Kifo cha CCM kimetimia

Kifo cha CCM kimetimia

Ndugu zangu, naona wazi kwa macho na akili yangu anguko kubwa sana la CCM kwenye uchaguzi mkuu 2015. Kweli sikio la kufa halisikii dawa. Pamoja na kuwa CCM inaona dalili zote hizi lakini bado haiamki toka usingizi wa kubweteka. CCM inabaki kuwa ndoto
 
Ikiwa ni muda mrefu umepita,tokea watanzania tupate uhuru, tukiwa chini ya utawala wa TANU, hatimaye CCM bado mabadiliko makubwa hayajafanyika kuonesha malengo ya kulipatia taifa letu maendeleo. Awamu ya kwanza ilianza vyema, lakini mawazo ya Mwalimu JK Nyerere yalipoanza kukiukwa katika awamu ya pili, ya tatu na hatimaye ya nne ndio sasa watanzania tunaona tuko katika jehanamu iliyojaa chuki,njama,ufisadi, na umaskini uliokithiri.

Ni ukweli usiofichika CCCM na uongozi wake wote imeshindwa kutatua matatizo yanayotukabili, na niseme imekuwa ikituongezea tabu kila kukicha. Nianze na MGOMO WA MADAKTARI, AJALI ZA ZANZIBAR, SUALA LA MUUNGANO,KILIMO n.k vyote vinatabiri kifo cha CCM, kwa kuzingatia kuongezeka kwa machafuko nchini.

Watanzania walio wengi wenye akili timamu na hekima nadhani tayari wameshajiandaa kufanya mabadiliko makubwa 2015 ,na namini itakuwa ndio mwisho wa utawala wa kidhalimuna dhaifu wa CCM!

NA HICHO NDICHO KIFO CHA CCM 2015!

-------------------------------

Hivi vijimambo tu, Mti wenye matunda ndo hupopoplewa mawe. mbona huko Afrika kusini kila siku mgomo wa wachimba migodi, huko kenya kila siku mgomo wa walimu, Kama muungano ni kifo cha CCM si CHADEMA kitakufa kabla ya 2014 kutokana na janja yao ya kutaka serikali tatu huku wakijua kabisa wana lengo la kuua muungano.
 
Ni mapema mno kukisomea buriani chama tawala. Sioni utayari wa chama kingine cha siasa nchini kuking'oa madarakani chama tawala hasa kwa kutumia mbinu wanazozitumia sasa. Bado kuna kazi kubwa wanatakiwa kufanya kama kweli wapinzania wanahitaji kufikia lengo lao la kushika dola. Wajue kuwa wanapambana na chama dola na kimeshaonesha mara nyingi kiwa hakisiti kutumia dola kubaki madarakani. Haya ni maoni ya mtu huru asiye na mfungamano na chama chochote cha siasa.

Mkuu CHADEMA hawajalijua hilo.
 
Sijui ni kwanini CDM wanajiaminisha wataishinda CCM 2015!
Nakiona CDM kikishindwa kama wenzao wa Zimbabwe MDC cha Morgan Tshangilai!

Mimi hata sea za CHADEMA sijui tena, wamekuwa wakitumia muda mwingi sana kujihami na tuhuma zinazowakabili na kuzihamishia kwa wapinzani wao badala ya kunadi sera. Wao ni waasisi wa uliberary na hata Mtei juzi kakiri lakini wakawabambikiza CUF, wamelipuana kwa mabomu wakasema ni CCM, Tindikali nayo wanasema eti ni mipango ya MWIGULLU, Video ya LWAKATAREakipanga mipango ya kuwadhuru akina Msacky nayo wakampambikiza kijana anayewatesa kwa sasa na kupelekea kumshambulia kwa zamu bila mafanikio.
 
ccm ata wakitumia trilion kwenye uchaguz ujao, kamwe awawezi shindwa.

Umeongea kinyume. CDM walisema arusha hata wakiweka jiwe litaishinda CCM, lakini juzi pamoja na kuwatisha wazee na akina mama kuwa kutatokea vita na wasiende kupiga kura, pamoja na kutumia chopa na timu nzima ya safu ya uongozi wa juu kabisa wa CDM, pamoja na kutumia zaidi ya bilioni 3 bado CCM ikiongozwa na vijana wadogo kabisa wawili, MWIGULLU na SHonza waliwatoa kamasi. Tukumbuke kuw 2015, kila mtu atasimama kama yeye kwenye kampeni kwenye jimbo lake, sijui kama CDM watapona katika majmbo ya arusha, Mbeya mjini, Iringa, Kawe na Kigoma kwa ZITTO baada ya kijana mwenye moano makubwa ZITTO kuona ni upuuzi kukaa kwenye chama chenye siasa za u-sisi, udini, na udikteta.
 
tatizo vijana wa kizazi hiki nakichukulia kama hamnazo,tatizo lenu tathimini mnazifanyia mkiwa mbele ya pc hamna ufahamu wa nn maana ya mageuzi.mtu anaehubili mageuzi hakuwahi hata kuandikishwa ktk kitabu cha wapiga kura lkn kelele nyingi kila kukicha mageuzi mageuzi.mageuzi hayo inakubidi yaanze na ww siyo kuyahubili kama makinisa yaliyoanzishwa hv juzi kati na watu wasiojielewa nn wanafanya kwa kulitangaza neno la Mungu kila kukicha.
 
Mkuu jichola3
Kwa kuwa tayari umeshadungwa sindano subili dawa ifanye kazi bila shaka upende usipende utapata nafuu au kufa kabisa 2015. Ugua pole mkuu.
 
Ndugu zangu, naona wazi kwa macho na akili yangu anguko kubwa sana la CCM kwenye uchaguzi mkuu 2015. Kweli sikio la kufa halisikii dawa. Pamoja na kuwa CCM inaona dalili zote hizi lakini bado haiamki toka usingizi wa kubweteka. CCM inabaki kuwa ndoto
Hizi siyo kelele za chura kweli?
 
tatizo vijana wa kizazi hiki nakichukulia kama hamnazo,tatizo lenu tathimini mnazifanyia mkiwa mbele ya pc hamna ufahamu wa nn maana ya mageuzi.mtu anaehubili mageuzi hakuwahi hata kuandikishwa ktk kitabu cha wapiga kura lkn kelele nyingi kila kukicha mageuzi mageuzi.mageuzi hayo inakubidi yaanze na ww siyo kuyahubili kama makinisa yaliyoanzishwa hv juzi kati na watu wasiojielewa nn wanafanya kwa kulitangaza neno la Mungu kila kukicha.
Mageuzi ya kwenye magazeti ya Tanzania Daima na MAWIO(MWANAHALISI), JF. Hawa ni watu wenye stress zao hawana lolote jipya la mageuzi .
 
Ndugu zangu, naona wazi kwa macho na akili yangu anguko kubwa sana la CCM kwenye uchaguzi mkuu 2015. Kweli sikio la kufa halisikii dawa. Pamoja na kuwa CCM inaona dalili zote hizi lakini bado haiamki toka usingizi wa kubweteka. CCM inabaki kuwa ndoto

kumbe ni kwa macho na akili zako? utakuwa na chongo na mtindio wa ubongo.
 
Kifo cha CCM kilitokea tangu uchaguzi wa 1995 aliposhinda MREMA wakachakachua. Hivyo tunaongozwa na MZIMU wa CCM na bado mzimu huu unaendelea kuchakachua. All in all sidhani kama 2015 itakufa kwani mzimu haufagi tena ni kwa maombi tuu ili utoweke.
 
Hizi siyo kelele za chura kweli?
Kwa kweli CCM chama changu hakina chake mwaka kesho na mwaka 2015 na bahati mbaya sana kimekata hata tamaa , huwezi kusikia leo CCM inafanya mkutano wa hadhara mkoa Fulani hata kata Fulani . Hizo ndo dalili za mtu kufa si uanza na kuzimia kama ilivyo CCM kwa sasa ilivyozimia. Na kama hakutakuwa na mabadiriko ya Uongozi wa juu na kuendelea kuwaacha hawa wenye kashfa kibaao ndo wanakichimbia kaburi kabisa. anayebisha na abishe .
 
Ni aibu kubwa sana kwa magamba wote kuanzia baba hadi mwana, wote kuwa na akili za hawavumi ila wapo, huku CDM wakiichukuliwa km ITV.....kila mwana CCM hadi top ambaye hakuna tena nafsi nyingine ya kwenda juu..bado ana akili za hawavumi...kwao kujipitisha mbele ya CDM , kuwchokonoa ili watajwe ktk media kuletea bifu kunawapa umaarufu, kunawafanya waonekane wana akili kuliko CDM, waonekane kuwa ni watoto w amjini kuliko CDM...kujipitisha kwa mbowe kunawafanya wajione kuwa wao ni wanasiasa kamili......hii mentality ni ngumu sana kuiondoa kwa waafrica.

Sijui hawavumi mwigulu aliyetoka kwa kujisugua makalio kwa CDM hadi JK akamwita kiboko yao..sijui m kuna single yoyote imeuzika tena..

JK alisifiwa na selasini na lipopewa na mbowe ilitosha kabisa kumfariji adhani keshatoka, magufuli alito ahotuba ya wizara yake akijichekesha sana kwa mbowe , ni list ndeefu ..hadi sasa Ndu gay kaamua tosa kiti nacho kiingie ktk hawavumi...
 
kila mhali maccm yapo busy kuandaa singo ya kuwakilisha CDM km hawavumi.
 
kila mhali maccm yapo busy kuandaa singo ya kuwakilisha CDM km hawavumi.

Mpango wao utashindwa na wataondoka kwa aibu,2015 tuko tayari kufa lakini tulinde kura kwa faida yetu(tutakaobaki hai) na watoto wetu!!
 
Back
Top Bottom