Ikiwa ni muda mrefu umepita,tokea watanzania tupate uhuru, tukiwa chini ya utawala wa TANU, hatimaye CCM bado mabadiliko makubwa hayajafanyika kuonesha malengo ya kulipatia taifa letu maendeleo. Awamu ya kwanza ilianza vyema, lakini mawazo ya Mwalimu JK Nyerere yalipoanza kukiukwa katika awamu ya pili, ya tatu na hatimaye ya nne ndio sasa watanzania tunaona tuko katika jehanamu iliyojaa chuki,njama,ufisadi, na umaskini uliokithiri.
Ni ukweli usiofichika CCCM na uongozi wake wote imeshindwa kutatua matatizo yanayotukabili, na niseme imekuwa ikituongezea tabu kila kukicha. Nianze na MGOMO WA MADAKTARI, AJALI ZA ZANZIBAR, SUALA LA MUUNGANO,KILIMO n.k vyote vinatabiri kifo cha CCM, kwa kuzingatia kuongezeka kwa machafuko nchini.
Watanzania walio wengi wenye akili timamu na hekima nadhani tayari wameshajiandaa kufanya mabadiliko makubwa 2015 ,na namini itakuwa ndio mwisho wa utawala wa kidhalimuna dhaifu wa CCM!
NA HICHO NDICHO KIFO CHA CCM 2015!
-------------------------------