Kifo cha CCM kimetimia

Kifo cha CCM kimetimia

kama pana ukweli vile lkn vigogo hawapendi haki mfumo waliouzoea ni kama cancer ya damu
 
kuna wtz walokamatw china n madawa ya kulevy na serkal imekaa kimya lkn serkal iliwatoa watu last yr.au yaliwahusu wao
 
kuna wtz walokamatw china n madawa ya kulevy na serkal imekaa kimya lkn serkal iliwatoa watu last yr.au yaliwahusu wao
Hao wanaosubiri kunyongwa ni punda, nawao walikubali kubebeshwa madawa, hapo wachina lazima wawachinje ili mkome kuwapelekea hilo sembe,halafu unapo kuwapunda thamani ya binadamu huna hivyo bismillah
ni halali yako.
 
ingekuwa ww ndo ndugu yako ambye unampenda ungehonga nn wachina il aachiliwe?
 
THANKS! kwa ccm kuchua hoja za wapinzani kwa 85% na kuzifanyia kazi kwa umakini HAKIKA KIFO CHA UPINZANI HICHO AROUND THE CORNER ona ktk kikao kilichoisha jinsi walivyokuwa hawana hoja za kimsingi mh.MWIGULU KAZA BUTI HEAL all wounds quickly step by step//piga mkutano ubungo huku wataalamu wa maji wakipiga kazi/mnamaliza mkutano mnaenda kusavei mafundi ktk mradi
 
Tangu mfumo wa vyama vingi umeingia Nchini mwetu, mwenendo wa kisiasa umekuwa ni wenye ushindani mkubwa hasa kwa miaka ya hivi karibuni. Kumeibuka vyama na wanasiasa ambao kwa njia moja ama nyingine wamekuwa wakileta ushindani mzuri katika siasa, hali ambayo imechangia kuleta fikra mpya katika uongozi wa vyama mbalimbali na hata serikali kwa ujumla.
Tumeshuhudia wanasiasa mbalimbali wenye fikra chanya za kimaendeleo kutoka ndani ya CCM na vyama vya upinzani, orodha yao ni ndefu. Vyama vya upinzani kwa ujumla vimekuwa vikijidhatiti na kujiimarisha ili kuchukua Dola wakati CCM nayo imekuwa ikijidhatiti ili kuendelea kuwa madarakani. Hali hii imesababisha siasa zetu kuwa ni zenye ushindani mkubwa hasa katika kipindi cha chaguzi mbalimbali.
kwa ujumla naweza kusema siasa zetu zinakua ingawa bado tunaendesha siasa za kizamani, siasa ambazo yule asiekubaliana na mawazo yako unamuona ni adui kiasi hata cha kutoaminiana. Hali hii imejitokeza baina ya vyama kwa vyama, lakini pia hata ndani ya vyama baina ya wanachama kwa wanachama. Hali ipo hivyo ndani ya vyama vyote hasa vyama vikubwa kama NCCR MAGEUZI, CUF, CHADEMA, CCM na kwa mbali TLP. Tumeshuhudia sakata la Maalim Seif Sharrif na Hamad Rashid, tumeyaona ya David Kafulila na NCCRR Mageuzi.
Bado tunaendelea kuyashuhudia ya Zitto Kabwe na CHADEMA. Ndani ya CCM pia hali si shwari. Ilifikia hatua ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Rais wa Nchi kutahadharisha kwamba chuki iliyopo imefikia hatua mbaya ya watu kutoaminiana kiasi cha kutopeana hata maji ya kunywa. Mheshimiwa Rais alikuwa sahihi kabisa. Kwangu mimi tahadhari hiyo ilipaswa ichukuliwe kwa uzito mkubwa na vyama vyote vyenye matatizo ya ndani. Siasa sio chuki, siasa ni maendeleo, hili linahitaji mjadala wake.
Pamoja na yote hayo ukweli uliopo ni kwamba Chama Cha Mapinduzi bado kinapendwa na Wananchi walio wengi ukilinganisha na vyama vingine. Hali hii itaendelea hivyo kwa muda mrefu hasa kama CCM itaendelea kufanya siasa za Mapinduzi kama ilivyokusudiwa (Mapinduzi ya Kifikra na Maendeleo). Wananchi wengi bado wana imani na CCM na Serikali yake. Tatizo kubwa kwa CCM ni baadhi ya Viongozi wake kujisahau na kufanya mambo ambayo ni kinyume na madhumuni ya CCM. Hali hiyo ndio iliyochangia CCM leo kuonekana ni Chama kinachopata shida sana kupata ushindi katika maeneo mengi ya miji mikubwa. Sababu zipo nyingi na zinaepukika.
Nasema ni baadhi ya viongozi kwa sababu ndani ya CCM kuna viongozi wasafi, wachapa kazi, wazalendo na pia wavumilivu. Rais Kikwete binafsi namuona kama mmoja wa Viongozi wa CCM wenye sifa hizo. Tukiacha propaganda za kwenye majukwaa ya kisiasa na kwenye mitandao ya kijamii, Kikwete anabaki kuwa Mwanasiasa Msikivu, Mzalendo na Mvumilivu, mwenye kujali matakwa ya wananchi ingawa kuna watu wanamkwamisha. Leo Nchi ipo katika mchakato wa kuandika Katiba mpya, ni kwa sababu ya maamuzi magumu yaliyofanywa na Kiongozi huyu. Kuongoza Nchi na Serikali kunahitajika chama cha siasa chenye misingi iliyojengeka toka chini kwenda juu. Kunahitaji chama cha siasa kisicho na migogoro ya mara kwa mara. Migogoro ndani ya vyama haiepukiki, lakini iwe ni migogoro yenye tija. Kinahitajika chama cha siasa kilicho ndani ya mioyo ya wenye Nchi ambao ni Wananchi wenyewe.
Tukiuzingatia UKWELI huo, bado CCM ina nafasi ya kuendelea kutuongoza kama Nchi. Maeneo ambayo CCM imeyapoteza kwa vyama vya upinzani, ni matokeo ya kutouona ukweli ndani ya CCM na badala yake kufanya kinyume na maamuzi ya wengi ndani ya Chama... Ni kama adhabu ambayo CCM imekuwa ikipewa na wanachama wake. Ni kama adhabu ambayo CCM imekuwa ikipewa na wananchi kwa niaba ya Serikali yake. Ni funzo ambalo likifanyiwa kazi, Wananchi wataendelea kuiamini kwa muda mrefu. Binafsi nina imani na CCM. Ni wakati sasa wa CCM kurudi katika misingi yake. Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliliona hili zamani na ndio sababu alitahadharisha na kutaka TUJISAHIHISHE!
 
watu wengi bado hawajajua nini maana ya maendeleo mdio maana bado wanaiunga mkono ccm lakini kadri watu wanavyojua nini maana ya maendeleo lazima waichukie ccm sasa kinachofanywa na ccm ni kuhakikisha watu wasipate hufahamu wa nini maendeleo ili wazidi kutawala ndio maana unaona watu wengi wa vijijini ndio wanaiunga ccm mkono pamoja na kuwa na hali ngumu ya maisha
 
Kifo cha hiki chama hakiepukiki kabisa kwani kila jitihada ya madaktar ya kukisaidia hiki chama ndio kinazidi kudhoofu. Kweli la kivunda halina ubani.
 
Najaribu kufikiria bara la Africa mpaka muda mwingine najiuliza hivi hili bara limelaaniwa au ni nini?pengine kwa mtazamo wa harakaharaka watu tunaweza tukachukulia poa kwa maana "kila mtu na maisha yake" lakini kimsiingi taifa hili linaenda mahali ambapo hapawezi kusemeka zaidi sana naona machafuko mbele yangu ambayo kwa mujibu wa maisha ya watanzaania tulivyokuwa tunapendana na tunaheshimiana,tunajaliana na tunasaidiana,tusiobaguana kwa itikadi za kidini,makabila wala tamaduni zetu tutakuja kua maadui wakubwa kama walivo wenzetu wa nchi jirani.

Nieleweke sichochei maafa!

Uwepo wa vyama vya siasa nchini si jambo baya laini vyama hivi vikikosa uweledi na uzalendo juu ya taifa hili la Tanzania ndipo hapa ambapo maono yangu yananibashiria.

Ebu angalia machafuko ya nchi mbalimbali duniani hasa za kiafrica zimekua na mapgano kutokana na SIASA na sio jambo lingine!nikiangaia mambo yanayoendelea bungeni yakutangaziana "kutoana vichwa" tunaliangalia kwa hali ya kizembe lakini si swala dogo.

Nchi hii ni nchi ya "amani" kama inavosemwa na bila shaka ukilinganisha na nchi zingine kama Nigeria au Kenya au Africa ya kati ni kweli tuna amani lakini wasiwasi wangu ni kwamba ni kwa jinsi gani wanasiasa wanalimbua swala hili na ni kwa jinsi gani wamekua na uzalendo wakuhakikisha TUNU YA AMANI YA TANZANIA inaendelea kulindwa na kuheshimiwa?

Inatupasa sana kufikiria juu ya ufuasi wa vyama ambavyo havina miongozo na sera za kimshikamano na badala yake tuwe wa kwanza kukemea kama wananchi,vinginevyo tusipofanya hivyo ipo siku tutasutwa na nafsi zetu.

Hivi hatuhisi wanasiasa wapo kwa maslahi binafsi?
 
Kama mtu anakiuka Katiba ili awe mtawala milele unategemea nini?
 
Ni kichwa cha habari kwenye front page ya gazeti la leo MAJIRA.
attachment.php


My take: Haogopi kushughulikiwa?
 
KAKAKUONA kushika kombe la dunia hana maana kwamba yeye ndiye atashinda, bali Brazil au Uholanzi. Vivyo hivyo Kutabiri CCM inaanguka inaweza kuwa CHADEMA
 
Yuko sawa si unaona wanavyotapatapa eti Oh Mbowe na slaa wangoke. Mziki mnene hawalali kaka
 
Meya kijana wa dar es salaam Jerry Slaa ameitabiria anguko kisiasa chama cha mapinduzi CCM.
Source: gazeti Majira
 
Back
Top Bottom