Kifo cha CCM kimetimia

Kifo cha CCM kimetimia

Dr. Kabangila aliyekuwa Makamo Mwenyekiti wa Chama Cha Madaktari Nchini na Mkufunzi wa Chuo Kikuu Cha Bugando huko Mwanza, ajiunga na Chadema Rasmi: Chanzo: Star Tv habari ya Leo Usiku!

Huyu ndio yule aliyekuwa anachochea migomo ili wagonjwa wasipate huduma. Kumbe alitumwa na Chadema!
 
Huwa nashangazwa na wanaoojiita wanamageuzi wa kweli wanaoamua kutoka chama kimoja cha upinzani na kuhamia chama tawala.

Nawaelewa wanaohamia vyama vingine vinavyohubiri mabadiliko kuliko wanaorudi au kwenda chama tawala.

Ni msukumo gani utampelekea mwanamageuzi wa kweli arudi au kwenda chama tawala? Akabadilishe nini ambacho mwanzo hakuweza?
 
Dr. Kabangila aliyekuwa Makamo Mwenyekiti wa Chama Cha Madaktari Nchini na Mkufunzi wa Chuo Kikuu Cha Bugando huko Mwanza, ajiunga na Chadema Rasmi: Chanzo: Star Tv habari ya Leo Usiku!
nanuunga mkono Dr Kabangila
 
Mimi c chadema ila ni mpinzani wa maovu ya ccm. Cpendi kufichaficha na kuwa mnafiki naweka wazi kwanini mi ni mpinzani wa ccm. 1.mauaji na manyanyaso kwa wapigania haki mfano mauaji ya mwangosi kupigwa kwa mwenyekiti wa madaktari. 2.ufisadi wa waziwazi na matumizi mabaya ya fedha za uma,kufichwa kwa balali ili kuweka siri uozo wa utawala wa ccm 3.kupigwa kwa wazee waliokuwa wanafanya kazi eac walipokuwa wanadai haki zao 4.ubakaji kwa watoto unaofanywa na maccm viongozi 5. Kudhorota kwa elimu huku watoto wa maccm wanasoma nje 6. Kudhorota kwa wizara ya afya huku wao wanaenda india 7. Kutumia kodi za wananchi kuuwa upinzani 8. Uuzaji wa madawa ya kulevya unadhaminiwa na watoto wao ili kuwamaliza vijana wa kibongo 9. Sheria kuwa chini yao na kumnyanyasa asie na pesa yaani sheria kuwa chini ya pesa 10. Arv feki
 
Salaam makamanda!

Wingi wa maneno sio ukweli wa mambo. Kwa kifupi CCM ina hali mbali sana kwenye siasa za hapa Tanzania, huo ni ukweli ulio wazi. Wenye upeo wa kutosha wameshang'amua hilo muda mrefu sana, wanasema its just a matter of time. Mabadiliko wananchi wanayataka iwe kupitia chadema ama kupitia njia yeyote ile lakini ccm bye bye hawataki kuisikia tena. HIKI NI KIZAZI KIPYA WANATAKA KUSIMIKA UTAWALA WAO IWE KUPITIA CHADEMA AMA CHAMA CHOCHOTE KILE, LAKINI LAZIMA WASIMIKE UTAWALA WAO. Fuatilia historia ya vyama vingine kwenye mataifa mengine vyenye hadhi ya CCM utanielewa kwa urahisi zaidi. Tazama haya machache:-

1.Viongozi njaa wa chadema wanatangaza kujiuzulu lakini hawatangazi wapi wanahamia, tofauti na miaka ya zamani kiongozi akihama anatangaza amehamia wapi asap

2.Zitto, Mkumbo, Samson wamesimamishwa nyadhifa zao lakini hawataki kuondoka, wanapambana wabaki mle!

3.Mtela, Habib, Juliana, Kisandu wamefukuzwa lakini bado wanang'ang'ania chadema; bado wana mapenzi ya moyoni na chadema; japo baadhi wapo ccm lakini ni kwa sababu ya dhiki tu si kwa kupenda. Mioyo yao ipo chadema

4.Beneficiaries wakubwa wa mfumo wa ccm (wenye upeo mkubwa wa kuona jinsi upepo wa mabadiliko unavyovuma nchini) hawajitokezi waziwazi kuiponda chadema badala yake wanawatumia akina Mwigulu Nchemba (aka aibu katibu mkuu wa ccm na sio naibu katibu mkuu wa ccm) na akina Nape Nnauye, wao wanafanya mambo yao kimya kimya kwa kuelewa kuwa ccm days are just numbered!

Lumumba FC B7 project wanatumika tu na wenye upeo kujaribu kuchelewesha siku za CCM kuondoka lakini mwisho wa siku ccm wanapoteza huu mchezo, huu sio utabiri ni hali halisi wenye upeo wa kutosha wananielewa! Lumumba FC b7 project hawapendi kutumika lakini dhiki iliyoletwa na ccm ndio inayowafanya kukubali kutumika na si vinginevyo! Unajua dhiki ikizidi unakuwa nusu msukule akili inastak kufikiri, nadhani naeleweka! Usidhani Simiyu Yetu na wenzake mfano chamvida wanafanya wanachojua la hasha tatizo ni dhiki kuu iliyoletwa na ccm, wamepumbazika ila soon watarejewa na ufahamu wao halisi!

5.Kwa ujumla chuki ni kubwa sana kwa ccm toka kwa watu wa kawaida na wasio wa kawaida

NB:Wingi wa maneno sio ukweli wa mambo, kwa kifupi ccm hours are numbered! Naomba tuishie hapo!

Wenu katika ukombozi! TeamChadema
 
Last edited by a moderator:
Ukweli mtupu,waondoke tu japokua tayari wameshaharibu vya kutosha,kila idara imekufa,wao wanapambana na CHADEMA mpaka wanasahau wajibu wao.
 
Ushahidi wa kuhonga watu wahuni ili walete sintofahamu kwenye mikutano ya secretary General wa CHADEMA utakao tolewa kabla ya feb 2014 ni bomu aina ya Scud ambalo CCM watalowa kwa jasho huku wakishindwa kutembea hadharani.Watapigwa za uso,makalio na begani maana kila mtanzania ataelimishwa juu ya kazia wasababishazo maccm.Uchaguzi wa diwani maccm yatapoteza diwani zao nyingi sana huku yakitarajia kugalagazwa vikali katika uchaguzi wa ikulu kuu aka serikali za mitaa.HAKIKA KUFIKIKA KWA CHADEMA VIJIJINI NI ANGUKO LA CCM TENA VIBAYA,HUWEZI KUDANYA PEOPLE KWA KUPANDA BAJAJI,TRENI AU KUNUNUA SAMAKI.KIPINDI CHA MAIGIZO KIMEPITA,SASA NI KIPINDI CHA KAZI KAZI TU.DR SLAA ONGOZA KIKOSI KAZI,HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE.
 
Ni kweli hiki ni chama cha mizigo !
Tena mzigo namba moja ni Mwigulu Lameck.
Tangu apewe madaraka sijawahi kumsikia akiongelea mambo ya maendeleo, yenye maslahi kwa taifa au hata kutetea wananchi.

Siku zote hoja za mwigulu ni mabomu, umwagaji damu, chuki, fitina, uzandiki, ngono, matusi nk.

Hakika hiki ni chama cha mizigo
 
...tena ni mizigo ya mabomu wakati wowote italipuka...
 
Vyama vyote mizigp tuu

huna nguvu ya kusimamia msimamo wako,pili mwepesi kurubunika,tatu mwepesi kukata tamaa,,hadi hapo tu huna sifa za kufuatilia siasa za tanzania kaendelee na facebook tu na mengineyo.
 
Kazi kweli kweli: kutoka Chama Cha Magamba (CCM) hadi Chama Cha Mizigo! Magamba yasipovuliwa yanakuwa mzigo!

Ni kweli hiki ni chama cha mizigo !
Tena mzigo namba moja ni Mwigulu Lameck.
Tangu apewe madaraka sijawahi kumsikia akiongelea mambo ya maendeleo, yenye maslahi kwa taifa au hata kutetea wananchi.

Siku zote hoja za mwigulu ni mabomu, umwagaji damu, chuki, fitina, uzandiki, ngono, matusi nk.

Hakika hiki ni chama cha mizigo
 
huna nguvu ya kusimamia msimamo wako,pili mwepesi kurubunika,tatu mwepesi kukata tamaa,,hadi hapo tu huna sifa za kufuatilia siasa za tanzania kaendelee na facebook tu na mengineyo.

Huwez kunibadilisha we penda chama chako tu nakwambia tena vyama vyote mzigo tuuuuu
 
CCM imepitia hatua nyingi sana kutoka hali ilipokuwa kuanzia enzi za Nyerere hadi sasa. Hadi kipindi hiki kimeshabadilisha mwelekeo aliouasisi mwl. Nyerere kutokana na kukumbatia rushwa, ufisadi na matendo mbalimbali maovu kinyume na maadili. Imefikia hatua hata mawaziri wa serikali ya CCM kuitwa MIZIGO kutokana na kutowajibika ipasavyo kwa wananchi na hii imethibitishwa na viongozi wa CCM wenyewe kwa kauli zao kwenye mikutano ya hadhara. Ni wazi kuwa CCM imefikia hatua mbaya na ya aibu kwa taifa.
 
Hilo halina ubishi maana hata katibu mkuu wa hicho CHAMA CHAKAVU KINANA amethibitisha hilo.
 
Back
Top Bottom