Kifo cha CUF hichoo... chaja! Upinzani kubaki CHADEMA pekee?

Ndibalema, lengo la angalizo ni kuweka shield mapema, wengi humu ni washabiki ama wa vyama, ama wa itikadi, watu tulio neutral ni wachache, ni vizuri kuweka wazi ili wanabodi wasije nihesabu na mimi ni mshabiki wa chama fulani.

Mkuu utaniwia radhi lakini hii post yako stinks of chadema fanaticism (i am not saying it is a bad thing, mbaya ni kutaka watu waaamine vyenginevyo)

hoja ya msingi kwenye post yako ni moja tu kuwa kwa vile ccm na cuf wameungana basi wapiga kura come 2015 hawataona faida ya kuwapigia Cuf kwa vile ni sawa na Ccm tu (hoja ambayo tunaweza kuuita ubashiri ambao una muelekeo kidogo)

kuliko bakia kote hakuna facts na ulipoweka fact basi si fact sahihi (rejelea punguo la ruzuku ya cuf)

inaonekana ziadi ni katika kujikosha kwa vile uliandika post iliyokosolewa vibaya na mkuu wa chadema na sasa umeamua uifagilie kuweka mambo sawa.
 
Ni rahisi cuf kupenyeza bara kuliko chadema kupenyeza zanzibar. Isitoshe cuf wanajua siasa na ni wakomavu katika hilo.
Wanaangalia maslahi ya taifa kwanza kinyume na viongozi wa chadema. Wewe ukisusa wengine wanakula.
Raha ya ngoma uingie ucheze na sio kutizama nje.
 
maslahi gani ya taifa kuchukua fedha za mafisadi kwa ajili ya kampeni?
 
Mkuu utaniwia radhi lakini hii post yako stinks of chadema fanaticism (i am not saying it is a bad thing, mbaya ni kutaka watu waaamine vyenginevyo)

hoja ya msingi kwenye post yako ni moja tu kuwa kwa vile ccm na cuf wameungana basi wapiga kura come 2015 hawataona faida ya kuwapigia Cuf kwa vile ni sawa na Ccm tu (ambao tunaweza kuuita ubashiri ambao una muelekeo kidogo)

kuliko bakia kote hakuna facts na ulipoweka facts si sahihi ( punguo la ruzuku ya cuf)

inaonekana ziadi ni katika kujikosha kwa vile uliandika post iliyokosolewa vibaya na mkuu wa chadema na sasa umeamua uifagilie kuweka mambo sawa tu.
Gaijin, kwa vile sina chama, sio mwanachama na sio mshabiki wa chama chochote, hainipi shida kudhaniwa lolote, ila nakiri mimi binafsi nina tatizo moja tuu, kuwa mkweli daima, being too franc is bad sometimes, imeshawahi kunicost sana in my life na mpaka hapa nilipo, bado naendelea kufidia/kulipia baadhi ya madeni.

Kwa vile hizi ni opinion zangu, haijalishi kama zitawaumiza CUF, Chadema au CCM kwa nia njema za kuifikia 2015 yenye demokrasia zaidi, kwa sasa CUF wamelamba dume na hii dose ninayotoa ni vidonge vichungu na hivi ndivyo vinavyotibu kweli.

Ile post ya CCM imechokwa na Chadema haijajipanga, bado nateremka nayo bila kujali washabiki wa Chadema wananionaje, hiyo dose wakikubali kuimeza sio lazima iponyeshe, ila itatibu, sambamba na CCM halikadhalika CUF, kama ni kweli wamewaambia wenzao wa bara, wasi team na CHADEMA bali wasupport CCM, huo ndio mwisho wao huku bara, down the drain they will go with CCM yao!.
 
Jamani tujadili hoja zaidi pale ambapo mtu hakubaliani napo au una wazo tofauti tuwekeeni hapa mawazo yenu kuhusu mnachoamini kina usahihi zaidi.Pasco ameeleza vizuri yu na ni mawazo yake ya nini kumuattack? lets challenge/correct him according to what we think we know better.
 
Gaijin, kwa vile sina chama, sio mwanachama na sio mshabiki wa chama chochote, hainipi shida kudhaniwa lolote, ila nakiri mimi binafsi nina tatizo moja tuu, kuwa mkweli daima, being too franc is bad sometimes, imeshawahi kunicost sana in my life na mpaka hapa nilipo, bado naendelea kufidia/kulipia baadhi ya madeni.

