Ishara tano(5) kwamba unakaribia kufa na nini cha kufanya unapoona

Jun 10, 2024
31
63
Habari wana Jf, niende moja kwa moja kwenye mada ya leo,ishara tano zinazoweza kumtokea mtu anayekaribia kufa, kabla sijaanza kupitia ishara hizo tano kwanza ningetoa mfano mmoja ambao Ni tukio la kweli kabisa, lililotokea kwny maisha yangu, tukio Hilo lilinifanya nianze kuwa mdadisi na kuanza kujufunza ili nijipatie hekima ambayo nitashare na ww hapa leo.

 Mwaka 2005
Mwaka huo mama yangu mzazi alifariki, lakini Kama wiki moja hivi kabla ya kifo chake Kuna kitu kilitokea, alimka asubuhi wkt anatoka nje ghafla mlangoni aliona mdudu flani hivi ndogo wa rangi Kama nyekundu iliyopauka ambaye Ni nadra sana kumwona, Mimi nikiwa ndani nikamsikia mama akisema, ukimwona mdudu huyu,kuna tukio la mauti linakwenda kutokea, ghafla mama alinza kuongea kwa huzuni akisema, nimeshamzika baba yangu, nimeshamzika ndogo wangu mdudu huyu anataka kuniletea msiba gani Tena?....(mama alijiuliza mwenyewe kwa mshangao!)

Wiki moja baadaye
Mama alifariki, kumbe yule mdudu alikuwa Ni ISHARA ya mauti yake,nikagundua kuwa Kuna taarifa au ishara flani hutokea kabla mtu hajafikwa na mauti na ile dhana ya kufa ghafla Ni matokeo ya ujinga au upuuziaji wa hizo ishara zinapojitokeza.

KIFO NI NINI?kunaweza kuwa na maana tofauti tofauti lkn hapa niseme tu kuwa kifo Ni ule mchakato wa hatua kwa hatua mpaka mtu anapofikwa na mauti, naweza kusema kuwa mtu Hafi tu ghafla huwa Kuna mchakato anapitia kwa muda mpaka Lile tukio la mauti linatokea,mtu Hafi tu siku moja, mchakato unaweza kuchukua miezi hata miaka, huu ni utaratibu wa asili kabisa wenye malengo makubwa mawili.

(1)uone ishara ya kifo, utengeneze Mambo yako Kama vile urithi,madeni,kuacha mabaya na nk, ili mauti yakitokea uwe katika fungu jema.

(2)lengo la pili, uweze kuchukua tahadhari kuzuia mauti yasitokee,Ni muhimu kujua kuwa kuona ishara za mauti haimaanishi lazima utakufa,wkt mwingine unaonyeshwa ili uwe na tahadhari au uchukue hatua flani ili mauti isitokee.

Sasa baada ya maelezo hayo nianze sasa kuelezea ishara tano(5)

ISHARA YA KWANZA
TAMKO LA MAUTI, kwa watu wa vitabu wanajua kuwa kifo kinaanzia kwenye Ulimi,yaani yale maneno ambayo mtu anayasema kwa kinywa chake au ule ukiri wa kinywa chake, kabla mtu hajafa huwa anaanza yeye mwenyewe kujitamkia kifo au kukiri kufa, wengine kwa kujua wengine kwa kutokujua, Mara kadhaa utamsikia mtu akisema maisha magumu bora nife ,wengine wanasema Kama utani matokeo yake wanakufa hivyohivyo kiutaniutani, mwingine kasalitiwa na mpenzi wake tayari keshajitamkia mauti kirahusi tu, mara nyingi huwa nawasikia watu kwenye daladala labda dereva akiendesha vibaya, mtu anasema we dereva utatuua....Hii imekuwa Ni kawaida lakini hii si kawaida Ni ISHARA inayomtokea mtu anayekaribia kufa, Kuna kiongozi mkubwa tu hapa Tanzania Kuna maneno alisikika akisema"ni bora kufa lakini unaifia nchi yako" mahali pengine alisema nimeya sacrifice maisha yangu kwa ajili ya watanzania maskini" baada ya muda kidogo alifariki, kauli hizi ni ishara kwa mtu anayejua lugha ya mauti,ila kwa asiyejua ataona Ni maneno ya kawaida.

Mwanahihop 2pac Shakur miezi miwili kabla ya kifo chake alitoa wimbo,ambao ulikuwa na mistari inayosema "I been shot and murdered" maneno hayo unaweza kuyatafasiri kuwa "nimepigwa risasi na kuuawa"mwezi mmoja mbele pac akapigwa risasi na kufa,kama alivyojiimbia mwenyewe kwny wimbo wake, kifo sio bahati mbaya,kifo Ni mchakato mrefu,maneno tunayotamka huwa yanakuwa recorded,soon or later yatatimia.

NINI CHA KUFANYA
Uwe makini sana na kile unachotamka hasa kinachohusiana na kifo, wakati mtu akiwa na hasira,au akiwa amekata tamaa hua ni rahisi kujitamkia kifo harafu baadaye Mambo yakikaa sawa anasahau kuwa aliwahi kujitamkia kifo,Zuia kinywa chako kisinene mabaya,kisinene laana,kisinene mauti Bali nena uzima,nena baraka nena mema.. kama itakulazimu kujitamkia mauti basi ujue ulichokisema kinamaanisha nini......itaendelea tena ...................
 
Umefungua ID jana ili uje kutuongopea?

Kwa hiyo mimi leo hii nikisema nitakufa maana yake nitakufa kwasababu ya kauli yangu au kwasababu ya asili ya ulimwengu kuwa kiumbe hai lazima kife?

Kwa tafsiri hiyo ni kwamba mabubu automatically wanakuwa wameepuka hicho kikombe.

Kwa hiyo mtoto mchanga anayefia tumboni kwa mama yake ye anakuwa na ishara gani huko kuwa atakufa?

Acha uongo
 
New member kuna vitu mhimu tunatafuta suluhu. Click & vote

 
New member kuna vitu mhimu tunatafuta suluhu. Click & vote

sasa wewe sijui ni demu au mani mbona unachomeka uzi katika kila uzi unaoletwa? Hebu tulia kwanza, leta hoja inayojitegemea. We ndio unajua leo kuwa kuna tatizo la ujifunzaji hesabu mashuleni? Hili tatizo lipo tangu siku nyingi na limeundiwa mikakati na semina za kuliondoa lakini bado lipo. Hebu tulia kwanza tuache tusome nyuzi zinazojiri
 
sasa wewe sijui na demu au mani mbona unachomeka uzi katika kila uzi unaoletwa? Hebu tulia kwanza, leta hoja inayojitegemea. We ndio unajua leo kuwa kuna tatizo la ujifunzaji hesabu mashuleni? Hili tatizo lipo tangu siku nyingi na limeundiwa mikakati na semina za kuliondoa lakini bado lipo. Hebu tulia kwanza tuache tusome nyuzi zinazojiri
Anataka uende huko stories of change ukapigie kura bandiko lake ashinde. Ambacho hajui ni kwamba anajiharibia tu!
 
Umefungua ID jana ili uje kutuongopea?

Kwa hiyo mimi leo hii nikisema nitakufa maana yake nitakufa kwasababu ya kauli yangu au kwasababu ya asili ya ulimwengu kuwa kiumbe hai lazima kife?

Kwa tafsiri hiyo ni kwamba mabubu automatically wanakuwa wameepuka hicho kikombe.

Kwa hiyo mtoto mchanga anayefia tumboni kwa mama yake ye anakuwa na ishara gani huko kuwa atakufa?

Acha uongo
Aiseeee, kuwa makini kutamka tamka kuhusu vifo. Tutarithi mkeo muda si mrefu.
 
Back
Top Bottom