Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

Kifo cha hawara (Mkono Wa Jini)

KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA KUMI NA NNE
MTUNZI: Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA MBILI : nilishangaa sana, maana niliwahi kufungua vitasa vizuri na vya kisasa, ambavyo ni vigumu zaidi kwa muda mfupi sana, lakini iweje hiki cha kawaida kabisa nimeshindwa kukifungua, “kumbuka huwezi kuufungua mlango ambao tayari upo wazi” nilikumbuka maneno ya professor Wang Sun, mkufunzi wa chuo cha ujasusi cha korea ya kusini, nikashika kitasa na kukinyonga mlango ukafunguka kirahisi kabisa, na nilipotazama vizuri niligundua kuwa kitasa kile kilikuwa kimevunjwa, hapo kengere ya tahadhari ikagonga kichwani mwangu……..ENDELEA….
“pumbavu, kuna mtu kanitangulia” nilijikuta najipa jibu kwa sauti ya kunong’ona, huku na chomoa bastora yangu kwenye kijifuko kidogo cha kwenye mkanda na kuishika vyema, halafu nikaingia ndani kwa tahadhari kubwa sana.
Ile naingia tu nikakajikuta kwenye korido refu lenye milango mitatu upande wa kushoto na mmoja kulia, ule wakulia ulikuwa ni wa jikoni na iIe ya kulia ilikuwa imefungwa, nilienda mpaka sebuleni nikakuta vitu vime vurugwa sana, na nilipotazama vizuri nikaona mashine inayo contor camera za ulinzi za nyumba ile ikiwa chini karibu na kona moja ya nyumba ile pale sebuleni, lakini mashine hiyo ilikuwa imefunguliwa, hapo nikajuwa kuwa tayari HD imesha ondoka, nilipo ikagua nikagundua kuwa ni kweli ilikuwa imesha nyofolewa, nikajaribu kukagua kidogo pengine ningeona kinachonifaa, ukweli sikubahatika kuona chochote, “kwahiyo muuwaji mwanzo hakujuwa kama kuna camera sasa amekumbuka vipi?” niliwaza hilo na kujipatia jibu, kwamba wakati tunajadili pale msibani lazima muuwaji au mshirika wa muuwaji alitoa taarifa kwa wenzake waje waichukue, kwa maana hiyo kuna ulazima wa kesho kwenda msibani kuchunguza muuwaji ni nani, maana lazima atakuwepo pale kwaajili ya kuangalia mwendo mzima wa kile alichokifanya
Sikuwa na sababu ya kuendelea kukaa pale, muda wowote polisi wangepewa taarifa na kuja kuisaka HD, nikaona itakuwa vyema kama nitaondoka zangu, hivyo nikatoka nje ya nyumba ile huku kichwani mwangu nikipata picha ya kwamba, aliefanya vile siyo jini, ila ni mtu wa kawaida ambae alidhamilia kuficha ushaidi kwa kile kilichomkuta kijana Masuod, sasa niliona kuna ulazima wa kuongeza juhudi za kufanya uchunguzi wa kina juu ya jambo lile, maana kulikuwa na dalili ya kwamba, muuwaji hakuwa jini, sasa swali lilikuwa ni vipi mtu akauke na kubadilika rangi kwa muda mfupi mara tu baada ya kuuwawa, swali hilo lilinisumbua hata wakati wa kulala, na leo ndio siku ambayo nilipiga simu kwa mkurugenzi, kumpa taarifa za mwanzo juu ya hisia zangu, kuwa muuwaji sio jini ila ni mtu wa kawaida, ambae amekumbuka kuja kuchukuwa HD, akiingia ndani kwa kuvunja mlango kitu ambacho jini asingekuwa na ulazima wa kupitia mlangoni, maana niliwahi kusikia jini ana uwezo wa kuingia sehemu kama upepo au kiumbe chochote kidogo.******
Siku ya pili niliamka mapema sana, nika abiria gari la mwasenga ambae alikuwa anaenda kuchukuwa walinzi kule mess, akaniacha gombani ambako nilikuta wanafunzi na walimu wanaanza kuingia, akiwepo mwalimu Aisha, “Eric umesikia kilicho tokea jana?” aliniuliza Aisha, wakati tunaanza kukusanya wachezaji na kuwapa maelezo ya jinsi itakavyo kuwa na mipangilio wakati wa mashindano, “kuhusu jini kufanya mauwaji?” nilimuuliza Aisha, “ndiyo huyo tena hilo litakuwa jini haswaaaa” alijibu Aisha, na kunipa maelezo jinsi alivyo sikia, haikuwa tofauti na yale ambayo niliyasikia.
