndio mida ambayo niliweza kumuona mschana Maimuna akiwa na wanafunzi wenzake wakike karibu na darasa lao, aliponiona alitazama chini kwa haraka akikwepesha macho yake yasikutane na macho yangu, na mimi ambae nilikuwa na mwalimu Aisha nilipotezea kama vile sikuwa namuona wala kuwa na mpango nae, na wakati huo huo ndio wakati nilipopata wazo la kwenda kwa mwalimu mkuu kutoa udhuru ili niende nikapumzike pale Green hous.
Nikafanya hivyo, nilienda kwa mwalimu mkuu na kumueleza kuwa nina omba niende benk nikachukuwe fedha za matumizi, nae akanikubalia, na mimi nikamuaga Aisha na kuelekea green house, ambako nilipoingia tu nikaingia bafuni kuoga, kisha nikajilaza kitandani kwaajii ya kutafuta usingizi.
Lakini wakati naanza kusinzia nikashtuliwa na nyayo za viatu vyenye visigino virefu, yani ungesema ni farasi au ng’ombe alikuwa anatembea kwenye lami au sementi, sambamba na harufu nzuri ya manukato mazuri ya kupendeza yaliyojaa ndani ya chumba changu, ni kama siku ile nilivyomuona Jessenia kwenye kichochoro cha pale chake chake, hapo nilihisi mwili ukisisimka kama vile umetambaliwa na nyenyele au chavi chavi wenye manyoya, kabla sijajuwa nini kinataka kunitokea nikasikia mlango ukigongwa, lakini nilikaa kimya ili kusubiria mgongaji wa mlango aite kwa sauti ili nimtambue kama ni Jessenia au mtu mwingine wa ajabu, “Eric naweza kuingia” ilikuwa sauti tamu ya kuvutia ambayo niliitambua kuwa ni sauti ya mwanadada Jessenia, hapo niliinuka haraka na kuufuata mlango kisha nika ufungua.
Naam hapo nikajikuta mbele ya mwanadada mrefu kiasi, alievalia baibui nyeusi ya kawaida tu, hijabu nyeusi na niqab nyeusi iliyoziba kabisa uso wake na kubakiza macho pekee, sikuwa na shaka kwamba huyu ni Jessenia aliekuwa amebeba bagi dogo la kike (hand bag) na pia mfuko fulani mkononi mwake ambao ulionekana kuwa umetuna kweli kweli, ukweli muonekano wa mschana huyu ulifanana na yule ambae nilimuona amebebwa kwenye piki piki na pia yule ambae maelekezo yake yalikuwa kwenye jarada la kesi ya mauwaji ya Abdulqadiri……nini kinaenda kumkuta mwalimu Eric? Hebu tuendelee kidogo tuone.
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA THERASINI NA MOJA
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
NUMBER +255 743 632 247
ILIPOISHIA SEHEMU YA THERASINI: Naam hapo nikajikuta mbele ya mwanadada mrefu kiasi, alievalia baibui nyeusi ya kawaida tu, hijabu nyeusi na niqab nyeusi iliyoziba kabisa uso wake na kubakiza macho pekee, sikuwa na shaka kwamba huyu ni Jessenia aliekuwa amebeba bagi dogo la kike (hand bag) na pia mfuko fulani mkononi mwake ambao ulionekana kuwa umetuna kweli kweli, ukweli muonekano wa mschana huyu ulifanana na yule ambae nilimuona amebebwa kwenye piki piki na pia yule ambae maelekezo yake yalikuwa kwenye jarada la kesi ya mauwaji ya Abdulqadiri……ENDELEA…….
Nilitoa macho kwa mshangao na hofu ya ndani kwa ndani, maana nilianza kuamini kuwa huyu mwanamke ni jini, tena ni jini ambalo linafugwa na babu Mangeu, “Jesse, umepajuwaje hapa” niliuliza kwa mshangao, huku namtazama usoni mwanamke yule aliekuwa amesimama mlangoni, lakini yeye hakujibu kitu, zaidi ya kicheko fulani cha aibu, huku ana kwepesha macho yake yasitazamane na mimi, “Eric utanikaribisha ndani au nitaishia hapa mlangoni?” aliuliza Jessenia huku ananikabidhi ule mfuko mmoja uliotuna tuna kwa vitu mbali mbali vilivyokuwa ndani yake, na mimi nikaupokea na kuingia ndani, “lakini umenishangaza Jesse, umewezaje kuijuwa hii nyumba tena mpaka chumba?” nilimuuliza tena Jessenia, huku nikianza kuvuta picha jinsi nitakavayo nyonywa damu na kukauka kama nyama iliyosahaulika jikoni, “Eric jamani, mbona unaharaka weye, mie sindio nimefika utajuwa tu” alisema Jessenia kwa sauti tamu ya kubembeleza, huku ananifuata ndani ya chumba kile, ambapo alipoingia tu nikamuona anatazama kushoto na kulia mbele na nyuma, halafu akatazama kitandani kabla hajatoa mkoba wake na kunikabidhi, kwamba niuweke sehemu ambayo niliona inafaa, nikafanya hivyo kwa kutundika kwenye msumari wa mlangoni “ila weye unalala haswaaa, ilikuwaje mpaka ukashindwa kupokea simu yangu” aliuliza Jessenia huku anatoa niqab yake usoni, akifuatia na hijab, ambavyo alinipatia niweke sehemu nzuri, “ujuwe jana ulinifanya nichelewe sana kulala, kwa sababu ulikuwa unapiga simu mara kwa mara” nilimjibu, huku naweka mezani ile hijab na niqab, lakini kichwani mwangu nilikuwa nawaza kitacho nitokea muda mfupi ujao, ni kama kilicho watokea wakina Vuai, na Abdulqadir, ukichukulia sehemu ambazo nilikuwa nae kwa uwazi huyu mwanamke ni sehemu ambazo alikuwa amevaa niqab, yani kile kitambaa cha kuziba uso, na mtu alieweza kututambua au kutuona tukiwa wawili ni babu Mangeu peke yake, ambae onyo lake kwangu ilionyesha wazi hakutaka niwe na mwanamke huyu ili niepuke jambo fulani linaloweza kunikuta, “bora wewe ulichelewa” alisema Jessenia huku anacheka cheka, nilipomtazama nilimuona anavua baibui lake na kubakia na kijigauni chepesi sana cha rangi fulani ya blue ya kupauka sana, kijigauni ambacho kiukweli kilinifanya nisahau yale yote niliyokuwa nawaza.
