Malumbano na minyukano yanayoendelea ndani ya ccm ni ishara tosha kuwa ccm mwaka 2015 itakuwa chama cha upinzani. Kwanza dharau kubwa iliyoonyeshwa na mh kikwete kwa kudharau viongozi wa chama chake kuhusu mawaziri mizigo. Pili mbio za kupata mgombea urais itakuwa hatari sana kwani kuna mh Lowasa, Benard Membe, Samwel Sitta, na Asharose Migiro. Kwa jinsi inavyo jionyesha mbio za kugombea urais zitakuwa na uhasama mkubw kiasi kwamba atakayeshinda hataungwa mkono na wale walioshindwa. Na hapo ndipo itakapo pelekea ccm kwenda vipande vipande na mgawanyiko huo utakuwa mtaji kwa wapinzani. Fikiria kama El akipata fursa ya kupeperusha bendera ya ccm, je Membe, Sitta, Mwakyembe, na makundi yao watakubali kumuunga mkono?. Kwa muonekano Lowasa amechanja mbuga mbali sana na kuwaacha wenzake kwa mbali. Hii inadhihirisha kabisa kuwa lowasa atashinda kupitia ccm lakini akashindwa kupitia uchaguzi mkuu kwani hatapata sapoti kupitia mahasimu wake wa kisiasa wenye ushawishi mkubwa kwenye kanda zao. Hivyo ndivyo chama cha mapinduzi kitakavyo poteza maisha 2015.