Kwa vile hizi ni opinion zangu, haijalishi kama zitawaumiza CUF, Chadema au CCM kwa nia njema za kuifikia 2015 yenye demokrasia zaidi, kwa sasa CUF wamelamba dume na hii dose ninayotoa ni vidonge vichungu na hivi ndivyo vinavyotibu kweli.

Ile post ya CCM imechokwa na Chadema haijajipanga, bado nateremka nayo bila kujali washabiki wa Chadema wananionaje, hiyo dose wakikubali kuimeza sio lazima iponyeshe, ila itatibu, sambamba na CCM halikadhalika CUF, kama ni kweli wamewaambia wenzao wa bara, wasi team na CHADEMA bali wasupport CCM, huo ndio mwisho wao huku bara, down the drain they will go with CCM yao!.

ni opinion zako tunakubali lakini unajaribu kuzibeba kwa facts ambazo si sahihi. Hatupingi uhuru wako wa kutoa mawazo, tunachopinga ni kupindisha uhalisia ili tu uweze kuthibitisha opinion hizo.

Na unapozinduliwa kuwa hizo facts si sahihi na ukaendelea kuzitetea ndipo unapofanya watu wakuite mshabiki hasa ukizingatia kuwa umefikia hadi umemnywesha maneno mtu aliyekufa ili tu kulalia upande mmoja kwenye hoja yako.

you can do better than this kama mwandishi wa habari.
 
Salute Pasco!!
Kwanza hongera kwa kuwa mmoja ya wana jamvi walio creative.Haijalishi kama hauko sahihi ama upo sahihi lakini ukamilifu na uzoefu huja si kwa kufanya mara moja bali mara nyingi.Wanasiasa na wachambuzi wengi wa Tanzania( u inclusive) wamekuwa wakijaribu kusimama katika kivuli cha Mwalimu Nyerere kwa kuja na quotes zake kila mara kutaka kuhalalisha mawazo na fikra zao.Kwanza naomba uamini Nyerere hakuwa nabii Bali alitumia akili zake kusoma alama za nyakati na bila kutumia ushabiki kuja na vitu ambavyo ni concrete na kila mtu anafikiri yote aliyosema nyerere llazima yatimie!Sikatai wewe pamoja na wengine kutumia quotes za Mwalimu ku "verify" hisia na maoni yenu!Ni Jambo jema kujifunza siasa kwa mifano lakini utambue pia ukitoa muda wako ukawa "objective enough" katika maandiko yako na ukawa "un- biased" analysit (kama unavyodai kuwa) utakuja na vitu vikubwa na pengine ukawa na ushawishi sana (who knows what tomorrow holds).

Tatizo lako Pasco,unadai kuwa neutral wakati kila mtu anafaham wewe umeegemea wapi kwa hiyo kupata challenges nyingi sana kwa articles zako jamvini( si vibaya they make u stronger though).Ukisema hufungamani na chama chochote inaweza ikawa sawa lakini bado "emotinally" watu wanatambua umefungamana na nani ingawa unaweza usiwe na card ya chama. Pasco tambua wengi ya Watanzania wasomi hawaridhiki na hali ya miasha na mifumo mibaya ya uongozi wa serikali yetu! Huwezi kuwalaumu CUF kuikubali serikali mseto ila unaweza kuwalaumu kwa nini waingie katika makubaliano na CCM wakati hili si jambo la makubaliano ya kivyama "it is rather a constitutional issue".Unapokuwa unafuta Vyeo vilivyotajwa kikatiba na Kuanzaisha vyeo Visivyotajwa na Katiba si makubaliano ya vyama Viwili kama ambavyo imefanyika. Pengine kesho CCM ikashinda na NCCR ikawa ya pili serkali ya mseto haitakuwepo kwa sababu tu CCM iliingia ndoa na CUF. Mimi nafikiri hapo ndio kasoro kubwa ya makubaliano yanapokuwa!Jambo jingine,kama CUF wakapata asilimia 49.1 na CCM akapata asilimia 50.9 kama ilivyotokea visiwani kwa bara ishu hii haitambuliki kwa sababu hawajakubaliana na CCM ya bara.Hatuwezi kuwa na mifumo ya ushirikishi wa vyama viwili kama ni ishu ya kitaifa.Kwa mawazo yangu CUF hawakusimama kaitka maslahi ya taifa bali walisimama katika maslahi ya kichama.Nikija katika wazo lako CUF kumezwa na CCM,kwa upande mmoja nitasema inawezekana lakini si lazima kutokea.

Fikra ya wanasiasa wengi ni kutaka zaidi,kwa hiyo mimi siamini kama CUF watajisahau kuwa wanahitaji zaidi kwa kuridhika na nafasi waliyonayo Visiwani. Maalim Seif( refer historia yake) amekuwa ni mtu wa movement kama ni kumezwa huyu jamaa nafikiri angekuwa kamezwa tangu zamani.Mi sioni kama sera ya wao kukubali serikali ya mseto itakuwa na effect katika ukubaliko wa CUF kwa wananchi isipokuwa kwa vyama pinzani ambavyo vinaona CUF wameisaliti demokrasia ya haki ya kikatiba.CCM kama kawaida kimekuwa kikiendeleza ubabe wa kisiasa kwa kujaribu kutumia kila mbinu kuhakikisha kinabaki madarakani.

Ninachoamini kitakachoitoa CCM madarakani si CHADEMA bali wananchi walioelimika. Kama CHADEMA watabaki kuwa na influence kwa wananchi na CHADEMA kama chama kuwa na uwakilishi wa kichama kuanzaia "grassroots" mpaka kitaifa watakuwa na wakati mrahisi sana kutumia kasoro za CCM na wanachama wake wakuu kuiondoa madarakani.Naamini kabisa itakuwu ngumu sana kuchukua nchi kwa sheria na katiba tuliyonayo kwa vyama vya upinzani,tunahitaji mabadiriko ya katiba na sheria ambazo zitakuwa hazikandamizi "minority".Kuwa na sheria butu ambazo zinageuzwa kadri watu wapendavyo kuwa na maana tofauti "Just to suite their claims".Raisi Kupunguziwa madaraka,haiwezekani raisi kuteua kila mtendaji mkuu wa mahakama,polisi ,jeshi,siasa(NEC),PCCB, Directors wa kila kitu.Kwa mwendo huu ni ishu kubwa sana maana wananchi hawana sehemu ya kukimbilia kote waendapo Rais na mkono wake!!

Bado tuna Mwnedo,sijaona CUF,CCM kupotea kwa miaka 15 ijayo.Bado vitaendelea kuwepo ingawa umaarufu unaweza kuwa mdogo sana.Vyama vingine vilivyobaki ni sawa na mgombea binafsi hivyo Battle kubwa kwa sasa ni CHADEMA,CCM na CUF!

"Samahani jamani mi si mchambuzi ni mtoa maoni niliekuwa na mtazamo wangu,yawezekana nisiwe neutral ila nimejaribu kuwa"
 
Pasco,

I beg to differ with you on this. Infact Muafaka give CUF more power and a significant chunk of voters come 2015. CUF played this strategically and watch out for their Union Presidential candidate 2015.

With CCM in shambles, and expectations Chadema will run the same play book again, the swing votes will not vote for CCM rather for CUF and they will emerge winners just simply based on who they field on the ticket.

Even though Kikwete branded them to be zealots, he has just simply created a winning ground for them 2015.

It is a fact that CCM will have to field a Christian, because of some stupid rule within CCM, and already Chadema not only are being branded Wachaga and Wakristo, either Freeman or Dr. Slaa may be running again. Then just like as it was this year, the voters will vote using religious sentiments and not true message of a party.

Mark my words, unless CCM pulls what they did 2005 with Mkapa picking Kikwete!
 
marshal, asante sana kwa maoni yako, in fact I have always been a political comentator, its now that I'm trying to write down what I think and everything I have posted is the 1st rough draft, I will refine little by little na his cricisim zinanisaidia kurefine, eventually nitaibuka na makala zangu kwenye baadhi ya magazeti siku za usoni as run off towards 2015.
 
Pasco,

I beg to differ with you on this. Infact Muafaka give CUF more power and a significant chunk of voters come 2015. CUF played this strategically and watch out for their Union Presidential candidate.

With CCM in shambles, and expectations Chadema will run the same play book again, the swing votes will not vote for CCM rather for CUF and they will emerge winners just simply based on who they field on the ticket.

Even though Kikwete branded them to vbe zealots, whe has just simply created a winning ground for them 2015.

It is a fact that CCM will have to field a Christian, because of some stupid rule within CCM, and already Chadema not only are being branded Wachaga and Wakristo, either Freeman or Dr. Slaa may be running again. Then just like as it was this year, the voters will vote using religious sentiments and not true message of a party.

Mark my words, unless CCM pulls what they did 2005 with Mkapa picking Kikwete!
Rev. Kishoka, asante, tangu nimeposti hii posti ya kifo cha CUF, hii posti yako ndio ya kwanza kunidhihirishia, I was wrong, nilioverlook the 'religious factor', na kusema kweli ukiangalia trend ya maeneo ambako Dr. Slaa amepata kura nyingi ukicompare na maeneo ambayo Prof. amezoa kura nyingi, ukianalyse with religious angle, it leaves much to be desired, and I addmit this is bad!, you are right, CUF will not dead yet, not so soon, but eventually.
 
Wanabodi,
Wale wa zamani kama mimi mtayakumbuka baadhi ya maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (RIP) akizungumzia upinzani wa kweli, alisema angependa kuona serious oppositions wa vyama viwili au vitatu na sio utitiri wa vyama, japo Mwalimu aliongezea "Upinzani wa Kweli Utatoka CCM!", by now atakuwa ameshabadili msimamo wake ule kwa kutuma salamu kupitia kwa mjukuu wake kuwa " Upinzani wa Kweli, Utatoka Chadema".

Tanzania tunavyo vyama 19 mpaka sasa, na hakuna limit number ya vyama vipya kusajiliwa, hii tayari ni utitiri wa vyama ambao hauna maslahi yoyote kwenye serious opposition zaidi ya kubakiwa na vyama vichache vyenye serious oppositions na vyama vilivyobakia kuwa ni vyama jina tuu, vyama mtu na vyama makaratasi tuu kule ofisi ya msajili.

Nikirudi kwenye vyama serious vya opposition viko vitatu tuu, ukiondoa CCM ambacho ni chama tawala, vyama serious vinabaki kuwa ni CHADEMA, CUF na NCCR MAGEUZI kwa mbali, na kujumlisha 'vyama watu' viwili UDP (ni Cheyo) na TLP (Mrema) ambavyo siviingizi kwenye hesabu ya 2015, just time in between will tell!, vyama vyote vingine vilivyobakia ni vyama jina au vyama makaratasi.

Kufuatia muafaka na CCM, sasa chama cha CUF ni mshirika mkuu wa CCM na juzi nimemona Katibu Mkuu wake, Maalim Seif, akijivinjari jijini Dar es Salaam na matunda ya muafaka, S-Class 3 zikitanguliwa na pikipiki. Hivyo kwa sasa Zanzibar inatawaliwa na chama kimoja kikuu kiitwacho 'Umoja wa Kitaifa' (CCM-CUF).

Kwenye kampeni za 2015, msifikiri tena kama kutakuwa na upinzani wowote wa maana kule Zanzibar, kwa sababu baada ya kuishuhudia hii miaka mitano ya amani, utulivu na ustawi wa Zanzibar, why vote for CCM or CUF any more, just vote for Umoja wa Kitaifa, maana popote utakapopiga kura, it doesn't matter anymore, kama keki tutakula wote kwanini kuigombania!..na huu ndio mwanzo wa kifo cha CUF!.

Tukija CUF bara, kwa vile CUF imefanikiwa kukishauri NCCR-Mageuzi na hivi vyama watu viwili (UDP na TLP) kuunda alliance yao dhidi ya Chadema, kwa maneno mangine vyama hivi vimekubali kuwa vyama vikaragosi vya CCM kupitia mlango wa nyuma wa mgongoni mwa CUF, hivyo kubakiwa na chama kimoja tuu cha upinzani cha kweli nchini ambacho ni Chadema.

Mwanzo niliwalaumu na kuwalaani Chadema, kuunda kambi ya upinzani peke yao, kumbe nilikuwa myopic, sikuweza kuona mbali kwenye bigger picture, niliwaona Chadema ni wabaguzi, wabinafsi na wenye umimi, bila kuifahamu hali halisia ya mambo.

Kupitia michango mbalimbali ya wana JF, nimefunguka macho na sio tuu kuanza kuielewa Chadema, bali kuikubali kuwa ndicho Chama Pekee cha upinzani kwa uchaguzi wa 2015 dhidi ya chama tawala CCM na msharika wake CUF na vyama vikaragosi vyao.

Nasisitiza huu ndio mwanzo wa kifo cha CUF na Neema kwa Chadema, kwa sababu baada ya uchaguzi huu, ruzuku ya mamilioni ya CUF yatakula panga la msajili sambamba na CCM ambayo sasa itakombwa na Chadema, na kama hakutatokea vita vya kimaslahi kugombea ruzuku hivyo (kama ilivyotokea kwa NCCR), na kuitumia kuimarisha chama, then 2015 Chadema itakuwa kwenye the best prospects kuchukua nchi.

Hivyo huu ushirikiano wa CCM na CUF na vikaragosi wao, ni very healthy kwenye safari ya kuelekea kwenye serious opposition kwa vyama utitiri kujifia natural death kwa kufuata kanuni law of the jungle ya 'Struggle for Existance, Survival for the Fittest', CUF inaelekea kufa na maneno ya Mwalimu ya serious oppositions yameanza kutimia.

Angalizo: Pasco wa JF sio mtafiti wa siasa bali ni mtazamaji na mfuatiliaji wa masuala ya kisiasa ambaye hafungamani na chama chochote, wala sio mfuasi wa itikadi yoyote, bali mshabiki wa demokrasia ya kweli ndani ya Bunge.
Una improve Pasco. Na hii inatokana na kukubali kukosolewa. Better than your last post on the same issue. Ila hii ya kusema uko neutral sidhani kama ni sahihi! Kila binadamu yuko biased. Tatizo ni kiwango na unazi ndipo tuna tofauti.
 
Pasco,

With CCM in shambles, and expectations Chadema will run the same play book again, the swing votes will not vote for CCM rather for CUF and they will emerge winners just simply based on who they field on the ticket.

Even though Kikwete branded them to be zealots, he has just simply created a winning ground for them 2015.

It is a fact that CCM will have to field a Christian, because of some stupid rule within CCM, and already Chadema not only are being branded Wachaga and Wakristo, either Freeman or Dr. Slaa may be running again. Then just like as it was this year, the voters will vote using religious sentiments and not true message of a party.

Mark my words, unless CCM pulls what they did 2005 with Mkapa picking Kikwete!

Rev. Kishoka nakubaliana nawewe kabisa hapo kwenye red japo hapo kwenye blue sijakupata, kama unaweza fafanua tafadhali.

Hii habari ya udini na kuihusisha CHADEMA na ukristo ndio ilikuwa silaha kubwa ya JK katika nyakati za mwisho mwisho wa kampeni zake. CCM walijenga chuki na kukuza mtazamo wa kidini miongoni mwa jamii ya watanzania. Na kama hakutakuwa na jitihada za dhati kwa serikali kutibu haya majeraha waliyoyasababisha basi ni dhahiri kuwa mpasuko baina ya makundi haya mawili katika jamii kuna uwezekano mkubwa sana ukazidi kutanuka.
 
If you can't beat them join them, then beat them from within. Mafanikio na madhara ya CUF kujiunga na CCM yatatokana na jinsi serikali ya umoja wa kitaifa itakavyoperform kati ya 2010-2015.

CDM wanaweza kucapitalise na kugain a lot kutoka kwenye hii ndoa ya CUF na CCM kama wakicheza karata zao vizuri.
 
Mkapa alisema CCM wamekubali serikali ya Mseto Zanzibar, lakini LAZIMA iongozwe na CCM au kwa maneno mengine lazima Rais wa Zanzibar awe ni kutoka CCM na tulishuhudia hayo. Kwenye facebook Mh. Jussa amekiri kwamba Maalim Seif alipokwa ushindi na alikubali matokeo kwa ajili ya amani na utulivu.

Nina tatizo kubwa sana na huo muafaka na kwanini Mkapa aseme lazima serikali ya mseto iongozwe na CCM?

Kikwete alisema kwamba serikali ya mseto si ya kudumu, bali watakuwa wanafanya evaluation kila baada ya miaka 5 ili ku-determine kama mseto uendelee au la. Kuna kitu CCM wanakifanya ambacho hatukijui na hivyo CUF wanatakiwa kuwa makini sana katika kipindi hiki cha miaka 5.

Ili CUF waweze kufanikiwa na kujiimarisha zaidi, lazima wahakikishe kwamba ndani ya hii miaka 5 wabadilishe Katiba na Kuunda upya Tume ya Uchaguzi (ZEC) ambayo itakuwa huru.

Serikali ya JMT haiko tayari kuona CUF wanaongoza serikali ya mseto Zanzibar, maana pindi CUF ikiongoza itakuwa ni chachu ya kutaka mabadiliko hata huku bara ikiwa ni pamoja na shinikizo la kutaka Katiba Mpya ya JMT, kwa kuwa Katiba ya JMT inagusa pia Zanzibar na serikali ya JMT ikigoma ndipo kunaweza kuwa na tishio la kuvunja Muungano, na CCM bara hawako tayari kuona Muungano unakufa mikononi mwao.

Muafaka huu ambao umezaa serikali ya mseto, kama CUF watautumia vyema inaweza kuwa kura ya turufu kwa CUF na upinzani kwa ujumla, lakini kama viongozi wake watabweteka na kuridhika ndio itakuwa imekula kwa CUF. Ni mapema sana kutoa tathimini ya future ya CUF kwa kuwa ndio kwanza mseto umeundwa, ngoja tuone watakavyocheza karata zao miaka 2 ya mwanzo.
 
Namshukuru pasco aliyeanzisha hii thread na wote walioichagia

ni wazi sasa kwamba CUF wanahaha na wanatumiwa na CCM kuhujumu upinzani. Wanahaha kwa sababu hawawezi sasa kuwa wasemaji rasmi bungeni kwani chadema itateua mawaziri kivuli wote kutoka chadema

wanatumika na ccm kwa sababu sasa wanashinikiza chadema imtambue rahisi. Hii pia inazuia cuf kushirikiana na chadema, jambo ambalo sass wanatamani sana ili wawe karibu na chadema waihujumu.
 
Wanabodi,
Nasisitiza huu ndio mwanzo wa kifo cha CUF na Neema kwa Chadema, kwa sababu baada ya uchaguzi huu, ruzuku ya mamilioni ya CUF yatakula panga la msajili sambamba na CCM ambayo sasa itakombwa na Chadema, na kama hakutatokea vita vya kimaslahi kugombea ruzuku hivyo (kama ilivyotokea kwa NCCR), na kuitumia kuimarisha chama, then 2015 Chadema itakuwa kwenye the best prospects kuchukua nchi.

Angalizo: Pasco wa JF sio mtafiti wa siasa bali ni mtazamaji na mfuatiliaji wa masuala ya kisiasa ambaye hafungamani na chama chochote, wala sio mfuasi wa itikadi yoyote, bali mshabiki wa demokrasia ya kweli ndani ya Bunge.

Baada ya matokeo ya Uchaguzi Mdogo wa Igunga, nimei revisit hii thread yangu niliyoipost November, 15 mwaka jana na kujifariji kuwa ni kweli, safari ya CUF bara kuelekea kaburini, imeanza rasmi kitambo.
 
Namshukuru pasco aliyeanzisha hii thread na wote walioichagia

ni wazi sasa kwamba CUF wanahaha na wanatumiwa na CCM kuhujumu upinzani. Wanahaha kwa sababu hawawezi sasa kuwa wasemaji rasmi bungeni kwani chadema itateua mawaziri kivuli wote kutoka chadema

wanatumika na ccm kwa sababu sasa wanashinikiza chadema imtambue rahisi. Hii pia inazuia cuf kushirikiana na chadema, jambo ambalo sass wanatamani sana ili wawe karibu na chadema waihujumu.
Gurudumu, asante kwa hili, nimeliona Igunga.
 
inajimaliza yenyewe,duh yaani umati wote ule ktk kampeni na kuja kupata 2000?
 
Back
Top Bottom