YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,908
- 51,906
Hivi kwa mfano Marehemu muislamu alikopa kwa mtu mfano mkopo wa kulipa kidogo kidogo kwa mwezi kwa miaka 20 akiwa na kaduka kake kadogo akifa mfano mwezi wa kwanza wa Deni Hilo Deni atalipa Nani Kama Mali za Marehemu hazifikii hata asilimia moja ya deni?Ukiona mali inaleta utata wa mirathi ujuwe si ya halali au warithi si wa halali.
Uislam raha sana, kwanza maiti azikwe kwa mali yake, pili ilipe madeni yake yote, itayobaki kama ni madeni au mali basi warithi watagawana kama ilivyoandikwa kwenye Qur'an, hesabu zake zipo wazi kabisa ndani ya Qur'an.
Urithi ni hata madeni, si mali tu. "Tajiri" Kama Mengi utakuta alikuwa anacheza na mikopo tu, sasa wacha warithi wagombanie madeni.
Tutaona muda si mrefu kila mmoja akijitoa kwenye mirathi.