Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
MTUNZI: Mbogo EDGAR
NUMBER +255 743 632 247
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA: na kujikuta nikiuliza kwa mshangao huku nainuka toka kwenye kiti, maana mschana mmoja mrembo kweli kweli alie achia tabasamu mwanana alikuwa amesimama mbele yetu, huku anapendeza kwa gauni lake ambalo nilishindwa kulijuwa rangi yake, kama ni nyekundu au nyeusi au ya blue, maana nikama ilikuwa inabadirika badirika rangi kila lilipotikisika, gauni ambalo lilimpendeza kutokana na urefu wa gauni ilo, na jinsi lilivyomshika mwilini, na kusanifu umbo lake mwanana la kibantu, tofauti na rangi yake ya kiarabu, kama nywele zake ndefu ambazo azikufunikwa na ijab, sawa na wanawake wengi mle ndani ambao waliachia nywele zao, zipate hewa, huyu alikuwa ni Jessenia binamu yake Ussi….. ENDELEA……
Ambae licha ya kuvaa nguo hizo nzuri za kung’aa, pia likuwa amevalia vito vya thamani karibu kila sehemu inayo faa kuveshwa, kuanzia pete vidoleni, chain shingoni, hata hear ring masikioni, hapo kikalipuka kicheko toka kwa mwalimu Aisha, huku Jessenia mwenywe akitabasamu huku anatazama chini kwa aibu, “karibu Seni, achana na huyu mnyamwezi mkorofi” alisema Aisha ambae kiukweli kabisa hakujuwa kama nimeshtuka sana baada ya kumuona Seni, na ukweli ni kwamba nilihisi kuwa namuona peke yangu, “kwahivo ulidhania mimi jini unaniona peke yako eeh? usije kukimbia tu, kama ulivyo nikimbia siku ile chake chake” alisema Seni, huku anakaa kwenye kiti kimoja ambacho sio tu kilikuwa kati ubavuni mwa meza, ambacho naweza kusema kilikuwa karibu kabisa na kiti changu, harufu ya manukato yaka mwagika na kusambaa puani mwangu, manukato ambayo yalinisisimua na kunitekenya mpaka kwenye sehemu zangu za siri kiasi cha kujikuta natamani kitumbua kwa ghafla.
Hapo mimi na Aisha tukacheka kidogo nikiwa nimesha thibitisha kuwa ni kweli Aisha alimsimulia Seni kama nilivyo msimulia kuhusu kumkimbia nikidhania jini, “natania bwana kwanini nimaanishe hivyo” nilijitetea, na wakati huo Mwasenga akaingia akiwa na Soda chupa mbili pamoja na chupa mbili za wine aina ya Mbogo land coco wine, na glass mbili akaweka mezani, “hoo! Kumbe kuna mgeni ameongezeka, utakunywa nini Seni?” aliuliza Mwasenga, huku anamtazama Seni ambae kwanza kabisa alimtazama Aisha huku anatabasamu la kujizuia kucheka, “mmhh! labda hii, endapo mwenyewe ataridhia” alisema Seni, huku anaonyeshea chupa ya wine, huku macho yake yakijaribu kunitazama mimi lakini ilishindikana kutokana na aibu iliyomsika mwanamke huyu mrembo na mzuri sana, hakika nilishangaa sana kwa mschana wa kipemba ambae ni mrembo kuliko urembo wa siku ya harusi au niliowahi kuusoma kwenye vitabu, kusema atatumia wine “kwani nisiridhie, karibu sana” nilisema kwa sauti iliyojaa uchangamfu, huku nachukuwa chupa moja ya wine na kuifungua, “basi ngoja nikaongeze glass” alisema Mwasenga na kuelekea kule counter, huku anapishana na afande Komba, ambae japo ilikuwa ni mapema lakini alionekana tayari kuwa amelewa aliekuwa anakuja kwenye meza yetu.
Music ulikuwa unalindima kweli kweli, vyombo vikipigwa kwa ufundi mkubwa huku waimbaji wakiimba kwa sauti za kupendeza, wapenzi na washabiki wa music huo walikuwa wakicheza kwa namna ya kupendeza sana ambayo ilinivutia sana, “vipi ticha, naona unapata vitu vyako” alisema afande Komba, mara baada ya kuifikia meza yetu, “yaah! Inavutia kwa kweli” nilimjibu Komba, huku namimina wine ile toka nchi ya kifalme ya mbogo Land kwenye glass zote mbili, yaani ya kwangu na ile ambayo ange tumia Jessenia, ambayo niliisogeza mbele yake, “asante” alisema Jessenia kwa sauti tulivu iliyotoka kwenye midomo yake ambayo ilikuwa na rangi nyekundu ambayo nilijilaumu kuitazama maana nayo ilinisisimua sana na kunifanya nizidi kutamani kitumbua, “hii ndiyo pemba kaka kula maisha” alisema Komba, ambae mara kwa mara macho yake aliyaelekeza kwa Seni, “ni kweli kaka pamenoga, hivi hii inakuwa kila baada ya muda gani?” niliuliza huku anachukuwa glass yangu ya wine na kuipeleka mdomoni, nikapiga funda moja na kuirudisha mezani, wakati huo Seni nae alikuwa anakunywa kidogo wine yake, “ni mpaka itokee, sema tutafanya utaratibu ili iwe angalau kila baada ya miezi miwili” alisema Komba, kisha akamgeukia kabisa Seni na kumtazama bila kificho, halafu akamtazama Aisha, “hooo! kumbe upo na warembo hapa, mambo vipi jamani” alisalimia Komba, kwa sauti ya uchangamfu wa kilevi, huku anawatazama kwa awamu, “safi tu, za kwako” aliejibu ni Aisha peke yake, huku Seni, akiinua tena grass na kuipeleka mdomoni, wakati huo huo kwa bahati mbaya nilipeleka macho yangu kwenye meza ya Ussi ambae nilimuona akinitazama kwa jicho moja kali sana, na macho yetu yalipo kutana Ussi aliyakwepesha mara moja na kutazama kwenye meza yake.
Ukweli sikushangaa sana, maana ni kawaida kwa ndugu wa kiume kutokufurahia kumuona dada yake akiwa na mwanaume mwingine, “ticha mukimaliza hiyo wine mutamuambia mwasenga aje achukue fedha akanunue nyingine” alisema Komba kisha akaondoka zake, hakuwa wa mwisho kutembelea meza ile, ukweli tulipokea watu wengi sana, kila dakika wote waliishia na kutoa offer ya wine, haikunishangaza sana, maana kwa uzuri wa Jessenia lazima kila mwanaume achanganyikiwe, “Eric hebu tazama kule” kuna wakati Aisha alinishtua, huku anaonyesha kule watu wanakoendelea kucheza, japo kulikuwa na mwanga hafifu, lakini nilipotazama nikamuona Maimuna akiwa anacheza na kijana mmoja ambae anaweza kuwa amenizidi miaka kadhaa, tena walikuwa wakicheza kugusananisha miili yao, “hooooo! Ni kweli kumbe nikatundu sana” nilisema huku Jessenia nae akitazama upande ule ule ambao sisi tulitazama, lakini sijui kama aliona tulicho kiona sisi, “nilikuambia ni katundu sana” alisema Aisha huku tuna shuhudia Maimuna akicheza kwa kuegesha makalio yake kwenye eneo la mbele la kijana yule, huku akikatika viuno taratibu akifuata music unavyoende, ilipendeza machoni, Jessenia alipoona hakuna anacho kiona akaamua kuendelea na kinywaji.
Tuliendelea kunywa wine huku tunaburudishwa na music wa mwambo katika mahadhi ya kisasa, mwanzo tulikuwa kimya kimya maongezi machache, ambayo mara zote mimi,mwasenga na Aisha, ndio tuliokuwa tunaongea, Jessenia alichangia mara chache, lakini kila muda ulivyozidi na sisi kuendelea na kinywaji, ambacho Seni alikuwa anakunywa kivivu sana, ndivyo tulivyozidi kuchangamka na kuongea kwa pamoja, hata Seni pia alionyesha kujiunga na sisi katika maongezi tukicheka na kufurahi kwa pamoja.
Kuna wakati nilikuwa najaribu kutazama kule kwenye meza ya Ussi, ambae nadhani ni kwaajili ya pombe alizokunywa hakuweza tena kufanya siri juu ya hasira zake kwangu, hasira ambazo nilihisi ni kukaa kwangu na binamu yake, sikutaka kumshirikisha mwasenga au Aisha au Jessenia mwenyewe, mida hii wengi walionekana kulewa zaidi, hata uchezaji wao ulizidi kuchangamka, na hapo ndipo nilipo mtania Aisha, “natamani kwenda kucheza” wote watatu wakacheka kufuatia kauli yangu, “ok! Ticha Eric twende tukacheze na mimi” alisema Jessenia huku anainuka toka kwenye kiti chake na kunishika mkono, akifanya kama vile ananiinua toka pale nilipokaa, ile kiganja cha mkono wake ulipokumbatia mkono wangu nilihisi joto fulani tamu sana toka kwenye mkono wake na kunipa raha, na wakati nainuka nikakumbuka kumtazama Ussi…… Endelea Kufuatilia

KIFO CHA HAWARA (mkono wa jinni)
SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
MTUNZI: Mbogo EDGAR
NUMBER +255 743 632 247
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI: sikutaka kumshirikisha mwasenga au Aisha au Jessenia mwenyewe, mida hii wengi walionekana kulewa zaidi, hata uchezaji wao ulizidi kuchangamka, na hapo ndipo nilipo mtania Aisha, “natamani kwenda kucheza” wote watatu wakacheka kufuatia kauli yangu, “ok! Ticha Eric twende tukacheze na mimi” alisema Jessenia huku anainuka toka kwenye kiti chake na kunishika mkono, akifanya kama vile ananiinua toka pale nilipokaa, ile kiganja cha mkono wake ulipokumbatia mkono wangu nilihisi joto fulani tamu sana toka kwenye mkono wake na kunipa raha, na wakati nainuka nikakumbuka kumtazama Ussi……ENDELEA…
Usisahau kutoa sapoti yako kwa mtunzi japo kwa buku tu ya bando... Huku nikisahau kumtazama Aisha na Mwasenga na watu wengine waliokuwa katika meza za jirani, ile nageuka kutazama meza ya Ussi nikakutana na mcho makali ya Ussi, ambayo hayakuwa na kificho kwa ukali wake na hasira alizokuwa nazo, nilidhania wakina Mwasenga na Aisha nao wameona jambo lile, hivyo nikawatazama ili nipime hisia zao, kwamba wanachukuliaje mtazamo wa Ussi kwangu, lakini ile nawatazama nikawaona wao pia wananitazama lakini kwa macho ya mshangao, ni kama hawakuamini kinachotokea, “mh! Seni, leo unaamua kucheza na weye?” aliuliza Aisha kwa mshangao, wakati huo nilikuwa nimesha simama, “kwani kuna ajabu?” aliuliza Jessenia kwa sauti ya uchangamfu akiwa bado amenishika mkono, na sasa alianza kunikokota kunipeleka kwenye sehemu ya kuchezea ambayo muda haikupungua watu, “Seni, ujuwe mimi sijui kucheza taarabu, na sijawahi hata siku moja kucheza” nilimueleza Jessenia, wakati tuna sogelea kwenye kundi la watu waliokuwa wanaendelea kujimwaya mwaya, kwa pea ya wawili wawili, “wala sio vigumu utaweza tu” alisema Jessenia kwa sauti yake tamu iliyochangamka, ambayo ilileta ladha nzuri masikioni mwangu.
Ni kweli sikuwahi kucheza music huu hapo mwanzo, lakini leo nilidhamilia kucheza music huu, kutokana na uzuri wa mschana huyu Jessenia, ambae baada ya kufika pale na kuanza kucheza tulianza kwa kucheza taratibu, pasipo kugusana, na hata ilipotokea kutazama usoni, basi wote tulitabasamu na yeye nilimuona akitazama chini kwa aibu, na wakati huo huo nikakumbuka kutazama tena kwenye meza ya Ussi, ambae kwa bahati nzuri safari hii hakuwa ananitazama, ila alikuwa anaongea na mtu mmoja ambae mwanzo sikumtambua, ni kama alikuwa anamnong’oneza jambo kwa umakini sana, maana alikuwa ameinama na kutegesha sikio karibu na mdomo wa Ussi, nikaona afadhari, kwamba Ussi aliachana na mimi, lakini kabla sijaacha kuwatazama nikaona kitu ambacho kilinishawishi kuendelea kuwatazama, niliona kama vile Ussi anamuelekeza jambo kuhusu kule tulipokuwepo sisi, maana nilimuona yule jamaa anageuza uso wake na kutazama upande wetu, yaani pale tulipokuwa tuna cheza music,, “hivi Jessenia, unadhani ni sahihi wewe kucheza na mimi?” nilimuuliza Jessenia, ambae kwanza alianza kwa kutabasamu, tabasamu ambalo lilionyesha kama amejawa na furaha na raha huku anainamisha uso wake chini, “mh! kwanini isiwe sawa, sina mume wala mchumba, mimi ni mtu mzima najiangalia mwenyewe” alisema Jessenia kwa sauti fulani ya chini nyororo iliyojawa na aibu ya kike kiasi kwamba nikajishtukia, maana kwa mtu wa mbali ambae hakujuwa tunazungumza nini angesema namtongoza.
Hapo nikajifanya sina habari yake yoyote, “mh! ina maana wewe hapo ulipo hauna hata boy friend?” niliuliza swali ambalo jibu lake nimeshapewa na watu wengi, kuwa licha ya wanaume wengi kumtaka kimapenzi lakini hakuna ambae amefanikiwa kuwa nae, “kwahiyo huamini eeh?” aliuliza Jessenia huku anajaribu kunitazama usoni, na mimi nikamkazia macho yangu ambayo niliyaweka katika mtindo wa ushawishi, na yeye akashindwa kuendelea kunitazama akatazama chini, “kwanini nisiamini wakati umeniambia wewe mwenyewe” niliongea kwa sauti fulani tulivu yenye swaga za kushawishi, nikamsikia anaachia kicheko laini cha kivivu, na wakati huo nikatazama tena kule alikokaa Ussi, nikamuona anatazama upande wetu, lakini hakuwa ananitazama mimi, ni kama alikuwa anamtazama mtu aliekuwa jirani yetu, nikavutika kumjua mtu aliekuwa anamtazama, “samahani kaka Eric hivi wewe ni mwalimu kweli au ni mwanajeshi?” niligutushwa na swali la Jessenia, alieniuliza huku anaushika mkono wangu kwa kiganja chake chenye joto lile ambalo sisi tuliosoma tabia za viumbe hai tuna fahamu ni joto ambalo humkumba mwanamke ambae anakuwa na hamu ya dudu, ile kunishika mkono wa kushoto nilidhania imetosha, lakini nikaona ananishika na mkono wa kulia, kumbe ilikuwa ni hatua ya kubadili mtindo wa uchezaji, hivyo tukaanza kucheza kama vile wafanyavyo wapendanao, nilicheka kivivu, “mimi ni mwalimu, kwanini unauliza hivyo?” nilimuuliza huku najaribu kutazama watu niliokuwa nao jirani, kuona Ussi alikuwa anamtazama nani, “naona unafahamiana na wanajeshi wengi sana” alijibu Jessenia, huku anacheka cheka kidogo, “kwasababu nimefikia kwenye nyumba yao” nilimjibu huku naendelea kutazama watu waliokuwa wanacheza jirani yangu, na wakati huo ndipo nilipomuona yule jamaa aliekuwa ananong’onezana na Ussi, akiwa anacheza hatua mbili pembeni yetu, tena alikuwa peke yake na ndio wakati ambao niliweza kumtambua huyu jamaa, ambae mwanzo sikumtambua mapema, nadhani nikutokana na uvaaji wake wa tofauti na ule ambao nilimuona nao kwa mara ya kwanza, ambayo ilikuwa siku ile niliyomuona akiwa na mwenzie kwenye pikipiki kubwa wanatoka tibirinzi, wakampatia Ussi kijimfuko.
Hapo sikujiuliza sana, nikajuwa moja kwa moja Ussi kwa wivu wake amemtuma mmoja wa wavuvi wake waje kuchunguza naongea nini na dada yake, hivyo nikapanga kupunguza sauti na kuongea sauti ya chini sana, wakati huo watu wengi sana walikuwa wanatutazama sisi, sikuelewa kwanini, “hoooo!, kwahiyo unakaa hapa messi eeh?” aliuliza Jessenia, huku tunaendelea kusakata taarab, “hapana! na kaa kule Ali Khamis camp” nilimjibu huku namtazama huyu mwana dada ambae ukiachilia uzuri wa sura na umbo lake pia sasa niliweza kuziona nywele zake nzuri ndefu ambazo kama sio kuzifunga kwa msuko wa mkia wa farasi na kuegesha mtandio wake mabegani ulioziba nywele ile basi ningeweza kuziona mpaka mgongoni, sikumjali tena yule jamaa ambae alikuwa anacheza karibu yetu, hakika nilitamani kumueleza Jessenia vile ninavyo muona, “Jesse kuna kitu nataka nikuambie, sidhani kama nitakuchukiza” nilimuambia kwa sauti tulivu huku namtazama usoni, na yeye akainua uso huku anatabasamu, “ushaanza Eric, inahusu nini?” aliuliza kwa sauti iliyolegea na kujaa aibu, huku anajichekesha chekesha na kuinua uso wake akinitazama usoni, “nataka nikuambie ukweli toka moyoni” nilisema kwa sauti ile ile, hapo nikamuona Jessenia anatabasamu, huku anakwepesha macho yake, ambayo sasa yalianza kulegea, “haya niambie nakusikia, lakini usinilazimishe nifurahie utakacho niambia” alisema Jessenia, huku tunaendelea kucheza music huu ambao sikuwahi kutegemea kama nitakuja kuucheza siku moja, “ukweli Jesse, toka siku ya kwanza nilipokuona niliuona uzuri wako wazi kabisa, tena nikakubali moyoni kuwa wewe ni mrembo, na nikakiri kuwa sijapata kuona mwanamke mrembo kama wewe, lakini leo nimegundua kuwa wewe ni mzuri sana, hongera Jesse, yaani umependeza sana usiku wa leo” niliyasema hayo kwa sauti moja tulivu sana, huku namtazama Jessenia usoni, nikamuona anainua uso wake na kunitazama usoni, macho yetu yakakutana nikamuona anaachia tabasamu la furaha huku anaachia mikono yangu na kuiamishia mikono yake begani kwangu kisha akalaza kichwa chake kwenye bega langu la kulia, na kufanya matiti yake yaguse kifua changu, “asante Eric, pia napenda unavyoliita jina langu” alisema Jessenia huku kwa sauti ya kitandani kabisa, huku nikihisi pumzi za mihemo yake ikitekenya shingo yangu na kunisisimua, nikajikuta napeleka mikono yangu kiunoni mwake na kumshika vyema kabisa huku tuna endelea kusakata taarab, hapo nikasikia akivuta pumzi ndefu na kuiachia kwa msisimko, mfano wa mtu aliemwagiwa maji ya baridi, “unajina zuri sana na linatajika kwa kila namna, ukitaja Jessy, Jesse, au hata Seni, au Senia, yote ni matamu kwangu” nilimueleza kwa sauti ya chini, na hapo nikasikia kicheko laini cha kivivu, kilichotoka mdomoni mwa Jessenia, hakika ilileta raha fulani moyoni mwangu, na kujikuta natamani kupata kitumbua cha mwanamke huyo, ambae kwa mara ya kwanza alinifanya nitamani kuwa na mke.
Naam tuliendelea kucheza taratibu, huku tunapeana maneno ambayo sikuwaza mwisho wake utakuwa nini, mara nikakumbuka kutazama meza ya Ussi, ukweli sikumuona Ussi, walibakia wale wanawake peke yao wakiendelea kunywa pombe, nikamtazama yule jamaa yake nae sikumuona kabisa, hilo sikuliwazia sana, maana nilihisi pengine Ussi ameenda chooni na yule mwingine sikuwa na muda nae, “Ticha, naona upo na Seni” ilisika sauti toka pembeni yetu, wote tuka tazama ilikotokea sauti, nikamuona afisa utawala bwana Malambo, ambae alikuwa anacheza na mschana moja hivi mrembo kiasi, ambae pia alikuwa anatutazama kama Malambo alivyofanya, “nakuona upo na shemeji” nilimuambia Malambo, huku wote tukiendelea kucheza na wenza wetu, “pamoja kaka” alisema Malambo, kisha kila mmoja akaendelea na hamsini zake, na wakati huo huo nikamuona Ussi akitokea nje ya ukumbi na kwenda kwenye meza yake huku anakata jicho upande wetu.
Baada ya hapo hatukucheza sana, tukarudi mezani kwetu na kuendelea na wine yetu, “yaani mlipendeza sana, unajuwa Seni sijawahi kuona ukicheza taarab” alisema Aisha kwa sauti ambayo ilionyesha wazi kuwa amestaajabishwa, “yani walipendezana utadhania ni mtu na mke wake” alisema Mwasenga, huku anatumiminia wine kwenye glass zetu, kwa maneno hayo nikajikuta na mtazama Jessenia, ambae pia alikuwa ananitazama macho yetu yalipokutana tukajikuta tuna tabasamiana, kisha Jessenia akakwepesha macho yake na kuitazama glass yake ya wine kisha akainyakuwa na kuipeleka mdomoni, na mimi nikafanya hivyo hivyo.
Naam tulimalizia chupa ya kwanza na kufungua ya pili, “tushakuwa walevi sasa, huwa nakunywa chupa moja tu” alisema Senia, huku wakati namkabidhi glass yake ya wine, “lakini mmekunywa nusu chupa na sasa kila mmoja ataenda kukamilisha chupa moja” alisema Aisha na wakati huo huo tukashtuka mtu akiwa amesimama pembeni yetu, “mambo vipi jamani, naona mnaendelea kuenjoy” wote tuka mtazama muongeaji, ambae sauti yake haikuwa ngeni masikioni mwetu, huyu alikuwa ni Ussi………. Itaendelea usiku
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom