Huu ndio ukweli usio pingika kuwa hizi ni saa za mwisho za chama cha mapinduzi kuwepo madarakani, na sababu zake ni kama zifuatazo. 1.wamekiuka miiko ya chama iliyo achwa na waasisi wa taifa hili ,j.k.nyerere ,r.m kawawa,j.s.walioba,na wengineo . Chama siyo cha mkulima na mfanyakazi,bali ni cha mabwanyenye na wala rushwa wakubwa mfano:epa,green dip,mikataba ya iptl ,rada,richmond,merermeta na mengineyo mengi tu! 2.watanzania wameichoka c.c.m mfano ni kwenye mikutano na maadhimisho mbalimbali bila kuweka kivutio kama vyakula ,vinywaji na kuwapatia watu usafiri hiyo sherehe au maadhimisho yatahudhuriwa na watu wachache sana tofauti na miaka ya 80,90 na mwanzo wa 2000 -2005 hivi watu walikuwa wanajaa sana. 3.ongezeko la vijana wengi wenye uelewa na wasiodanganyika ambao wana maliza shule za sekondari za kata na nyinginezo kwa wingi. Hawa vijana wanaushawishi mkubwa kwa jamii na hawadanganyiki kirahisi ,kinachotakiwa ni kuwaelmisha ili wajiandikishe kwenye daftari kwa kila m. wewe umesahau msemo wa "chenga twawala lakini kufungwa twafungwa" wananchi wanapigia kura ccm.