Kifo cha CUF hichoo... chaja! Upinzani kubaki CHADEMA pekee?

Kwa kweli kukosekana kwa ruzuku kwa miaka 5 ijayo hali ya CUF itakuwa mbaya sana. Kitabaki kuwa cha wanaharakati wachache tu by 2020!
 
Wanabodi,
Wale wa zamani kama mimi mtayakumbuka baadhi ya maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (RIP) akizungumzia upinzani wa kweli, alisema angependa kuona serious oppositions wa vyama viwili au vitatu na sio utitiri wa vyama, japo Mwalimu aliongezea "Upinzani wa Kweli Utatoka CCM!", by now atakuwa ameshabadili msimamo wake ule kwa kutuma salamu kupitia kwa mjukuu wake kuwa " Upinzani wa Kweli, Utatoka Chadema".

Tanzania tunavyo vyama 19 mpaka sasa, na hakuna limit number ya vyama vipya kusajiliwa, hii tayari ni utitiri wa vyama ambao hauna maslahi yoyote kwenye serious opposition zaidi ya kubakiwa na vyama vichache vyenye serious oppositions na vyama vilivyobakia kuwa ni vyama jina tuu, vyama mtu na vyama makaratasi tuu kule ofisi ya msajili.

Nikirudi kwenye vyama serious vya opposition viko vitatu tuu, ukiondoa CCM ambacho ni chama tawala, vyama serious vinabaki kuwa ni CHADEMA, CUF na NCCR MAGEUZI kwa mbali, na kujumlisha 'vyama watu' viwili UDP (ni Cheyo) na TLP (Mrema) ambavyo siviingizi kwenye hesabu ya 2015, just time in between will tell!, vyama vyote vingine vilivyobakia ni vyama jina au vyama makaratasi.

Kufuatia muafaka na CCM, sasa chama cha CUF ni mshirika mkuu wa CCM na juzi nimemona Katibu Mkuu wake, Maalim Seif, akijivinjari jijini Dar es Salaam na matunda ya muafaka, S-Class 3 zikitanguliwa na pikipiki. Hivyo kwa sasa Zanzibar inatawaliwa na chama kimoja kikuu kiitwacho 'Umoja wa Kitaifa' (CCM-CUF).

Kwenye kampeni za 2015, msifikiri tena kama kutakuwa na upinzani wowote wa maana kule Zanzibar, kwa sababu baada ya kuishuhudia hii miaka mitano ya amani, utulivu na ustawi wa Zanzibar, why vote for CCM or CUF any more, just vote for Umoja wa Kitaifa, maana popote utakapopiga kura, it doesn't matter anymore, kama keki tutakula wote kwanini kuigombania!..na huu ndio mwanzo wa kifo cha CUF!.

Tukija CUF bara, kwa vile CUF imefanikiwa kukishauri NCCR-Mageuzi na hivi vyama watu viwili (UDP na TLP) kuunda alliance yao dhidi ya Chadema, kwa maneno mangine vyama hivi vimekubali kuwa vyama vikaragosi vya CCM kupitia mlango wa nyuma wa mgongoni mwa CUF, hivyo kubakiwa na chama kimoja tuu cha upinzani cha kweli nchini ambacho ni Chadema.

Mwanzo niliwalaumu na kuwalaani Chadema, kuunda kambi ya upinzani peke yao, kumbe nilikuwa myopic, sikuweza kuona mbali kwenye bigger picture, niliwaona Chadema ni wabaguzi, wabinafsi na wenye umimi, bila kuifahamu hali halisia ya mambo.

Kupitia michango mbalimbali ya wana JF, nimefunguka macho na sio tuu kuanza kuielewa Chadema, bali kuikubali kuwa ndicho Chama Pekee cha upinzani kwa uchaguzi wa 2015 dhidi ya chama tawala CCM na msharika wake CUF na vyama vikaragosi vyao.

Nasisitiza huu ndio mwanzo wa kifo cha CUF na Neema kwa Chadema, kwa sababu baada ya uchaguzi huu, ruzuku ya mamilioni ya CUF yatakula panga la msajili sambamba na CCM ambayo sasa itakombwa na Chadema, na kama hakutatokea vita vya kimaslahi kugombea ruzuku hivyo (kama ilivyotokea kwa NCCR), na kuitumia kuimarisha chama, then 2015 Chadema itakuwa kwenye the best prospects kuchukua nchi.

Hivyo huu ushirikiano wa CCM na CUF na vikaragosi wao, ni very healthy kwenye safari ya kuelekea kwenye serious opposition kwa vyama utitiri kujifia natural death kwa kufuata kanuni law of the jungle ya 'Struggle for Existance, Survival for the Fittest', CUF inaelekea kufa na maneno ya Mwalimu ya serious oppositions yameanza kutimia.

Angalizo: Pasco wa JF sio mtafiti wa siasa bali ni mtazamaji na mfuatiliaji wa masuala ya kisiasa ambaye hafungamani na chama chochote, wala sio mfuasi wa itikadi yoyote, bali mshabiki wa demokrasia ya kweli ndani ya Bunge.
Hii ni rejea tuu.
Pasco
 
Hili litamaliza na lipumba atakua historia. Hichi chama kina watu wazoefu na wenye malengo ya muda mrefu. Lipumba anao watu wanaompigia debe lakini majority ni mamluki tu. Hawa watapiga kelele siku mnile tatu na mambo yatabaki salama. Hatuainayofata ni kuwagukuza mamluki wotr ndani ya chama.
Wanaomtaka arudi wana mihemko hawana hoja ya msingi.
Cuf kitaubuka mshindi dhidi ya mamluki hawa wanaoleta mgawanyiko baada ya kuoewa fedha na lipumba ambaye naye amepewa na majirani kwa kazi hio. Watavuka bila ya shaka
 
Mimi natofautiana mleta mada kwa sababu Prof. Lipumba japo kitaaluma ni mchumi, ila kiukweli he is a politician by professional, ameifanya siasa ndio ajira yake ya kudumu na hana shughuli nyingine yoyote ya kufanya, au jambo jingine lolote la kufanya ili kuendesha maisha kama yule dr mihogo!.

Mtu amegombea mara 4 na zote amekataliwa hakuwahi kupata hata asilimia 5% lakini kila baada ya miaka 5 lazima awe mgombea wa CUF hadi kufikia yeye na sharubu kujihesabu wao ndio wagombea pekee wa kudumu wa CUF kwenye urais, ndio maana kuliko kukosa kugombea, bora apokee kile kidogodogo cha CCM, na kujitoa ili CUF ivunjike!, kajitoa, CUF haikuvunjika!, fungu alilopewa ni kiduchu tuu!, afadhali mwenzake kapewa mkataba mrefu, yeye fungu limeishamuishia na hana namna nyingine yoyote ya kuendesha maisha yake!.

Sasa CUF wasipomrudisha atafanya nini kingine?!, kwa sababu ubunge au udiwani hawezi kupata kwa sababu hachaguliki!, unategemea nini kwa mtu kama huyu?!, nawaomba CUF please mrudisheni tuu Prof. Lipumba kwenye nafasi yake.

Pasco
Laiti viongozi wa CUF wangelisoma bandiko langu hili, haya yanayowafika yasingefika hapa yalipofika.

Mtu umri umesonga na hana shughuli nyingine yoyote ya kufanya, uzoefu wake ni kuwa Mwenyekiti wa CUF kwa zaidi ya miaka 20 na hawezi kufanya shughuli nyingine yoyote, unategemea nini? . He can do anything hata ikibidi chama kimegeke au hata kife, kife tuu kama ilivyo kwa punda lakini mzigo ufike salama kwenye kiti cha uenyekiti! .

Safari ya kifo cha CUF imeanza rasmi jana.
Pasco
 
Wanabodi,
Wale wa zamani kama mimi mtayakumbuka baadhi ya maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (RIP) akizungumzia upinzani wa kweli, alisema angependa kuona serious oppositions wa vyama viwili au vitatu na sio utitiri wa vyama, japo Mwalimu aliongezea "Upinzani wa Kweli Utatoka CCM!", by now atakuwa ameshabadili msimamo wake ule kwa kutuma salamu kupitia kwa mjukuu wake kuwa " Upinzani wa Kweli, Utatoka Chadema".

Tanzania tunavyo vyama 19 mpaka sasa, na hakuna limit number ya vyama vipya kusajiliwa, hii tayari ni utitiri wa vyama ambao hauna maslahi yoyote kwenye serious opposition zaidi ya kubakiwa na vyama vichache vyenye serious oppositions na vyama vilivyobakia kuwa ni vyama jina tuu, vyama mtu na vyama makaratasi tuu kule ofisi ya msajili.

Nikirudi kwenye vyama serious vya opposition viko vitatu tuu, ukiondoa CCM ambacho ni chama tawala, vyama serious vinabaki kuwa ni CHADEMA, CUF na NCCR MAGEUZI kwa mbali, na kujumlisha 'vyama watu' viwili UDP (ni Cheyo) na TLP (Mrema) ambavyo siviingizi kwenye hesabu ya 2015, just time in between will tell!, vyama vyote vingine vilivyobakia ni vyama jina au vyama makaratasi.

Kufuatia muafaka na CCM, sasa chama cha CUF ni mshirika mkuu wa CCM na juzi nimemona Katibu Mkuu wake, Maalim Seif, akijivinjari jijini Dar es Salaam na matunda ya muafaka, S-Class 3 zikitanguliwa na pikipiki. Hivyo kwa sasa Zanzibar inatawaliwa na chama kimoja kikuu kiitwacho 'Umoja wa Kitaifa' (CCM-CUF).

Kwenye kampeni za 2015, msifikiri tena kama kutakuwa na upinzani wowote wa maana kule Zanzibar, kwa sababu baada ya kuishuhudia hii miaka mitano ya amani, utulivu na ustawi wa Zanzibar, why vote for CCM or CUF any more, just vote for Umoja wa Kitaifa, maana popote utakapopiga kura, it doesn't matter anymore, kama keki tutakula wote kwanini kuigombania!..na huu ndio mwanzo wa kifo cha CUF!.

Tukija CUF bara, kwa vile CUF imefanikiwa kukishauri NCCR-Mageuzi na hivi vyama watu viwili (UDP na TLP) kuunda alliance yao dhidi ya Chadema, kwa maneno mangine vyama hivi vimekubali kuwa vyama vikaragosi vya CCM kupitia mlango wa nyuma wa mgongoni mwa CUF, hivyo kubakiwa na chama kimoja tuu cha upinzani cha kweli nchini ambacho ni Chadema.

Mwanzo niliwalaumu na kuwalaani Chadema, kuunda kambi ya upinzani peke yao, kumbe nilikuwa myopic, sikuweza kuona mbali kwenye bigger picture, niliwaona Chadema ni wabaguzi, wabinafsi na wenye umimi, bila kuifahamu hali halisia ya mambo.

Kupitia michango mbalimbali ya wana JF, nimefunguka macho na sio tuu kuanza kuielewa Chadema, bali kuikubali kuwa ndicho Chama Pekee cha upinzani kwa uchaguzi wa 2015 dhidi ya chama tawala CCM na msharika wake CUF na vyama vikaragosi vyao.

Nasisitiza huu ndio mwanzo wa kifo cha CUF na Neema kwa Chadema, kwa sababu baada ya uchaguzi huu, ruzuku ya mamilioni ya CUF yatakula panga la msajili sambamba na CCM ambayo sasa itakombwa na Chadema, na kama hakutatokea vita vya kimaslahi kugombea ruzuku hivyo (kama ilivyotokea kwa NCCR), na kuitumia kuimarisha chama, then 2015 Chadema itakuwa kwenye the best prospects kuchukua nchi.

Hivyo huu ushirikiano wa CCM na CUF na vikaragosi wao, ni very healthy kwenye safari ya kuelekea kwenye serious opposition kwa vyama utitiri kujifia natural death kwa kufuata kanuni law of the jungle ya 'Struggle for Existance, Survival for the Fittest', CUF inaelekea kufa na maneno ya Mwalimu ya serious oppositions yameanza kutimia.

Angalizo: Pasco wa JF sio mtafiti wa siasa bali ni mtazamaji na mfuatiliaji wa masuala ya kisiasa ambaye hafungamani na chama chochote, wala sio mfuasi wa itikadi yoyote, bali mshabiki wa demokrasia ya kweli ndani ya Bunge.
CDM ilishafariki tangu ilipomteua Mgombea Urais mwaka Jana! Sasa hivi hakina nguvu kabisaaa! Mwaka 2019 Uchaguzi wa Serikali uchochorooooo!
 
wabunge 50 wa chadema sasa wamewanyima vipi ruzuku Cuf ambao na wao wamepata viti zaidi kuliko uchaguzi uliopita?

Labda uzungumzie ruzuku ya Ccm ambao kwa ajili ya kampeni na kuimarisha chama wanao ufisadi hawajali na ruzuku kiasi hicho.

mkuu unapoandika jaribu kuweka facts tu kujiita mfuatiliaji na kuja na maneno 'mapya' ya mtu aliyekufa kunatupa mashaka wasomaji, tunaanza kutilia shaka hata zile facts unazotoa.
Unafikiri kwa masaburi we sio bure kabisaaa!
 
Na chadema wakae mkao wa kula, siku viongozi kina tundu lissu na wenzake wakienda kinyume na atakavyo lowassa na hapa namaanisha lowassa taasisi, hapa tatizo sio lowassa yeye moja kwa moja bali watu walio nyuma yake, wafuasi na wale wazee wa ulipo tupo, kutakuwa na mpasuko wa hali ya juu, na mpasuko huu nauona ikifika 2019 ndo utaamza, mark my words!
 
Pasco nakupa hongera sana. No vizuri pia tukatoa ushauri zaidi kwa vyama vya upinzani maana bila kuwa na uponzani imara nchi itasonga ili mradi siku zinasogea. Lipumba kaja kumaliza CUF sasa, CCM wanafurahi na vyombo vyake vinatangaza kwa nguvu. CHADEMA nafikiri iko pale kwa sababu ya Mwenyekiti wake na hazina ya vijana wanaoiunga mkono na kuwekwa kwenye level ya kufanya maamuzi, ingekuwa Mwenyekiti ni Dkt Slaa basi Chadema leo ingekuwa kama CUF. Bado nina imani na CHADEMA kuwa main opposition changamoto ni moja tu kuwa Maskini haaminiki ndiyo maana CCM inamchukia sana Mbowe. Zamani nilimpenda siasa za Zitto kabwe ile kuanzisha Chama chake akiwa ndani ya Chama kingine nikagundua naye ni mamluki.
 
Pasco natambua nguvu kubwa sana inayotaka kutumika kuhakikisha CUF inavyorugwa hata kwa gharama yoyote kwa kumtumia Lipumba niwaambieni ukweli huo mpango hatofanikiwa kamwe. Kila chama kinaendeshwa kwa kufuata katiba na sheria za vyama husika. [HASHTAG]#Lipumba[/HASHTAG] yule angekuwa na busara bora asingefanya alichokifanya jana ila kwa sababu anasapoti kubwa kutoka kwa wakubwa ndo maana ana kiburi ila mpango wake hatofanikiwa.
 
Back
Top Bottom