Nusu saa baadae gari la shule ya utahani, liliingia na kushusha wanafunzi huku raia wegine wakianza kushuka toka kwenye basi, “asalem Alaykum mwalimu Pross” ilikuwa salamu ya mwanafunzi wa kike, salam ambayo ilinishtua sana, maana jina hili nilijitambulisha kwa wanafunzi wachache sana hapa pemba, hivyo nilishawishika nigeuze uso wangu na kumtazama mwanafunzi huyo, ambae alikuwa amevalia nguo za kiraia yaani gauni refu na kitambaa kichwani yani hijab kama wanafunzi wengine waliokuja kutazama mashindano, alikuwa ni Maimuna, hapo nikajikuta nacheka kidogo, “hooooo! Maimuna walaykum salam…. Hivi na wewe… ni mwanafunzi wangu” nilisema huku moyoni nikijihisi noma flani, maana Maimuna ni yule mschana nilie kutana nae kule kwenye uwanja wa mpira wa kikapu kule chake chake, “ndiyo nasoma form three” alisema Maimuna, ambae sikutaka kuongea nae sana kwa wakati ule.
Michezo ilienda vizuri watu walikuwa wengi wake kwa waume, muda mwingi nilikuwa karibu na mwalimu Aisha, na nilipotengana nae kidogo, nilimuona Maimuna akisonga songa, “kwahivyo mwalimu wewe unakaa pale Ali Khamis, sivyo” aliuliza Maimuna, ambae alikuwa ananukia udi, “yes, nakaa green mess nilikosa nyumba mtaani” nilimjibu, Maimuna ambae ilikuwa haishi kujichekesha, “hooo kumbe, hivyo umekuja na mke wako?” aliuliza tena maswali, huku nikiona mswali yake nikiona kuwa sio ya mwanafunzi na mwalimu, “hapana Maimuna nipo peke yangu” nilimjibu huku nacheka kidogo, “hivi mwalimu, Aisha ni mwanamke wako eeh?” aliuliza Maimuna, swali ambali lilinishangaza kidogo, inakuwaje mwanafunzi anauliza mswali kama yale, “hapana sio mwanamke wangu” nilijibu pasipo kumtazama Maimuna, “mwalimu Pross, vipi leo utakuja mazoezini kule nyumbani” aliuliza Maimuna na hapo nikatulia kidogo, na kupanga ratiba yangu haraka haraka.
Ukweli ilikuwa lazima niende msibani, yaani mazishini ili kujaribu kupata habari ambazo zinaweza kunisaidia, nilihisi muuwaji au mshirika wa mauwaji atakuwepo pale msibani, kujuwa nini kinaendelea, baada ya hapo niende kuongea na Hassan muhudumu wa Madungu guest House na pia niende hospital ya pale chake chake kupata majibu ya vipimo ya mwili wa Masoud, hospital ambayo ipo karibu kabisa na uwanja wa baskert ambao Maimuna alikuwa anauzungumzia, “yah! nitafika mazoezi jioni, kuna kitu unaniandalia” niliuliza kwa utani, pasipo kudhamilia kuhusu kuandaliwa kitu.
Kwanza nilimuona Maimuna akiachia kicheko flani hivi, ambacho sikuweza kukipa jina kama cha aibu au cha raha, au vyote sawa, “kwani unataka nikuandalie kitu eeh?” aliuliza Maimuna, huku kile kisauti chake cha lafudhi ya kipemba, kikinifurahisha na kutamani kuendelea kuisikiliza, “mh! hapana Maimauna, japo mimi ni mwalimu wako, lakini sidhani kama nitaweza kukaribia kwenu au kupokea chochote pale uwanjani, labda siku nyingine” nilisema hivyo huku namtazama huyu mschana ili kujiridhisha kwamba na yeye alikuwa katika utani kama mimi, lakini macho yetu yaka kutana halafu mwanafunzi huyu akatazama chini kwa aibu huku anacheka cheka, “sawa basi jumatatu” alisema kwa sauti iliyojaa furaha, huku anaondoka kwa kukimbia, nadhani unaweza kupata picha aina ya mbio za kike zile za kujishauwa alizo kimbia Maimuna, ambae kiukweli alinishangaza kidogo, japo niliondoa shaka baada ya kukumbuka maadili waliyonayo watoto wa huku, ambao siku zote wazazi wao hutumia muda mwingi kuwaonya kuto kujihusisha na ngono za mapema.
Kitu kinginine ambacho niligundua sekunde chache baadae ni pale nilipomuona mwl Aisha akija pale niliposimama, ikiwa ni sekunde chache baada ya Maimuna kuondoka, ilionyesha kuwa Maimuna alimuona Aisha aliekuwa anakuja, ndio akaamua kuondoka zake, ina maana huyu mwanafunzi alikusudia kabisa kuongea na mimi, sasa kwanini anafanya hivi, hata hivyo nilipotezea maana mabinti wa huku pemba hawajiusishi na ngono kabla ya ndoa.
Saa tano michezo iliisha, tulifanikiwa kushinda baskrt ball, kwa wanaume na volleyball kwa wanawake, tulipoteza volley ball kwa wanaume, ukweli muda wa michezo niliona kama napoteza muda, maana nilitakiwa kuhudhuria mazishini ambako nilihisi kuwa mtu ambae alitambua uwepo wa HD kwenye nyumba ya Masoud alikuwepo, hivyo basi sikutaka kuelekea kambini kwanza nilielekea moja kwa moja mjini, na kwa kutumia usafiri wa chai maharagwe, lile gari la abiria lenye mlango kama wa kabati, sikutumia usafiri wa jeshi kwasababu tayari lilisha tangulia msibani kuwapeleka wakina Malambo.
Saa sita na robo ndio muda ambao nilishuka toka kwenye gari pale njia panda ya juu, kabla ya kupita inayo elekea msingini, yaani pale tulipopita jana usiku, haikuwa ngeni kwangu nilitembea nayo taratibu huku nikitazana yale mazingira vizuri kabisa na sasa niliweza kuyaona vyema, nilipita majumba ya kifahari na nilikuja kushangaa kile kijumba cha udongo ambacho sasa niliweza kukiona vyema kabisa jinsi kilivyo, ukweli kilikuwa ni kibanda dhaifu cha hali ya chini sana, japo kilikuwa na dalili ya mtu kuishi ndani yake, lakini hakukuwa na dalili ya uwepo wa mtu kwa muda ule, maana hata mlango uliotengezwa kwa bati chakavu ulikuwa umeegeshwa kwenye sehemu yake, nilitembea kwa haraka ili niwahi eneo la msiba, ambapo sikujuwa mazishi ni saa ngapi, huku nalipita eneo lile lenye nyumba chakavu na kuufikia ukuta mkubwa wa uzio wa nyumba ya kifahari ambayo leo hii niliweza kubaini kuwa ilikuwa ni ya ghorofa mbili, ilikuwa ni nyumba nzuri sana tena ya kifahari.
Naam dakika tano baadae nilikuwa nimesha karibia kabisa eneo la tukio, nikifanikiwa kuliona gari la jeshi, na ukweli ni kwamba nilikuwa nimesha chelewa sana, maana nilikuta watu ndio wanaanza kula, tayari walishatoka mazishini na sasa walikuwa wanapata chakula ili watawanyike kwenda majumbani kwao, “Eric, ungepumzika maana mazishi yalifanyika saa tano kasoro alinieleza Malambo wakati ninakaa karibu yake, “sikuona vyema kuacha kuja kwenye mazishi, unajuwa huyu marehemu nilifahamiana nae juzi na jana mchana kabla haja uwawa nilimuona kwa mara ya mwisho” nilifafanua kwa Malambo, yani yule afisa utawala wa jeshi, “ok! tuguse guse tukajazie mess” alisema Malambo, wakati huo nilikuwa naletewa chakula na maji ya kunawa.
Nilianza kula huku macho yangu yakipepesa kushoto na kulia nyuma na mbele kama ningeona chochote cha kunisaidia, lakini ukweli mpaka namaliza kula sikuweza kuona chochote, ila wakati na nawa, “hivi mahadhi huyo jinni alipotea poteaje” niliweza kusaikia vijana fulani wakiongea mita chache toka pale nilipokuwa nanawa, nikageuka kuwatazama, nikawaona vijana watatu walio simama pamoja, mmoja wao nilimtambua kuwa nilikuwa nae kwenye mazoezi juzi kule chake chake, “yani mimi nilipomuona anatoka kwa haraka huku ana wasi wasi nikajuwa wamegombana na kaka Masoud, nilisubiri kwanza aondoke, na alipopotelea kule upande wa Makondeko ndipo nikakimbilia ndani ili nikaendelee kucheza game, maana sikuwa na haja ya kuuliza kilichotokea mpaka yule mwanamke akaondoka haraka, ile kuingia ndani nilimkuta kaka Masoud akiwa amelala sakafuni pale sebuleni huku amekuwa mweusi sana, tayari amesha kufa, ndio nikapiga kelele kuita watu” alisema kijana mmoja ambae alionekana ni mdogo kuliko wale wote na alionekana kuwa na huzuni kubwa sana, hapo sikuhitaji kuuliza wala kupewa ufafanuzi kujuwa kuwa huyu kijana, ndie yule alie kuwa nyumbani kwa Masoud wakati Masoud alipokuja na mwanamke mwenye niqab.
Ukweli maongezi yale haya kuniacha salama yalinifanya nisogelee kati yao, “oya kaka niaje” nilisalimia kwa salam ya ujana, nikimtazama yule ambae nilikuwa namfahamu, “hooo! Pross mambo vipi, mbona jana hukuibuka mazoezi?” aliuliza yule jamaa ambae sikumfahamu kwa jina, ila alichangamka kama rafiki wa muda mrefu, akiniita jina nilililojitambulisha kwa Maimuna, “jana nilienda gombani kulikuwa na mzoezi ya wanafunzi wa Fidel Castory, ila leo jioni nitakuja” nilimueleza yule jamaa, ambae katika maongezi ya pale niligundua kuwa alikuwa anaitwa Suleyman, “nilisikia mukiongelea habari ya jini, ina maana huyu jamaa ndie aliemuona jini jana, napenda kusikia jinsi alivyo, maana sijawahi kuona jini” niliongea kama mtu mwenye nia thabiti ya kujuwa nilicho maanisha, kumbe nilikuwa nataka kujuwa hadithi ya tukio la mauwaji ya Masoud, wawili kati yao walicheka kidogo, ila yule aliesema kuwa alikuwepo alitabasamu tu!, “unadhani jini utamuona akiwa na pembe au mkia?” aliuliza Suleiman, na hapo yule kijana mdogo, akadakia, “yaani kaka asikuambie mtu, huyo mwanamke bomba la demu, nadhani angekuwa hajavaa niqab ningeona jinsi alivyo mzuri, yaani ukiona mpaka braza Masoud ameamua kumchukuwa yule mwanamke na kumpeleka nyumbani, basi huyo mwanamke ni mzuri kweli kweli” alisema yule kijana mdogo, na hapoo akaanza kusimulia, wacha na mimi nikueleze kama alivyo eleza yule jamaa, ambae nilimsikiliza kwa umakini sana.
Ilikuwa hivi, kijana huyu ambae jina lake ni Mahamud, akiwa sebuleni ndani nyumbani kwa Masoud Vuai anacheza game kwenye computer, ni kawaida yake kufanya hivyo mara kwa mara, ndipo aliposikia ngurumo ya vesper ikisimama nje ya nyumba ile ya bwana Masoud, yeye akajuwa kuwa lazima atakuwa yeye mwenyewe mwenye nyumba, lakini ilimshangaza kidogo, kwa sababu mida ile ilikuwa ni mida ya ibada ya ijumaa, hivyo akatulia kwanza kuona kama ni yeye au kuna mgeni mwingine amekuja na shida zake, “karibu sana, ondoa shaka, huku ni mbali sana, hakuna mtu atajuwa kama tupo huku” kijana Mahamud, alimsikia Masoud akimkaribisha mtu, “sikusikia mtu akijibu, lakini nilisikia kicheko cha sauti ya kike” alisema Mahamud, na walipoingia ndani ndipo Mahamud akabahatika kumuona mschana alietangulizana na Masoud, “yaani japo alivaa niqab lakini ni mzuri huyo mwanamke, ana umbo kama mnyamwezi (mtu kutoka bara)” alisema Mahamud, akiendelea kusimulia kuwa, Masoud alimsalimia Mahamud kisha wao wakapitiliza kuelekea upande wa vyumbani, wakimuacha Mahamud anaendelea kucheza game kwenye computer pale sebuleni, huku kichwani mwake, akiwaza kuhusu kitendo cha Masoud kuingiza mwanamke pale nyumbani kwake, “hata hivyo nilijipa moyo kuwa pengine ndie mwanamke anae hitaji kuishi nae, maana haikuwahi kutokea hapo mwanzo yeye kuingiaza mwanamke pale nyumbani kwake” alisema Mahamud, kisha akaendelea “lakini dakika mbili baadae, Masoud akatoka huku amevaa bukta tumbo wazi, akasema kuwa niwapishe kidogo akitoka nitarudi kuendelea na game langu, na mimi nikafanya hivyo nikatoka na kuelekea nyumbani” alisema Mahamud, ambae alieleza kuwa pale nyumbani kwao aliingia ndani kwaajili ya kuangalia kama kungekuwa na chakula, lakini dakika kama tano baadae akasikia ngurumo ya vesper nje ya nyumba, lakini ilikuwa inakuja hivyo hakuangaika nayo, “ila nilipoisikia tena inaondoka nikajuwa kuwa tayari Masoud anaondoka, japo nilishangaa sana kwanini imekuwa kwa muda mfupi kiasi kile, lakini nikatoka nje kwenda kuchungulia kama ni yeye au laa” alieleza Mahamud, ambae alisema kuwa, hakufanikiwa kumuona mwendesha pikipiki hiyo aliyoisikia ikipita nje zaidi ya vumbi lililotawanyika kutokana na mvumo wa pikipiki hiyo, aina ya vesper, “ilionyesha kwamba mtumiaji wa pikipiki hiyo alikuwa katika mwendo mkali sana, na hiyo sio tabia ya Masoud ninayo ifahamu katika uendeshaji wa Vesper” alisema Mahamud, na kueleza kuwa, aliamua kutoka nje pengine ange muona vizuri mwendesha vesper mwenye fujo, lakini licha ya kutoka nje hakuona hata dalili ya vesper zaidi ya vumbi la pale uwanjani.
Mahamud alisema kuwa, pale nje hakuwa peke yake ila aliweza kuona baadhi ya watu, nao walitoka majumbani mwao kuishangaa ile pikipiki, huku kila mmoja akidai kuwa hakuna alieiona sura ya mwendesha pikipiki, ni kama ulizuka mjadala wa muda kuhusu pikipiki na uendeshaji wake, na tukiwa tunaedelea kuongea ili na lile mara nikamuona yule mwanamke akitoka nyumbani kwa Masoud na kuanza kutembea kuja upande wa uwanjani, na mimi nikakimbilia nyumbani kwa Masoud ili nikaendelee kucheza game” alieleza Mahamud, ambae anasema kuwa alipofika pale nyumbani kwa Masoud akakuta mlango umeegeshwa na Vesper ipo nje, akausukuma mlango na kuingia ndani na ile anaingia tu sebuleni, akakutana na mwili wa mtu alielala sakafuni, mtu mweusi zaidi ya mtu mweusi, “kilicho nifanya nimtambue kuwa ni Masoud ni ile bukta aliyokuwa ameivaa, vitu vilikuwa kama nilivyo viacha, hakukuwa na chochote kilicho vurugwa” Hakika Mahamud alishtuka sana baada ya kutambua kuwa Masoud alikuwa ameuwawa, na akaamini kuwa yule mwanamke alikuwa ni jini na ndie aliemuuwa, hivyo akakimbilia nje huku anapiga kelele za “jini jamani jini” akimaanisha yule mwanamke ambae alitegemea ange muona kule nje, lakini haikuwa hivyo hakuweza kumuona yule mwanake mwenye niqab usoni mwake, alikuwa amesha toweka, kweli hakumuona mwanamke zaidi ya watu wengine waliokuwa wanajadili kuhusu pikipiki, na walipomsikia akipiga kelele wakakimbilia nyumbani kwa Masoud, “walipoona kilichotokea wakanisaidia kupiga simu polisi, nao wakasema tusiuguse mwili wa Masoud mpaka watakapofika wao” huo ndio ulikuwa mwisho wa maelezo ya Mahamud, maelezo ambayo yalianza kunipa mwanga mzuri sana katika katika kazi yangu, “dah! kwa kweli inatisha” nilisema hivyo, huku nageuza uso wangu kutazama kule walipokuwepo wakina Malambo, lakini kabla sijawaona wao nikamuona yule babu wa jana usiku, mwenye makovu usoni, makovu ambayo yalionyesha wazi kuwa aliwahi kushambuliwa au kukatwa na mapanga, aliekuwa amesimama mita chache sana kushoto kwangu, nivkama alikuwa anatusikiliza tulicho kuwa tunaongea, moyo wangu ulishtuka sana kumuona yule mzee mahali pale, nilitamani kujuwa zaidi kuhusu yule mzee, ambae nilianza kumtilia mashaka kutokana na kujitenga kwake na utazamaji wake……hivi huyu mzee ni nani? je mashaka ya Eric yataenda bure,?
ITAENDELEA MUWE NA USIKU MWEMA
 
Msimuliaji kama itakupendeza, weka Episode moja muda wa mchana:
Usiku wasomaji wakiwa wametulia vitandani wawekee Episode mbili ili wapate usingizi mzuri baada ya kupata burudani ya Hawala:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom