Umezaliwa na makadirio ya maisha ya Mtz ndio yanayoonyesha umefikia mwisho wa uhai wako ,tulikupenda ila bwana amekupenda zaidi na hatutasahau wala kuwacha kukumbuka ,uzee wako umeiwachia Tanzania maafa ya aina yake na kupigiwa mfano duniani ,ajali zinazowamaliza waTz zimekuwa zikikusindikiza bila ya wewe mwenyewe kujua ,CCM hakuna lisilo na mwisho ,dalili la jina lako CCM (Chukua Chako Mapema) limeshika kasi kwa viongozi walioshika bendera za chama chako wakizidi kuwahi ,wakijua wasipowahi leo kaburini hakuna kitu.
Ondoka kwa salama ,ingawa viashiria vinaonyesha dalili ya kifo chako ,yaani utakufa kwa kupapatika vibaya sana na kukuru kakara zitashinda kishindo cha mwendawazimu wa malaria ,ila vyombo vya dola havitakaa mbali nawe ili usisababishe maafa makubwa ,na vitakuwahi kwa kukufunga kamba za miguu na mikono na hata madaktari watakudunga sindano za kukuvunja nguvu ili ufariki kwa taratibu sana,
Poleni wafiwa,