Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

Naam Kwa Mara Nyingine Tena, Hii Ni Kwa Wale Wapenzi Wa Simulizi Mzuri Zenye Kusisimua Kutoka Kwa EDGAR MBOGO Leo Nakuletea Simulizi Mpya Inayokwenda Kwa Jina La (KIFO CHA HAWARA (Mkono Wa Jini) Itakayo Kujia Hapa Hapa JamiiForums Mwanzo Mwisho, Hii Sio Ya Kukosa, Na Kama Ulipitwa Na Simulizi Zilizotangulia Basi Utazipata Kupitia Kiunganishi Hiki
👇
1) NYUMA YA MLANGO WA ADUI
Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui | JamiiForums Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

2)ASALI HAITIWI KIDOLE
Thread 'SIMULIZI: Asali haitiwi kidole' SIMULIZI: Asali haitiwi kidole
3) TEMBELE LA UWANI
SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO) | JamiiForums SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

Sapoti Yako Inahitajika Kwa Mtunzi Ili Kumpa Moyo Na Kumpa Hamasa Ya Kuboresha Na Kukuza Kipaji Chake Atuburudishe Zaidi, Kama Una Lolote Iwe Ushauri Au Maoni Au Hata Mchango Wa Bando Au Kifuta Jasho Basi Mawasiliano Yake Ni Haya
+255 743 632 247
Tuwe Pamoja Hadi Mwisho...
Mrembo Shunie
 
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA ISHILINI NA NNE
MTUNZI: Mbogo EDGAR
NUMBER +255 743 632 247
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA TATU: Naam tulimalizia chupa ya kwanza na kufungua ya pili, “tushakuwa walevi sasa, huwa nakunywa chupa moja tu” alisema Senia, huku wakati namkabidhi glass yake ya wine, “lakini mmekunywa nusu chupa na sasa kila mmoja ataenda kukamilisha chupa moja” alisema Aisha na wakati huo huo tukashtuka mtu akiwa amesimama pembeni yetu, “mambo vipi jamani, naona mnaendelea kuenjoy” wote tuka mtazama muongeaji, ambae sauti yake haikuwa ngeni masikioni mwetu, huyu alikuwa ni Ussi……..ENDELEA……
Ambae alinishangaza kidogo, maana tofauti na wakati ule amekaa kwenye meza yake alivyokuwa na uso wa hasira, sasa alionekana amaechangamka huku anaachia tabasamu la kirafiki, “tupo kaka naona una wacheki JKU wanafanya yao” alijibu Mwasenga huku mimi nikiwa bado katika mshangao na mduao, huku moyoni nikijipatia jibu la kwamba nilikuwa nawaza tofauti juu ya Ussi, “ndiyo bwana si unajuwa mambo yetu haya, ila ticha hayajui haya, amezowea bongo flever” alisema Ussi na hapo wote tukacheka kidogo, kasoro Jessenia peke yake, ambae ndio kwanza alikuwa anainua glass ya wine na kuipeleka mdomoni, na kwa mtazamo wangu wa haraka ni kama hakupenda ujio wa Ussi pale kwenye meza yetu, “haya mambo hata kwetu yapo bwana, kwani hujaona nilivyokuwa nacheza?” nilisema hivyo na wote
tukacheka tena kasoro Jessenia kama ilivyokuwa mwanzo, yeye alikuwa busy na kinywaji chake, “poa wakubwa mimi naomba niwanyang’anye huyu mwarabu, anaenda kupumzika” alisema Ussi, kwa sauti ya kirafiki kabisa, yaani usingeamini kuwa yeye ndie yule alikuwa ananikata jicho baya.
Hapo nikamuona Jessenia anaitazama saa yake mkononi huku uso wake ukionyesha wazi kuwa amenuna, “jamani kaka, mbona muda bado ndio kwanza saa tano” alisema Jessenia kwa sauti ya kulalamika, “shauri yako bwana, kama hutaki kuondoka sasa hivi utajuwa mwenyewe utakavyo rudi nyumbani” alisema Ussi kwa sauti ile ile ya uchangamfu, kisha akaondoka zake kuelekea nje ya ukumbi, na sisi tukimsindikiza kwa macho, tukisaidiana na Jessenia, ambae kiukweli alikuwa amenyongea kidogo.
Kiunyonge Jessenia akageuza shingo yake kumtazama Aisha, “sasa Aisha mie naenda zangu tutaonana basi” alisema Jessenia, huku ananishika mkono wangu na kuinuka toka kwenye kiti, akiwa ameushikilia mkono wangu kwa maana ya kwamba alihitaji tuinuke wote, “haya Seni, mungu akijalia tutaonana” alisema Aisha, huku yeye na Mwasenga wakitutazama kwa mshangao, maana hawakuelewa maana ya tukio lile la Jessenia kunitaka na mimi niinuke pamoja nae, kwa haraka haraka hata mimi sikuweza kumuelewa Jessenia, ila nikaelewa baada ya sekunde kadhaa kuwa Jessenia alitaka nimsindikize nje.
Sikuwa mbishi niliinuka na kuanza kutembea kuelekea nje, huku amenishika mkono ungesema ni watu ambao tupo kwenye mahusiano ya kimapenzi, “sijui kwanini huyu mjinga ananitoa mapema hapa wakati taarab ndio inaanza kunoga” alisema Jessenia, wakati tunakatika kwenye makundi ya watu kuufuata mlango wa kutokea nje, huku macho ya watu yakitufuatilia, “pengine amechoka kukaa hapa” nilijibu kirahisi huku tunazidi kuusogelea mlango, “hakuna cha kuchoka wivu wake tu, hapo amesha waza kuwa mimi na wewe ni wapenzi” alisema Jessenia, kwa sauti ile ambayo sasa ilionekana kuwa na chuki ya wazi, “kwani ulikuja nae?” nilimuuliza swali fulani la kizushi, maana huwa nasikia kuwa siku zote huwa anakuja na shangazi yake, “ndio leo amenileta yeye, maana shangazi ameenda unguja na mjomba, wameondoka leo saa tisa kwa ndege” alisema Jessenia, na hapo nikashangaa kidogo, kwanini Ussi aje na dada yake kisha akamuacha anatafuta meza huku yeye anaponda raha na wale wanawake, wakati huo tulikuwa tunauvuka mlango wa kuingilia ukumbini, nakuibukia nje, ambako tulimuona Ussi amesimama hatua kadhaa toka kwenye mlango ule, ni wazi kama alikuwa anatusubiri sisi, “Ticha asante sana kwa kumpa kampani dada yangu, naona leo amefurahi sana kuliko siku zote, maana sikuwahi kumuona akicheza music” alisema Ussi kwa uchangamfu mkubwa, mimi na Jessenia tukacheka kidogo, japo niliona wazi kuwa Jessenia alikuwa ana jilazimisha kucheka, “lakini yeye ndie alikuwa mwalimu wangu” nilimuambia Ussi, huku tunazidi kumsogelea Ussi, ambae sasa alikuwa anaanza kutembea kulifuata V8 lililokuwa limeegeshwa kwenye maegesho ya magari pale Wawi Messi ambapo palikuwa na magari machache likiwepo gari la Mwasenga, yani lile land lover defender la jeshi, “basi poa kaka wacha nimuwaishe huyu” alisema Ussi huku anafungua mlango wa gari, “poa poa bro” nilijibu huku najaribu kujipapatua toka kwenye mkono wa Jessenia, ambae hakuwambishi kuniachia, ni kama na yeye alijishtukia kwa kuning’ang’ania mkono kwa muda mrefu, “asante sana Eric, nilipenda kuwa hapa muda mrefu lakini ndio kama hivyo tena” alisema Jessenia ambae hakusubiri niongeze neno, yeye akaondoka zake kuelekea kwenye gari, nikishuhudia makalio yake yakitikisika kwa fujo kutokana na mwendo wa haraka aliokuwa anautembea, hakika aliutekenya moyo wangu na kusababisha usukume damu nyingi kwenda chini ya mwili, ambako ilijaa kwenye mishipa ya damu iliyotambaa kwenye dudu na kuisimamisha, kama sio suruali ya jinsi niliyovaa kuwa ya kubana kidogo, basi ningeumbuka, maana lazima ingeonekana wazi ikivimba mbele ya suruali yangu, na kitu kilichonishangaza na kunisisimua zaidi, nipale alipopiga hatua kadhaa na kugeuka kunitazama, macho yetu yalipokutana nikamuona akitabasamu kwa aibu, nilijistukia kwamba amegundua nilikuwa na tazama nini kwenye mwili wake, lakini sikuacha kumsindikiza kwa macho, nilimtazama mpaka alipoufikia mlango wa gari na kuufungua ndipo alipogeuka na kunitazama tena, na kuniona bado ninamtazama akatabasamu huku ananipungia mkono, kisha akaingia ndani ya gari na Ussi akaliwasha gari na kuliondoa kwa fujo kutoka pale kwenye eneo la Wawi Messi, sikuweza kuona ndani, maana gari lilikuwa na vioo vya giza, yaani tinted.
Nililisindikiza kwa macho gari lile mpaka lilipotoweka kuelekea mjini, nikarudi ndani huku moyo wangu ukiwa mwemwele kwa furaha ungesema mtoto amepewa nguo ya sikukuu, yani ile kukumbatiwa na mwanamke ambae watu wanasema kuwa amesha tokewa na wanaume kibao na amewatosa na mpaka anaondoka anaonekana kuwa bado anatamani kuendelea kuwa na mimi, unajuwa kuna kitu msomaji hujakielewa vizuri, ni kwamba unaposikia mwanamke mzuri basi naamini ujawahi kukutana na Jessenia, hapa namzungumzia mwanamke mmoja mzuri haswaaa, tena mrembo kisawa sawa, urembo ambao umenifanya nianze kuweweseka, hasa ninapo kumbuka kicheko chake na ile tabasamu lake.
Naam wakati natembea nikikatiza kwenye makundi ya watu waliokuwa wanaendelea kucheza taarab, nikashtuka nikingusa mtu mmoja kwa bahati mbaya, “hooo! samahani” nilisema huku na geuka kumtazama mtu huyo niliemgusa, alikuwa ni kijana mmoja aliekuwa anacheza na mwanamke, ambae alikuwa amekumbatia na nae kabisa, na alipata faida ya mwanga hafifu uliokuwepo kumshika maziwa yule mwanamke, “usijali kaka” alijibu yule kijana huku yule mwanamke aliekuwa anacheza nae alikiinua uso kunitazama, hapo nikajikuta uso kwa uso na mwanafunzi wangu, yaani Maimuna, ambae ile kuniona tu akakwepesha uso wake haraka sana, sikuhitaji kumsemesha kwa vile alimua kuficha uso wake, hivyo nikaondoka zangu kuifuata meza yetu ambayo sasa nilimuona Aisha peke yake, Mwasenga hakuwepo, “hivi we mwanamume unakizizi gani toka huko kwenu bara?” aliuliza Aisha, mara tu nilipoifikia meza, japo swali nililiona kama utani lakini ukweli ni kwamba Aisha hakuwa na dalili ya utani, “kwanini Aisha?” nilimuuliza nikijifanya sijaelewa anachomaanisha, “mh! Eric, hivi unajuwa umewashangaza wengi, kuweza kumuinua Seni kwenda kucheza nae?” aliuliza tena Aisha, japo niliamini anachoongea ni cha kweli lakini sikutaka kuonyesha kuwa na mimi naamini hivyo, “kwani mimi ndie nilimuinua au yeye ndie alieniinua?” nilijifanya kama vile sikuwa na mpango wowote na jambo lile, “sasa hilo ndilo jambo la ajabu zaidi, achilia kama wewe ungemuomba mukacheze, yaani hata mwanaume ange mbembeleza vipi asingeinuka kabisa, sikuwahi kumuona akicheza labda na mwanamke mwenzie” alisema Aisha, akionyesha kushangaa sana, hapo sikutaka kuchangia lolote, nikajifanya kupotezea kwa kuchukuwa glass ya wine na kupeleka mdomoni, nikapiga funda moja kisha nikaweka glass mezani na kutazama kule kwenye meza ya Ussi, ambako niliweza kuwaona wale wanawake wawili wakiwa pale pale, wanaendelea kunywa vinywaji vyao, “ila kaka anawivu na dada yake yule unaweza kusema anatembea nae yeye mwenyewe” alisema Aisha, na wakati huo nikamuona mwasenga anakuja na chupa ya Wine mkononi, “kaka hii nimekuletea kama hongera, maana kama ni kizizi basi hicho chako ni noma” alisema Mwasenga huku anaweka ile chupa mezani, “kaka utaniua hii moja ndio kwanza ninaianza” nilisema huku nacheka kidogo, “utaibeba, utapiga kesho magetoni” alisema Mwasenga huku anaisogeza ile chupa karibu yangu, “haya bro asante sana”
Tuliendelea kunywa na kuongea mawili matatu, huku tuna tazama watu walivyokuwa wanasakata taarab, mara zote nilipokea wageni kwenye meza yetu wakinisifu na kunipongeza kwa kuweza kung’oa mtoto Jessenia, ndivyo walivyo amini wao, ila mimi ndie niliejuwa ukweli kwamba sikuwa nimemtongoza mwanamke yule, na hata sikujaribu kufanya hivyo, kati ya watu waliokuja kunipongeza ni Komba na mwenzie Malambo, pia nakumbuka dakika ishirini baadae toka Jesenia aondoke pale wawi messi, nikamuona Ussi akiwa amerudi na kujiunga na wale wanawake wake, sikutaka kushangaa sana, maana nilijuwa kuwa pengine Ussi alimrudisha dada yake ili apate mwanya wa kustarehe vyema na wale wanawake, ukiachilia habari ya bwana Ussi pia nilieweza kumuona yule jamaa wa Ussi akienda kujiunga na bwana Ussi, sikutaka kujuwa kwanini alitoweka kwa muda.*****
Naam onyesho lile liliisha saa saba za usiku, tulimfikisha Aisha nyumbani kwake na mwasenga akanipeleka Green House nikiwa na chupa yangu ya wine, ambako kiukweli sikuchukuwa hata nusu saa nikapitiwa na usingizi, ambao ulinibeba mpaka saa mbili ya asubuhi, nikiamshwa na ngurumo za gari zilizokuwa zinapita kwenye barabara ya kuelekea vitongoji mpaka makahani, niliamka nikiwa nahisi kichwa kizito kidogo, sio kama vile nikinywa bia, nikaingia bafuni nakujimwagia maji, kisha nikaenda kupata supu ya kuku yenye pili pili nyingi na soda ya cola yenye ubaridi mwingi, hapo nikaona nipo sawa, nikarudi green house na kujifungia ndani, sasa nilijilaza kitandani na kuanza kutulia kwa sekunde nikitafakari baadhi ya mambo niliyo yaona jana, maana ukiachilia kuonekana nyota kwa kuwa karibu na Jessenia, pia niliwaza kuhusu mambo kadhaa ambayo nilihitaji majibu yake, kwanza ni ule wivu wa Ussi kwa dada yake, hakika ulikuwa ni wivu mkubwa sana, ni wivu ambao ungeweza kusema ni wivu wa mtu kumuonea mpenzi wake, nilitaka kuamini kuwa kwa kuwa ni binamu yake pengine anatembea nae, lakini ingewezekana vipi wakati na yeye ameonekana yupo na wanawake, ambao naamini kuwa mmoja ni mpenzi wake, pili ni namna ambavyo Jessenia alivyokuwa ananitendea, ungesema ni mtu ambae tunafahamiana kwa muda mrefu sana, japo ndio siku ya kwanza kukaa pamoja, maana hata siku ile pale uwanjani, nilipishana nae tu na sio kuongea nae kama ilivyokuwa leo, niliwaza hayo mpaka nilipopitiwa na usingizi na kulala fofofo, mpaka mida ya saa saba za mchana, niliposhtuliwa na mlio wa simu yangu, nikaichukuwa pembeni ya mto na kuitazama kwenye kioo kutazama jina la mpigaji, ilikuwa ni simu toka ofisini dar es salaam kwa mkurugenzi wa MSC, yaani bwana Winfred, hapo nikakumbuka kuwa nilishasahau kuhusu kazi iliyonileta huku Pemba na kutopea kwenye matamanio ya kingoni……… Itaendelea Muwe Na Usiku Mwema
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom