Kifo cha CUF hichoo... chaja! Upinzani kubaki CHADEMA pekee?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,834
2,000
Wanabodi,
Wale wa zamani kama mimi mtayakumbuka baadhi ya maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (RIP) akizungumzia upinzani wa kweli, alisema angependa kuona serious oppositions wa vyama viwili au vitatu na sio utitiri wa vyama, japo Mwalimu aliongezea "Upinzani wa Kweli Utatoka CCM!", by now atakuwa ameshabadili msimamo wake ule kwa kutuma salamu kupitia kwa mjukuu wake kuwa " Upinzani wa Kweli, Utatoka Chadema".

Tanzania tunavyo vyama 19 mpaka sasa, na hakuna limit number ya vyama vipya kusajiliwa, hii tayari ni utitiri wa vyama ambao hauna maslahi yoyote kwenye serious opposition zaidi ya kubakiwa na vyama vichache vyenye serious oppositions na vyama vilivyobakia kuwa ni vyama jina tuu, vyama mtu na vyama makaratasi tuu kule ofisi ya msajili.

Nikirudi kwenye vyama serious vya opposition viko vitatu tuu, ukiondoa CCM ambacho ni chama tawala, vyama serious vinabaki kuwa ni CHADEMA, CUF na NCCR MAGEUZI kwa mbali, na kujumlisha 'vyama watu' viwili UDP (ni Cheyo) na TLP (Mrema) ambavyo siviingizi kwenye hesabu ya 2015, just time in between will tell!, vyama vyote vingine vilivyobakia ni vyama jina au vyama makaratasi.

Kufuatia muafaka na CCM, sasa chama cha CUF ni mshirika mkuu wa CCM na juzi nimemona Katibu Mkuu wake, Maalim Seif, akijivinjari jijini Dar es Salaam na matunda ya muafaka, S-Class 3 zikitanguliwa na pikipiki. Hivyo kwa sasa Zanzibar inatawaliwa na chama kimoja kikuu kiitwacho 'Umoja wa Kitaifa' (CCM-CUF).

Kama CUF ina wenye busara, adui mliokuwa mkigombea naye mkate, anapokukaribisha mumegeane huo mkate ambao mwanzo mligombana sana kuugombea, then utaupokea ulikiwa very cautious usije kuwa umetiliwa sumu ya polonium 210 which kills slowly and very softly. "I fear the Greeks especially when they bring gifts.

Kwenye kampeni za 2015, msifikiri tena kama kutakuwa na upinzani wowote wa maana kule Zanzibar, kwa sababu baada ya kuishuhudia hii miaka mitano ya amani, utulivu na ustawi wa Zanzibar, why vote for CCM or CUF any more, just vote for Umoja wa Kitaifa, maana popote utakapopiga kura, it doesn't matter anymore, kama keki tutakula wote kwanini kuigombania!..na huu ndio mwanzo wa kifo cha CUF!.

Tukija CUF bara, kwa vile CUF imefanikiwa kukishauri NCCR-Mageuzi na hivi vyama watu viwili (UDP na TLP) kuunda alliance yao dhidi ya Chadema, kwa maneno mangine vyama hivi vimekubali kuwa vyama vikaragosi vya CCM kupitia mlango wa nyuma wa mgongoni mwa CUF, hivyo kubakiwa na chama kimoja tuu cha upinzani cha kweli nchini ambacho ni Chadema.

Mwanzo niliwalaumu na kuwalaani Chadema, kuunda kambi ya upinzani peke yao, kumbe nilikuwa myopic, sikuweza kuona mbali kwenye bigger picture, niliwaona Chadema ni wabaguzi, wabinafsi na wenye umimi, bila kuifahamu hali halisia ya mambo.

Kupitia michango mbalimbali ya wana JF, nimefunguka macho na sio tuu kuanza kuielewa Chadema, bali kuikubali kuwa ndicho Chama Pekee cha upinzani kwa uchaguzi wa 2015 dhidi ya chama tawala CCM na msharika wake CUF na vyama vikaragosi vyao.

Nasisitiza huu ndio mwanzo wa kifo cha CUF na Neema kwa Chadema, kwa sababu baada ya uchaguzi huu, ruzuku ya mamilioni ya CUF yatakula panga la msajili sambamba na CCM ambayo sasa itakombwa na Chadema, na kama hakutatokea vita vya kimaslahi kugombea ruzuku hivyo (kama ilivyotokea kwa NCCR), na kuitumia kuimarisha chama, then 2015 Chadema itakuwa kwenye the best prospects kuchukua nchi.

Hivyo huu ushirikiano wa CCM na CUF na vikaragosi wao, ni very healthy kwenye safari ya kuelekea kwenye serious opposition kwa vyama utitiri kujifia natural death kwa kufuata kanuni law of the jungle ya 'Struggle for Existance, Survival for the Fittest', CUF inaelekea kufa na maneno ya Mwalimu ya serious oppositions yameanza kutimia.

Angalizo: Paskali sio mtafiti wa siasa bali ni mtazamaji na mfuatiliaji wa masuala ya kisiasa ambaye hafungamani na chama chochote, wala sio mfuasi wa itikadi yoyote, bali mshabiki wa demokrasia ya kweli ndani ya Bunge.

Paskali
 
Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,817
0
Wanabodi,
Wale wa zamani kama mimi mtayakumbuka baadhi ya maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (RIP) akizungumzia upinzani wa kweli, alisema angependa kuona serious oppositions wa vyama viwili au vitatu na sio utitiri wa vyama, japo Mwalimu aliongezea "Upinzani wa Kweli Utatoka CCM!", by now atakuwa ameshabadili msimamo wake ule kwa kutuma salamu kupitia kwa mjukuu wake kuwa " Upinzani wa Kweli, Utatoka Chadema".

Pasco wa JF ambae ni mtazamaji na mfuatiliaji ameshafika hadi ulimwengu wa watu waliokufa na kuja na kauli hii?

Tukija CUF bara, kwa vile CUF imefanikiwa kukishauri NCCR-Mageuzi na hivi vyama watu viwili (UDP na TLP) kuunda alliance yao dhidi ya Chadema, kwa maneno mangine vyama hivi vimekubali kuwa vyama vikaragosi vya CCM kupitia mlango wa nyuma wa mgongoni mwa CUF.

Nasisitiza huu ndio mwanzo wa kifo cha CUF na Neema kwa Chadema, kwa sababu baada ya uchaguzi huu, ruzuku ya mamilioni ya CUF yatakula panga la msajili sambamba na CCM ambayo sasa itakombwa na Chadema, na kama hakutatokea vita vya kimaslahi kugombea ruzuku hivyo (kama ilivyotokea kwa NCCR), na kuitumia kuimarisha chama, then 2015 Chadema itakuwa kwenye the best prospects kuchukua nchi.

Hapa Mkuu unazungumza kama vyama vinawania 'ruzuku' na sio kupigania haki ya mwananchi. Isitoshe hujaeleweka mkuu, kama chama cha CUF na CCM na vyama vyengine vya majina vitakufa katika kipindi cha miaka hii mitano, hadi kufikia mwaka huo 2015 bado Chadema itakuwa haijakomba hayo mamilioni ya ruzuku kutoka hivyo vyama vitavyokufa.

Unavyozungumza ni sawa na kusema ushindi unatokana na kiwango cha ruzuku kwneye chama, kama ni hivyo kwa logic yako Chadema haiwezi kuchukua nchi 2015 kwa kuwa itakuwa bado kupata ruzuku ya kutosha, labda tusubiri 2020 au?
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,834
2,000
Pasco wa JF ambae ni mtazamaji na mfuatiliaji ameshafika hadi ulimwengu wa watu waliokufa na kuja na kauli hii?

Hapa Mkuu unazungumza kama vyama vinawania 'ruzuku' na sio kupigania haki ya mwananchi. Isitoshe hujaeleweka mkuu, kama chama cha CUF na CCM na vyama vyengine vya majina vitakufa katika kipindi cha miaka hii mitano, hadi kufikia mwaka huo 2015 bado Chadema itakuwa haijakomba hayo mamilioni ya ruzuku kutoka hivyo vyama vitavyokufa.

Unavyozungumza ni sawa na kusema ushindi unatokana na kiwango cha ruzuku kwneye chama, kama ni hivyo kwa logic yako Chadema haiwezi kuchukua nchi 2015 kwa kuwa itakuwa bado kupata ruzuku ya kutosha, labda tusubiri 2020 au?
Kifo cha CUF kitatokana na kumezwa na CCM. Ushindi wa Chadema, wabunge 50 utaimega ruzuku ya CUF na CCM hivyo kukiimarisha Chadema. Kwa upande wa CCM, yenyewe haifi bali itaanguka na kubinuka chini juu kwa kubadilishwa jina toka Chama tawala mpaka chama cha upinzani.
 
Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,817
0
Kifo cha CUF kitatokana na kumezwa na CCM. Ushindi wa Chadema, wabunge 50 utaimega ruzuku ya CUF na CCM hivyo kukiimarisha Chadema. Kwa upande wa CCM, yenyewe haifi bali itaanguka na kubinuka chini juu kwa kubadilishwa jina toka Chama tawala mpaka chama cha upinzani.

wabunge 50 wa chadema sasa wamewanyima vipi ruzuku Cuf ambao na wao wamepata viti zaidi kuliko uchaguzi uliopita?

Labda uzungumzie ruzuku ya Ccm ambao kwa ajili ya kampeni na kuimarisha chama wanao ufisadi hawajali na ruzuku kiasi hicho.

mkuu unapoandika jaribu kuweka facts tu kujiita mfuatiliaji na kuja na maneno 'mapya' ya mtu aliyekufa kunatupa mashaka wasomaji, tunaanza kutilia shaka hata zile facts unazotoa.
 
Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,958
2,000
Angalizo: Pasco wa JF sio mtafiti wa siasa bali ni mtazamaji na mfuatiliaji wa masuala ya kisiasa ambaye hafungamani na chama chochote, wala sio mfuasi wa itikadi yoyote, bali mshabiki wa demokrasia ya kweli ndani ya Bunge.
Kwanini umetoa angalizo hilo?
kama unataka kuongelea jambo just talk na sio kujihami kwa maangalizo.
Inawezekana hilo angalizo sivyo hasa ulivyo bali inaweezekana ni kinyume chake ila unatoa angalizo kujihami.
 
Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,252
2,000
Wanabodi,

Nasisitiza huu ndio mwanzo wa kifo cha CUF na Neema kwa Chadema, kwa sababu baada ya uchaguzi huu, ruzuku ya mamilioni ya CUF yatakula panga la msajili sambamba na CCM ambayo sasa itakombwa na Chadema, na kama hakutatokea vita vya kimaslahi kugombea ruzuku hivyo (kama ilivyotokea kwa NCCR), na kuitumia kuimarisha chama, then 2015 Chadema itakuwa kwenye the best prospects kuchukua nchi.

Mkuu Pasco,

Hiyo ruzuku iliyoongezeka kwa Chadema ndio kansa ya mageuzi hapa Tanzania. Ruzuku iliwekwa kama chambo kwa vyama vya upinzani na kila anayewajua watanzania atakubaliana nami kuwa inapofikia suala la maslahi ya pesa huwa hakuna itikadi.

Jambo lingine ni kuwa, support base ya mageuzi inabadilika kulingana na uimara wa uongozi wa vyama hivi katika kipindi husika. Nakumbuka wale tuliomuunga mkono Mrema 1995, NCCR walipolikoroga tuliishia kuhamia CUF mwaka 2000 na hata wimbo wetu wa Chama Cuf wakauchukua! Nilipofuatilia wagombea wa Chadema mwaka huu hapa Dar hasa ngazi ya udiwani, niligundua wengi wao walikuwa Cuf 2005.

Na hili suala la Chadema kuchukua makapi ya ccm linaongeza idadi ya opportunists ndani yake na sidhani kama litaleta matokeo yoyote ya maana.
 
Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
15,370
2,000
Heshima kwako Pasco,

Mkuu naomba kutokubalina na wewe kwamba CUF itamezwa na CCM.Binafsi naona CUF wanaweza kutumia vyema mwanya wa kuwepo serekalini kubali baadhi ya mambo ambayo ni kikwazo kwa vyama vya upinzani kushinda chaguzi mbali mbali.

Ruzuku ya CHADEMA itakuwa kubwa lakini itategemea jinsi itakavyotumika ikitumiwa vizuri chama kitendelea kunawiri ikitumiwa vibaya mfarakano ikibisha hodi tegemea chama kusamabaratika.
 
TUKUTUKU

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
11,775

Yote yanawezekana cha msingi ni kusubili na kuona!!
 
Mwera

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
965
0
Heshima kwako Pasco,

Mkuu naomba kutokubalina na wewe kwamba CUF itamezwa na CCM.Binafsi naona CUF wanaweza kutumia vyema mwanya wa kuwepo serekalini kubali baadhi ya mambo ambayo ni kikwazo kwa vyama vya upinzani kushinda chaguzi mbali mbali.

Ruzuku ya CHADEMA itakuwa kubwa lakini itategemea jinsi itakavyotumika ikitumiwa vizuri chama kitendelea kunawiri ikitumiwa vibaya mfarakano ikibisha hodi tegemea chama kusamabaratika.

ngongo umenena,uliyosema yote nisahihi na ukweli mtupu,thanks mkuu kwamawazo yaliyoenda shule
 
Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
1,195
Hujui unachokiandika bro wait and see.....

Unaandika kwa mapenzi uliyonayo kwa Chadema na sio kwa nchi yako sioni mantiki na analysis zako za kufa kwa CUF labda mpenye Zanzibar na hasa pemba lakini as long as coastal area na pemba itaendelea ku exist basi na CUF itaendelea kuwepo!
 
Mtabe

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
675
0
Pasco huyu kwani si ndie yule aliandika mada hapa jf ya kuwashauri chadema? Baadae akajibiwa direct na dr slaa? Au sie huyu? Kama ndie siku ile huyu pasco alijitambulisha kua yeye ni mchambuzi wa kisiasa halafu leo anasema kinyume hapa vipi? Pasco naona unaendeleza ile tabia ya watanganyika ya kumuabudu nyerere lkn kama ni hivyo basi ni nyerere huyo huyo aliesema kua vyama vyote vya upinzani tanzania vitakufa ispokua CUF. Na hili pia nukuu watu wakuskie.
 
Epifania

Senior Member
Oct 18, 2010
132
0
Heshima kwako Pasco,

Mkuu naomba kutokubalina na wewe kwamba CUF itamezwa na CCM.Binafsi naona CUF wanaweza kutumia vyema mwanya wa kuwepo serekalini kubali baadhi ya mambo ambayo ni kikwazo kwa vyama vya upinzani kushinda chaguzi mbali mbali.

:crazy:
 
Ndachuwa

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
6,273
2,000
Inaweza kuwa ni tofauti na unavyobashiri kwani badala ya CUF kuanguka inaweza kuimarika zaidi kwa sababu moja kuu; Viongozi wake wakuu waliokuwa wanategemea kulipwa na chama mfano Katibu mkuu hivi sasa wanalipwa na serikali hivyo CUF kuanzia 2011 watakuwa na pesa nyingine za kujiimarisha tofauti na 2005 - 2010. Isitoshe idadi yao ya wabunge nayo imeongezeka sana kitu ambachi kitawaongezea ruzuku ya chama
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,834
2,000
Kwanini umetoa angalizo hilo?
kama unataka kuongelea jambo just talk na sio kujihami kwa maangalizo.
Inawezekana hilo angalizo sivyo hasa ulivyo bali inaweezekana ni kinyume chake ila unatoa angalizo kujihami.
Ndibalema, lengo la angalizo ni kuweka shield mapema, wengi humu ni washabiki ama wa vyama, ama wa itikadi, watu tulio neutral ni wachache, ni vizuri kuweka wazi ili wanabodi wasije nihesabu na mimi ni mshabiki wa chama fulani.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,834
2,000
Hujui unachokiandika bro wait and see.....

Unaandika kwa mapenzi uliyonayo kwa Chadema na sio kwa nchi yako sioni mantiki na analysis zako za kufa kwa CUF labda mpenye Zanzibar na hasa pemba lakini as long as coastal area na pemba itaendelea ku exist basi na CUF itaendelea kuwepo!
Sokomoko, Serikali ya umoja wa kitaifa ni jambo jema kwa utulivu, ushirikiani na mshikamano wa Wanzaibar kwa ustawi wa Zanzibar, lakini kwenye upinzani, kuipigia kura CUF ni sawa na kuipigia CCM, what difference does it make, na hiki ndicho kifo chenyewe kilipolalia kwa huku bara, kuipigia CUF ni kupigia CCM, come 2015, CUF will be reduced to nothing chama pinzani Bara kitabaki Chadema tuu.

Kwa taarifa sina mapenzi yoyote kwa Chadema wala kwa chama chochete, bali naunga mkono chama chochote chenye matumaini ya kutupeleka kwenye demokrasia ya kweli, I can see some light in Chadema.
 
Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
1,250
Nasisitiza huu ndio mwanzo wa kifo cha CUF na Neema kwa Chadema, kwa sababu baada ya uchaguzi huu, ruzuku ya mamilioni ya CUF yatakula panga la msajili sambamba na CCM ambayo sasa itakombwa na Chadema, na kama hakutatokea vita vya kimaslahi kugombea ruzuku hivyo (kama ilivyotokea kwa NCCR), na kuitumia kuimarisha chama, then 2015 Chadema itakuwa kwenye the best prospects kuchukua nchi.

Hivyo huu ushirikiano wa CCM na CUF na vikaragosi wao, ni very healthy kwenye safari ya kuelekea kwenye serious opposition kwa vyama utitiri kujifia natural death kwa kufuata kanuni law of the jungle ya 'Struggle for Existance, Survival for the Fittest', CUF inaelekea kufa na maneno ya Mwalimu ya serious oppositions yameanza kutimia.

TATIZO LAKO PASCO UKO VERY JUDGEMENTAL KAMA AMBAVYO YOU WRONGLY JUDGED CHADEMA ULIPOKUWA POLITICAL ANALYST; NAHISI UNAFANYA MAKOSA HAYO HAYO YA KUIFANYIA CUF N.K NEGATIVE JUDGEMENT UKIWA
"sio mtafiti wa siasa bali ni mtazamaji na mfuatiliaji wa masuala ya kisiasa ambaye hafungamani na chama chochote, wala sio mfuasi wa itikadi yoyote, bali mshabiki wa demokrasia ya kweli ndani ya Bunge".

NAHISI KUWA KADRI UTAKAVYO KUWA UKIBADILISHA HUKUMU ZAKO BILA KUTOA VIELEELZO ALIVYOKUOMBA DR W SLAA, NDIVYO PIA UTAKAVYOKUWA UKIBADILISHA TITLES ZAKO.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,834
2,000
Pasco huyu kwani si ndie yule aliandika mada hapa jf ya kuwashauri chadema? Baadae akajibiwa direct na dr slaa? Au sie huyu? Kama ndie siku ile huyu pasco alijitambulisha kua yeye ni mchambuzi wa kisiasa halafu leo anasema kinyume hapa vipi? Pasco naona unaendeleza ile tabia ya watanganyika ya kumuabudu nyerere lkn kama ni hivyo basi ni nyerere huyo huyo aliesema kua vyama vyote vya upinzani tanzania vitakufa ispokua CUF. Na hili pia nukuu watu wakuskie.
Mtabe, huu ndio uzuri wa JF, tunatumia pen names zozote unazoona zinakufiti, ndio maana tuna maprofesa, mpaka majerali. Ni kweli mwanzo nilijiita mchambuzi wa siasa, baada ya kupewa somo na wana JF mchambuzi anatakiwa aweje, ndipo nikajigundua kumbe hata sifa ya mchambuzi sina, nimejipima nikajiona sifa ya mtazamaji na ufuatiliaji inanifiti zaidi, hivyo mimi sasa sio mchambuzi ni mtazamaji tuu.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,834
2,000
Nasisitiza huu ndio mwanzo wa kifo cha CUF na Neema kwa Chadema, kwa sababu baada ya uchaguzi huu, ruzuku ya mamilioni ya CUF yatakula panga la msajili sambamba na CCM ambayo sasa itakombwa na Chadema, na kama hakutatokea vita vya kimaslahi kugombea ruzuku hivyo (kama ilivyotokea kwa NCCR), na kuitumia kuimarisha chama, then 2015 Chadema itakuwa kwenye the best prospects kuchukua nchi.

Hivyo huu ushirikiano wa CCM na CUF na vikaragosi wao, ni very healthy kwenye safari ya kuelekea kwenye serious opposition kwa vyama utitiri kujifia natural death kwa kufuata kanuni law of the jungle ya 'Struggle for Existance, Survival for the Fittest', CUF inaelekea kufa na maneno ya Mwalimu ya serious oppositions yameanza kutimia.

TATIZO LAKO PASCO UKO VERY JUDGEMENTAL KAMA AMBAVYO YOU WRONGLY JUDGED CHADEMA ULIPOKUWA POLITICAL ANALYST; NAHISI UNAFANYA MAKOSA HAYO HAYO YA KUIFANYIA CUF N.K NEGATIVE JUDGEMENT UKIWA "sio mtafiti wa siasa bali ni mtazamaji na mfuatiliaji wa masuala ya kisiasa ambaye hafungamani na chama chochote, wala sio mfuasi wa itikadi yoyote, bali mshabiki wa demokrasia ya kweli ndani ya Bunge".

NAHISI KUWA KADRI UTAKAVYO KUWA UKIBADILISHA HUKUMU ZAKO BILA KUTOA VIELEELZO ALIVYOKUOMBA DR W SLAA, NDIVYO PIA UTAKAVYOKUWA UKIBADILISHA TITLES ZAKO.
Jatropha, I'm just too franc, sio judgementat, nilifuta ujinga kidogo kwenye somo la historia kusoma the past ukilinganisha na the present hivyo you can pre-determine the future. CUF ilikotoka, ilipo na inakokwenda, imetumia ile formular ya "IF YOU CAN BEAT THEM, JOIN THEM" they are one now and together they will fall, CCM will survive, CUF will die, just natural death.
 
Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
1,250
mtabe, huu ndio uzuri wa jf, tunatumia pen names zozote unazoona zinakufiti, ndio maana tuna maprofesa, mpaka majerali. Ni kweli mwanzo nilijiita mchambuzi wa siasa, baada ya kupewa somo na wana jf mchambuzi anatakiwa aweje, ndipo nikajigundua kumbe hata sifa ya mchambuzi sina, nimejipima nikajiona sifa ya mtazamaji na ufuatiliaji inanifiti zaidi, hivyo mimi sasa sio mchambuzi ni mtazamaji tuu.

to be analyst in whatever field you must have some basic qualifications. kwa kuwa umeshajitambulisha kama political analyst while you are not that is impersonation not withstanding the nick names with use in jf. Haina tofauti na awle wateja wa msemakweli wenye fake degrees.

Sasa kwa kuwa umegundua una weakness zako ndio utuletee habari za kuwakera wengine tena bila utafiti wa kutosha. Sijaona mahali popote kwenye sheria za jf kuwa ni lazima mtu aanzish thread hata kama hana facts.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom