KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA THERASINI NA MBILI
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA THERASINI NA MOJA: Naam wakati naendelea kumtazama Jessenia alienda kusimama mbele ya meza na kushika mfuko ule aliokuja nao, nika sikia kama kitu fulani kinagusa dirisha, mwanazo nilidhania kelele za mfuko, lakini baadae nikasikia dirisha likitikisika, pasipo kufunguka, niwazi kulikuwa kuna mtu anajaribu kufungua kwa nje…….. ENDELEA…….
Nikainuka na kusogeza panzia pembeni na kuchungulia nje kama ningeona chochote, lakini sikumuona mtu yoyote, wala kitu ambacho labda kingekuwa kimegusa dirisha, “vipi Eric kuna nini?” aliuliza Jessenia akionyesha hali flani ya wasi wasi, niliona kama nilimueleza hisia zangu kwamba nahisi kuwa kuna mtu alikuwa anachunguli basi nitamfanya avae nguo zake na kuondoka mara moja na kunifanya nikose utamu ambao leo nilipanga niuonje, hata kama niutamu wakitumbua cha jini, “hakuna mtu, nilikuwa natazama nje” nilijibu huku na funika tena panzia, nakugeuka kumtazama mwana dada huyu, ambae sasa alikuwa ameshika karatasi maalumu lisilopooza chakula, lililoviligiwa vitu fulani ndani yake, “unantisha bwana” alisema Jeseenia huku anakuja kitandani na kukaa pembeni yangu, kisha kaanza kufungua ile karatasi maarufu kama foil, hapo ikatangulia harufu nzuri ya samaki.
Nikweli kulikuwa na samaki wawili walio kaangwa na ndizi nne sambamba na kachumbari kwa pembeni, “waooo umeamua kunionjesha mapishi yako” nilisema huku natazama kile chakula ambacho kilinipa hamu ya kula tena japo saa nne nilikuwa nimekula, “utajaonja mpaka ukinai, nimekubebea vitu kibao” alisema Jessenia huku anakata kipande cha ndizi na kunisogezea mdomoni, na mimi nikakipokea kwa mdomo na kuanza kutafuna nikisikilizia ladha yake, “huuuu! nitamu” nikweli ilikuwa tamu, “tule kwanza halafu tuanze kunywa hiyo wine” alisema Jessenia na hapo ndipo nilipokumbuka kuwa sikuwa na grass, “tena umenikumbusha, ngoja nifanya mpango wa glass” nilsema huku nainuka kwenda kuchukuwa simu yangu mezani, kisha nikaandika ujumbe kwa Mwasenga, “kaka upo wapi mida hii?” kisha nikautuma kwa Mwasenga huku narudi kitandani, ambako nilikutana na kipande cha mnofu wa samaki kilichosogezwa mdomoni mwangu na wakati huo huo ujumbe ukaingia kwenye simu yangu, “nipo hapa eneo la magesho, vipi kuna inshu?” ndivyo ulivyosomeka ule ujumbe toka kwa Mwasenga, ambae kwa maelezo yake alikuwa hapa hapa kambini, “nina shida kidogo kaka, nahitaji glass mbili, sijui tunafanyaje?” niliandika hivyo na kumtumia mwasenga, lakini safari hii hakujibu mapema kama kawaida yake, nikatulia kusikilizia jibu lake huku tunaendelea kula samaki na ndizi, na kufanyiana michezo ya kimahaba.
Wakati tunaendelea kufanya hivyo, kuna kitu niligundua kwa Jessenia, yaani alikuwa ananitazama kwa umakini, na nilipomshtukia alikuwa anaishia kutabasamu na kutazama pembeni, ni kama kuna kitu alikuwa anatamani kusema lakini alikuwa anasita.
Dakika kumi baadae sms ikaingia kwenye simu yangu, nikaifungua na kuitazama “upo hapo green house?” ilikuwa ni sms toka kwa Mwasenga, hapo nika jibu kwa haraka sana, “ndiyo kaka nina mgeni” na dakika moja baadae ikaingia sms toka kwa mwasenga, “kaka we kiboko” sikuelewa anamaanisha nini mwasenga kwa kusema hivyo, na wala sikujuwa nijibu nini kwa ile sms yake, lakini wakati naendelea kujiuliza nikasikia nyayo za mtu zikiondoka usawa wa dirisha, safari hii tulisikia wote, yaani mimi na Jessenia, ambao tulitazamana kwa sekunde kadhaa kabla sijapata wazo la kuinuka haraka na kufunua panzia, halafu nikatazama nje, nikabahatika kumuona mtu mmoja akielekea barabarani kwa mwendo wa haraka sana, akiwa amevalia nguo za kwaida tu kama vijana wengine, alivaa suruali ya jinsi na tishert chini alivaa buti za kaki, mkononi alikuwa ameshika mfuko fulani wa Rambo kama tunavyoita, na alipoifikia barabara nikamuona ananyoosha mkono, kama vile anamuita mtu flani, na hapo ukafwatia ngurumo ya pikipiki iliyokuwa inakuja kwa kasi, nilipoitazama vizuri nikaiona pikipi kubwa ikitokea upande wa vitongoji, yaani kule ambako kuna shule ya Fidel Castor na kuja kusimama karibu kabisa na yule jamaa, ambae alipanda na piki piki ikaondoka kwa kasi, pikipiki ambayo haikuwa ngeni machoni pangu, nipiki piki ya vijana wa Ussi, ambayo walimletea kile kijimfuko siku ambayo Vuai aliuwawa, “Eric unawafahamu wale watu?” aliniuliza Jessenia akionyesha kuwa na hofu kubwa, kumbe na yeye aliinuka kuchungulia, “wajinga wale achana nao” nilimjibu Jessenia, na wakati huo huo nikamuona Mwasenga anakatiza pale nje akiwa amebena mfuko mdogo mkononi mwake, yeye hakutazama dirishani, hivyo nika rudisha panzia na kuufuata mlango, “Eric usichelewe huko” alisema Jessenia, ambae alikuwepo bado kitandani, akionyesha hofu kubwa, “wala siendi mbali, napokea glass” nilimjibu huku nafungua mlango na kutoka nje nikakutana na Mwasenga, ambae aliponiona tu akaanza kucheka kichini chini, “kaka unatisha, umesha mnasa yule mtoto” alisema Mwasenga kwa sauti ya chini, nikajifanya sijamuelewa, “mtoto yupi huyo kaka?” niliuliza ili nisikie atasema nini, “haaa! Kaka si yule mtoto chotara Seni, mdogo wake Ussi” alisema Mwasenga akionyesha wazi kuwa na uhakika na anacho kisema.
Ukweli nilishangaa kidogo, hapo nika mtupia swali, “kaka we kiboko, umejuwaje?” nilimuuliza huku nikiwa na mshangao wa wazi kabisa, “ujuwe nini, kuna wakati Ussi alinipigia simu kuniuliza kama wewe upo hapa ghetoni, nikamuambia kuwa umeelekea shuleni, sikujuwa kwanini ameniuliza lakini uliponiambia upo na mgeni na jinsi hii harufu ya perfume ninavyo isikia nikajuwa mtoto yupo ndani tu!” alisema Mwasenga huku ananipatia mfuko wenye glass, hapo nikapata jibu kwamba wale vijana walitumwa na Ussi kuja kuchunguza kama dada yake yupo hapa, swali ni je wamejuwaje kama Jessenia amekuja huku, au aliondoka nyumbani wako bila kificho, na wamejuwaje anakuja hapa, au babu Mangeu ndie aliemfuatilia na kutoa taarifa, je baada ya hapo wata fanya nini, au ndiyo mpango wa kuniuwa kwa kutumia jini, na je hilo jinni ndio lipi, au ni huyu nilie nae ndani ni mtu gani ambae hajuwi hata sura ya mzazi wake mmoja, “kaka we nenda kafaidi mzigo, achana na wivu wa Ussi, hizi ni za hapo Mess utampa yule koplo” alisema Mwasenga huku anaondoka, na mimi nikatulia nikimsindikiza kwa macho kichwani kwangu nikitafakari juu ya mamb yalivyo kuwa yanaenda, na kabla hajafika mbali akasimama na kunitazama, ukiwa na shida yoyote nichek hewani” alisema Mwasenga nakutokomea zake nje.
Hapo nikapanga niingie ndani nikamtoe huyu mwanamke, ila busara zina hitajika, maana nilijijuwa kuwa siku na uwezo wa kumuondoa kwa nguvu hasa kama kweli ni jini, lakini ile nageuka tu, nikamuona Jessenia akiwa amesimama mlangoni ananitazama kwa macho ya tabasamu, Eric, nitanawa wapi” aliuliza Jessenia kwa sauti tamu kama kawaida yake, kijicheko cha aibu kikitawala usoni mwake na kumfanya azidi kupendeza na kuwa mzuri zaidi, ukweli ile habari ya kumtoa nje iliishia hapo, nikajikuta natabasamu, “ngoja nikakunawishe mke wangu” niliongea hivyo huku naingia chumbani na kuweka glass, kisha nikatoka na kuongoza bafuni, “jamani mimi sijazowea kukaa hivi mbele ya mwanaume, bora chumbani kuna giza” alesema Jessenia ambae leo alikuwa mwingi wa aibu, “utaonaje aibu wakati upo na mimi” nilimjibu huku naanza kumnawisha mikono kama mtoto, huku ninasugua viganja vya mikono yake taratibu kama vile namtekenya, “tayari bwana au kuna mengine?” alihoji Jessenia, huku anacheka kidogo, ni baada ya kuona kuwa ninachomfanyia tofauti na kunawa.
Tulirudi chumbani na yeye akajilaza kitandani na mimi nikachukuwa tahadhari ya kuufunga ule mlango kwa komeo la ndani, nikichelea mtu asije akavamia na kuingia mule ndani kwa ghafla, baada ya hapo nikaifungua wine na kuweka katika glass zote mbili kisha nikampa mmoja Jessenia ambae hakusubiri hata kidogo, akaipeleka mdomoni na kupiga funda moja na mimi nikanywa kidogo, kisha nikapanda kitandani tukawa tumekaa pamoja tena kwa kukaribiana huku meza yetu ikiwa ni kiti ambacho nilikivuta na kukiweka karibu na kitanda, na hapo ndipo nilipoona huo ndio muda wa kuanza kuhoji vitu ambavyo ningepata majibu ya kuniondoa hofu, “hivi Jesse, yule mzee Mangeu ana undugu wowote na mjomba wako?” nilimuuliza Jessenia, ambae aliachia mguno wa chuki, “ana uhusiano gani na mjomba huyo mwanga?” alisema Jessenia kwa sauti iliyojaa chuki, huku ananipatia glass yake ya waine na yeye kuegemea kwenye bega langu, sikushangazwa na chuki ya Jessenia kwa mzee yule maana watu wengi walimchukulia tofauti, “natamani kumfahamu yule mzee na kazi zake, maana ni kama namuona tofauti hivi sana” nilisema hivyo huku na jaribu kumnywesha wine yake, ambayo alikunywa kidogo huku anatembeza mkono wake kwenye kifua changu kilichokuwa wazi na kupapasa vijichuchu vyangu, na hapo anamaliza kumeza funda lake la wine, akaanza kuongea, “yupo tofauti kweli mimi mwenyewe nashindwa kumuelewa na uchawi wake, yaani pale unavyo muona ndio vile vile, huoni ndugu wakimtembelea, hakuna siku anaugua, hafanyi kazi yoyote Zaidi ya kulima mihogo pale nje kwake anakotoa hela anajuwa yeye” alieleza Jessenia, ambae aliendelea kueleza kuwa, mzee Mangeu anaogopwa na kila mtu, “kuna wakati anaweza kutoweka hata mwezi mzima pasipo mtu yoyote kujuwa ameenda wapi” kwa kweli hiyo ilikuwa ni habari mpya kwangu, “unadhani kwanini wanamuogopa?” nilimuuliza Jessenia, ambae akaanza kunifanyia uchokozi, maana sasa alikuwa anabinya binya chuchu zangu za kiume, na kunisisimua akisabaisha dudu ianze kututumka, “ni mchawi yule mzee, hakuna asiejuwa, yaani mjomba na mali zake zote niliwahi kumkuta akifokewa kama mtoto, sijuwi alimfanya nini, na mjomba hakujibu kitu alikuwa kama mtoto ameinamisha kichwa chini” alisema Jessenia na kunifanya nishangae kimoyo moyo, maana ilistaajabisha kidogo, “dah! Vipi lakini aliwahi kukunyoesha dalili ya kukuchukia wewe au kaka yako Ussi?” niliuliza huku na mtazama mschana huyu, ambae sasa niliona kuwa uchokozi wake umezidi….. Itaendelea