Naam hakika siku zote nilikuwa sijawahi kuliona umbo halisi la mwanadada huyu, lakini leo ndiyo niliweza kuona mwanamke huyu, jinsi alivyoumbwa akaumbika, ukiachia rangi ya mwili wake, urefu wa nywele zake nyeusi ndefu alizo zifunga kwa msuko mmoja na kuzifanya ziwe kama mkia wa farasi, pia niliweza kuona jinsi alivyo jaliwa umbo zuri matata la kuvutia, hips pana makalio yake makubwa ya wastani, tumbo dogo mguu mzuri ambao ulipendeza kwa kila kiatu, kifuani sasa ndio balaa, maana matiti yake yalikuwa makubwa kidogo, ila chuchu ndio zilisimama ungesema zile sindano za langoni pa mfalme Herode, “Eric niwekee hii” alisema Jessenia ambae alikuwa ananipatia lile baibui lake niliweke mezani, “ha! Sijui nilikuwa nawaza nini?” nilisema kwa sauti ya chini, huku napokea lile baibui na kuliweka mezani, “nakushangaa unavyo mshangaa mkeo, utadhani anapita kumbe amekuja kwako” alisema Jessenia kwa sauti iliyojaa utani na kicheko cha aibu, huku anapanda kitandani mzima mzima na kujilaza kiubavu ubavu, ukweli ilitamanisha sana.
Naam wakati nashangaa nikamuona Jessenia anainuka ghafla na kutazama madirisha yote mawili, yaani moja ambalo lilikuwa upande wa ubavuni mwa kitanda, ambako ndio upande wa barabara iendayo vitongoji kutoka wawi, na dirisha la pili ni upande wa miguuni mwa kitanda, ambalo lilikuwa linatazama njia ya kuingia ndani ya kambi, madirisha yote mawili yalikuwa wazi na hata mapanzia yalikuwa wazi pia, kwa mtazamo ule nilikumbuka jambo, jinsi nilivyopata maelezo ya kule madungu guest house dirisha lilikutwa wazi, japo sikuwa naamini kuwa Jessenia ndie mschana alieingia na Abdulqadiri pale madungu, lakini kuna mambo yalinifanya nisijiamini moja kwa moja, “vipi una wasi wasi tunaweza kuchunguliwa” nilimuuliza Jessenia huku napanda kitandani na kufunga lile dirisha kisha nika shusha panzia, na hivyo hivyo nilifanya kwenye dirisha la pili, “kwani wewe unajiamini sana, kwamba watu hawawezi kuchungulia ndani?” aliuliza Jessenia huku anajilaza kitandani, kama safari akikusana mito na kuilalia akiwa amelala chali, “kwanini unaogopa kuchunguliwa, wakati umepumzika kwa mpenzi wako?” nilimtania kidogo, huku na sogea kwenye switch na kujaribu kuwasha fan ya juu, panga boy, ambayo toka nianze kukaa hapa sikuwahi kuitumia, nashukuru ilikuwa nzima, maana vinginevyo sijui kama tungepoteza hata nusu saa kabla hatuja ondoka mule ndani.
Jessenia hakuweza kunijibu swali langu, Zaidi alicheka kidogo huku anaziba uso wake kwa mikono miwili, nadhani aliashiria kuwa ninajuwa kinachotaka kutokea, pale watu wawili wanaojiita wapenzi wanapokuwea sehemu kama hii iliyozibwa kama hivi, “karibu sana Jesse, ila pole kwa jana naona nilikushtukiza sana” nilimuambia Jesse, ambae hakujibu kitu Zaidi ya kujichekesha huku anaziba uso wake, wakati huo mimi nasogea kwenye mezani na kuwasha computer yangu ndogo, na kuweka music laini nikiitengenezea play list ndefu sana, kisha nikarudi kitandani na kujilaza pembeni yake.
Giza lilikuwa limetanda mule chumbani, Zaidi ni mwanga hafifu wa computer ndio uliosalia na kutuwezesha kuonana usoni, “humu unaishi peke yako?” aliuliza Jessenia, huku akipelekea macho yake kuzunga chumba kizima, kama vile anakikagua, “ndio naishi mimi tu! Labda na wewe” nilimtania kidogo, na yeye akacheka kidogo huku anajiegemeza kichwa chake kifuani kwangu, na kufanya nywele zake ndefu zinitekenye na kunisisimua mwili wangu, hamu ya kitumbua ikanipanda kwa haraka, ukweli mpaka hapo nilikuwa na maswali kadhaa ya kujiuliza ambayo nilihitaji majibu yake, japo sikumuona mtu wakunipa majib.
Jessenia anaweza kuwa na miaka kati ya ishirini na tatu au ishirini na nne, taarifa za mwanzo zinasema kuwa wanaume wengi walisha maliza sendo kama sio matairi ya gari zao na pesa zao kumfuatilia mschana huyu, na waligonga mwamba, sasa mimi ninakipi cha ziada ambacho mpaka sasa kina nifanya niwe na mwanamke huyu hapa ndani, tena amejilaza kifuani kwangu, na kwanini iwe ghafla hivi, halafu kwanini jana alikuwa katika hali kama ile ya kuondoka ghafla huku akionyesha wasi wasi, “unawaza nini Eric, kwani unaogopa tutafumaniwa na Aisha?” aliniuliza Jessenia kwa sauti fulani ambayo inaviashiria vya utani, “kwani aisha ni nani wangu mpaka atufumanie?” nilimjibu kwa utani pia, huku nikipeleka mkono wangu kwenye kichwa chake na kuanza kuchezea nywele zake kama vile nina zikuna kuna hivi, kuanzia usawa wa sikio mpaka kwenye kisogo, hapa chini karibu na shingoni, nikamwona anavuta pumzi na kuishusha kwanguvu, “yeye si anapafahamu hapa na huwa anakuja mara kwa mara, anaweza kuja kukutazama muda wowote” alisema Jessenia na hapo ndipo nilizidi kuhisi kuwa huyu mwanamke sio wa kaiwada, sikutaka kujuwa amejuwaje nikichelewa kumkasirisha, maana hadithi ambazo niliwahi kuzisikia za majini huwa yana jiweka wazi pale unapoonyesha kuyashuku au kuyang’amua, na likijiweka wazi basi umekwisha, hivyo nikaamua kulifanyia uchunguzi wa kimya kimya, “sasa ndio kutufumania huko, si atakukuta upo kwako, hapa ni sawa na kwako” niliongea lugha moja ya kimapenzi ya ndani kabisa, nikamuona Jessenia anatabasamu na kuinua kichwa kunitazama usoni, na kunipa nafasi ya kuchungulia matiti yake kwenye kijigauni chake chepesi, ambapo hakuwa amevaa sidiria, “una maneno weye” alisema Jessenia huku anaficha uso wake kifuani kwangu, yaani alishindwa kunitazama, wakati huo nilisikia kama kuna vishindo vinatembea kwa nje kuja upande wa dirisha.
Nikatulia kidogo kusikilizia, siku sikia tena vishindo, hapo nikamtazama Jessenia ambae nae aling’amua ukimya wangu, maana nae pia alikuwa ananitazama, ukweli mschana huyu ni mzuri sana, “mh! Lakini jini anawezaje kunywa Wine” niliwaza hivyo huku nikikumbuka siku tatu zilizopita pale wawi mess kwenye taarab kwamba mschana huyu alikunywa Wine, lakini je inawezekana jini la mzee Mangeu likawa linachukuwa sura ya Jessenia, na kwamba kuna kuwa na Jessenia wawili mmoja jini mmoja Jessenia halisi, yaani yule ambae hataki kuwa karibu na wanaume na huyu ambae nipo nae kitandani, sasa je yupi ni yupi, hapo nikaamua kufanya kitu cha msingi, “Jesse kuna wine hapa tuna weza kujichangamsha kidogo, nilimueleza Jessenia nikimpima kama atakubali, “sawa tu, lakini nisijekulewa sana nikafika nyumbani mjomba akajuwa” alisema Jessenia huku anainuka toka kwenye kitanda kuifuata meza, huku nikiweza kujionea jinsi makalio yake yalivyo kuwa yanatikisika, ungesema hakuvaa nguo yoyote ndani.
Naam wakati naendelea kumtazama Jessenia alienda kusimama mbele ya meza na kushika mfuko ule aliokuja nao, nika sikia kama kitu fulani kinagusa dirisha, mwanazo nilidhania kelele za mfuko, lakini baadae nikasikia dirisha likitikisika, pasipo kufunguka, niwazi kulikuwa kuna mtu anajaribu kufungua kwa nje…….. Jamani Jamani MUWE NA USIKU MWEMA