Kifo cha Ghaddafi chamgusa Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kifo cha Ghaddafi chamgusa Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Power G, Oct 31, 2011.

 1. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Asema anaamini kuuawa kwake si sahihi
  Ahofia yanayotokea Libya kuingia nchini
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesema yeye ni miongoni mwa watu wanaoamini kuwa kifo cha Kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, hakikuwa sahihi.

  Akizungumka katika misa ya mavuno ya Parokia ya Mtakatifu Petro Oysterbay jana ambako pia aliendesha harambee na kufanikiwa kupata Sh milioni 111.65 zikiwa ni fedha taslimu na ahadi, Pinda awataka Watanzania kuenzi amani iliyopo nchini kwani yanayoendelea katika nchi za jirani yanatisha na si ya kuomba yatokee kwa Watanzania.

  "Tuangalie yanayotokea Libya, si mambo mazuri hata kidogo. Mimi ni miongoni mwa watu wanaoamini kuwa kifo cha Gaddafi si sahihi hata kidogo, ni bora angekamatwa akashtakiwa kuliko watu kujiamulia kutoa roho ya mtu mwingine hivi hivi. Watanzania tuombeane tusifike huko," alisisitiza.

  Source: Nipashe

  My Take: Iwapo CCM wataendeleza jadi yao ya kubaka demokrasia na kuchakachua katiba ili watawale daima, wajue wazi kwamba ya Libya yatawakuta tu.
   
 2. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 1,522
  Trophy Points: 280
  Watakaotufikisha huko ni viongozi wetu na CCM ambao hawakubali kushindwa na wanaamini nchi hii ni ya kwao peke yao, pia ni hii ardhi inayogawiwa kama njugu inaweza kutufikisha huko.. kuombeana pekee hakutoshi
   
 3. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,795
  Likes Received: 2,564
  Trophy Points: 280
  Kifo cha kujitakia. Ameaambiwa mapema jiweke pembeni,nenda uhamishoni bana, akadhania utani.
   
 4. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Vipi hajamwaga chozi?
   
 5. Jeremiah

  Jeremiah JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 641
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kifo cha Gadafi ni sahihi. Hiyo ndiyo dawa ya viongozi wasiotaka kushindwa. je pinda anajua kaburi liko wapi?
   
 6. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hata yale ya Nyamongo hayakuwa mazuri, wale ni binaadamu kama Gadafi. Tuache unafiki. Juzi igunga kuna kijana amekufa kame Gadafi, vipi?
   
 7. C

  Chakusonje Member

  #7
  Oct 31, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzee pinda acha kuuma na kupuliza, chama chako ndiyo chanzo cha kuelekea huko leo, unasemea kanisani. Acheni kubaka demokrasia nchi itakuwa salama, Ghadafi alianza kwa kuua waandamanaji kama mlivyo fanya arusha na bado hamjajifunza! Siyo vizuri kujadili vibanzi vya wenzetu hu sisi tuna boliti machoni.
   
 8. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,550
  Likes Received: 4,675
  Trophy Points: 280
  Na siku kikiwaka hapa aliyofanyiwa Gadafi mbona cha mtoto, tutawafanyia kweli hasa nyie na familia zenu za kifisadi, saa yaja na haiko mbali.
   
 9. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,834
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Sisi Tunaangalia Kuwa Roho ya Ghadaffi Ilitolewa kwa Kupigwa Risasi!! Je na hao Wote waliokufa Katika Hizo harakati za Kuhakikisha Ghadafi roho yake inatolewa Ni PANYA?

  Ijulikane roho ya binadamu ina Thamani sawa kwa Mungu!! Hivyo si Vyema Kumjali Ghadafi Kama Ghadafi ni Bora kujali roho za wote waliotutoka katika harakati Hizo!!

  Nadhani ni more Than 200,000 peoples!! Kama Gadaffi angekubali Mapema roho kibao zingepona!! Shame on Gadafi Bora angekufa mapema zaidi!!

   
 10. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Mimi nadhani kama angekuwa si mnafiki kama walivyo viongozi wote wa ccm, angewaeleza wananchi yale ambayo ccm imejifunza kutokana na matukio ya Libya, siyo kuwaambia watu waombe Mungu. Anadhani Libya, Misri nk walikuwa hawaombi Mungu?
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  I wish kifo kama icho kingewakuta baadhi ya viongozi wetu wa sasa ili waijue nguvu ya UMMA
  Pls dont quote me wrong nimesema nguvu ya umma na si ya NATO
   
 12. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,023
  Likes Received: 7,403
  Trophy Points: 280
  Ikifikia hatua watu wanaanza kuingiza kichwani na hatimaye kuruhusu wazo la uasi 'dhidi ya amani' litawale na mwisho maungo yao yafanikishe uasi huo hapo elewa fika wamegundua kuwa kile kinachoitwa amani ni mrija utumikao kuwanyonya na pia nyundo itumikayo katika kuwagonga na kuwakandamiza. Hakuna tena sababu ya kuienzi nyenzo ya aina hiyo.

  Kwenye Lime color, hakuna aombaye yatokee yatokeayo kwa wenzetu ila kwa style ya uongozi na tabia za watawala, jamii inaona kuwa hilo ndiyo jambo pekee na muafika tunalihitaji kulitumia ili kufikia zile angalau/nafuu za kimaisha.

  Kwenye Red, Waziri mkuu anatakiwa kuelewa kuwa yaliyotokea Libya ni machafuko ambayo chanzo chake ni madaraka (Ung'ang'anizi, ukombozi, kiu ya madaraka). Hivyo nashangaa kuona waziri mkuu akisikitishwa na kilichompata Gaddaf, waliopoteza maisha ni wengi katika mapambano nchini Libya, ila kwa namna alivyosikitishwa na kifo cha Gaddaf ni kama vile Gaddaf ndiye mtu pekee aliyeuawa katika mapambano yale.

  Je amechagua kumlilia Gaddaf kwa kuwa ni mtawala mwenzao na kuacha wafu waliliane wao kwa wao na kuzikana? Pinda...naomba nikutaarifu kuwa siamini kuwa Sentensi yako imefika mwisho, naamini unakohoa au unafuta machozi (kama kawaida yako)ili uendelee na speech yako na mimi naahidi kuendelea kukusubiri uimalizie sentensi yako, sitaki kuku quote vibaya.

  Membe yeye najua ameshamaliza na kilichofanya aumizwe tunakijua.
   
 13. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #13
  Oct 31, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  What a pinhead. Foreign minister alishatumwa kutoa diplomatic stance ya Tanzania, Waziri Mkuu huwezi kuibukia kwenye makanisani kutoa opinion zako, huruhusiwi kuwa na opinion in public, any publicly stated opinion ya Waziri Mkuu ni foreign policy ya nchi, huwezi ku supplant statement za Bernard Membe ambazo zimepata approbation ya Ikulu.
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Oct 31, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,406
  Trophy Points: 280
  Imeandikwa wapi kuwa ukiwa "waziri mkuu huwezi kuibuka kwenye makanisani na kutoa opinion zako"? Halafu "kwenye makanisani" ndiyo nini?

  Imeandikwa wapi kuwa ukiwa waziri mkuu basi "huruhusiwi kuwa na opinion in public"?

  Na imeandikwa wapi kuwa "any publicly stated opinion ya Waziri Mkuu ni foreign policy ya nchi"? Imeandikwa kwenye katiba ya nchi?
   
 15. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #15
  Oct 31, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,543
  Likes Received: 1,892
  Trophy Points: 280
  Pinda amekosea kwenye conclusion yake.
  Unapowaambia wananchi tuombe Mungu tusifike huko na wakati hamuwasikilizi,basi ni kama mnawatisha na kuwaingizia hofu kama mlivyofanya kipindi kile cha vita ya Rwanda.

  Kifupi ni wengi ambao hatukufurahishwa na alichofanyiwa Gaddafi,however nilishasema kuwa la kujifunza kutoka Libya ni kuwasikiliza wananchi.

  Wao kama viongozi wanatakiwa kuwasikiliza wananchi hata kama wanadhani maslahi yao ya uongozi yamo hatarini,ni bora ku work things out kuliko ku ignore ama kuwanyamazisha wananchi kwa kutumia dola.
   
 16. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #16
  Oct 31, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Sasa huu nao si utu hata kidogo.. Mhe! inaonekana roho ya tamaa ya madaraka haijamwachia bado. si ndio huyu Mzee aliyemwambia mkewe aanze kumkampenia chinichini.. akazimishwa na KK. si uungwana Hata kidogo, kama Kiongoza wa jamii angepaswa kusikitika kwa vifo vya raia wengi wasio na hatia yoyote kule Libya, Kumlenga na kumtetea kiongozi mkuu ni ubinafsi na inaonyesha picha ya wazi kwamba mzee huyu hayuko kwa maslahi ya wananchi bali viongozi.

  Embu ona, Mfano mdogo tu wa Jumatatu ya sept,12 ambapo Muamar Gadaffi aliamuru wafuasi wake kufanya shambulizi la Hujuma na kushambulia kisima kikubwa cha mafuta huko Benghazi, na kujeruhi mamia ya watu vibaya huku ikiokotwa miili 15 ya watu waliokufa vibaya waliobahatika kuonekana na wengine kumezwa kabisa kwa moto.

  Sasa wale wahandisi, wahudumu, mafundi na wengine wafanyakazi wa mgodi huo wa mafuta wana kosa Gani. Hawako upande wowote, wao wanazalisha tu mafuta. Unapowaua bila huruma maskini hao wengine hata hawajui mtutu wa bunduki ukoje una maana gani?. Leo Basi Tusikie Viongozi wa nchi wakilaani mauaji kama hayo badala yake wanamlilia Gadaffi.

  Wanawake na watoto wasio na kosa wameuawa, leo hii mtu anamlilia Gadaffi.. JINGA!! JINGASSSS!! HII ndio tafsiri ya UROHO WA MAARAKA ULIOPINDUKIA. angalau angewaasa viongozi wa Dini kuliombea taifa ili Maafa kama ya Juzi ya Kuzama kwa MV Islanders Yasitoke Nchini na kuangamiza mamia ya watanzania.. Yeye anawazia tu Gadafffi.. Gadafiii.. watanzania wenzake wamezama na kufia Chini ya Bahari 300m.. Jamaa hilo halijamgusa kabisa.. analia Gadafiii.. gadafiiii... SHIT!
   
 17. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #17
  Oct 31, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Magamba huwa hayafahamu kama wananchi pia ni binaadamu na wana haki ya kuishi. Wanawasikitikia madikteta wenzao tu.
   
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,312
  Likes Received: 1,783
  Trophy Points: 280
  Ana bahati yeye kimemgusa! Wapo kilio watoa machozi maana wamekosa mfadhili wa kampeni zao
   
 19. A-town

  A-town JF-Expert Member

  #19
  Oct 31, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
   
 20. F

  FJM JF-Expert Member

  #20
  Oct 31, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145


  Na mauaji ya watu wa Benghazi ni sahihi au la? Haki ni kwa watu wote na sio watu fulani.
   
Loading...